Geita: Wanawake wasusiwa mazishi, wanaume wagoma kushiriki kisa wakituhumiwa kuua waume zao

Wanawake katika Kijiji cha Imaramawazo, Mtaa wa Ibongo, Kata ya Ludete, Wilaya ya Geita wamesusiwa kuchimba kaburi na kufanya mazishi ya Zawadi Mchele mkazi wa kijiji hicho aliyefariki kwa kuugua ghafla, sababu ikiwa ni wanawake hao kuhusishwa na tuhuma za mauaji ya wanaume katika kijiji hicho.

Baadhi ya wanawake waliochimba kaburi wamesema wanawake hao walisusiwa zoezi hilo baada ya kuhusishwa na imani za kishirikina ambapo wanaume wengi wamekuwa wakifariki bila kuugua ikilinganishwa na wanawake kijijini hapo.

"Leo wanawake ndio wamechimba kaburi, na hii inatokana na kwamba wanaume wamechoshwa na matukio ya wanaume pekee kufaliki ghafla wakati mwingine hata bila kuugua.

“Kwa hiyo hii imefanywa kama adhabu kwa wanawake kwamba kama wanaua basi wawajibike kufanya mazishi,"- Eunice Mabula, Mkazi wa Kijiji cha Imaramawazo.

Mwenyekiti wa mtaa huo, Coronel Petro anasema alishangaa kupigiwa simu za jeshi la Polisi juu ya sintofahamu ya wanaume kwenye kijiji hicho kutoshiri mazishi ndipo yeye pamoja na Jeshi la Polisi wakafika kwenye kijiji hicho na kuwaamuru wanaume kijijini hapo kushiriki mazishi.

Hata hivyo, baada ya Jeshi la Polisi kuamuru mazishi yafanywe na wanaume, wakazi wa mtaa huo (wanaume) kwa kushirikiana na wanawake kutoka kijiji cha jirani wakafanikisha mazishi hayo ambayo wanawake wa kijiji husika hawakushiriki kutokana na kuogopa kususiwa tena mazishi.


Source: East Africa TV

View attachment 2215270
Kumbe hata bila ya kuwezeshwa wanaweza.
 
Back
Top Bottom