Geita: Wanawake wasusiwa mazishi, wanaume wagoma kushiriki kisa wakituhumiwa kuua waume zao

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Wanawake katika Kijiji cha Imaramawazo, Mtaa wa Ibongo, Kata ya Ludete, Wilaya ya Geita wamesusiwa kuchimba kaburi na kufanya mazishi ya Zawadi Mchele mkazi wa kijiji hicho aliyefariki kwa kuugua ghafla, sababu ikiwa ni wanawake hao kuhusishwa na tuhuma za mauaji ya wanaume katika kijiji hicho.

Baadhi ya wanawake waliochimba kaburi wamesema wanawake hao walisusiwa zoezi hilo baada ya kuhusishwa na imani za kishirikina ambapo wanaume wengi wamekuwa wakifariki bila kuugua ikilinganishwa na wanawake kijijini hapo.

"Leo wanawake ndio wamechimba kaburi, na hii inatokana na kwamba wanaume wamechoshwa na matukio ya wanaume pekee kufaliki ghafla wakati mwingine hata bila kuugua.

“Kwa hiyo hii imefanywa kama adhabu kwa wanawake kwamba kama wanaua basi wawajibike kufanya mazishi,"- Eunice Mabula, Mkazi wa Kijiji cha Imaramawazo.

Mwenyekiti wa mtaa huo, Coronel Petro anasema alishangaa kupigiwa simu za jeshi la Polisi juu ya sintofahamu ya wanaume kwenye kijiji hicho kutoshiri mazishi ndipo yeye pamoja na Jeshi la Polisi wakafika kwenye kijiji hicho na kuwaamuru wanaume kijijini hapo kushiriki mazishi.

Hata hivyo, baada ya Jeshi la Polisi kuamuru mazishi yafanywe na wanaume, wakazi wa mtaa huo (wanaume) kwa kushirikiana na wanawake kutoka kijiji cha jirani wakafanikisha mazishi hayo ambayo wanawake wa kijiji husika hawakushiriki kutokana na kuogopa kususiwa tena mazishi.

Source: East Africa TV

GEITA1.jpg
 
Baadhi ya wanawake waliochimba kaburi wamesema wanawake hao walisusiwa zoezi hilo baada ya kuhusishwa na imani za kishirikina ambapo wanaume wengi wamekuwa wakifariki bila kuugua ikilinganishwa na wanawake kijijini hapo.

"Leo wanawake ndio wamechimba kaburi, na hii inatokana na kwamba wanaume wamechoshwa na matukio ya wanaume pekee kufaliki ghafla wakati mwingine hata bila kuugua.

“Kwa hiyo hii imefanywa kama adhabu kwa wanawake kwamba kama wanaua basi wawajibike kufanya mazishi,"- Eunice Mabula, Mkazi wa Kijiji cha Imaramawazo.
Huko si ndiko wafu wanafufuka kishirikina!!?

Usikute hata hilo kaburi wamechimba haohao wanaume bila kujijua kwahiyo adhabu haijawakuta walengwa
 
Mwenyekiti wa mtaa huo, Coronel Petro anasema alishangaa kupigiwa simu za jeshi la Polisi juu ya sintofahamu ya wanaume kwenye kijiji hicho kutoshiri mazishi

Huyo mwenyekiti anapewa taarifa na polisi kwani yeye anaishi wapi?
 
Wenye imani haba. Waache ushamba wa kubugia ma energy wakati hawajala chochote,pombe kali,stress,kuwa na wanawake wengi etc
Acheni kuua wanaume wenzetu hapo Geita

Mnaua wanaume Kwa ushirikina alafu unakuja jf kusingizia wanakufa na energy drinks na pombe Kali...we ulisikia wapi?

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom