Gazeti Mwananchi: CHADEMA sasa Vipande viwili!

Gazeti Mwananchi: CHADEMA sasa Vipande viwili!

"Ninaunga mkono Dk Slaa kuwania tena nafasi ya urais mwaka 2015. Mwenyekiti amemtangaza baada ya kupata baraka ya vikao vya chama," alisema Mtei.
 
Nafikiri kwa mtazamo wa muandishi vipande viwili anavyo visema yeye ni kuonekana kuna wagombea 2. Yaani pande moja ni upande wa Zitto na pande lingine ni upande wa Slaa, jumla mapande mawili.

Sasa pa kujiuliza katika hayo mapande mawili yamegawa vipi chama na wanachadema hadi kuonekana chadema iko vipande?! Muandishi alitakiwa aonyesha bila chembe ya shaka kwenye hili.

Kwa kuwa ameonyesha obwe na matobo kwenye habari yake, kwangu naona mwandishi ameandika akiwa anafikiria sana mapande kuliko walaji watakavyo yapokea mapnde hayo na kuya-digest.

Wewe ni mmoja ya wale wanaompiga vita zitto kabwe nakushangaa unaposhangaa habari hii kwa taarifa yako mzee mtei ndio mwenye kauli ya mwisho nani agombee hayo mambo ya kamati kuu ni uongo ZITTO nakuonea huruma umekaa na watu wanafiki
 
Ningeshangaa kama usinge changia kwa kauli kama hii! Hebu nenda mbele zaidi na useme kwa kusadifu mizania. Zk nae alikuwa kwa maagizo ya nani?! Kabla kamati kuu haijapitisha mgombea weka kwenye mizani majina mawili uone la nani linamzidi mwenzake uzito halafu peleka ripoti Lumumba uone ukiwa una wakabidhi ripoti nyuso zao zitakuwaje.

Asubuhi njema! Naona wewe ndio umeingia kazini rasmi kama kawaida 24/7 baadae kidogo kaka.

"Ninaunga mkono Dk Slaa kuwania tena nafasi ya urais mwaka 2015. Mwenyekiti amemtangaza baada ya kupata baraka ya vikao vya chama," alisema Mtei.
 
Nilikutana siku moja na afisa masoko wa mwananchi,aliniambia siku wakiandika habari za CDM gazeti huwa linanunuliwa sana.

Ndiyo maana leo unakuta limeandika hivyo ili wale wanaopenda migogoro ndani ya chama wanunue, na wale wasio penda migogoro wanunue wakitaka kujua ni mgogoro gani huo ili hali mwenye kiti amesema hakuna makundi?

Kwa ujumla gazeti la mwananchi linafanya biashara, wanafanya hivyo ili watu tujue kuna mgogoro ili gazeti linunuliwe kwa wingi.
 
w umeuona huo mgawanyiko wa vipande viwili???
coz zzk hajasema lolote, mtei na heche wamekubaliana na kauli ya mwenyekt wao, huo mgawanyiko upo wapi??
mi nimelisoma nkabaki hata sielewi
"Ninaunga mkono Dk Slaa kuwania tena nafasi ya urais mwaka 2015. Mwenyekiti amemtangaza baada ya kupata baraka ya vikao vya chama," alisema Mtei.
 
w umeuona huo mgawanyiko wa vipande viwili???
coz zzk hajasema lolote, mtei na heche wamekubaliana na kauli ya mwenyekt wao, huo mgawanyiko upo wapi??
mi nimelisoma nkabaki hata sielewi

Kupenda noma,chongo unaita kengeza.
 
Sijaona mahusiano ya mojakwamoja ya kichwa cha habari hii na ?maelezo yaliyotolewa Dr mwenyewe kasema wanachama wakiamua na si mwenyekiti akiamua haya kwa mtazamo wangu ni mawazo ya mwenyekiti. Ingekuwa upande wa piloi mawazo ya mwenyekiti ni amri lakini hukui CHADEMA hakuna kitu hicho.
"Ninaunga mkono Dk Slaa kuwania tena nafasi ya urais mwaka 2015. Mwenyekiti amemtangaza baada ya kupata baraka ya vikao vya chama," alisema Mtei.
 
Uandishi njaa at work, anataka kuuaminisha umma huku hana vigezo mwisho wa siku ni blah blah blah!!!!

"Ninaunga mkono Dk Slaa kuwania tena nafasi ya urais mwaka 2015. Mwenyekiti amemtangaza baada ya kupata baraka ya vikao vya chama," alisema Mtei.
 
Kumbe ni maagizo ya Mtei.

"Ninaunga mkono Dk Slaa kuwania tena nafasi ya urais mwaka 2015. Mwenyekiti amemtangaza baada ya kupata baraka ya vikao vya chama," alisema Mtei.
 
Nafikiri kwa mtazamo wa muandishi vipande viwili anavyo visema yeye ni kuonekana kuna wagombea 2. Yaani pande moja ni upande wa Zitto na pande lingine ni upande wa Slaa, jumla mapande mawili.

Sasa pa kujiuliza katika hayo mapande mawili yamegawa vipi chama na wanachadema hadi kuonekana chadema iko vipande?! Muandishi alitakiwa aonyesha bila chembe ya shaka kwenye hili.

Kwa kuwa ameonyesha obwe na matobo kwenye habari yake, kwangu naona mwandishi ameandika akiwa anafikiria sana mapande kuliko walaji watakavyo yapokea mapnde hayo na kuya-digest.

Vipande viwili mbona vinaonekana wazi kwenye hiyo habari. Nilitegemea ukanushe kuwa Mtei hakutoa kauli kuwa kauli ya Mbowe ina baraka ya chama. Ila cha kushangaza kundi moja la Pr Baregu na Kitila Mkumbo hawana taarifa na maamuzi hayo ya chama. Wakati huo huo Godbless Lema anakubaliana na hiyo kauli ya Mbowe. Mwandish ametaja vipande viwili nilivyobold hapo.

Msijitie upofu wa mawazo, ni kitu kibaya sana kwa chama kama CHADEMA kinachojiita chama cha DEMOKRASIA!
 
“Ninaunga mkono Dk Slaa kuwania tena nafasi ya urais mwaka 2015. Mwenyekiti amemtangaza baada ya kupata baraka ya vikao vya chama,” alisema Mtei.

Masalia at work
 
habari hii, ina kitu ndani yake. nimeona magazeti na taarifa nyingi humu jf kama zimejaribu ama kupotosha kwa misingi ya kuuza magazeti au ule usemi mwamba ngoma huvutia kwake. nilichokisoma kwa mh MBOWE ni taarifa yake kuwa hatogombea nafasi hiyo ya URAIS, isipokuwa atasimamia ipasavyo kumpata mgombea madhubuti atakaye peperusha vyema bendera ya CDM kuelekea IKULU.

Baada ya hapo magazeti na watu wenye hisia zao tofauti ama kumchokoza fulani au kutaka huo unaoitwa mpasuko utokee ndipo linapotajwa jina la SLAAA ndilo mwenyekiti alilolipendekeza. na siamini kama kweli mzee Mtei kayasema hayo yaliyoandikwa kama kayasema kweli basi ndo ile REMOTE , mh LEMA kama na yy aliyoyasema ni kweli bila shaka REMOTE, naye bwana Heche sina shaka siasa za kufuata mkumbo REMOTE imetumika, kama kweli prof Baregu hayo yaliyoandikwa ndiyo aliyosema.

Anapaswa kupongezwa kwani CDM si chama cha mtu mfukoni, analoamua yy wengine wafyate chama ni vikao halali kwa wakati muafaka. dr MKUMBO naye alichosema sina shaka nacho kama ni sahihi ,kwani ndicho haswa kinacholenga kutoa mgombea ambaye kila mwana CDM na mwananchi kwa ujumla atajivunia upatikanaji wake kwa maana tumeshinda pamoja na tumeshindwa pamoja tushikamane.

MWISHO heko zako ZZK umeonesha ukomavu wa khali ya juu, naamini huamini hicho kilichoandikwa ndicho alichosema mwenyekiti wako. Unaamini haiwezi kuwa hivyo kwa kuburutwa bila vikao. ndo maana hujachangia lolote BIG UP. hata mzee Slaa nakupa 5, kwa kile ulichokisema.

Unamaanisha hata ulipoteuliwa wakati ule hukuomba, uliombwa basi hata sasa ukiombwa utatafakari maana vikao vikikaa ukiona taratibu zote zimefutwa bila kuathiri chama unaweza kukubali . KUMBUKENI MZEE MTEI NA MZEE MAKANIN [R.i.p] walitaka kuburuzana ngoma ikalala msirudie huko.
 
“Ninaunga mkono Dk Slaa kuwania tena nafasi ya urais mwaka 2015. Mwenyekiti amemtangaza baada ya kupata baraka ya vikao vya chama,” alisema Mtei.

Kuwepo kundi la PM7 hakulipi
 
Tunakoenda ndio muda wa vyombo vya habari kuwatumikia wanasiasa na sio wananchi tena.?
 
Mtei bana... ZZK alipotanganiza nia, Mtei alikuja juu na kumwambia huu si wakati muafaka na atakivuruga chama. Mbowe kamtangaza Slaa..Mtei anaona ni wakati muafaka na si kuvuruga chama. Siasa za Bongo ni full usanii na Umimi.
 
Vipande viwili mbona vinaonekana wazi kwenye hiyo habari. Nilitegemea ukanushe kuwa Mtei hakutoa kauli kuwa kauli ya Mbowe ina baraka ya chama. Ila cha kushangaza kundi moja la Pr Baregu na Kitila Mkumbo hawana taarifa na maamuzi hayo ya chama. Wakati huo huo Godbless Lema anakubaliana na hiyo kauli ya Mbowe. Mwandish ametaja vipande viwili nilivyobold hapo.

Msijitie upofu wa mawazo, ni kitu kibaya sana kwa chama kama CHADEMA kinachojiita chama cha DEMOKRASIA!

Kundi la Masalia linapumulia mashine.Hata mkibadili ID mara ngapi tutawajua tu.
 
Back
Top Bottom