Gazeti letu la Udaku JF..

Iwepo kona ya waliopigwa BAN na Mod na pia coner ya wageni wa wiki waliojiunga JF
 
akikushika?
 
FF akutwana na baibui kumbe dume polisi wamchoma ndani!!Afro danzi afumwa akila uroda na Rejao,Kiranja mkuu wakutwa live Da sofi wakienda clinic na wamebeba mtoto wao!!Preta akutwa live na KakaKiiza calabash!
 
sitaki makuu mwaka huu ..i will just go to church....wewe unataka nini? kwenda wapi?

Saint Ivuga ajiandaa kuumalizia mwaka Kanisani:
asema mabalaa yote yaliyomtokea ni kwa sababu ya kumweka Mungu pembeni.
Aapa kuacha ulevi, aanza harakati za kutafuta kimwana wa kuoa baada ya kukimbiwa na mke
 
Sikonge akamatwa na Wanajeshi wa Wanyamapori:

Yule Mwanachama asiye maarufu sana wa JF, aliyekuja na msemo wa "Changia JF, Mkono mtupu haulambwi", amekamatwa na wanajeshi wa wanyamapori katika kijiji cha Kipanga, umbali kidogo kutoka Sikonge Mjini. Sikonge alikutwa akiwa amelewa chakali na chupa mbili za gongo za ukubwa wa nusu lita, huku moja ikiwa imeisha na nyingine ikiwa imebaki nusu.

Kisa cha kukamatwa na askari hao ilikuwa ni vipande vya Nyama Pori alivyokuwa akitumia kupozea hilo gongo lake huku akiimba nyimbo nyingi za kinyamwezi na zaidi kupendelea ule wenye kutoa lugha chafu kama Wamarekani weusi yaani M.F., jambo ambalo si la kawaida kwa makabila mengi ya Tanzania. Hata Tupac alivyotaka kutukana kwa Kiswahili, ilibidi aunge unge maneno maana neno MF kwa Kiswahili halipo.

Wimbo huo, gongo hilo na nyama hizo zilikuwa zimemnogea kiasi kwamba akawa kazungukwa na washabiki kadhaa wakimsaidia kuuimba wimbo huo "Nguluwe ikulyaga twingi Vayaya................. Nani wamleta, Mt**a Nina kumlye masumule........."

Alipopekuliwa zaidi, alikutwa na LAPUTOPU aliyopewa wakati wa Kampeni za Ubunge na Kandambilimbili wa JF huku ikiwa imefunikwa SIKIRINI (Screen) bila kuzimwa (Logoff) na ilipofunguliwa, walikuta kumbe alikuwa katika kuandika makala nyingine ndani ya JamiiForums ili kuwakumbusha member wengine wapya na wa zamani kwamba:

CHANGIA JF, MKONO MTUPU HAULAMBWI.

( https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/22767-changia-jf-mkono-mtupu-haulambwi-16.html )
 

Hahahahahaaaa,, Mkuu umeua!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…