Gazeti la Mwananchi limeripoti juu ya sakata linaloendelea kuhusu uuzwaji wa Kiwanda cha NPC Kiuta

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
September 14, 2023, kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania.
photo_2023-09-14_18-14-08.jpg
Wajumbe watano wa bodi ya Kiwanda cha Uchapaji cha Taifa (Kiuta), wanakabiliwa na tuhuma za kuuza hati ya kitalu namba 13 ya eneo la kiwanda hicho bila kushirikisha uhalali wa idadi kubwa ya wamiliki.

Kutokana na tuhuma hizo, wajumbe hao wamefunguliwa kesi namba 265 Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi itakayosomwa kesho kupinga uhalali wa wajumbe wawili kuidhinisha mauzo hayo kwa Kiwanda cha kuzalisha bidhaa tofauti cha Superdoll Group, kwa mujibu wa Mwanasheria anayetetea wanahisa hao, Ambrose Nkwera.

Akizungumza na Mwananchi juzi, aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi hiyo, Patrick Nyundo alisema endapo kuna ukiukwaji alioufanya mahakama itaamua ukweli wa tukio hilo.

“Hilo suala lipo mahakama ya Wajumbe wa bodi ya KiutaardhinaSeptemba15kesiitaendelea kwa hiyo ukweli utajulika na huko, nisingependa kueleza lolote,” alisema.

Tuhuma hizo zimepata kasi zaidi wiki hii baada ya baadhi ya wana hisa na waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda hicho kukusanyika kiwandani hapo na kutangaza kupinga kuuzwa kwa kiwanda hicho huku Jeshi la Polisi likiwatuliza.

Mwananchi halikuthibitisha idadi ya wanachama wasiokubaliana na mauzo ya kitalu hicho kwa Sh10 bilioni ikihusisha ardhi, majengo, mitambo ya uchapaji waliomiliki Miaka 21….

Habari zaidi kwenye Gazeti la Mwananchi
 
Back
Top Bottom