Wanaume na mtihani mgumu wa kuchagua kati ya mama au mke

Malaria 2

JF-Expert Member
Oct 17, 2023
2,648
3,938

Wanaume na mtihani mgumu wa kuchagua kati ya mama au mke. Hii na makala katika gazeti la mwananchi. Uislam unasemaje?​

Kaa tayari upate

kutoka kwa Anas bin Nadhwiri Al-Ashijainiy amesema: Siku moja mama yake Ibn Mas'uud (Radhwiya Allaahu 'anha) alitaka maji ya kunywa na ilikuwa usiku – kwa mwanawe Ibn Mas'uud, akaenda kumletea maji, kurudi akamkuta keshalala, Ibn Mas'uud akabaki amesimama na maji mbele ya kichwa chake mpaka asubuhi, na walipofika Abu Muwsaa Al-Ash'ariy na Abu 'Aamir kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakampa Bay'ah (kiapo cha utii) na wakasilimu.

Nabiy akawauliza (amefenya nini yule mwanamke, miongoni mwenu aitwaye kadhaa wa kadhaa?

Nabiy akasema: (Kwa sababu ya kumtendea mama yake akasema, alikuwa ana Mama bibi kizee, mara akawajia muonyaji akisema, hakika adui anakusudia kuwadhuruni, Mama huyu (Mama Ibn Mas'uud) akambeba mama yake mgongoni mwake, akichoka anamtua chini (anapumzika) kasha anakutanisha tumbo lake na tumbo la Mama yake (yaani anambeba kwa kumkumbatia tumboni) ikawa miguu yake iko chini ya miguu ya Mama yake kutokana na kumkinga na joto kali, mpaka akaokoka na adui yule).

[Ameitoa 'Abdur-Razaaq katika Muswannaf yake].
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom