DOKEZO Wanahisa wa NPC KIUTA wafungiwa kiwandani kwa siku tatu, wagoma kutoka wakidai Kiwanda chao kinauzwa kitapeli

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest

Watumishi na Wanahisa waliofungiwa ndani ya Kiwanda cha NPC KIUTA kutokana na mgogoro unaoendelea.
Wafanyakazi wa Kiwanda cha Uchapaji cha Taifa au NPC National Printing Company Limited (KIUTA) ambacho kwa ufupi kunatambulika kwa jina la NPC KIUTA wanapitia wakati mgumu, baadhi yao wakiwa wanalala ndani ya kiwanda hicho kwa siku kadhaa huku wengine wakifungiwa kwa nje na kuzuiwa kuingia ndani kutokana na sakata linaloendelea kiwandani hapo.

Kiwanda hicho chenye Watumishi zaidi ya 130 kikiwa chini ya umiliki wa Wanahisa 152, kipo katika mgogoro mkubwa dhidi ya majirani zao, Kiwanda cha Superdoll.

Baadhi ya Watumishi wa NPC KIUTA wanadai kuwa waliokuwa wajumbe wawili wa Bodi ya Wakurugenzi wamehusika katika kuuza kiwanda hicho (Kitalu Namba 13) kwa Kiwanda cha Superdoll kwa kificho.

Taarifa kutoka NPC KIUTA zinaeleza kuwa waliohusika na uuzwaji huo ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi, Peter Nyundo na mjumbe mwingine wa Bodi, Pastory, wakati wajumbe wengine watatu wa Bodi wao walikataa kushiriki katika mauzo hayo na hivyo kuandika barua ya kujiuzulu.
6dc88964-ec43-43a0-a382-98deee7fb6a7.jpeg

Watumishi na Wanahisa waliofungiwa ndani ya Kiwanda cha NPC KIUTA kutokana na mgogoro unaoendelea.

Chanzo kutoka NPC KIUTA kinaeleza Kampuni ya Superdoll inatumia nguvu kubwa ya uchumi wake kuweza kuwakandamiza Watumishi hao 130 na Wanahisa ndio maana licha ya kwenda kwenda kuripoti mamlaka mbalimbali hadi Wizara ya Ardhi bado kumekuwa na ugumu wa kupata haki yao.
5aeb531e-a16a-408d-ab63-02eef7961676.jpeg

Mazingira ya NPC KIUTA

Chanzo kimoja kimesema “Kiwanda hiki kilikuwa kinamilikiwa na Serikali miaka ya nyuma, baadaye ikauzwa na kikawa kinamilikiwa na Wafanyakazi wenyewe kwa mfumo wa Hisa chini ya Bodi ambao ndio waliokuwa wakiendesha kampuni.

“Hapo kati Mwenyekiti Patrick Nyundo akasimamishwa na wanahisa kutokana na baadhi ya mienendo yake kuonekana haipo sawa, akiwa amesimamishwa kuna siku ikaingia Tsh Bilioni 2.5 kwenye akaunti ya Kampuni tulipofuatilia ndipo tukasikia ni sehemu ya mauzo ya Kitalu Namba 13 imeuzwa pasipo ridhaa ya Wanahisa.

“Tumefanya juhudi kadhaa hadi kumuona Waziri wa Ardhi ambaye awali aliahidi kutupa ushirikiano, akatukabidhi kwa maofisa na Kamishna pale Wizara ya Ardhi lakini hatujpata msaada.

“ Mbali na hapo kuna Afisa wa Ardhi anaitwa Said Chumvi, wamekuwa upate wa Kampuni ya Superdoll na kutumia nguvu kubwa kuhakikisha tunashindwa katika madai yetu.

“Tumefungua kesi Mahakamani baada ya kuona kila tunachofanya kinashindikana na inatarajiwa kuanza kusikilizwa Ijumaa Septemba 15, 2023.”
3e4612fe-006e-443b-afb6-7cdfd5fab516.jpeg

eef4389a-60c6-4c7a-a3c7-b851a6ea7ea7.jpeg

Mazingira ya NPC KIUTA kwa nje, baadhi ya Wafanyakazi wakiwa nje ya Kiwanda.
Chanzo kingine kilichopo ndani ya Kiwanda cha NPC KIUTA kimesema “Tumefungiwa ndani tangu Jumapili (Septemba 10, 2023), wengine wamefungiwa nje, Mabaunsa waliotumwa wamekuja kufanya fujo, wamepiga baadhi ya Wafanyakazi na hadi sasa hali bado ni tete.

“Wengi wanaomiliki Hisa na watumishi ni watu wazima, wamejikuta katika hali mbaya, tunamuomba Rais Samia na viongozi wa juu Serikalini watusaidie kwani inavyoonekana hao majirani zetu wanatumia nguvu kubwa ya uchumi waliyonayo kutukandamiza sisi.”

e64a6faa-37b8-4216-9d81-e2558530cfba.jpeg
 
View attachment 2746762
Watumishi na Wanahisa waliofungiwa ndani ya Kiwanda cha NPC KIUTA kutokana na mgogoro unaoendelea.
Wafanyakazi wa Kiwanda cha Uchapaji cha Taifa au NPC National Printing Company Limited (KIUTA) ambacho kwa ufupi kunatambulika kwa jina la NPC KIUTA wanapitia wakati mgumu, baadhi yao wakiwa wanalala ndani ya kiwanda hicho kwa siku kadhaa huku wengine wakifungiwa kwa nje na kuzuiwa kuingia ndani kutokana na sakata linaloendelea kiwandani hapo.

Kiwanda hicho chenye Watumishi zaidi ya 130 kikiwa chini ya umiliki wa Wanahisa 152, kipo katika mgogoro mkubwa dhidi ya majirani zao, Kiwanda cha Superdoll.

Baadhi ya Watumishi wa NPC KIUTA wanadai kuwa waliokuwa wajumbe wawili wa Bodi ya Wakurugenzi wamehusika katika kuuza kiwanda hicho (Kitalu Namba 13) kwa Kiwanda cha Superdoll kwa kificho.

Taarifa kutoka NPC KIUTA zinaeleza kuwa waliohusika na uuzwaji huo ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi, Peter Nyundo na mjumbe mwingine wa Bodi, Pastory, wakati wajumbe wengine watatu wa Bodi wao walikataa kushiriki katika mauzo hayo na hivyo kuandika barua ya kujiuzulu.
View attachment 2746763
Watumishi na Wanahisa waliofungiwa ndani ya Kiwanda cha NPC KIUTA kutokana na mgogoro unaoendelea.

Chanzo kutoka NPC KIUTA kinaeleza Kampuni ya Superdoll inatumia nguvu kubwa ya uchumi wake kuweza kuwakandamiza Watumishi hao 130 na Wanahisa ndio maana licha ya kwenda kwenda kuripoti mamlaka mbalimbali hadi Wizara ya Ardhi bado kumekuwa na ugumu wa kupata haki yao.
View attachment 2746764
Mazingira ya NPC KIUTA

Chanzo kimoja kimesema “Kiwanda hiki kilikuwa kinamilikiwa na Serikali miaka ya nyuma, baadaye ikauzwa na kikawa kinamilikiwa na Wafanyakazi wenyewe kwa mfumo wa Hisa chini ya Bodi ambao ndio waliokuwa wakiendesha kampuni.

“Hapo kati Mwenyekiti Patrick Nyundo akasimamishwa na wanahisa kutokana na baadhi ya mienendo yake kuonekana haipo sawa, akiwa amesimamishwa kuna siku ikaingia Tsh Bilioni 2.5 kwenye akaunti ya Kampuni tulipofuatilia ndipo tukasikia ni sehemu ya mauzo ya Kitalu Namba 13 imeuzwa pasipo ridhaa ya Wanahisa.

“Tumefanya juhudi kadhaa hadi kumuona Waziri wa Ardhi ambaye awali aliahidi kutupa ushirikiano, akatukabidhi kwa maofisa na Kamishna pale Wizara ya Ardhi lakini hatujpata msaada.

“ Mbali na hapo kuna Afisa wa Ardhi anaitwa Said Chumvi, wamekuwa upate wa Kampuni ya Superdoll na kutumia nguvu kubwa kuhakikisha tunashindwa katika madai yetu.

“Tumefungua kesi Mahakamani baada ya kuona kila tunachofanya kinashindikana na inatarajiwa kuanza kusikilizwa Ijumaa Septemba 15, 2023.”
View attachment 2746765
Mazingira ya NPC KIUTA kwa nje, baadhi ya Wafanyakazi wakiwa nje ya Kiwanda.
Chanzo kingine kilichopo ndani ya Kiwanda cha NPC KIUTA kimesema “Tumefungiwa ndani tangu Jumapili (Septemba 10, 2023), wengine wamefungiwa nje, Mabaunsa waliotumwa wamekuja kufanya fujo, wamepiga baadhi ya Wafanyakazi na hadi sasa hali bado ni tete.

“Wengi wanaomiliki Hisa na watumishi ni watu wazima, wamejikuta katika hali mbaya, tunamuomba Rais Samia na viongozi wa juu Serikalini watusaidie kwani inavyoonekana hao majirani zetu wanatumia nguvu kubwa ya uchumi waliyonayo kutukandamiza sisi.”

1. Kiumeuzwa?
2. Waliouza wana capacity kisheria?
3. Kuna consideration?
4. Wamefuata taratibu za kodi?

Kama majibu yote ni Yes, nendeni nyumbani kapambaneni na maisha. Bandari inauzwa hatuna cha kufanye sembuse NPC!!
 
Hapa yenyewe Kuna tatizo yaani kampuni ilikua ya serikali ghafla ikamilikiwa na wafanyakazi wenyewe kwa mfumo wa hisa..

Yaani wafanyakazi ndio share holders na ndio wameajiri management na bodi? Shareholders 150 ambapo hao hao ndio among wafanyakazi 130?

Kuna kitu hakipo sawa, hasa kwenye kuhamisha umiliki kutoka serikalini kwenda kwa mtu binafsi/wafanyakazi. Otherwise hapo wangekimbilia mahakamani kuweka zuio ndio waendelee na maandamano otherwise kama bodi iliridhia kuuza na wakatia sign hakuna kitu wanaweza fanya tena.

Tutangulize sheria sio mihemko na jazba.
 
Back
Top Bottom