Gazeti la Majira litutake radhi Wakurya

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,898
11,745
Katika toleo la jana gazeti la majira limeandika ukurasa wa juu "Wakurya waiba gari wakamatiwa Simiyu" kitendo hiki ni cha kiudhalilisha chenye lengo la kutugawa kikabila.

Habari hiyo imelenga kuonyesha kuwa Wakurya wote tumeiba gari katika nchi yenye makabila mengi sio vizuri kutumia watu wachache kusimama kwa ajili ya kabila lote kwani ingeweka wezi baadala ya wakurya ingepunza nini?

Tunaomba mhariri wa gazeti hilo atuombe radhi Wakurya kabla hatua nyingine hazijachukuliwa kupinga udhalilishaji huo.
 
Umepeleka malalamiko yako kwa mhariri kabla ya kuja hapa?? Nadhan mtafute kwanza mhariri akieleze kwanini kafanya hizo japo naungana na wewe kafanya kosa la ujumuisho
 
Huo ni ukiukwaji wa uandishi wa Habari. Nami nilishangaa sana kuona title hiyo. Kesho wanaweza kuandika wakristo au waislam waiba gari.
Ukute mwandishi wa habari hiyo ni msomi wa elimu fasaha ya uhandishi na ukimlinganisha na saed kubenea ambaye ametoa maelezo ya elimu yake ambapo hana elimu sana ya uhandishi lakini ndiye anayeongoza kwa habari za investigation na kupendwa sana!.
 
Umepeleka malalamiko yako kwa mhariri kabla ya kuja hapa?? Nadhan mtafute kwanza mhariri akieleze kwanini kafanya hizo japo naungana na wewe kafanya kosa la ujumuisho

Nina uhakika mtandao huu ni mkubwa sana hivyo malalamiko haya yatamfikia.
 
Na huyo mwandishi atakuwa mhaya.

mkuu nakubaliana na wewe 100% kuwa huyo mwandishi na pengine hata mhariri watakuwa ni watani zetu WAHAYA au WAHA au WANYIRAMBA na WANYATURU au WARANGI kwani hao WAMILIKI wa hiyo media Familia ya Mzee Mbuguni kuanzia huyo Kaka yao Mkubwa aliyepo hapo Gerezani Ofisini, mdogo wao Nicky na Dada yao wanaujua kabisa mziki wa WAKURYA na nakumbuka Kaka zangu WAMEWATESA sana kipindi cha miaka 90 wakiwa pale mtaa wa Chole Road kwa nyuma japo sometimes walikuwa WAKITUSHINDA kwa kutufungulia Mbwa wao ambao SIFA yao kubwa ilikuwa ni kufunga mtaa. Poti wangu ( Mwana Mkoa wa Mara mwenzangu ) usijali kwa hiyo HEADING japo kiukweli na sisi wana Mkoa wa MARA kwa kiasi fulani TUMEZIDI " usela mavi " hivyo si vibaya tukajirekebisha na hakuna asiyejua kuwa matukio haya ya UJAMBAZI au MAUAJI yapo sana kwetu japo kidogo sasa yanapungua. tujirekebishe Wana Mara!
 
***** hao jamaa kuanzia leo hilo gazeti linageuka toilette paper na kuoshea vioo nyumbani kwangu. Nyamafu sana hao waandishi, eti utani.
 
Katika toleo la jana gazeti la majira limeandika ukurasa wa juu "Wakurya waiba gari wakamatiwa Simiyu" kitendo hiki ni cha kiudhalilisha chenye lengo la kutugawa kikabila.

Habari hiyo imelenga kuonyesha kuwa Wakurya wote tumeiba gari katika nchi yenye makabila mengi sio vizuri kutumia watu wachache kusimama kwa ajili ya kabila lote kwani ingeweka wezi baadala ya wakurya ingepunza nini?

Tunaomba mhariri wa gazeti hilo atuombe radhi Wakurya kabla hatua nyingine hazijachukuliwa kupinga udhalilishaji huo.
hivi gazeti hilo bado lipo? halijafa tu? waandishi wa gazeti la majira ni NJAA KALI...wako tayari kuandika upuuzi wowote ili kuvutia wasomaji. hili gazeti ni moja ya VIPEPERUSHI ambavyo vinatakiwa kufungiwa na Nape Nnauye kama kweli ana nia ya kujenga taaluma ya habari hapa nchini.
 
Umepeleka malalamiko yako kwa mhariri kabla ya kuja hapa?? Nadhan mtafute kwanza mhariri akieleze kwanini kafanya hizo japo naungana na wewe kafanya kosa la ujumuisho
amelileta hapa kwa kuwa nina imani kwamba wahariri wa KIPEPERUSHI hicho wako humu na wanaweza kujitetea laivu hapa hapa tukamaliza kesi.
 
Back
Top Bottom