Prof. Kighoma Ali Malima na gazeti la Uhuru

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,857
30,208
GAZETI LA UHURU LILIPOSEMA KUWA PROF. MALIMA ATAJITOA CCM MSIKITINI TABORA 1995

Ijumaa moja tarehe 15 Julai mwaka wa 1995 gazeti la Uhuru, lilibeba kichwa cha habari katika wino mweusi uliokoza likisema kuwa siku hiyo Prof. Kighoma Ali Malima atatangaza kujitoa kwake CCM kutoka Msikiti Mkuu wa Ijumaa Tabora baada a Sala ya Ijumaa.

Habari hii ilileta mzizimo wa aina yake nchi nzima Malima akawa kapakwa rangi kuwa ni mtu hatari anetaka kusababisha mgogoro mkubwa wa kidini nchini.

Mjini Tabora Ijumaa ile mji ulikuwa na hali isiyokuwa ya kawaida kutokana na taarifa ya gazeti la Uhuru.

Habari zilikuwa zinaenea kama moto wa makumbi kuwa Prof. Malima yuko Tabora na atawahutubia Waislam katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa.

Hata jua halijapanda sawasawa msikiti ukawa umejaa hadi nje barabara zimefungwa Waislam wamejazana kuuzunguka msikiti na misala yao na mikeka waswali Ijumaa kwenye jua kali kisha wamsubiri Malima kupanda katika membar kuwahutubia kuwaeleza kuwa anajitoa CCM.

Watu wa usalama walikuwa wamejichanganya na Waislam ndani na nje ya msikiti kwani jana yake Regional Police Commander (RPC) alifika ofisi za BAKWATA na kufanya kikao na uongozi akawafahamisha kuwa taarifa zao zinaonyesha kuwa Prof. Malima atazungumza na Waislam ndani ya Msikiti wa Ijumaa kwa hiyo BAKWATA wasimruhusu kufanya hilo kwani huko ni kuchanganya dini na siasa.

Muda mfupi kabla ya khutba Sheikh Mavumbi kutoka BAKWATA akaletwa msikitini pale na gari la polisi akisindikizwa na RPC.

Sheikh Mavumbi moja kwa moja akaenda kibla akachukua kipaza sauti akawaonya Waislam hatari ya kuchanganganya dini na siasa.

Msikiti ulikuwa umetulia kimya kabisa Waislam wanamsikiliza sheikh wa Mavumbi kutoka BAKWATA akiwanasihi.

Sheikh Mavumbi akasema anazo taarifa kuwa Prof. Malima atazungumza msikitini hapo na yeye amekuja kuzuia jambo hilo.

Allahu Akbar.
Vumbi zito likatimka.

Alipotaja tu jina la Prof. Malima msikiti ulilipuka Waislam wakimuuliza hizo taarifa yeye kapewa na nani?

Kelele zikajaa msikitini.

Waislam kila mmoja anazungumza anamuuliza Sheikh Mavumbi nani aliyempa taarifa hizo?

Sheikh Mavumbi akawa kachanganyikiwa hakutegemea kabisa kuwa Waislam watamghadhibikia kiasi kile.

Imam Mkuu wa msikiti ule Sheikh Issa Mzee, miaka ile kijana mdogo wa kiasi cha miaka 30 katikati akasimama kuwatuliza Waislam lakini hakuna aliyemsikiliza.

Vurugu ikaendelea msikitini.

Waislam waliokuwa nje ya msikiti kusikia kelele zile
wakanyanyuka wakawa wanaminyana milangoni wakitaka kuingia ndani msikitini.

Dalili zote zikawa wazi kuwa sasa heshima na hadhi ya msikiti ilikuwa taratibu inatoweka msikiti unageuka kuwa uwanja wa vurugu, fujo na mapambano baina ya Waislam na sheikh mmoja kutoka BAKWATA.

Hapo ndipo Mzee Bilal Rehani Waikela aliposimama akachukua kipaza sauti na kwa sauti yake ya upole ikasikia kutoka ''speaker'' za msikiti ndani na nje akisema, ‘’Waislam msalieni Mtume,’’ akiyarudia maneno haya.

Hakuna mtu Tabora amae hakuwa anaijua sauti ile achilia mbali kumjua mwenye sauti ile.

Kwa pamoja palisikika kibwagizo cha Waislam wakimwitika wakimsalia Mtume ndani na nje ya msikiti.

Utulivu ukarejea msikitini Waislam wakakaa chini wametulia.

Mzee Waikela kwa utulivu akamuuliza Sheikh Mavumbi wapi kapata taarifa kuwa Prof. Malima atakuja kuzungumza hapo msikitini.

Sheikh Mavumbi hakuwa na jibu.

Mzee Waikela akamwambia Sheikh Mavumbi aangalie kama anamuona Prof. Malima mle ndani msikitini.

Mzee Waikela akawauliza Waislam, ‘’Ndugu zangu kuna yeyote kamuona Prof. Malima hapa msikitini?

Prof. Malima si kuwa hakuwepo mle msikitini bali hata hapo Tabora mjini pia hakuwapo.

Mhariri wa Uhuru siku ya Jumamosi wala hakuwataka radhi wasomaji wake kuwa katika toleo lililopita alikuwa ameandika habari ambazo hazikuwa za kweli kuwa Prof. Malima atajitoa CCM ndani ya Msikiti wa Ijumaa Tabora.

Wala Uhuru halikufungiwa likaendelea na vita vyake dhidi ya Prof. Malima hadi umauti ulipomchukua mwezi kama huu wa August 1995.

Historia huwa na kawaida ya kujirudia.

Screenshot_20210813-064647_Gallery.jpg

Screenshot_20210813-065020_Facebook.jpg

Screenshot_20210813-065254_Facebook.jpg

Screenshot_20210813-072630_WhatsApp.jpg

Mtangazaji wa Radio Tehran, Iran Abdufatah Mussa akinifanyia mahojiano kuhusu Prof. Malima mwaka wa 2001.
 
GAZETI LA UHURU LILIPOSEMA KUWA PROF. MALIMA ATAJITOA CCM MSIKITINI TABORA 1995

Ijumaa moja tarehe 15 Julai mwaka wa 1995 gazeti la Uhuru, lilibeba kichwa cha habari katika wino mweusi uliokoza likisema kuwa siku hiyo Prof. Kighoma Ali Malima atatangaza kujitoa kwake CCM kutoka Msikiti Mkuu wa Ijumaa Tabora baada a Sala ya Ijumaa
We babu lea wajukuu acha kutuletea mavitu ya kijinga yasio na msaada ktk vizazi vijavyo
 
Telegram,
Sijapatapo kuandika ujinga maishani mwangu.

Kalamu yangu iko katika maktaba nyingi duniani na kazi zangu zimechapwa na wachapaji wakubwa kama Oxford University Press.

Ikiwa wewe hupendezewi nami acha kusoma.

Nina wasomaji wengi hapa JF.
Si ustaarabu kuja hapa kunitukana.
 
Msamehe bure Mzee Mohamed vijana wamejaa laana siku hizi
 
Kighoma Malima aliwapigania waislamu, lakin waislamu wakamtumpa. Kuanzia ishu ya namna ya kusahihisha mitihani ya taifa na ufaulu wa watoto wa kiislamu
 
Last...
Kighoma Malima hakupatwa kutupwa na Waislam hadi anaingia kaburini.

Ikiwa wewe una taarifa kuwa Waislam walimtupa itakuwa vizuri ukaeleza hili.
 
GAZETI LA UHURU LILIPOSEMA KUWA PROF. MALIMA ATAJITOA CCM MSIKITINI TABORA 1995

Ijumaa moja tarehe 15 Julai mwaka wa 1995 gazeti la Uhuru, lilibeba kichwa cha habari katika wino mweusi uliokoza likisema kuwa siku hiyo Prof. Kighoma Ali Malima atatangaza kujitoa kwake CCM kutoka Msikiti Mkuu wa Ijumaa Tabora baada a Sala ya Ijumaa.

Habari hii ilileta mzizimo wa aina yake nchi nzima Malima akawa kapakwa rangi kuwa ni mtu hatari anetaka kusababisha mgogoro mkubwa wa kidini nchini.

Mjini Tabora Ijumaa ile mji ulikuwa na hali isiyokuwa ya kawaida kutokana na taarifa ya gazeti la Uhuru.

Habari zilikuwa zinaenea kama moto wa makumbi kuwa Prof. Malima yuko Tabora na atawahutubia Waislam katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa.

Hata jua halijapanda sawasawa msikiti ukawa umejaa hadi nje barabara zimefungwa Waislam wamejazana kuuzunguka msikiti na misala yao na mikeka waswali Ijumaa kwenye jua kali kisha wamsubiri Malima kupanda katika membar kuwahutubia kuwaeleza kuwa anajitoa CCM.

Watu wa usalama walikuwa wamejichanganya na Waislam ndani na nje ya msikiti kwani jana yake Regional Police Commander (RPC) alifika ofisi za BAKWATA na kufanya kikao na uongozi akawafahamisha kuwa taarifa zao zinaonyesha kuwa Prof. Malima atazungumza na Waislam ndani ya Msikiti wa Ijumaa kwa hiyo BAKWATA wasimruhusu kufanya hilo kwani huko ni kuchanganya dini na siasa.

Muda mfupi kabla ya khutba Sheikh Mavumbi kutoka BAKWATA akaletwa msikitini pale na gari la polisi akisindikizwa na RPC.

Sheikh Mavumbi moja kwa moja akaenda kibla akachukua kipaza sauti akawaonya Waislam hatari ya kuchanganganya dini na siasa.

Msikiti ulikuwa umetulia kimya kabisa Waislam wanamsikiliza sheikh wa Mavumbi kutoka BAKWATA akiwanasihi.

Sheikh Mavumbi akasema anazo taarifa kuwa Prof. Malima atazungumza msikitini hapo na yeye amekuja kuzuia jambo hilo.

Allahu Akbar.
Vumbi zito likatimka.

Alipotaja tu jina la Prof. Malima msikiti ulilipuka Waislam wakimuuliza hizo taarifa yeye kapewa na nani?

Kelele zikajaa msikitini.

Waislam kila mmoja anazungumza anamuuliza Sheikh Mavumbi nani aliyempa taarifa hizo?

Sheikh Mavumbi akawa kachanganyikiwa hakutegemea kabisa kuwa Waislam watamghadhibikia kiasi kile.

Imam Mkuu wa msikiti ule Sheikh Issa Mzee, miaka ile kijana mdogo wa kiasi cha miaka 30 katikati akasimama kuwatuliza Waislam lakini hakuna aliyemsikiliza.

Vurugu ikaendelea msikitini.

Waislam waliokuwa nje ya msikiti kusikia kelele zile
wakanyanyuka wakawa wanaminyana milangoni wakitaka kuingia ndani msikitini.

Dalili zote zikawa wazi kuwa sasa heshima na hadhi ya msikiti ilikuwa taratibu inatoweka msikiti unageuka kuwa uwanja wa vurugu, fujo na mapambano baina ya Waislam na sheikh mmoja kutoka BAKWATA.

Hapo ndipo Mzee Bilal Rehani Waikela aliposimama akachukua kipaza sauti na kwa sauti yake ya upole ikasikia kutoka ''speaker'' za msikiti ndani na nje akisema, ‘’Waislam msalieni Mtume,’’ akiyarudia maneno haya.

Hakuna mtu Tabora amae hakuwa anaijua sauti ile achilia mbali kumjua mwenye sauti ile.

Kwa pamoja palisikika kibwagizo cha Waislam wakimwitika wakimsalia Mtume ndani na nje ya msikiti.

Utulivu ukarejea msikitini Waislam wakakaa chini wametulia.

Mzee Waikela kwa utulivu akamuuliza Sheikh Mavumbi wapi kapata taarifa kuwa Prof. Malima atakuja kuzungumza hapo msikitini.

Sheikh Mavumbi hakuwa na jibu.

Mzee Waikela akamwambia Sheikh Mavumbi aangalie kama anamuona Prof. Malima mle ndani msikitini.

Mzee Waikela akawauliza Waislam, ‘’Ndugu zangu kuna yeyote kamuona Prof. Malima hapa msikitini?

Prof. Malima si kuwa hakuwepo mle msikitini bali hata hapo Tabora mjini pia hakuwapo.

Mhariri wa Uhuru siku ya Jumamosi wala hakuwataka radhi wasomaji wake kuwa katika toleo lililopita alikuwa ameandika habari ambazo hazikuwa za kweli kuwa Prof. Malima atajitoa CCM ndani ya Msikiti wa Ijumaa Tabora.

Wala Uhuru halikufungiwa likaendelea na vita vyake dhidi ya Prof. Malima hadi umauti ulipomchukua mwezi kama huu wa August 1995.

Historia huwa na kawaida ya kujirudia.

View attachment 1890269

View attachment 1890270

View attachment 1890271

View attachment 1890294
Mtangazaji wa Radio Tehran, Iran Abdufatah Mussa akinifanyia mahojiano kuhusu Prof. Malima mwaka wa 2001.
Nakupenda sana Mzee Wangu Mohamed Said , Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu yaliyojaa heri na fanaka
 
Last Emperor,
Tulimsaidia nini unauliza.

Mjadala unahitaji lugha iliyotulia ili ustawi.

Namna ulivyoliuliza swali hili la kwanza haipendezi unahitaji kuliuliza swali hilo bila shutuma.

Hii itawasaidia wachangiaji Waislamu unaowalaumu kujiunga na mjadala kuchangia kwa utulivu na kwa ustaarabu.

Swali la pili unataka kujua Waislam wangapi walimfuata NRA.

Ili kupata jibu la swali hili ni lazima ifahamike kwanza idadi ya wanachama waliochukua kadi za NRA baada ya mkutano wa Tabora.

Hapa ni lazima upate register ya wanachama kutoka matawi yote.

Swali hili haliwezi kujibika bila kufanya utafiti huo.

Pili patakuwa na Waislam waliokuwa wanamuunga mkono lakini si wanachama wenye kadi za NRA.

Njia gani itumike ili kujua idadi ya hawa?

Zipo njia za kupita kupata majibu.

Nimekupa hayo ili uliulize swali lako upya kwa kuzingatia hayo niliyokueleza hapo juu.
 
asante sana mzee wangu mzee Mohamed Said machapisho yako yanatupa wasaa wa kutafakari mengi yaliyopita ambayo hatukupata wasaa wa kujifunza .......shukran sana
 
Telegram,
Sijapatapo kuandika ujinga maishani mwangu.

Kalamu yangu iko katika maktaba nyingi duniani na kazi zangu zimechapwa na wachapaji wakubwa kama Oxford University Press.

Ikiwa wewe hupendezewi nami acha kusoma.

Nina wasomaji wengi hapa JF.
Si ustaarabu kuja hapa kunitukana.
Binafsi ni mfatiliaji sana na maandiko yako, MUNGU akupe maisha marefu.
 
Telegram,
Sijapatapo kuandika ujinga maishani mwangu.

Kalamu yangu iko katika maktaba nyingi duniani na kazi zangu zimechapwa na wachapaji wakubwa kama Oxford University Press.

Ikiwa wewe hupendezewi nami acha kusoma.

Nina wasomaji wengi hapa JF.
Si ustaarabu kuja hapa kunitukana.
Sahihii kabisa. Hana sababu yoyotee ya kukutusi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom