Gari ya wanafunzi/primary imewekwa Tinted

Mowwo

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2015
Posts
1,725
Reaction score
2,540
Wakuu
Katika harakati zangu wiki iliopita saa 12 asubuhi nilikutana na hii gari ya watoto wa nursery imepigwa tinted vioo vyote(hadi cha dereva) ispokua kioo cha mbele.
Kwa kushamiri kwa matukio ya unyanyasaji wa kingono na ukatili dhidi ya watoto, hili linawezekanaje? Unamlaumu nani
1.
Kwanini mamlaka husika hawajawaamuru kuzitoa?
2. Mzazi unampakia mwanao kwenye hii gari, unawaaminije watakua hawana mambo meusi?
20250729_065143.jpg
20250729_065141.jpg

Unaweza kumruhusu mwanao atumie usafiri huu wa shule kupanda saa 12 asubuh? Dkt. Gwajima D una maoni gani?
 
Wazazi wengi sasa hivi ni huwa hawajali kabisa watoto wao. Mzazi anaamka anaenda kituoni na mtoto wake "school bus" inafika imejaa watoto wamepakatana watatu halafu na yeye anampakiza mwanae humohumo. Taratiibu anarudi nyumba roho kwatu na pesa kila mwezi analipa. Sasa jiulize wewe mleta uzi umeona hilo gari barabarani na umekuwa "concerned" lakini wazazi wote wa hiyo shule wao wanaona sawa tu na kila siku wanawapakia watoto wao humo. Na utakuta hakuna mmoja amewahi kuulalamikia uongoizi wa shule. Anyway kuna jina nilitaka kuwapa wazazi wote wa hiyo shule lakini ngoja niache maana hilo jina ni kama tusi tu.

Halafu ukienda kwenye mikutano ya shule ukihoji jambo la msingi kama hilo utashangaa kabla ya uongozi wa shule haujaanza kujibu linatoke libaba au limama upande wazazi linaanza kujibu kutetea walimu na makofi linapigiwa na wazazi wengine.

Subiri sasa siku likitokea la kutokea hao hao wazazi viherehere ndio wa kwanza kuulaumu uongozi wa shule wakati kila siku kwenye mikutano ya shule wao ndio walikuwa vihere vihere wa kuutetea uongozi.
 
Wenye dhamana wamelala hawajali wanakula kwa urefu wa kamba zao.
Mambo yanaendeshwa kiholela holela sana.
Mambo haya yanayapa nguvu madai ya Humphrey Pole ya kubadili viongozi wa juu.
Wasaidizi wao huko chini hawajali na hawaogopi, hawatekelezi majukumu yao.
 
Wazazi wengi sasa hivi ni huwa hawajali kabisa watoto wao. Mzazi anaamka anaenda kituoni na mtoto wake "school bus" inafika imejaa watoto wamepakatana watatu halafu na yeye anampakiza mwanae humohumo. Taratiibu anarudi nyumba roho kwatu na pesa kila mwezi analipa. Sasa jiulize wewe mleta uzi umeona hilo gari barabarani na umekuwa "concerned" lakini wazazi wote wa hiyo shule wao wanaona sawa tu na kila siku wanawapakia watoto wao humo. Na utakuta hakuna mmoja amewahi kuulalamikia uongoizi wa shule. Anyway kuna jina nilitaka kuwapa wazazi wote wa hiyo shule lakini ngoja niache maana hilo jina ni kama tusi tu.

Halafu ukienda kwenye mikutano ya shule ukihoji jambo la msingi kama hilo utashangaa kabla ya uongozi wa shule haujaanza kujibu linatoke libaba au limama upande wazazi linaanza kujibu kutetea walimu na makofi linapigiwa na wazazi wengine.

Subiri sasa siku likitokea la kutokea hao hao wazazi viherehere ndio wa kwanza kuulaumu uongozi wa shule wakati kila siku kwenye mikutano ya shule wao ndio walikuwa vihere vihere wa kuutetea uongozi.
Umeongea na kuwasilisha vizuri sana nilichokusudia.
Sielewi tu wazazi wanachuliaje hili jambo. Hakika likitokea jambo utaskia kelele za lawama nyingi sana
 
Wakuu
Katika harakati zangu wiki iliopita saa 12 asubuhi nilikutana na hii gari ya watoto wa nursery imepigwa tinted vioo vyote(hadi cha dereva) ispokua kioo cha mbele.
Kwa kushamiri kwa matukio ya unyanyasaji wa kingono na ukatili dhidi ya watoto, hili linawezekanaje? Unamlaumu nani
1.
Kwanini mamlaka husika hawajawaamuru kuzitoa?
2. Mzazi unampakia mwanao kwenye hii gari, unawaaminije watakua hawana mambo meusi?View attachment 3435529View attachment 3435531

Unaweza kumruhusu mwanao atumie usafiri huu wa shule kupanda saa 12 asubuh? Dkt. Gwajima D una maoni gani?
Duh hii hatari, wazazi tufuatilie watoto wetu
 
Oil kivip, sijaelewa

MKuu wewe Hadi umeona ila mamlaka wao kumbe si viziwi tu kama wavyojinasibu bali na kuona hawaoni?

La kuvunda lini likawa na ubani? Unalosema hapa ni Moja tu. Wapi tuko salama?Au wewe huoni hivyo? Tukimwaga oil tutaanza upya.

Tunastahili mwanzo mpya.
 
Back
Top Bottom