Gari hili gari gani?

Nimefuatilia kwa mafundi.. mmoja alikuwa ni muwazi kabisa kasema nenda tu kwa manufacturer ukileleta kwangu nitalitengeneza lakini nitakulia hela tu kwani hata mimi itabidi niende huko huko kwa mtengenezaji! Mtengenezaji anataka nimuachie ili alipime kila kitu.. ndio anipe makisio ya gharama.. sasa nikimuachia gari ndo itakuwaje kuhusu safari zangu, nitatufe la kuazima?
 
Gari gani limekuwa kama mganga wa kienyeji!? Kila siku.. lete kuku, lete mayai, lete mbuzi pacha, mara lete vifaranga vya kijani.. kwenda halendi limebakia kuunguruma tu!! Mwisho watu wanaanza kudandia madaladala hivi hivi!!

....ha ha ha... ebana weeee!

Isije ikawa dereva bado mwanafunzi? kama si mwanafunzi iweje ufundi ukushinde?
 
Belinda.. unajua wakati mwingine hadi uwe na gari kwa muda fulani ndio unajua uzuri wake na matatizo yake. Kuna watu wengine hawaoni ugumu kutumia kiasi chochote na kwa namna yoyote kulihudumia gari lao ili kuhakikisha linaendelea ndio maana nimewahi kupita kijiji fulani nikakutana na jamaa wanaendesha "kombi" ya 1960 na linadunda tu! Cha kushangaza waliokuja na magari yao haya ya kisasa mengine hata mwaka hayakumaliza!

Hilo nalo neno mkuu MMK!..Basi kabla ya kununua gari inabidi kuuliza kwa wazoefu kuwa gari gani niimara ili kuwa nalo!..Mana mengine hayadumu, spea za shida, yanakunywa sana mafuta nk..
 
Back
Top Bottom