Gari hili gari gani?

Wale walioniuzia hilo gari kwa mara ya kwanza walinirembeshea kweli.. yaani, ati ni 'automatic transmission", kwamba "liko fully loaded" na wakanionesha jinsi lilivyo safi kwa nje na ndani! Halafu kunogeshea bei yake! ilikuwa sawa na dezo.. mzee wa watu nikasema nataka nikalijaribu kidogo, jamaa wakanipa nikapiga kona mbili tatu, gari ngurumo utadhani linabembeleza!

Kurudisha moyo umesuuzika, nikasaini mapepa yote kama nina kichaa; nikaondoka mwenyewe na gari yangu na mluzi juu! siku ya kwanza gari linanipa raha, siku ya pili.. mara mwezi likaanza kukongoloka, mara honi hailii, mara breki zinafunga katikati ya safari, mara steering haigeuka liko ka' gogo.. mwisho naona vurugu tu. Nikarudi haraka kwa jamaa

wananionesha pepa moja niliyosaini inasema "SOLD AS IS"!!!!

NIkalowa utadhani nimemwagiga maji mafinga!
 
Gari gani limekuwa kama mganga wa kienyeji!? Kila siku.. lete kuku, lete mayai, lete mbuzi pacha, mara lete vifaranga vya kijani.. kwenda halendi limebakia kuunguruma tu!! Mwisho watu wanaanza kudandia madaladala hivi hivi!!

Mmh! Siyo uendeshe gari kwa vile ni gari tubali angalia kuwa gari la aina gani?!...ha ha
 
Mmh! Siyo uendeshe gari kwa vile ni gari tubali angalia kuwa gari la aina gani?!...ha ha

Belinda.. unajua wakati mwingine hadi uwe na gari kwa muda fulani ndio unajua uzuri wake na matatizo yake. Kuna watu wengine hawaoni ugumu kutumia kiasi chochote na kwa namna yoyote kulihudumia gari lao ili kuhakikisha linaendelea ndio maana nimewahi kupita kijiji fulani nikakutana na jamaa wanaendesha "kombi" ya 1960 na linadunda tu! Cha kushangaza waliokuja na magari yao haya ya kisasa mengine hata mwaka hayakumaliza!
 
mwanangu ee mimi nnayo peugeot 3or6 moja iyo wala
sometimes aiitaji ata mafuta bora batery iwe na charge
tu mambo mswano''''''shauri yako we ngangania GX100
uone inavyokula mafuta
 
Mzee mwanakijiji nunua zako baiskeli itakutoa, haina gharama ni tairi tu. tena kwa shamba ni bomba sana, unafunga jembe lako nyuma. achana na mambo ya mjini yatakutia wazimu bureeeee!
 
mkuu hiuzi nyimbo hazisaidii inatakiwa tutafute walau hendeli ya kuiamsha hii gari.FOR REAL
 
umesehaau kuwa gari lenyewe linapenda starehe, lina matumizi makubwa kweli, na linamnyonya mnunuaji/mwenye nalo. mara lete kanga, kofia na T-shirt za njano ati uziweke juu kwenye carrier yake......mwenye nalo anaumia sana lakini pamoja na kwamba anayaona magari mengine yenye ufanisi zaidi, na yanayotumia mafuta na garama kidogo, yeye bado anang'ang'ania na hili gari lake, ati ni la kizamani kwahiyo ni kuukuu pamoja na kwamba limejaa kutu. mmhhhh!
 
Ni GARI lililokosa injini ndio maana haliendi. Wamejaribu kuunganisha injini za pikipiki, baiskeli naona sasa wanajaribu injini ya bajaji lakini makenika amesema wameagiza vipuri toka ng'ambo vikifika vitafungwa na gari litakuwa barabarani kwa full speed. Gari hilo litapita linawachukua wale wote waliokuwa wanasubiri vituoni miaka nenda miaka rudi. Kondakta wake hawezi kuwa mchina wala mjapani wala mhindi wala mcanada wala mmarekani atakuwa ni mtanzania halisi.
 
Gari gani limekuwa kama mganga wa kienyeji!? Kila siku.. lete kuku, lete mayai, lete mbuzi pacha, mara lete vifaranga vya kijani.. kwenda halendi limebakia kuunguruma tu!! Mwisho watu wanaanza kudandia madaladala hivi hivi!!
du naona hili gari ni sawa na mke asiye na uaminifu nyumbani tamaa zimemjaa
 
mimi sio kama nakulaumu mwanakijiji, wapo wengi waliozania kuwa hilo ni gari zuri, ni kweli tulikuwa tunajua ni gari la zamani , zamani tena sana, kwani lilianza na jina lingine na baada ya kuunganisha spear za magari mawili ndio wakalibadilisha na jina pia

lakini kilichotuvutia ni huyu dereva mpya maana alituambia hilo gari sasa ni jipya kabisa , kwani LINA NGUVU MPYA, NA LINA KASI MPYA YA AJABU, na kwa sisi tulipomwangalia kuwa derva ni kijana basi tuliona anaweza kurifurusha vizuri, kumbe gari bado ni bovu
 
manunuzi ya Gari hiyo yanatupa somo moja kuwa lazima tuwe waangalifu maana nasikia wauzaji walewale wanataka kutuuzia model ile ile ya gari, wakitutaka radhi kuwa gari la awali iliingia maji ya bahari wakati wakiisafirisha kuja hapa nyumbani, sasa wanakuja wakiwa na kikosi kipya cha madalali huku wakituaminisha kosa si kosa ila kosa kurudia kosa, tuwape nafasi ili watuletee gari nyingine kama ile ya awali ambayo imeboreka zaidi.....
 
Shida ni kwamba - hata ukitaka kununua gari aina ingine - gari hili linajinadi na kuzuia magari aina nyingine yasinunuliwe - sidhani kama tutafika kwani gari halina spidi tena - linakula tu mafuta, matengenezo kibao - sasa - tuamue tusiwe na gari aina yoyote kabisaaaaaaa - tutembee kwa miguu yetu aliyotupa muumba wetu
 
gari hii linasumbua na kuumiza kichwa kwani mwasisi wake ameshakufa yy ndo alijua ugonjwa ulipo na tiba yake walobaki wababaishaji ugonjwa awajui ulipo na tiba awajui gari wanalitesa wanaliburuza limekuwa screpper ujanja wa kulikarabati upya awana awajui password ya kifimbo
 
Inabidi uwasiliane na manufacturer wa gari akupe mbinu Mbadala

manufacturer alishakufa aliyepewa manual anaelekeza majibu awataki kwani inawabana gari alitaki liendeshwe na mafisadi gari lina maadili ya azimio la arusha wameliharibu gari wamelibebesha mizigo mizito ambayo si saizi yake ufisadi,ubinafsi,
 
Mwanakijiji upo wapi mbona kimya au na wewe umepewa nafasi ya ukondakta kwenye hilo gari huku ukiahidiwa kuwa utakuwa karibu na dereva ili ujifunze gear?,

njoo utupe kinachoendelea kwenye hilo gari
 
Gari laweza kurudi barabarani likipata service yanguvu lkn kama halifai kabisa basi huna budi kununu agari jipya maana kudandia madaladala kuna kadhia yake pia
 
Back
Top Bottom