Vituko vya matajiri Moshi na Arusha miaka hiyo

nzalendo

JF-Expert Member
May 26, 2009
10,684
9,862
Namkumbuka Mzee Maeda...alikuwa na majumba na mabasi ya Kilimanjaro Bus Service (1967) Ltd.

Yeye na mkewe walikuwa ni wachapa kazi balaa...mzee yuko stand anabeba mizigo kama kuli na kuipandisha juu ya carrier.

Kuna siku basi imepakia abiria dereva kaingia kwenye basi kalewa,mama akamshusha dereva na kuitoa gari stand kwa mbwembwe Leyland CD inavyopiga mayowe, stand nzima ilizizima watu wanashangilia mama akapiga gari mpaka Moshi.

Kuna siku mzee amekwenda kuwinda...zamani kati ya Arusha na Namanga walikuwa wanapatikana wanyama....huku na kule mzee Maeda kakosa mnyama...kama kawaida wamasai na mifugo yao hawakosekani maeneo hayo....Mzee Maeda akaamua kutandika risasi kambuzi kamoja,huyoo mpaka Arusha...huku na kule kesho yake wamasai wakaandamana mpaka Arusha wamebeba sime, marungu,mikuki n.k....wanauliza..."

Wapi Maiida"... kwa lafudhi ya kimasai...watu wakamtonya Maeda akakimbilia polisi...wamasai nao hawakuchelewa wakaenda kuzingira kituo cha polisi....anyway kwa kifupi baadae wamasai wakajikuta ghafla wamekuwa marafiki na mzee "Maiida" mara kwa mara wakawa wanakutana wakipata kinywaji pamoja na kuchoma nyama.

Tajiri mwingine alikuwa ni mjenzi wa majumba Philips Construction huyu kwa kifupi ndiye mmiliki wa Arusha by night...huyu ni Tajiri pekee aliyekuwa na uwezo wa kutukanana na vibarua na mafundi na akashinda..alijaaliwa kwa maneno .........siku hiyo mafundi aidha ni kwa makusudi au bakhti mbaya walipindisha ukuta kwenye majengo yaliyokuwa yakijengwa opposite na Arusha school....akiwa kavaa kaunda ya rangi ya maziwa...akatoa amri ukuta uvunjwe....

Kisha akakamata mwiko na kono bao...mzee akaanza kujenga ukuta...watu walishangilia vifijo na miluzi....anatoa amri lete udongo..ofcouse anachanganya na matusi...kazi ikaendelea...Mara kaagiza bia...anakunywa huku anapiga kazi...wanaovuta ganja akawaagizia fegi ni za kumwaga kazi ilipigwa mpaka usiku wa manane...hakujali suti yake kuchafuka.

Huyu mzee kila alhamisi alikuwa na utaratibu wa kwenda kijijini kwao kwa mapumziko.....kwa hiyo anaendesha Mercedes yake mpaka Moshi kijiji cha kikarara akifika huko anakutana na wapambe wake wanaanza kumpa gazeti kinachoendelea hapo kijijini.

Basi anatoa amri watu wanywe mbege.....watu ni kupiga maji kwa kwenda mbele....ghafla anabadilisha frequency watu wanaanza kula bia...uzuri alikuwa habagui vibibi...vibabu...vijana woote ni furaha...basi wakilewa wanaanza kuropoka kijana mmoja akomtonya fulani anasema wewe unajifanya Tajiri ( wakati huo kuna kanisa lilikuwa linajengwa hapo kijijini)... lakini fulani huyo anasema wewe unawaibia na kuwapa waumini bei ya ki kontrakta....jumapili ikafika....baada ya ibada....akatoa sauti...wee fulani kuja hapa....hapo watu kibao....zingatia huyo fulani ni mtu mzima mwenye mke na watoto....akamwambia umesema maneno gani.?

Fulani mara ooh aah mzee unajua watu fitna....mzee hakukawia kampa maneno machafu halagu mwishoni kamponda wewe mpaka leo unakaa kwenye nyumba ya baba yako( na no kweli) huna hata choo....unathubutu vipi kutamka maneno hayo???

Siku hiyo yupo na watu kibao anawanywesha pombe pale kiborlony mara mmoja wa marafiki zake ( kinyala)aka mis behave...akamkamata akamuweka kwenye gari mpaka kituo cha polisi....akamwambia polisi andika huyu akija nyumbani kwangu nitamvunja miguu kwa risasi....polisi kabaki ameduwaa....akaambiwa....andika...andikaa...polisi kwa sababu anamfahamu ni mtu wa vimbwanga akaandika...Kisha akaondoka nae mpaka anapokaa akamkabidhi kwa familia yake...

Anyway kwa uchache...
Siku nyingine...kadogoo....babu Sambeke....kina Olotu wezi wa magari...Hawa walifanya vituko Mbeya mtu na kaka yake wanarushiana risasi kisa wamedhulumiana.

Nitaendelea......
 
Inafurahisha sana. Tajiri lazima uwe ngangari. Ukilegea watu watakuzingua sana. Kuna mmoja alisema mzee wake alikuwa anafanya biashara ya mazao. Siku moja vibarua wakagoma kushusha mzigo wanataka waongezewe pesa. Yule don akavua shati na kuanza kupakua gunia mwenyewe. Anaenda tu trip, nenda rudi. Vibarua wakaona hapa tutakosa hata hela ya msosi, ikabidi waingie kazini.
 
Namkumbuka Mzee Maeda...alikuwa na majumba na mabasi ya Kilimanjaro Bus Service (1967) Ltd.

Yeye na mkewe walikuwa ni wachapa kazi balaa...mzee yuko stand anabeba mizigo kama kuli na kuipandisha juu ya carrier.

Kuna siku basi imepakia abiria dereva kaingia kwenye basi kalewa,mama akamshusha dereva na kuitoa gari stand kwa mbwembwe Leyland CD inavyopiga mayowe, stand nzima ilizizima watu wanashangilia mama akapiga gari mpaka Moshi.

Kuna siku mzee amekwenda kuwinda...zamani kati ya Arusha na Namanga walikuwa wanapatikana wanyama....huku na kule mzee Maeda kakosa mnyama...kama kawaida wamasai na mifugo yao hawakosekani maeneo hayo....Mzee Maeda akaamua kutandika risasi kambuzi kamoja,huyoo mpaka Arusha...huku na kule kesho yake wamasai wakaandamana mpaka Arusha wamebeba sime, marungu,mikuki n.k....wanauliza..."

Wapi Maiida"... kwa lafudhi ya kimasai...watu wakamtonya Maeda akakimbilia polisi...wamasai nao hawakuchelewa wakaenda kuzingira kituo cha polisi....anyway kwa kifupi baadae wamasai wakajikuta ghafla wamekuwa marafiki na mzee "Maiida" mara kwa mara wakawa wanakutana wakipata kinywaji pamoja na kuchoma nyama.

Tajiri mwingine alikuwa ni mjenzi wa majumba Philips Construction huyu kwa kifupi ndiye mmiliki wa Arusha by night...huyu ni Tajiri pekee aliyekuwa na uwezo wa kutukanana na vibarua na mafundi na akashinda..alijaaliwa kwa maneno .........siku hiyo mafundi aidha ni kwa makusudi au bakhti mbaya walipindisha ukuta kwenye majengo yaliyokuwa yakijengwa opposite na Arusha school....akiwa kavaa kaunda ya rangi ya maziwa...akatoa amri ukuta uvunjwe....

Kisha akakamata mwiko na kono bao...mzee akaanza kujenga ukuta...watu walishangilia vifijo na miluzi....anatoa amri lete udongo..ofcouse anachanganya na matusi...kazi ikaendelea...Mara kaagiza bia...anakunywa huku anapiga kazi...wanaovuta ganja akawaagizia fegi ni za kumwaga kazi ilipigwa mpaka usiku wa manane...hakujali suti yake kuchafuka.

Huyu mzee kila alhamisi alikuwa na utaratibu wa kwenda kijijini kwao kwa mapumziko.....kwa hiyo anaendesha Mercedes yake mpaka Moshi kijiji cha kikarara akifika huko anakutana na wapambe wake wanaanza kumpa gazeti kinachoendelea hapo kijijini.

Basi anatoa amri watu wanywe mbege.....watu ni kupiga maji kwa kwenda mbele....ghafla anabadilisha frequency watu wanaanza kula bia...uzuri alikuwa habagui vibibi...vibabu...vijana woote ni furaha...basi wakilewa wanaanza kuropoka kijana mmoja akomtonya fulani anasema wewe unajifanya Tajiri ( wakati huo kuna kanisa lilikuwa linajengwa hapo kijijini)... lakini fulani huyo anasema wewe unawaibia na kuwapa waumini bei ya ki kontrakta....jumapili ikafika....baada ya ibada....akatoa sauti...wee fulani kuja hapa....hapo watu kibao....zingatia huyo fulani ni mtu mzima mwenye mke na watoto....akamwambia umesema maneno gani.?

Fulani mara ooh aah mzee unajua watu fitna....mzee hakukawia kampa maneno machafu halagu mwishoni kamponda wewe mpaka leo unakaa kwenye nyumba ya baba yako( na no kweli) huna hata choo....unathubutu vipi kutamka maneno hayo???

Siku hiyo yupo na watu kibao anawanywesha pombe pale kiborlony mara mmoja wa marafiki zake ( kinyala)aka mis behave...akamkamata akamuweka kwenye gari mpaka kituo cha polisi....akamwambia polisi andika huyu akija nyumbani kwangu nitamvunja miguu kwa risasi....polisi kabaki ameduwaa....akaambiwa....andika...andikaa...polisi kwa sababu anamfahamu ni mtu wa vimbwanga akaandika...Kisha akaondoka nae mpaka anapokaa akamkabidhi kwa familia yake...

Anyway kwa uchache...
Siku nyingine...kadogoo....babu Sambeke....kina Olotu wezi wa magari...Hawa walifanya vituko Mbeya mtu na kaka yake wanarushiana risasi kisa wamedhulumiana.

Nitaendelea......
Joel maeda mayor wa kwanza mweusi
 
Back
Top Bottom