Gaddafi alikuwa na utajiri wa Sh 140 trilioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gaddafi alikuwa na utajiri wa Sh 140 trilioni

Discussion in 'International Forum' started by mojoki, Oct 23, 2011.

 1. mojoki

  mojoki JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 1,333
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  KIONGOZI wa Libya aliyeuawa juzi na wapiganaji wa Serikali ya Mpito (NTC), anadaiwa kuacha utajiri wa Sh 139 trioni kiasi ambacho ni sawa na bajeti ya Tanzania kwa miaka 12.

  Habari zilizopatikana jana zimeeleza kuwa fedha hizo ni zile zinazofahamika, alizoweka kwenye benki za nchi kadhaa duniani, huenda alikuwa na hazina zaidi mbali na hiyo. Kwa mujibu wa habari hizo, Gaddafi alikuwa anamiliki Pauni 29 bilioni nchini Uingereza (Sh78 trilioni), Dola 32 bilioni nchini Marekani (Sh54 trilioni), Dola 2.4 bilioni nchini Canada( Sh4 trilioni) na Dola 1.7 bilioni nchini Australia (Sh3 trilioni). Kwa fedha ya Tanzania.

  Pauni moja ya Uingereza ni sawa na Sh 2,720, Dola moja ya Marekani Sh 1,704, Dola moja ya Canada, Sh 1,692 na Dola ya Australia ni Sh 1,769. Fedha hiyo kwa ujumla wake ni sawa na bajeti ya Tanzania kwa miaka 12.

  Juni mwaka huu, Bunge lilipitisha jumla ya Sh11 trilioni kwa matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/2012 .Kiasi hicho kikizidishwa mara miaka 12 zitakuwa Sh132 trilioni, hivyo ukichukulia kiwango hicho, inamaana kuwa fedha za Gaddafi zinatosha kuendesha Tanzania kwa miaka 12 na bado zitabaki Sh trilioni saba.
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Very interesting ... alioucha ... Na aliondoka nao ni ...? This life ... is a big Joke!!!!!??
   
 3. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Safi sana Ghadhaf ungetusaidia sana ungelikuwa hai,hivi hii bajeti ya Tanzania 2011/2012 itaendelea kuwa hivyo bila kubadilika kwa muda wa miaka 12? Hii Serikali miyeyusho duniani. Nalog off
   
 4. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,980
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Hata Tanzania ni tajiri saana ila fedha zetu zimetolewa zinachukuliwa na wakoloni mambo leo eti wawekezaji!

  Fanya utafiti kidogo tu ujue dhahabu kiasi gani inakwenda nje ya nchi bila kulipa hata tone la ushuru? Tanzanite kiasi gani, na vito vingine watu hao hawalipi ushuru eti wanalipa mrahaba, hizo fedha zinaingia mfuko wa nani?

  Funguka ndugu Mtanzania funguka ni wakati wa kupambana kukomboa nchi mikononi mwa mafisadi wanaofilisi nchi hii!!!! Ghadafi alitumia falsafa ya ukombozi akaitoa Libya mikononi mwa wafalme, akaimalisha uchumi wa nchi yake, kosa lake hakusoma alama za nyakati watu wanabadilika!

  Tanzania inahitaji ukombozi tutoke mikononi mwa makanjanja mafisadi wanaojilimbikizia utajili tena eti wagombee Urais!
   
 5. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Tena hata aibu hawana wanatufanya Watanzania ni watu mambumbumbu nalog off
   
 6. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,705
  Likes Received: 322
  Trophy Points: 180
  Uzuri wake hizo pesa zipo kwa juna la The People of Libya sio Muamar Gadafi.
   
 7. hKichaka

  hKichaka Senior Member

  #7
  Oct 23, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 199
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  NI SAWA NA BAJETI YA TANZANIA KWA MIAKA 12Waandishi WetuKIONGOZI wa Libya aliyeuawa juzi na wapiganaji wa Serikali ya Mpito (NTC), anadaiwa kuacha utajiri wa Sh 139 trioni kiasi ambacho ni sawa na bajeti ya Tanzania kwa miaka 12. Habari zilizopatikana jana zimeeleza kuwa fedha hizo ni zile zinazofahamika, alizoweka kwenye benki za nchi kadhaa duniani, huenda alikuwa na hazina zaidi mbali na hiyo.source: GAzeti la mwananchi la leo Jumpili
   
 8. N

  NgomaNgumu Senior Member

  #8
  Oct 23, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inawezekana ameacha kiasi hicho ispokua nafikiri cha kuangalia nini aliwafanyia raia wake. Shule bure mpaka university, Hospital bure. Nyumba bure kwa wasio nauwezo mapaka pesa za kuowa bure.

  Challenge kubwa iliyopo je wazungu na viongozi wengine wataweza kumeet standard ya maisha ya Walibya au wataangalia interst zao. Watu wengi wanataja neno freedom lakin kuna wasiwasi mkubwa kua hawajui maana yake. Anaglia kesi ya Iraq.

  uditeta sio mzuri lakin kama ukimuondoa dicteta kwa nia nzuri na sio kwa kuangali intest zako wakti raia wanasafa. Inatakikana watu kuamka na maneno kama freedom na mengineyo.
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Zitaifishwe tu na zirudishwe kwa Walibya, walipe hizi trilion 3 nato, then wajipange sasa wajiletee democrasia na maendeleo.
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Abacha mwengine huyu, tamaa yake imemtokea puani. Hayo mahela yote alikuwa na chance ya kuhamia kwa fisadi mwenzake Mugabe akaishi raha mustarehe kama Mengistu anavoishi.
   
 11. K

  Kanyigo JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 959
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  alistahili.
   
 12. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #12
  Oct 23, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,169
  Likes Received: 8,191
  Trophy Points: 280
  aise reta habar
   
 13. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #13
  Oct 23, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,738
  Likes Received: 6,014
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo kwenye red; hebu kajipange uje na hoja zenye mashiko. Kwa ufupi, hata (iwe raia wa kawaida au kiongozi wa ngazi yoyote) ungefanya mazuri namna gani; hata kama ukiwa kiongozi (kama Gadafi) ungewezesha wananchi wako waishi maisha mazuri kama peponi bado HUNA HAKI YOYOTE YA KUIIBIA NCHI AU KUJILIMBIKIZIA KINYUME NA UTARATIBU. Hili liko wazi hata vitabu vitakatifu vinaeleza hivyo! Tukiruhusu upuuzi uliopo hapo kwenye red, tutaleta maafa.
   
 14. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #14
  Oct 23, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  NgomaNgumu
  nadhana unayoanzisha ya kubarikiki uwzi wa mali ya umma kwa maelezo yeyote hata kama aliwapa nin bure haikubaliki. Let us be ethical and principled. Tunapoteza utu na na thamani ya ubinadamu wetu kwa kukosa ethics na principles za msingi.
   
 15. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #15
  Oct 23, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,554
  Trophy Points: 280
  Asante Rais wangu wa moyoni kwa kuja jamvini.tunashabikia matokeo bila kutafakari msingi wake! Tukiwa tuna hoji msingi hata wa mema wa kiwango gani tutashinda mengi.(angalizo tu mkuu wangu,usipokuwa rais 2015 tutalipa gharama yake kwa miaka mingi.)
   
 16. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #16
  Oct 23, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,019
  Likes Received: 8,498
  Trophy Points: 280
  Huh..mkuu willbroad nawe ukiupata ulaji usilaze damu mzee.personal interest first mengine baadae usiwe kama kambarage kaacha watoto wanashindia strungi(strongtea)kwa mihogo.. Hah..mtizamo wangu tu jama msije mkanitoa macho
   
 17. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #17
  Oct 23, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Umesema kweli Rais wa Watanzania, tuonyeshe Benghazi ya Tanzania tuanzishe ukombozi, tumechoshwa na Longolongo, hatuwezi kutawaliwa na familia ya mtu akishirikiana na kakundi ka mafisadi. Tutangazie Benghazi yetu.
   
 18. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #18
  Oct 23, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Gadhafi and Libya
  1.There was no electricity bill in Libya; electricity was free for all its citizens
  2. There was no interest on loans, banks in Libya are state-owned and loans given to all its citizens at 0% interest by law
  3. Home considered a human right in Libya –Gaddafi vowed that his parents would not get a house until everyone in Libya had a home. Gaddafi's father has died while him, ...his wife and his mother are still living in a tent
  4. All newly weds in Libya receive $60,000 Dinar (US$50,000) by the government to buy their first apartment so to help start up the family
  5. Education and medical treatments are free in Libya. Before Gaddafi only 25% of Libyans are literate. Today the figure is 83%
  6. Should Libyans want to take up farming career, they would receive farming land, a farming house, equipments, seeds and livestock to kick-start their farms –all for free
  7. If Libyans cannot find the education or medical facilities they need in Libya, the government funds them to go abroad for it – not only free but they get US$2,300/mth accommodation and car allowance
  8. In Libya, if a Libyan buys a car, the government subsidized 50% of the price
  9. The price of petrol in Libya is $0.14 (N22) per litre
  10. Libya has no external debt and its reserves amount to $150 billion – now frozen globally
  11. If a Libyan is unable to get employment after graduation the state would pay the average salary of the profession as if he or she is employed until employment is found.
  12. A portion of Libyan oil sale is, credited directly to the bank accounts of all Libyan citizens
  13. A mother who gave birth to a child receive US$5,000
  14. Gaddafi carried out the world's largest irrigation project, known as the Great Man-Made River project, to make water readily available throughout the desert country

  So What's the Problem with Libyans?
   
 19. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #19
  Oct 23, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumbe ndiyo maana MEMBE ana weweseka kwasababu ya huo utajiri wa Gaddafi, yawezekana keshachukua chake hadi kufikia kutoa tamko la kuomboleza
   
 20. J

  J_Calm Senior Member

  #20
  Oct 23, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawashangaa wanao mkataa Gadhaf na mema yake aliyo yafanya, lakini pia aliyo yatafuta mwenyewa, kwani Libya ni nchi ya kwanza kutoa mafuta duniani? Na je, yakwanza imefikia mafaniko kama hayo? Je Tanzania ina rasilimali kiasi gani na bado bajiti ya taifa inategemea pombe na sigara? Tuangalie ukweli jamani, democrasia yetu ni njaa tupu na unyanyasi tz.
   
Loading...