PreGE2025 G55 Moshi na Temeke waondoka CHADEMA

PreGE2025 G55 Moshi na Temeke waondoka CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Let them gooooooooooo! Those are the people made CHADEMA dormant !
Team Mbowe ndio ilikuwa ikiipaisha CHADEMA ndani na nje sababu Mbowe alikuwa hajipaishi kimataifa kibinafsi alikuwa akipaisha taasisi ya CHADEMA ndani ya nchi ipate wanachama wengi na kudhibiti wadiondoke huku kimataifa akijenga brand ya CHADEMA sio Mbowe

Tofauti na huyu Lisu wenu mhangaika kujenga brand name jina lake ndani na nje badala ya Chama
 
Unamjua Grace Kiwelu wewe? Huyo ni bilionea mtoto wa marehemu wa Bilionea Ndesamburo Mzee ambaye anamiliki mahoteli na makampuni kibao ndani ya nchi na nje ana helikopta kibao Tanzania Kenya nk na mmoja wa wanachama wa mwabzo kabisa wa CHADEMA wafadhili wakuu wa CHADEMA

Zile Helicopter hata Lisu alikuwa akitumia zilikuwa zinakodiwa kampuni ya baba yake Grace Kiwelu ,Mzee Ndesamburo na alikuwa ndio mfadhili mkubwa wa CHADEMA alipoondoka kufariki mali zake karithisha huyo Grace Kiwelu

Tajiri bilionea anaondoka CHADEMA unasema unasema anaondoka malaya
Ana impact yeyote.Nyerere alienda UN kwa pesa za tone tone 😅😅😅
 
Ninafurahishwa sana na kinachoendelea CHADEMA. Wanavyoraruana inaleta faraja kuu kwenye nafsi yangu. Mbona Joyce Mukya hatamki chochote? Sema bado mapema kutabiri mshindi ndani ya CHADEMA kwa sababu wanaojitoa karibu wote walikuwa wafuasi wa Mbowe na wanufaika wa ruzuku chini ya utawala wa Mbowe hivyo wanakuwa hawashtui sana. G55 wafanye ujanja CHADEMA Tarime, Serengeti, Mbeya, Mwanza, Bukoba mjini na Iringa nao wafanye press za kujitoa CHADEMA. Hizi press za wanaCHADEMA wenye asili ya Machame ni kama zinazidi kumpandisha chati Lissu na genge lake.

Kimaro, Massawe, Lema, au Kweka wakisema wamejitoa ni rahisi watu kuwapuuza na kudai wamekosa fursa ya pesa. Lakini ikiwa kina Chacha, Mwabukusi, Nyamhanga, Rutashobya, Rhobi au Mwakipesile ndo wamefanya kujitoa lazima watu wajiulize maswali na kuleta sintofahamu.
Rudini studio mkapange sinema upya, hii imewafanya wapanga sinema muonekane mazuzu. Uzuri hao wachaga hawacheki kwenye hela, mkiwapa wanazichota tu. Wafuasi wa cdm wengi wanajitambua hivyo hawashutishwi na hayo maigizo. Kama walihama toka enzi za kuunga juhudi na bado ccm inategemea wizi wa kura, kuna mtu atatishika kweli?
 
🤣🤣🤣Hoja za G55 eti wanatukanwa, wakiambiwa na nani? Hakuna majibu
kwakweli identity ya wanachadema kwa sasa ni ama kuropoka au kutukana matusi mazito mazito bila sababu yeyote gentleman.

so ,
Chadema as party,
wanatukana mbaya sana aise 🐒
 
Nimefurahi Sana huyu dada kujitoa, Kila mwaka alikuwa anataka nafasi ya viti maalumu eti chama ni Chao, lissu ameikomboa chadema
Ni kweli gentleman,
huyo kibaka wa siasa ameikomboa Chadema kutokea katika heshima na ustaarabu na kuitumbukiza katika uropokaji na uporomoshaji mitusi mazito mazito dhidi ya wale wote wenye maoni tofauti na yake.

Amefanya kazi kubwa kuimarisha misingi ya chuki na migawanyiko,
na sasa wanachama maeneo mbalimbali nchini wanajiengua kila uchwao huku maskini yeye mwenyewe uropokaji ukiendelea kumsotesha korokoroni bila msaada wowote 🐒
 
Wakuu,

Mpango wa kupiga kelele kwenye media ili wasisahaulike unaendelea :KEKLaugh: hivi hawaoni walivyokuwa majinga? Ukiamua kumla chura hakikisha unachagua aliyenona, sasa unakula chura afu unachagua chenye kimedhoofu na utapia mlo, unamla, anakuua, inakuwa ni fezea:KEKLaugh::BearLaugh::BearLaugh:

Wacha tuendelee kukinga maji yanayovuja tukaflashie chooni!

Pia soma Pre GE2025 - Ogopa Teknolojia na Mungu! Sasa ni rasmi G55 wametumwa kuifumuafumua CHADEMA mpaka isambaratike

Moshi wameanza kuunguruma


Meza kuu inajumuisha
  • Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Moshi DC - Exaudi Wilson Mamuya
  • Mwenyekiti Mstaafu wa Halmashauri ya Moshi DC - Michael Kilawila
  • Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Kilimanjaro - Grace Kiwelu
  • Katibu wa BAVICHA Kanda ya Kaskazini - Rachel Sadiki
  • Mwenyekiti wa Mkoa wa Kilimanjaro - Gervas Mgonja
  • Katibu wa Mkoa wa Kilimanjaro

Gervas Mgonja Mwenyekiti wa Mkoa wa Kilimanjaro
Mwenendo wa chama chetu hauridhishi, tuliokuwa tunamsapoti Mbowe tumekuwa hatuishi kwa amani ndani ya kipindi hiki. Najivua rasmi vyeo vyangu na uanachama wa CHADEMA kuanzia leo Mei 11, 2025.

Rachel Sadiki Mwanachadema & na Founder wa CHADEMA jimbo la Mkinga-Tanga
Nilipeleka harakati kwa mara ya kwanza CHADEMA, nilifanya kazi mpaka nikafukuzwa serikalini, nikafirisika. Tulishauri lakini tulichukuliwa kama wahalifu. Hatujapewa haki ya kujieleza wala kusikilizwa, suala la kuondolewa/kushughulikiwa kwetu lina baraka za chama, sioni mwanga huko tunapoenda. Ninajitoa uanachama wa CHADEMA na kujivua nyadhifa zilizonazo na kufanya shughuli nyingine kama alivyosema Mbowe

Grace Kiwelu Mwenyekiti BAWACHA Kilimanjaro, Mwenyekiti Kamati ya Fedha Kanda ya Kaskazini, Mjumbe Kamati Tendaji BAWACHA Taifa

Tulizunguka nchi nzima na Mbowe kuitangaza CHADEMA toka 1992, badala ya kuvuna heshima tunavuna matusi. Tunawezaje kuzuia uchaguzi bila kushiriki? Kusema wananchi waandamane, nikiwaangalia wananchi kule vunjo wataanzia wapi kuandamana? Viongozi wanaona matusi hawakemei, kosa ni kumuunga mkono Mbowe. Nilimuunga kweli Mbowe kwasababu niliona kazi aliyoifanya ya mageuzi ndani ya chama na nchini, bila Mbowe tusingekuwa na CHADEMA ambayo tunayo leo. Kuanzia leo Mei 11, ninajiondoa CHADEMA, ninakwenda nyumbani kupumzika, nakwenda kulea mjukuu wangu, nimechoka matusi ya mtandaoni.

Michael Kilawila Mwenyekiti Mstaafu wa Moshi DC, na Mwenyekiti wa Mkoa Awamu ya 3 Kilimanjaro

CHADEMA yenye upendo na mshikamano imeanza kupotea, chuki ilianza baada ya kutompendelea mtu mmoja ili achaguliwe kugombea ubunge jimbo la Korogwe mwaka 2020. Kuna mtu alikimbia na familia yake na kutuacha hapa akataka tumpokee kishujaa wakati yeye sio shujaa, mimi na Basil tukaanza kushughulikiwa. Nimeamua kuondoka na maamuzi yangu binafsi, nimeona CHADEMA sio mahali salama tena pa kuendelea kufanya siasa. Leo Mei 11, 2025 ninaachana na CHADEMA, ninaenda kupumzika, kadi yangu nitaitunza ili wajuu wangu waje waione wajifunze kwenye historia kwamba nilitukanwa sana. CCM wasinipigie simu, sitaenda CCM, hamtasikia kwamba nimeenda CCM lakini lazima nitafute chama ambacho naona kitafikia malengo yale ambayo wananchi wanataka.

Exaudi Wilson Mamuya Makamu Mwenyekiti wa Moshi DC
Nimekuwa mwananchama wa CHADEMA toka nikiwa na umri mdogo, nimekitumikia chama kwa wivu mkubwa na mapenzi mpaka sasa tumefika mahali naumia moyoni. Kwenye uchaguzi Mkuu sisi tulichagua kumuunga mkono Mbowe, tulipambana pamoja naye kipindi cha magufuli na tulisimama naye kwenye uchaguzi wa chama kwakuwa tulimuamini, lakini baada ya uchaguzi tumekuwa tukiishi kwa hali ngumu sana, tunaonekana waasi, tutakaa pembeni wao waendelee. Leo Mei 11, ninatangaza kuachana na chama, nitapumzika kwa kipindi hiki kifupi lakini sitaacha siasa. Najua timu ya G55 tuna ushawishi, tutakuwana na wananchi tutawashawishi na tutafanya siasa kupitia chombo kingine cha siasa.

Answari Kimaro Mjumbe wa Kamati ya TEHAMA Kanda ya Kaskazini
Mimi nilimuunga Odero, lakini sasa hivi kuna ugomvi kati ya pande mbili, hatuwezi kufika popote. Nina ushahidi, watu walipewa nafasi kwasababu wanamuunga Lissu mkono si sababu wanna sifa. Natangaza kuondoka CHADEMA na nnajivua vyeo vyangu vyote! Pia nawapa changamoto waende kwenye kata yangu pale, wakipata hata mtu mmoja wa CHADEMA Mungu afanye atakachopenda.


Wengine waliojivua uanachama ni pamoja na;

- Mwenyekiti wa Moshi Vijijini - Rose Masuruali
- Kumsapoti Mbowe siyo kosa - Nimejitoa CHADEMA, nitaenda kwenye chama kingine - si CCM

- Katibu wa Vunjo Joseph Mosha
- CHADEMA kulikuwa na jambo ninaloliamini, sasa hivi hakuna - Nimejitoa CHADEMA na najivua rasmi nafasi zote nilizokuwanazo, nitatafuta forum sahihi ya kwenda kuwasemea wananchi

- Katibu Same Mashariki - Magreth Mbwambo - Nimeihangaikia CHADEMA kwa hela, nguvu na jasho na hatukupata chochote. Zamani chama kilikuwa na upendo, sasa ni manyanyaso, nikipata sehemu ambako kuna mwanga nitaenda - Najiondoa CHADEMA

- Katibu Mwanga - Togolani Sinzira - Viongozi wa chama taifa wanakumbatia watu wanaotutukana, tutafakari pa kwenda lakini sio CCM - Najiondoa CHADEMA

- Katibu Same Magharibi - Haika Ngowi - Chama chetu kimekuwa cha wanaharakati na diaspora, hao ndio wanakishauri chama, hakuna tena upendo, chama kimekuwa cha matusi - Nimejitoa CHADEMA, na kujivua vyeo vyote, naenda kutafakari niangalie pa kuelekea lakini sio CCM

- Katibu wa Jimbo la Same Mashariki
- Nimehangaikia chama sana lakini matokeo yamekuwa haya, wakati natumikia chama nilishaletewa bahasha na chama tawala, nikaikataa, kwahiyo sitegemei kurudi huko, sina mpango na CCM, wale niliokuwa nawaongoza tutafute mwelekeo mpya. Ilinipa uchungu kutosaini uchaguzi halafu baadaye wanakwambia tutaangalia namna, hiyo namna ni ipi? - Nimejivua uanachama CHADEMA

Wawakilishi wa Manispaa ya Moshi (G55) kwa niaba ya wengine, Halmashauri ya Moshi na Vunjo (G55) Jasmine Minja, Pius Mrema, Haika Letuu, Lilian Kimei, Vicky Massawe Mwenyekiti BAWACHA Moshi DC sitaenda CCM, Fredy Shayo Katibu BAZECHA na Mweka Hazina nasubiri G55 iniambie inaenda wapi ili nami niingie, Jabir Weta - Tunaondoka CHADEMA sababu ya ubaguzi kisa tulimsapoti Mbowe, walitakiwa kumpa tuzo Mbowe na si tuzo ya matusi

G55 Temeke


Meza kuu inajumuisha;

Mwenyekiti CHADEMA Mkoa wa Temeke - Herman Kiloloma najivua uanachama wangu CHADEMA pamoja na wenzangu kwasababu tumeona hatuko salama ndani ya chama chetu toka uongozi mpya upatikane, tunabaguliwa. Sababu nyingine ni ajenda ya chama kutoshiriki uchaguzi - mimi binafsi nilibaguliwa na Heche, watu 80 tuliokuwa nao hapa na wenyewe wanaondoka CHADEMA. Waliobaki tunawaheshimu na tunaowaacha waheshimu pia uamuzi wetu, tusishambuliwe na maneno. Tutawaita waandishi tutakapotaka kwenda kujiunga na chama kingine

Mwenyekiti Mstaafu Jimbo la Temeke Idi Mahuta

Mratibu wa BAWACHA Mkoa wa Temeke - Yvonne Haule
- Kokote utakapopita najulikana kama mama wa CHADEMA kwa uchungu sana, nawatakia wote wanaotaka kunifuata tunawakaribisha tutakapoenda- najivua uanachama CHADEMA

Mwenyekiti wa Kata ya Makangalawe - Josephine Mwenda - Najivua uananachama mimi na baadhi ya wananchi wangu amabo wananifuata.

Mwenyekiti wa Wilaya ya Temeke - Hamza Kinyema - Tumejitolea sana kwenye chama lakini sasa hivi kuna visa na visasi, kama sisi tunabaguliwa itakuaje kwa wananchi? Tunatukanwa sana kwenye magroup, nimezima simu siingii kabisa kwenye magroup sababu ya matusi. Tutashawishi na wananchi kwenye kwenye chama ambacho tutaelekea. Waandishi wa habari nahitaji kipindi maalum ili tuweze kuzungumzia mambo kwa undani - najivua uanachama wa CHADEMA,

Sa100 acha kuchezea pesa za walipa kodi na maskini wa Tz.
 
Team Mbowe ndio ilikuwa ikiipaisha CHADEMA ndani na nje sababu Mbowe alikuwa hajipaishi kimataifa kibinafsi alikuwa akipaisha taasisi ya CHADEMA ndani ya nchi ipate wanachama wengi na kudhibiti wadiondoke huku kimataifa akijenga brand ya CHADEMA sio Mbowe

Tofauti na huyu Lisu wenu mhangaika kujenga brand name jina lake ndani na nje badala ya Chama
Huo ni mtazamo wako mkuu, wengine wanamuona mbowe hakujenga Chama kama taasisi Bali Cha mtu binafsi....ushaidi unaona watu wanachama chama kisa mtu wao kashindwa uchaguzi🤣🤣🤣
 
Team Mbowe ndio ilikuwa ikiipaisha CHADEMA ndani na nje sababu Mbowe alikuwa hajipaishi kimataifa kibinafsi alikuwa akipaisha taasisi ya CHADEMA ndani ya nchi ipate wanachama wengi na kudhibiti wadiondoke huku kimataifa akijenga brand ya CHADEMA sio Mbowe

Tofauti na huyu Lisu wenu mhangaika kujenga brand name jina lake ndani na nje badala ya Chama
Really! I see the opposite it killed the real opposition!
 
kitu ninachojiuliza, kwani hawa watu walikuwa na wafuasi wengi sana au Lisu ndo mwenye wafuasi. na pia, hii ondoka ondoka kama wamepewa mpunga, mpango wao ni kwamba Lisu hata akitoka awe hana pesa ya kuitisha mkutano wa kuchagua viongozi wapya au nini, manake ni kweli hana pesa na wazungu hawawezi kupenyeza pesa na wanachadema mtaani huwa hawachangi. mbona kama ccm wanacheza karata vizuri sana kukivunja miguu chama?
 
Kwa kasi ya viongozi wa chadema kuachia ngazi, mpaka kufikia uchaguzi mkuu kitakuwa having uongozi wowote mikoani.

Sisi wapambanaji wa chadema online tuwe makini, inaweza kuwa chama saiti hakipo sisi tunahangaika kuchoma bando
Chiembe uwe mzalendo kama kwenye izi ulioambiwa angalao akili imetumika,sii kujidhoofisha akili,ubongo,haiba na mwili kwa viwango hivi.
 
Kwa kasi ya viongozi wa chadema kuachia ngazi, mpaka kufikia uchaguzi mkuu kitakuwa having uongozi wowote mikoani.

Sisi wapambanaji wa chadema online tuwe makini, inaweza kuwa chama saiti hakipo sisi tunahangaika kuchoma bando
hii itasaidia kupunguza bei ya kitanda kwa mtanzania wa kawaida pale muhimbili?
kwa sasa ni shilingi elfu 50000 kwa siku. hili hata mama yako na wewe mnalijua.
ni watanzania wangapi wanaweza kulipia gharama za kitanda za shilingi elfu 50000/= kwa siku?
je chadema na ccm nani alipelekea gharama hizi kufikia hapo ? jitafakari.
chadema siyo adui wa watanzania. adui wa watanzania ni ccm ndo mana hata mwenyekiti alijipitisha mwenyewe kuwa mgombea pale dodoma
 
Back
Top Bottom