Fursa za ajira na biashara makaburini

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,904
Kuna fursa nyingi makaburini nawapa wale wavivu wa kufikiri ziko za kuanzia kuchimba na kujenga makaburini, kuuza Sanda na majeneza, kukodisha mahema na viti na kuviweka makaburini, kukodisha spika na microphone, kuuza maji ya kunywa kwa waombolezaji, mashada ya maua, chakula, usafiri nk

Ukienda makaburini unakutana na madalalali wanakupa kila kitu hata ukitaka zile gari za kubeba maiti ni mfuko wako ni one stop center hata kama huna choir watakuletea huna shehe au padri au Mchungaji watakuletea huna Kikosi cha waombolezaji watakuletea at a cost of course hiyo inaitwa funeral service providers na ofisi zao au kijiwe chao kinakuwa eneo la makaburini au jirani napo. wanatoa full service.

Mtaji waweza kuwa mdomo wako tu unachohitaji kujua kipi kiko wapi na simu zao uwe nazo wote wenye huduma wewe kazi kula cha juu au kumchaji au commission ya udalali ila kila kitu unakifanikisha kwa spidi na ubora aliyefiwa anabaki katulia tuli wewe ukichapa kazi kwa niaba yake. Utachaji kiasi gani juu yako
 
Aisee! Kumbe ndiyo maana mlikuwa mnapinga kwa nguvu sana vita dhidi ya Corona?

Kwa hiyo sasa mambo yenu ni sawa sawa?
 
Back
Top Bottom