Furaha tupatazo JF na kusahau shida

Vaislay

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
4,504
2,000
Jamani ndugu wanakijiji cha JF hebu leo tushare Furaha tuzipatazo jf, Kama mimi nikiona avatar na comment za Vin Diesel zinakufurahisha sana,

kuna Thread za mshana jr ni za ucommedy sana mi huwa siishi kucheka huyu jamaa yani utafikiri matukio yoote ya dunia hii anakutana nayo yeye,

Jukwaa la siasa kule watu ni wa kali si mchezo,huku MMU kiukweli tunafugana sana na comment zetu

Elezea hata huko mtaani unayokutanana nayo na kukufanaya ukafurahi, TUpunguze stress za kulia na matukio yanayotukumba jamani,
Kama ujuavyo MOYO ukiandamwa na huzuni ,streess hata sura inapoteza nuru...

Ehee wenzangu hebu tuambiane
 
Last edited by a moderator:

Khantwe

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
53,491
2,000
Yan huyu Evelyne Salt mi ananipaga raha kweli. Kuna mtu anaitwa Asprin nae ananifanya maisha yangu yawa marefu..majibu yake sijui huwa anayatoa wapi
 

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,161
1,250
Madiskasheni mengi tu yana faida sana sijawahi kupata mawazo ya wadada wakifunguka zaidi ya humu......nawashukuru sana maana najifunza mengi sana!!!!!!!!!

Brothers wengi nao wanatoa experience a maisha so sio mbaya kuokota wenzako wanafanya nini kimaisha kwa ujumla!!!!! Hili linanipa sababu ya kuweka kila nijualo kuhusu maisha hata kama mengine ni kama yanagusa uhuru wangu ila kama naamini wengine watajifunza au nitakosolewa ili nijirekebishe nabwaga mchana kweupeeee mbuzi wanakula majani!!!!!

Utani na furaha yaani huwezi ingia ukabaki na stress zako au makunyanzi!!!!!!!

Kikubwa zaid nimeongeza ndugu na jamaa wengi sana na I hope kuna siku ntakutana nao live na kuwachukua kama ndugu kabisa wa karibu shida zao ziwe zangu na furaha yangu iwe yao!!!!!!!!

Yaani kwa ufupi ni kwamba sijawahi kujuta..............:grouphug:
 

Ximena

JF-Expert Member
May 17, 2014
623
500
michango ya watu ndo inanifurahisha na kunifundisha mengi, maana kuna dada alikuja kulalamika humu eti wifi yake kaja hajawahi kufika jikoni.....loh watu walivyomuwakia humu harudii tena hakyanani!!!!!!
 

Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
61,727
2,000
Yan huyu Evelyne Salt mi ananipaga raha kweli. Kuna mtu anaitwa Asprin nae ananifanya maisha yangu yawa marefu..majibu yake sijui huwa anayatoa wapi

Sijajua kama wewe ni ke au me. Kama ni Ke ningekuomba PM ili tukadiskashen kwa kina zaidi. İla kwa ufupi, siri ya napopatia majibu ni kubwa sana. Hii tunaijua tuliozaliwa alhamis usiku kwa sababu lazima baba zetu waliwakabidhi mama zetu mimba za alfajiri kabla jogoo hajawika.

Baada ya kusema hayo naomba turudi kwenye mada, aliyejua maziwa alizıgunduaje chuchu??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom