Fungukeni mliolelewa na Mzazi Mmoja

Fungukeni mliolelewa na Mzazi Mmoja

Simplicity.

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2013
Posts
2,636
Reaction score
1,664
Kufutia Thread hii https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/742486-single-mums-and-dads-come-this-way.html.

Iliyoanzishwa na mdau mmoja wa JF, ambaye ameuliza maswali ya msingi yaliyosababisha mtanange na maoni tofauti kwa wachangiaji mbalimbali kuhusu wamama waliolea/wanaolea watoto peke yao bila baba zao. Kinachonifanya nilete mada hii hapa, ni akina mama/baba/watu wanaoona kwa mitazamo yao au wale ambao wapo au wamepitia hali hiyo kulichukulia swala la kulea peke yao bila baba/mama, na swala la makuzi ya mtoto bila mapenzi ya baba na mama kama jambo la kawaida kabisa tena lisilo na athari yoyote ya kihisia, kiakili, kisaikolojia na hata kifizikia kwa mtoto.

Kuhusu baadhi ya akina mama kudai kulea mtoto/watoto peke yao ni jambo wanalojivunia, nimeona sio kweli kwa mjibu wa michango yao, kwani ukiisoma kwa makini utaona ishara ya kuwa na hasira, uchungu, kulalamika, kujutia na hata kuwachukia waliowatelekeza. Sasa hawa akina mama na wadau wengine pamoja na michango yao kupingana na uhalisia, wameenda mbali zaidi kwa kuonesha hata watoto wanaolelewa au waliolelewa na mzazi mmoja hawapati athari zozote bali wana "experience" maisha kawaida kama wengine na hawaoni tofauti yoyote.

Je, watu mliolelewa na mzazi mmoja, ni athari au faida zipi mlizipata/mnazozipata/mtakazozipata ambazo mnadhani msingezipata/hamtazipata kama mngelelewa na wazazi wawili?

NB: Kuna jambo ambalo nadhani watu wengi hawalielewi: Wanadhani kulea ni matterially tu! Kwamba ukiwa na rasilimali za kutosha kama vile hela, nyumba, magari na mengineyo, halafu una uwezo wa kumpatia mtoto kila anachohitaji basi ndio malezi yanaishia hapo. Je, ni kweli? Wewe una mtazamo gani? Nauliza hivi kwa sababu kila leo nimewasikia wanawake wakijinadi kwa kusema, "Hata akiniacha mtoto nitalea bila shida, kwani nina uwezo hawezi kunishinda".

Naongeza maswali mengine kwa hisani ya watu wa haki za binadamu:

Je, baada ya kuzaliwa na kujikuta unalelewa na mama au baba tu, halafu ukaamua kumwuuliza huyo mzazi: Baba/Mama yangu yuko wapi? Halafu hataki kukujibu, au anakujibu yupo lakini unamtaka wa nini? Unajisikiaje, utajisikiaje? Je, akikupa jibu la uongo halafu baadaye ukaja kugundua sivyo alivyokuambia, utajisikiaje? Je, unaona ni haki/sawa mama/baba yako kukataa kukuonyesha, au kukuelezea kuhusu baba yako kama amekwishafariki? Je, swala la wewe kutokumjua kabisa baba/mama yako maishani linakuathirije?

NANDERA Kongosho charminglady Kilaza ram na wengineo
 
Hii mada hainihusu mkuu... Iliyokuwa inanihusu ni ile kuleee.... Ngoja nisome maoni pekee!!
 
Unataka tufunguke nini LifeHacker
Nadhani hii inamhusu mtoto wangu na bado hajafikia umri wa kuingia kwenye mitandao ya kijamii so kuwa mvumilivu akikua atakujibu
 
Last edited by a moderator:
Unataka tufunguke nini LifeHacker
Nadhani hii inamhusu mtoto wangu na bado hajafikia umri wa kuingia kwenye mitandao ya kijamii so kuwa mvumilivu akikua atakujibu

Kuna watu wengi mkuu wamelelewa na mzazi mmoja, kwa hiyo usiwe na shaka wanaweza kuwakilisha mawazo ya dogo.
 
Nilichoona kwenye ile mada ni athari za globalisation tu, attitude iliyojengeka kwa mtu kulea peke yake. Watu hawajaanza kuachana/kuzaa kabla ya ndoa wala kufiwa leo, but hii sensitivity ya single parent inakuzwa mno.

Nachelea kusema mengi nisiumize hisia za watu wengine bure, but kuna some sort ya 'self pity', not right, not fair kwa mzazi.
 
Mkuu Kilaza kumbe mheshimiwa anahusika!

pitia uzi wake kule jukwaa la siasa aliandika mwenyewe tena hilo jina la kigwangalla sio la mzee wake ni la babu mzaa mama

zamani hamisi kigwangalla alikuwa anaitwa "said bagalile"mzee akala dili la kwenda mbele akamtelekeza dogo na mama mbaya kabisa akaondoka na vyeti vya mama yake (mama alikuwa nurse) hivyo akopoteza kazi akarudi kuwa mama ntilie

mzee kasugua kucha ulaya weeeeeeee dogo akabadilisha jina akaitwa hamisi sasa mzee amefulia na sasa karudi bongo kakuta dogo ni mbunge anajipendekeza tena mbaya zaidi analalamika kwenye media dogo hamisi kamtelekeza kisa anaumwa cancer
 
huyo mzee ndezi kweli
huko ulaya si angejitibu huyo ht mi namkimbiza mbayaaw
 
Ninachoona kwenye hii mada ni athari za globalisation tu, attitude iliyojengeka kwa mtu kulelewa na mama au baba peke yake ni issue. Watu hatujaanza kulelewa na mzazi mmoja leo but hii sensitivity ya kuwa single parented inakuzwa mno. Nilishaongea kuwa nilijiskia vipi na niliathirika vipi kwenye mada iliyokuwa inasema "msamaha ndio kila kitu". tafadhali rejea.
 
Nilichoona kwenye ile mada ni athari za globalisation tu, attitude iliyojengeka kwa mtu kulea peke yake. Watu hawajaanza kuachana/kuzaa kabla ya ndoa wala kufiwa leo, but hii sensitivity ya single parent inakuzwa mno.

Nachelea kusema mengi nisiumize hisia za watu wengine bure, but kuna some sort ya 'self pity', not right, not fair kwa mzazi.
Naenda mbali kidogo watu weusi tuna matatizo sana kwakweli,wao wanalichukulia swala la single4 parents kama mama/baba alikuwa mlaya akazaa akalea mwenyewe,na kwa asilimia 90 wanalirelate na wanawake tu kwamba kazaa kabla au kaiba mume wa mtu akazaa huko au alipachikwa mimba akakataliwa hii ndio maana halisi yao ya single parents.

Kongosho kuna watu wanafiwa na mzazi mmja,wengine wamebakwa akapatikana ,wengine wamekataliwa na wababa wao,wengine mama alipoachika alimpeleka kwa baba au alimtupia baba mtoto,wengine aliiba mume wa mtu ikawa ndio zawadi yake.

KAMA KABLA YAKURAISE HII MADA KWENYE UBONGO WAKO KUH SINGLE PARENTS WANGEKUWA WANAWAZA MAMBO HAYO WASINGELETA HIZI MADA ZA KIJINGA HUMU NDANI.SHUKURU MUNGU TU AWE KALELEWA NA KAKUA NA UHAI UPO PIA HATA KAMA AMELELEWAJE NI KUSHUKURU MUNGU HAKUUWAWA UHAI UPO,HAYO MENGINE YATAJISETI TU MBELE YA SAFARI.
JAMANI FIKIRINI NJE YA BOX.MMIMI NILIFIWA NA MAMA YANGU TUKIWA WADOGO BABA YETU ALITURAISE HUKU ANAHANGAIKA TUTASOMAJE MAANA NI WA KIPATO CHA WASTANI ANA AMEHAKIKISHA TUMEPATA DEGREE WOTE WATANO HUYO BABA MWENYEWE ,JE LEO HII MIMI NIMEHARIBIKA KWAKUKUZWA NA BABA TU MTAMLAUMU BABA YANGU BADALA YA KUSHUKURU KUWA KATUFIKISHA HAPA?????
 
Mkuu LifeHacker , Ningependa kusema kwamba circumstances zinatofautiana kwenye hili swala la single parenthood, kuna wengine mwanaume/mwanamke alikataa mtoto, mwingine hawajui nani mzazi wa mtoto, kuna mwingine alibakwa na pia kuna wale ambao baba au mama alifariki.
Kutoka maisha yangu binafsi ni kwamba nimelelewa na mama pekee baadaya baba kufariki wakati tupo wadogo sana. Kusema kweli sijapata athari zozote za kukosa malezi ya baba, I'm very proud to have being raised by a single mother, a strong woman indeed; I have turned out to be a good example in my society, successful in my life and a loving family alongside.
 
Last edited by a moderator:
Nimelelewa na upande wa baba na si na baba kiviiile,wazaz wangu walitengana nikiwa na miaka 10 na wadogo zangu wa kiume wawili wakinifuatia,baba hakutaka mama aondoke na sisi,baba alikua mfanya biashara wa kusafirisafiri,mara leo tunaletewa aunt tuishi naye kesho bibi,keshokutwa sijui nani,baada ya muda mzee akaoa mke mwingine tukaish nae yule mama akafariki bado tukiwa wadogo nakumbuka i was std VI,then wakaja watu wengine tena kuish na sisi si chini ya watatu,me nikaja kupelekwa sehem nyingine kuish na bibi yangu mwingine(hapo mama tunaenda kumuona likizo tena kwa kulalamika sana ndo tunaenda,au yeye huja kutuona),wakat me naish na bibi yangu ndugu zangu wakabak peke yao,mmoja akaja akachukuliwa na shangaz yangu,yule mwingine anayenifuata akabak peke yake,huku anasoma,huyu alochukuliwa na shangaz yangu nae akawa anasomeshwa,akafaulu kwenda sekondari O'levo mdogo wangu nae akafaulu O'levo kwenda advance nami nikaenda advance wote tukaenda Elimu ya juu vyuo tofautu,kazi yetu ikawa kumsomesha mdogo wetu ambaye alipofaulu O'levo naye alienda advance Pugu,akaingia chuo wakat sisi tunamaliza,baba yeye japo alikua mtu wa mzunguko ila alikomaa kutusonesha,mpaka sasa wote tumemaliza elim ya juu,baba alifariki ila mama ndo yupo hai,ila tulimiss mapenz ya wazaz wetu na binafs yameniathiri kisaikolojia kwa kiasi kikubwa tu
 
pitia uzi wake kule jukwaa la siasa aliandika mwenyewe tena hilo jina la kigwangalla sio la mzee wake ni la babu mzaa mama

zamani hamisi kigwangalla alikuwa anaitwa "said bagalile"mzee akala dili la kwenda mbele akamtelekeza dogo na mama mbaya kabisa akaondoka na vyeti vya mama yake (mama alikuwa nurse) hivyo akopoteza kazi akarudi kuwa mama ntilie

mzee kasugua kucha ulaya weeeeeeee dogo akabadilisha jina akaitwa hamisi sasa mzee amefulia na sasa karudi bongo kakuta dogo ni mbunge anajipendekeza tena mbaya zaidi analalamika kwenye media dogo hamisi kamtelekeza kisa anaumwa cancer

okay,now hakuna haja ya kumlaumu juu ya upuuz wowote atakaoufanya
 
Back
Top Bottom