Fungukeni mliolelewa na Mzazi Mmoja

Fungukeni mliolelewa na Mzazi Mmoja

pitia uzi wake kule jukwaa la siasa aliandika mwenyewe tena hilo jina la kigwangalla sio la mzee wake ni la babu mzaa mama

zamani hamisi kigwangalla alikuwa anaitwa "said bagalile"mzee akala dili la kwenda mbele akamtelekeza dogo na mama mbaya kabisa akaondoka na vyeti vya mama yake (mama alikuwa nurse) hivyo akopoteza kazi akarudi kuwa mama ntilie

mzee kasugua kucha ulaya weeeeeeee dogo akabadilisha jina akaitwa hamisi sasa mzee amefulia na sasa karudi bongo kakuta dogo ni mbunge anajipendekeza tena mbaya zaidi analalamika kwenye media dogo hamisi kamtelekeza kisa anaumwa cancer

Bado hajafa tu?
 
Mimi nimelelewa na my sista tangu nikiwa 5yrs mpaka najitegemea. Sio kwamba wazazi wangu hawapo ila wako mkoa tofauti....tofauti iliyopo kati ya mimi niliyelelewa na mlezi mmoja na wale waliolelewa na walezi wawili sijaiona labda wanaonitazama ndo wanaweza kugundua tofauti
 
Bado hajafa tu?

hahahahahahah una hasira nae eeehhh.....mh.kigwangalla ana huruma sana yaani kamnunulia badoboda ili mzee apate pesa za kahawa na rojo bado kamuwekea billi hospitali nadhani ni Agha khan mzee akiumwa anatibiwa kwa billi ya mh.

lakini bado mzee ana shukrani nilimuona ameenda EATV analalamika kigwangalla kamtelekeza eti anaomba msaada
 
Unajua nini Kilaza,wazee wengine unaweza kuwakaba koo kwa hasira.
Umeamka salama lakini?
 
Mkuu LifeHacker , Ningependa kusema kwamba circumstances zinatofautiana kwenye hili swala la single parenthood, kuna wengine mwanaume/mwanamke alikataa mtoto, mwingine hawajui nani mzazi wa mtoto, kuna mwingine alibakwa na pia kuna wale ambao baba au mama alifariki.
Kutoka maisha yangu binafsi ni kwamba nimelelewa na mama pekee baadaya baba kufariki wakati tupo wadogo sana. Kusema kweli sijapata athari zozote za kukosa malezi ya baba, I’m very proud to have being raised by a single mother, a strong woman indeed; I have turned out to be a good example in my society, successful in my life and a loving family alongside.

Hii thread imeibuliwa na thread nyingine kama nilivyoeleza hapo juu, lengo hasa sio waliolelewa na mzazi mmoja baada ya mwingine kufariki, bali waliolelewa na mzazi mmoja hali mwingine yupo na kamkataa mtoto au baba/mama hataki kumwonyesha mtoto mzazi wake mwingine! Ahsante mkuu.
 
Nivea focus sio waliolelewa na mzazi mmoja baada ya mwingine kufariki, ingawa wanaweza kutupa ushuhuda wa maisha yao. Lengo hapa ni mtu ambaye wazazi wake wote wawili wapo hai lakini mmoja au ikiwezekana wote wamemkataa kata kata! Je, ameathirikaje?
 
Last edited by a moderator:
Binafsi sioni kama kuna tatizo nimekuwa na mama peke yake na maisha yangu nayaona sawa tu
 
Mimi nimelelewa na my sista tangu nikiwa 5yrs mpaka najitegemea. Sio kwamba wazazi wangu hawapo ila wako mkoa tofauti....tofauti iliyopo kati ya mimi niliyelelewa na mlezi mmoja na wale waliolelewa na walezi wawili sijaiona labda wanaonitazama ndo wanaweza kugundua tofauti

Kulea sio kubebwa mgongoni au kulishwa au physical attachment, ingawa vinaweza kuwa ni sehemu ya malezi.

Kama wazazi wako walikuwa wanakupenda na kukubali kuwa wewe ni mtoto wao, wamekulea hata kama walikuwa wanaishi Pluto! Tunaongelea mtu ambaye amelelewa na mzazi mmoja kwa sababu amekataliwa na mzazi wa pili!
 
Since i was young nimelelewa na my daddy na nimejifunza mengi tu ya maisha kupita uwezo wangu mana kulelewa pande moja bila mwingine kume nifanya niwe strong ku face any challenge na kujiamini ingawa kulelewa pande moja kuna madhara ya ku feel lolness ukihitaji kitu cha kukufariji kwa karibu like mom huna msaada hali iliyo nipelekea ukimya wa kupindukia even if na shida cwezi ku express to anyone it affect me psychologically but hiyo situation inatokea kulelewa upande mmoja kwa sababu zisizo epukika no way out zaidi ya kukubali
 
Nivea focus sio waliolelewa na mzazi mmoja baada ya mwingine kufariki, ingawa wanaweza kutupa ushuhuda wa maisha yao. Lengo hapa ni mtu ambaye wazazi wake wote wawili wapo hai lakini mmoja au ikiwezekana wote wamemkataa kata kata! Je, ameathirikaje?

Lakin hao wote ni victim wa kulelewa na upande mmoja awe hai au amefariki acha watu wawe free ku.share ideas bila limit mana hao wote ni victim ingawa wanatofautiana
 
Last edited by a moderator:
Nimelelewa na mama baada ya baba kumuacha kwa sababu hakuwa wa kabila lake. Nadhani nimekuwa mtu bora katika jamii kuliko hata hao ndugu zangu wa kwa baba waliolelewa na baba na mama.
 
Mimi nimelelewa na my sista tangu nikiwa 5yrs mpaka najitegemea. Sio kwamba wazazi wangu hawapo ila wako mkoa tofauti....tofauti iliyopo kati ya mimi niliyelelewa na mlezi mmoja na wale waliolelewa na walezi wawili sijaiona labda wanaonitazama ndo wanaweza kugundua tofauti

Kulelewa na dada hakuwezi kuwa sawa na kulelewa na mzazi mmoja...
Si umeona single parent walivyo na machungu...

Wewe huna sifa za kuitwa umelelewa na single parent.

Mfano ungekuwa ushikiki dada yako angeweza bado kuwashirikisha wazazi wako; kwa sababu wapo na hawajakukataa...
Hata wewe unaweza kuwa na hofu ya baba au mama yako hata kama haukuwa unaishi nao kwa kuwa unajua dada anaweza kunishitaki akiona na misbehave...kwa ufupi umelelewa na dada, mama na baba pia...japo walikuwa mbali

Unaweza kuwa kwenye group jingine na topic mpya...
 
Nivea focus sio waliolelewa na mzazi mmoja baada ya mwingine kufariki, ingawa wanaweza kutupa ushuhuda wa maisha yao. Lengo hapa ni mtu ambaye wazazi wake wote wawili wapo hai lakini mmoja au ikiwezekana wote wamemkataa kata kata! Je, ameathirikaje?
dude nafikiri unakwenda nje ya mada ,nimeeleza kwa kifupi sababu at least zinazopelekea kulelewa na mzazi mmja ,kufiwa na wote hiyo ni mada nyingone mpya na ni ngumu kuijadili kuliko unavyofikiri maana utawatoa wengi machozi.inawezekana wote wapo duniani na ukalelewa na mmja.umekataliwa na bab mzazi,mama mzazi,umepatikanna katk mazingira tatanishi ,mama yako kazaa na mume wa mtu au mama kawa mlevi ,mhuni bb akakuchukua nakukulea,
 
Back
Top Bottom