Fumbo la mke wa Lutu na Sodoma na Gomora

Fumbo la mke wa Lutu na Sodoma na Gomora

Du kwa hiyo kama musa alikuwa mweusi bila shaka wana Wa Israel waliokombolewa misri walikuwa weusi .swali hilo taifa la Israel la Leo mbona weupe!
Hili swali mbona nishalijibu?

Hao unaowaona na wanaojiita waisraeli walikusanywa kutoka Ulaya huko wala siyo Waisraeli wa damu....
 
Hili swali mbona nishalijibu?

Hao unaowaona na wanaojiita waisraeli walikusanywa kutoka Ulaya huko wala siyo Waisraeli wa damu....
Je walitumia vigezo vipi kuwakusanya maana ktk biblia mungu alisema atawatanya kisha atawakusanya niambie hao waisrael halisi walipotelea wapi kwa hiyo mungu aliahidi uongo?
 
"mshana jr, post: 21596145, member: 98741"]Pale niliposema walitengeneza mvinyo hukupaona kwani[/QUOTE]

Huwezi kutengeneza zabibu porini bila vineyard.nana vyvyombo vya kuandalia how can u convice us that this is wrong
 
E="B40, post: 21596424, member: 402152"]Mkuu hivi ulanzi Na mnazi si unagema tu[/QUOTE]


Ila mvinyo huwezi kugema mkuu
 
="Eiyer, post: 21596621, member: 42137"]Hili swali mbona nishalijibu?

Hao unaowaona na wanaojiita waisraeli walikusanywa kutoka Ulaya huko wala siyo Waisraeli wa damu....[/QUOTE]


Sasa wana wa Israel wa damu ni akina nani? Ungemalizia unalotaka kusema

mkuu
 
Majibu yapo Mkuu!

Kiufupi ni kwamba Lutu alipata Neema ya Kuokoka, Biblia haielezei kama familia yake ilikuwa nayo inamcha Mungu. Neema ya Wokovu kwa Lutu ikaifunika mpaka na familia yake, hivyo Mungu akainusuru Familia ya Lutu kutokana na Lutu kuwa mcha Mungu. Hata kikawaida, kwenye Nyumba kukiwa na mtu anaabudu Mungu au miungo, moja kwa moja yeye na uzao wake au familia inatambulika na Mungu au miungu.

Unapopata wokovu Neema ya wokovu hupaswi kutamani au kutenda yale matendo ambayo Mungu alikuwa akichukizwa nayo. Ukisoma 1Wakorinto 5:17 inasema kuwa mtu ukiwa ndani ya Yesu umekuwa kiumbe kipya ya kale yamepita.

Kuambiwa kwa akina Lutu na familia isigeuke nyuma ina maana kuwa wasitamani wala kutenda yale matendo yao yaliyopita ya zamani.

Biblia ina lugha flani ngumu ngumu na mafumbo ndani yake, hata Mussa alivyoambiwa avue viatu Mungu hakumaanisha viatu vya miguuni ila alimaanisha ajiondoe ktk laana ya umwagaji damu na dhambi zake ili Mungu aweze kumtumia. Miguu ktk Ulimwengu wa roho inabeba maana ya Utayari, yaani utayari wa kufanya kazi ya Mungu. Ukisoma ile Waefeso kama sikosei inazungumzia silaha 6 za Mungu, inasema kuwa uvae utayari miguuni.


Natumia simu, samahani kwa kujibu kifupi na kwa mpangilio usio mzuri sana.
 
Je walitumia vigezo vipi kuwakusanya maana ktk biblia mungu alisema atawatanya kisha atawakusanya niambie hao waisrael halisi walipotelea wapi kwa hiyo mungu aliahidi uongo?
Sijui walitumia vigezo gani kuwakusanya...

Pia,sielewi ni kwanini unasema Mungu alidanganya.Halafu ni Mungu siyo mungu,zingatia hizo tofauti....
 
"mshana jr, post: 21596145, member: 98741"]Pale niliposema walitengeneza mvinyo hukupaona kwani

Huwezi kutengeneza zabibu porini bila vineyard.nana vyvyombo vya kuandalia how can u convice us that this is wrong[/QUOTE]
In the professional way you need a lot of stuffs! Locally hapana
 
Aslam alyekum. Sifa njema ni zake Allah(s.w),Rehma na Amani zimfikie kiongozi wa umma Nabii Mohammad(s.a.w) na ahali zake na maswahaba zake.

Mshana Jr Quran ni kitabu cha haki kimeelezea kisa cha Nabii Lutt(a.s) na umma wake.Quran11:6-9
Kumbuka wageni wawili walipokuja kwa Nabii Ibrahim (a.s) wakati wa jioni walikaribishwa na Ibrahim akawaomba wajitambulishe wageni wakasema "Sisi ni wajumbe kutoka kwa M/Mungu tumetumwa kwa kaumu ya Lutt.Ibrahim akawaambia lakini kuna Lutt,Wajumbe wakasema tutamwokoa Lutt na ahali zake zake isipokuwa mke wake.Wajumbe wakasema" TUMETUMWA KWA KAUMU YA WAKOSEFU YA NABII LUTT KUWA HILIKI TUTAMWOKOA LUTT NA AHALI ZAKE ISIPOKUWA MKE WAKE TUNAKADILIA NI MWENYE KUBAKI NYUMA.Wajumbe walishasema kuwa mke wa Lutt hakuwa miongoni mwa waje wema Hivyo ange adhibiwa tu.
Kwani hata Wajumbe wale walipofika na Kaumu ya Lutt,Lutt alikuwa mnyonge sana kwa kuwa alijuwa tabia za Umma wake.Baada ya kufika wageni wale ndipo watu wake walikuja kwa Lutt mbiombio kuwafuta wageni wale.Lakini wageni wakamwambia Lutt usiwe na wasi wasi sisi tumetumwa na M/Mungu kuja kuwaangamiza Hivyo ondoka usiku na watu wako(walio mfwata Lutt) isipokuwa mke wako atakuwa miongoni mwa watakaoangamia.Kwa hiyo utaona kuwa hukumu ya mke wa Lutt ilikuwa imshatolewa zamani na M/Mungu ilikuwa bado utekelezaji tu.
My take;Hakukuwa na fumbo lolote Katika hukumu ya mke wa Lutt.Mshana kr
 
View attachment 522601utabiri unatimia?
View attachment 522602mabaki haya yalikutwa kwenye mji wa Sodoma na Gomorrah... Ni wanaume wawili waliokuwa wanashughulikiana
Actually wanatheolojia, wanahistoria na wanaanthropolojia wengi wanaamini kuwa dhambi iliyoangamiza Sodoma na Gomora siyo homosexuality bali ni ulafi (glutton). Biblia za mwanzo na maandishi ambatano ya wakati ule yanaonyesha kuwa watu wa miji ile walikuwa walafi na wachafu na uchafu huo hautajwi. Baadaye sana watafsiri wa Biblia ndiyo wakatafsiri huo uchafu kama sexual immorality (u.firaji + uzinzi) na katika tafsiri zilizofuatia uzinzi wa kawaida ukaondolewa na ikabakia homosexuality na neno Sodom baadaye likatoholewa kumaanisha u.firaji. Kuna documentary imeandaliwa na profesa wa Harvard inaongelea mambo haya na mengineyo (gharika ya Nuhu, kuanguka kwa ukuta wa Yeriko na mengineyo)

Hiyo picha likely ni ya kizaazaa cha volkeno ya Pompei.
 
Inaendelea......

Katika mwanzo 19 tunaona Malaika wale wawili wanaingia katika mji wa Sodoma na Lutu alikuwa amekaa mlangoni mwa Sodoma akawaona na akaenda kuwalaki na kuinama hata kifudifudi akawakaribisha nyumbani mwake,tunakuja kuona yaliyoendelea pale watu wa mji ule wanawataka wale malaika,Lutu anawasihi sana na anakuwa tayari hata kuwatoa binti zake wawili ambao walikuwa bikra wafanywe na wale watu wa mji ule vyovyote vile watakavyo na si wale malaika, bado watu wa mji ule wakakataa mpaka malaika wakaingilia kati kwa kuwapofusha macho watu wale wakubwa kwa wadogo wakatafuta mlango wa Lutu hata wasiweze kuuona(Mwanzo 19:1-11) yaani kutembea nje ya kusudi ni mbaya sana nakaa nafasi ya Lutu inaumiza kiasi gani mzazi anakubali kutoa binti zake wafanywe vyovyote vile,ni uchungu mzito na maamuzi magumu sana,jamani tufanye maamuzi mazuri na tutembee njia nzuri tusijewapa gharama watoto wetu na vizazi vijavyo mambo ambayo hawakustahili kupata,kuyaona wala kuyasikia, inaumiza sanaa!!! ( Mungu turehemu tu).

Mungu wetu ni wa rehema bado katikati ya hukumu anatangaza rehema,anaamua kuiokoa nyumba yote ya Lutu na jamaa zake wote(Mwanzo 19:12). Lutu anajulishwa kinachoendelea na kitakachoendelea(Mstari wa 13). Katika mstari wa 12 tunaona Lutu alikuwa na nafasi kubwa sana ya kuwaokoa wengi maana anaambiwa..." na wowote ulionao katika mji uwatoe mahali hapa"....ilikuwa ni fursa kubwa sana ya kutoka na wengi katika mji huo lakini anashindwa kuiona fursa na anashindwa kuitumia vyema fursa hiyo,kwa rehema aliyopewa alikuwa na uwezo wa kuambukiza rehema hiyo kwa wengine,akaja akawafundisha mema watu wale ambao angetoka nao na kuanza upya na Bwana.

Mstari wa 14,Lutu anawakumbuka wakweze ambao walikuwa wamewaposa mabinti wale,lakini akawa kama achezaye machoni pa wakweze,Mhh!! Mara nyingu Mungu kabla hajaleta adhabu huwa anatujulisha na kutuonya lakini mara nyingi tumekuwa watu wa kupuuza tu na kudharau(rejea wakati wa Nuhu pia).

Katika Mstari wa 15 Lutu anaambiwa aondoke amtwae mke wake na binti zake wawili ili asipotee katika maovu ya mji huo, Mstari wa 16..Lutu akawia-kawia maana yake akawa anajivuta-vuta,anajichelewesha,kama vile bado haamini- amini,kama vile bado anaipenda penda bado sodoma ikabidi Malaika wale wawashike mkono Lutu,mkewe na binti zake wakamtoa kwa nguvu wakamweka nje ya mji ule kwa jinsi Bwana alivyokuwa anamuhurumia. KOSA LINGINE LUTU ANAFANYA BADO MOYO WA LUTU ULIKUWA SODOMA PAMOJA NA KUAMBIWA KILA KITU KINACHOENDELEA KATIKA MSTARI WA 13 BADO LUTU ALIJIVUTA- VUTA,HAKUWA TAYARI KUIACHIA KIRAHISI SODOMA,TENA ALIAMBIWA AONDOKE MWENYEWE LAKINI BADO HAKUTAKA MPAKA MALAIKA WANAAMUA KUMTOA KWA NGUVU, Mara nyingi nasi Mungu anatutaka tutoke kwenye maovu ila hatusikii tunamwambia bado bado Mungu subiri mimi ikifika uzee nitakuwa mtakatifu,au ndo nitakutumikia,au subiri Mungu kidogoo nifanye hili nitaacha uovu kabisa,NDUGU YANGU TUBADILIKE TUSIKIAPO SAUTI YA MUNGU TUSIFANYE MIOYO YETU MIGUMU.

Mstari wa 17 Lutu anapewa agizo ajiponye nafsi yake asitazame nyuma wala asisimame katika hilo bonde popote,ajiponye mlimani asije akapotea... Kumbuka ni Lutu aliyepewa agizo hili,ni Lutu aliyekuwa anajua nini kinaendelea toka mwanzo,ni Lutu aliyeambiwa katika mstari 13 kwamba mahali pale panaenda kuangamizwa,Ni Lutu ambaye ni kichwa cha Familia,Ni Lutu mwenyewe aliyejichagulia nchi ile,ni Lutu mwenyewe aliyeamua kutoka Uru pamoja na Ibrahimu,its all about Lutu,sijui Lutu alimtoa wapi huyu mke wake,nimejaribu kutafuta sijaona tufanye uchunguzi sote tujue mke wa Lutu alikuwa wa taifa gani? .....Je tujiulize mimi na wewe Lutu alisimama vyema katika nafasi yake?,hii inaumiza sana!! Turejee Edeni kwa Adamu (Mwanzo 2:16-17),Adamu naye ndiye aliyepewa agizo na Mungu ndiye aliyeumbwa kwanza,sijui alihakikisha jambo hili linatimilika vipi kwa mkewe Eva?,Lutu anafanya makosa ambayo Adamu aliyafanya.

WANAUME SIMAMENI KATIKA ZAMU ZENU,WANAUME NINYI NDIYO KICHWA CHA NYUMBA,NINYI NDIYO MLIOPEWA MAAGIZO NA MUNGU,MWANAUME AKIWA GIZA NI UWEZEKANO MKUBWA GIZA HILO LITAENDELEA KATIKA FAMILIA NZIMA,MWANAUME AKIKOSEA DUNIA YOTE IMEKOSEA,MWANAUME JITAMBUE UMEBEBA MAJUKUMU MAZITO,WANAUME MBONA MMEMPOTEZA LENGO NA KUSUDI MLILOKUWA MMEUMBIWA NALO(naandika nabubujikwa na machozi),LAITI MNGELIJUA NYIE NI KINA NANI? LAITI MNGELIJUA WAJIBU WENU?,LAITI MNGETAMBUA ILE NAFASI MLIYONAYO KWA MUNGU?,Ni rahisi sana leo kutoa shutuma za kila aina kwa mke wa Lutu kama ilivyo rahisi kutoa shutuma kwa Eva,sikatai wanawake tunamakosa yetu(hili nalo ni somo jingine),JE LUTU ALIHAKIKISHA VIPI HILI AGIZO LINAUKAMATA MOYO WA MKE WAKE,LINAPENYA VIPI KIASI HALIGEUZI MOYO WA MKE WAKE NA KUMRUDISHA NYUMA?....TUKUMBUKE MAKOSA YOTE YALIANZIA TOKA MWANZO NA LUTU MWENYEWE KISHA HATA KATIKA HATARI BADO LUTU ANALETA UZEMBE WA KUJICHELEWESHA-CHELEWESHA,ALISHAAMBIWA AONDOKE MWENYEWE LAKINI ANAJIVUTA VUTA TU MPAKA ANATOLEWA KWA NGUVU,HII NI HATARI KUBWA SANA!!.....KWA UZEMBE HUU ULITEGEMEA MKE WAKE NAYE AWE NI WA TOFAUTI? AISEEE VILE ULIVYO NDIYO NA MKE WAKO ALIVYO!! MWANAUME UNA WAJIBU/NAFASI KUBWA SANA WA KUMJENGA MKE WAKO AU KUMUANGAMIZA,MKE NI MSAIDIZI TU ANATAKIWA KUPOKEA MAELEKEZO KUTOKA KWAKO, KAZI KWAKO KUHAKIKISHA MAAGIZO YAKO YANATEKELEZWA......ASHUKURIWE MUNGU AMERUDISHA ILE MANHOOD YA MWANAUME KUPITIA YESU KRISTO,TENA ASHUKURIWE MUNGU AMEUMBA JAMBO JIPYA DUNIANI KWAMBA MWANAMKE ATAMLINDA MWANAUME(Yeremia 31:22).

Inaendelea....
 
Actually wanatheolojia, wanahistoria na wanaanthropolojia wengi wanaamini kuwa dhambi iliyoangamiza Sodoma na Gomora siyo homosexuality bali ni ulafi (glutton). Biblia za mwanzo na maandishi ambatano ya wakati ule yanaonyesha kuwa watu wa miji ile walikuwa walafi na wachafu na uchafu huo hautajwi. Baadaye sana watafsiri wa Biblia ndiyo wakatafsiri huo uchafu kama sexual immorality (u.firaji + uzinzi) na katika tafsiri zilizofuatia uzinzi wa kawaida ukaondolewa na ikabakia homosexuality na neno Sodom baadaye likatoholewa kumaanisha u.firaji. Kuna documentary imeandaliwa na profesa wa Harvard inaongelea mambo haya na mengineyo (gharika ya Nuhu, kuanguka kwa ukuta wa Yeriko na mengineyo)

Hiyo picha likely ni ya kizaazaa cha volkeno ya Pompei.
Kwahiyo wanapingana na maandiko?
tapatalk_1497335902316.jpeg
 
Inaendelea...

"Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea. Lutu akawaambia, Sivyo, bwana wangu! Tazama, mtumwa wako ameona kibali machoni pako, nawe umezidisha rehema zako ulizonifanyia kwa kuponya nafsi yangu, nami siwezi kukimbilia mlimani nisipatwe na yale mabaya, nikafa. Basi mji huu u karibu, niukimbilie, nao ni mdogo, nijiponye sasa huko, sio mdogo huu? Na nafsi yangu itaishi. Akamwambia, Tazama, nimekukubali hata kwa neno hili, kwamba sitauangamiza mji huo uliounena. Hima, ujiponye huko, maana siwezi kufanya neno lo lote, hata uingiapo humo. Kwa hiyo jina la mji ule likaitwa Soari."
MWANZO. 19:17‭-‬22.

Tukiangalia mistari hiyo hapo juu Lutu bado anaendelea kufanya makosa, amepewa maagizo kwanza asitazame nyuma ili ajiponye nafsi yake,pili asisimame katika bonde hilo popote pale ajiponye nafsi yake aende milimani asije akapotea....ameshaambiwa wapi aende nini afanye lakini Lutu akakataa ushauri ule na kusema kwamba hataweza kukimbilia mlimani asipatwe na mabaya yale asije akafa,akachagua mji mdogo ulio jirani yake ambao ulikuwa kwenye plan ya kuangamizwa,akafanya makosa ya uchaguzi kama aliyofanya mwanzo lakini hapa anapata rehema anaambiwa amesikilizwa mji huo hautaangamizwa. Mungu wetu ni wa rehema huchukuliana nasi hata katika madhaifu tuliyonayo.

Mstari wa 23-26 tunaona Lutu akiwasiri Soari na ndipo miji ya sodoma na Gomora ilipoangamizwa,sijui Lutu alikuwa anasisitiza kiasi gani kwa familia yake walitii agizo hilo,sijui alikuwa akiwakumbusha familia yake namna gani yale waliyoambiwa kwamba Mungu anaenda kuangamiza miji ile?

Mstari wa 26 tunaona mkewe akigeuka nyuma na anageuka kuwa nguzo ya chumvi,nyuma tunaweza kutafsiri vyovyote vile tupendavyo au tunaonavyo na kama nilivyosema awali kila mtu anaweza kufunuliwa kama Bwana apendavyo na kwa ufahamu wake aweze kuelewa,kama ambavyo ilikuwa agizo kwa Adamu asile tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya(kumbuka kulikuwa na miti mingi pale ila katikati kulikuwa na mti wa uzima na mwingine wa ujuzi wa mema na mabaya,mti huu kila mtu anatafsiri vile apendavyo,na ndiyo hapo shetani alipomuweza mwanamke) "Agizo ni moja tu usigeuke nyuma ujiponye nafsi yako,Usile tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya maana utakapokula Hakika utakufa".....Je ni kwa namna gani tunatii maagizo ya Mungu anayotuagiza ni hilo tu ndo Mungu anataka,anasema utii ni bora kuliko sadaka( 1Samweli 15:22)...undani wa kile kitu wakati mwingine hauhitajiki kuujua mambo yote utayajua baada ta kutii,ndo hapa ambapo palimfurahisha Mungu hata kumuita Ibrahimu ni rafiki yake,kwanza alimtii kuondoka katika jamaa yake kwenda kusikojulikana,alitii kumtoa Isaka Sadaka hata hakutaka kujua maisha yangekuwaje bila ya Isaka,vipi ahadi za Mungu zingetimia baada ya Isaka kutolewa sadaka je ungekuwa mwisho wa uzao wake? ALITII TU KAMA BWANA ALIVYOMUAGIZA.

Tuendelee kujifunza kwa Lutu katika Mwanzo hiyo 19.....

Mstari wa 29 unatuthibitishia moja kwa moja Lutu na nyumba yake aliokolewa kwa neema tu ni kwasababu ya Ibrahim,agano la Ibrahimu na Mungu lilipiga kelele na ikawa neema hata kwa ndugu yake,kumbe sisi tukisimama imara tukatembea vizuri na Mungu tunakuwa sababu ya wengine kuponywa kupitia sisi.

Lutu anaendelea kufanya makosa tu, Mstari wa 30 anatoka Soari akakaa katika pango yeye na binti zake,tukumbuke katika mstari wa 20 yeye mwenyewe ndo aliomba akae katika mji huo na akapata kibali cha Mungu,halafu yeye mwenyewe tena anaogopa kukaa hapo anaenda tena mahali ambapo hapakuwa na kibali cha Mungu,hivi alitegemea angekuwa na mwisho mzuri? Mungu amemrehemu amemleta tena kwenye kusudi akakataa option ya Mungu kwenda mlimani ikawa siyo tatizo kwa Mungu,akajichagulia alipopataka akapewa baraka zote bado tena anapakimbia!!,naamini Lutu angeendelea kukaa Soari wokovu wa Bwana ungemtokea huko maana mahali pale palikuwa na kibali tayari cha Mungu.

Anakimbilia pangoni yeye na wanawe tu,hivi tujiulize tu kwa akili zetu ndogo nini kingeendelea tena pale? Kama si Lutu kuwabaka wanae basi ndo kama hivyo wanae wakambaka baba yao,tunajifunza kwamba mazingira nayo yanachangia sana haijalishi ni nini wala nini miili yetu ni dhaifu,tunashinda ni kwa neema ya Bwana,usiintatein(chochea) mazingira ya kutenda dhambi,usijitengenezeee nafasi ya kutenda dhambi,mara nyingi tunamsingizia shetani eti alinipitia,kweli umepita anga zake utegemee utoke salama kweli??? Tuache visingizio visivyo na maana!!!

Lutu hakuwa na mwisho mzuri yeye na uzao wake,uzao wake ukaja kuwa adui wakubwa wa Israel(Waamoni na Wamoabi)dhambi ya uzinzi na usaliti wa sheria za Mungu hakuwaacha,Katika yote haya yamemfikisha Lutu hapo alipokuwa ni sababu ya kutotembea katika kusudi lake,hata alipoletwa kwenye kusudi lake bado akashindwa,Inaumiza sana kupoteza mke uliyempenda,inaumiza sana kulala na watoto wako wa kuwazaa,inaumiza sana kuwa na kizazi chenye maovu. Inaumiza sana kuishi maisha ya kutanga tanga.

Mungu tusaidie tusahihishe makosa yetu,Mungu tusaidie tukuelewe pale unaposema nasi,Mungu tusaidie tulielewe kusudi la kuumbwa kwetu hapa duniani.Sisi peke yetu hatuwezi ila tunayaweza mambo yote katika wewe ututiaye nguvu,Katika Jina la Yesu tunarudi kwenye kusudi letu,Amina.

mshana jr asante sana kutumiwa na Mungu kuleta mada hii nimejifunza mengi,Umenifanya nami nijitafakari kwa upya safari yangu,Mungu amesema nasi sisi sote,ubarikiwe sana na Bwana azidi kukutumia na akufunulie siri nyingine nyingi ambazo macho hayakupata kuona,wala sikio halikupata kusikia wala hayakuwepo katika moyo wa mwanadamu yoyote yule.
 
Kwa Nyongeza muhimu sana:-

Wanawake tuna udhaifu wa kutotii,ndo maana tumeonywa sana juu ya hili la Utii(waefeso 5:22, Wakolosai 3:18,1 Petro 3:1) Wanaume tusaidieni tuwe watii mbele za Mungu na kwenu pia,hakikisheni by hooks and cooks tunakuwa watii(ehhh sijaruhusu vipigo ila ukiwa na ushirika mzuri na Mungu atakupa tu nini ufanye ili mke wako awe mtii).

Wanaume mmepungukiwa upendo,jitahidini mtupende kama Kristo alivyotupenda sote,(wakolosai 3:19,Waefeso 5:25) ukimpenda mtu utamlinda,utahakikisha hakuna baya lolote linamfikia,hutaachia anapotoka,upendo wa Kweli katika 1 Wakoritho 13, mkitupenda kwa dhati kiukweli hata kazi yetu ya usaidizi na Ulinzi itaenda vyema....hapa tena linamrudi mwanamke umekabidhiwa majukumu mapya ya Ulinzi,Mlinzi ana majukumu mazito kuhakikisha lindo lake liko salama muda wote,wanawake tuna la kujibu mbele za Mungu kwa majukumu mapya tuliyopewa,tuhakikishe by hooks and cooks mwanaume huyu hapotei anatimiza vyema kusudi la Mungu.Tujifunze kwa Abigail jinsi alivyo muokoa mumewe Nabali na nyumba yote licha ya mumewe kuwa mpumbavu,kazi ya mlinzi ilisimama vyema,tuache ujinga kusema atajiju mwenyewe na kufanya mambo ya kitototo tu eti amemwaga mboga namwaga ugali na kuzima jiko,shauri yako hata wewe haupo salama utaangamia na wewe na nyumba yako pia.Pigania nyumba yako uokoe kizazi chako.

Wanaume mmeambiwa mkae na sisi kwa akili(1Petro 3:7)tumieni akili zenu vyema,fikirisheni bongo zenu vyema katika kutimiza kusudi la Mungu muwapo hapa duniani,ombeni akili safi na bora kutoka kwa Mungu,akili safi za kina Yusufu,akili za Kina Daniel,Akili bora za Ibrahimu kwa kutii,Akili safi za kina Eliya n.k mtatawala na kumiliki kama Bwana alivyokusudia, tena mkiishi kwa akili msisahau kutupa heshima kama chombo kisicho na nguvu,kumuheshimu mke wako siyo ubwege ndugu zangu ni agizo toka kwa Mungu,sasa nyie takeni kuishi kimabavu na kwa njia zenu mnazozijua mtakavyoona wake zenu wanawafanya kheeeeee!!.

Tumia akili baba,kuna mambo ya kijinga jinga tu wake zenu wanafanya eti mnasema demokrasia,eti uhuru wa mapenzi shaurieni yatawarudi hayo!!,ukicheka na nyani utavuna mabua.....siyo kila jambo mkeo analileta kwako ni sahihi,fikicha akili muulize Mungu vizuri ni sahihi ama si sahihi,likiharibika hilo tunakuruka futi 100,Muulize Ibrahimu alipozaa na Hajiri ilikuwaje wakati ni Sara mwenyewe ndo alitoa wazo la Ibrahimu azae na mfanyakazi wao,Ibrahimu masikini akasahau maagizo na ahadi zote alizohaidiwa na Mungu kwa kupenda kumfurahisha mkewe akafanya,ohhh!! siyo kila jambo unapaswa umfurahishe mkeo!!,kuwa na msimamo kama Ayubu pamoja na Mke wake kumshawishi amkane Mungu sababu alimjua Mungu wake kibinafsi hakuyumbishwa pamoja na ushawishi wote wa mkewe na rafiki zake.

Halafu ukishindwa kukaa vizuri kwa akili na mkeo ujue hata maombi yako yanazuiliwa,ndo maana ndoa ikianza kusumbua unashangaa hata mambo mengine pia yanasumbua,afya,uchumi n.k. Kila mmoja asimame kwenye zamu yake ili tule mema ya nchi kuanzia hapa duniani mpaka mbinguni.
 
Katika dhambi kubwa ambazo hata manabii uchwara wa hivi leo wanazikwepa mno ni kuzini.
Km wanafanya watajitahidi ili isivuje kwa kuwa ni dhambi kubwa.
Iweje itokee kwa nabii wa ukweli tena tunaeaminishwa kuwa anapokea kauli kutoka kwa mungu wake kwa kila linalojiri mbele yake iweje afikie kubakwa pasi na yeye kujua na je? Hv mnabii wa mungu anazini na wanawe waumini nao wakigegeda watakatazika.
Na sifa ya kuondokewa na akili ni ya watu wa kawaida ambao ulevi huwasababishia hv yawezekana nabii kupokea mapokezi toka kwa muumba wake akiwa na hangover?
Nahitaji kujua ndugu na yapo makosa ambayo yanafahamika yakawaida kwa manabii kama vile kumezwa na chewa ila kuzini bado panahitajika tafiti.
Sidhani kama.jamaa alikiwa nabii
 
Kuna uwezekano cain alikuja kuzaa huku Afrika na alikuwa mtu mweusi [emoji12]

Au alikuja na dada yake mmoja kwasbb Adam alikuwa na watoto wa kike pia
Kwahiyo Cain awe mweusi na mama yake hawa awe Mzungu??
 
Back
Top Bottom