Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,666
- 729,819
Sodoma na Gomorrah ni miji iliyokuja kuangamizwa kwa sababu wakazi wake walifanya kufuru ya starehe mpaka kumsahau Mungu kabisa....na kibaya zaidi ni ile dhambi ya kutenda kinyume na maumbile
Ndani ya miji ile akawepo mchamungu mmoja naye alikuwa Lutu...mweledi mnyenyekevu na msikivu sana.. Baba wa mke mmoja na mabinti wawili
Mungu alikasirika na kuamua kuiteketeza ile miji miwili.,lakini akaamua kumuokoa mtumishi wake Lutu na familia yake ila kwa sharti moja! Kwamba Lutu aondoke na familia yake kabla miji ile haijateketezwa lakini 'ATAKAYEGEUKA NYUMA' atageuka jiwe la chumvi
Kwanini kugeuka nyuma? Fumbo la Sodoma hilo! Mke wa Lutu aligeuka nyuma na akageuzwa kuwa jiwe la chumvi!je naye alikuwa mteja!?
Lutu na mabinti zake hawakugeuka nyuma na wakaenda kuishi mlimani mpaka Lutu alipokuwa mzee kabisa!
Mabinti zake wakajiongeza wakaona baba anazeeka mama hayupo na sisi ni mabinti! Tusipofanya namna kizazi kitapotea
Makatengeneza mvinyo mkali wakampa mzee akanywa akalewa, wakampa unyumba baba yao....wakashika ujauzito na kizazi kikaendelea(hakuna ubaya hapa!)
Kinachonitatiza kwanini Mungu alisema atakayegeuka nyuma atageuka kuwa jiwe la chumvi?
Leo ni jumatatu twendeni kazini..mambo mengine hayana majibu
=========
Mchango
Ndani ya miji ile akawepo mchamungu mmoja naye alikuwa Lutu...mweledi mnyenyekevu na msikivu sana.. Baba wa mke mmoja na mabinti wawili
Mungu alikasirika na kuamua kuiteketeza ile miji miwili.,lakini akaamua kumuokoa mtumishi wake Lutu na familia yake ila kwa sharti moja! Kwamba Lutu aondoke na familia yake kabla miji ile haijateketezwa lakini 'ATAKAYEGEUKA NYUMA' atageuka jiwe la chumvi
Kwanini kugeuka nyuma? Fumbo la Sodoma hilo! Mke wa Lutu aligeuka nyuma na akageuzwa kuwa jiwe la chumvi!je naye alikuwa mteja!?
Lutu na mabinti zake hawakugeuka nyuma na wakaenda kuishi mlimani mpaka Lutu alipokuwa mzee kabisa!
Mabinti zake wakajiongeza wakaona baba anazeeka mama hayupo na sisi ni mabinti! Tusipofanya namna kizazi kitapotea
Makatengeneza mvinyo mkali wakampa mzee akanywa akalewa, wakampa unyumba baba yao....wakashika ujauzito na kizazi kikaendelea(hakuna ubaya hapa!)
Kinachonitatiza kwanini Mungu alisema atakayegeuka nyuma atageuka kuwa jiwe la chumvi?
Leo ni jumatatu twendeni kazini..mambo mengine hayana majibu
=========
Mchango
Ngoja nisaidie kuelezea kidogo Kwa ufahamu kidogo nilio nao kwenye Hii knowledge
Mke wa Lutu alikaidi amri ya Mungu Ndio maana akageuzwa kua nguzo ya chumvi sababu alikua miongoni mwa hao wana sodoma Na Mungu alijua Ndio maana akasema usiangalie nyuma hata Safari ya wana wa Israel wale walio mlalamikia Musa amekuja kuwaua jangwani utaona Ni wale walio ungana Na akina Kora kutengeneza ndama wa dhahabu Na wakaanza kumwabudu Na hao Ndio walio mezwa Na ardhi Ndio chanzo cha ardhi kumeza watu live Sasa sijasema wanaomezwa Na ardhi Ni walio abudu sanamu.
Binti Za Lutu walikosea kuzaa Na baba Yao Kwani ndio walio zaa waboamu ambao kulitengeza Kabila lililokuja kuwa pinga Sana wana wa Israel Ni Kabila ambalo Mungu alililaani Na ndio maana Mungu kwenye kitabu cha mambo ya walawi(Leviticus )alitoa amri kadhaa pale Na adhabu zake ambazo waarabu mpk Leo wanazitumia kuadhibu moja wapo Ni mtu akikutwa amezini adhabu ya kupigwa mawe hadi kufa
Sasa uzinzi Au tamaa ya kuzini iko hivi :kwenye kitabu cha Mithali kina sema (Azinie Na mwanamke hana akili kabisa afanya mambo ya kuikosesha Nafsi yake Na kumsababishia aibu )
Tunarudi Kwa mke wa Lutu aibu mpk Leo ya kugeuzwa jiwe la chumvi..
Natumai hata Kwa pacent ndogo Sana kuna mtu ataelewa
Asante sana mshana jr kutufikirisha haya.
Neno la Mungu ni jipya kila siku na ukitulia na Mungu vizuri kupitia Roho Mtakatifu utafunuliwa mambo ya ajabu ambayo hata ulimwengu haukuyajua wala sikio halikusikia wala macho hayakupata kuyaona. Na kazi ya Roho Mtakatifu ni kufumbua mafumbo ya Mungu( 1Wakoritho 2:9-11,Yohana 16:7-15,Yohana 14:17,26 N.B mambo ya Rohoni hutafsiriwa na Watu wa rohoni kama siyo wa rohoni huwezi yaelewa haya itakuwa upuuzi tu kwako).
Katika hili la mke wa Lutu yapo mambo mengi sana ya kujifunza ambayo kila mtu anaweza kufunuliwa kwa namna ya pekeyake kadri Mungu anavyotaka mtu huyo aelewe kwa lugha yake na kulingana na ufahamu wake. Yote yaliyosemwa humu yanaweza kuwa sahihi kadri kila mtu alivyofunuliwa kama Bwana na Roho yule yule apendavyo.
Mimi kwangu nataka tujifikirishe kidogo kosa lilianzia wapi mpaka haya yote yakatokea,Lutu alikosea wapi,au alianzia wapi? Napenda tujifunze zaidi chanzo ambacho tukikijua wote hatutafanya makosa kama aliyofanya Lutu.
Tukisoma Mwanzo 12 tunakutana na Habari ya Lutu na Abram,ila tukianzia Mlango wa 11 utajifunza kuanzia kizazi cha Abram kilitoka wapi hadi ule mstari wa 24 tunaona baba yake Abram anazaliwa ambaye ni Tera,halafu mstari wa 27 tunaona Abram na Lutu wanatokea. Sasa basi katika Hiyo Mwanzo 12 tunaona Abram anaambiwa na Mungu atoke yeye katika jamaa yake na nyumba ya baba yake na Mungu anampa ahadi ya kuwa taifa na uzao mkubwa. Mstari wa 4 tunaona Abram anatii lakini Lutu akaondoka pamoja naye(hapa pana somo la kujifunza sijui Lutu alilia/alijiamuria tu kuondoka na Abram au sijui Abram aliamua kumbeba???) Makosa pia yalianzia hapa.... usidandie baraka za mtu funuliwa na wewe vyako uvikamatie,usiige vya mtu,Abram aliitwa yeye kama yeye na Mungu alimtaka yeye peke yake atoke so Lutu anaanzia hapa Kufanya makosa,anatembea katika njia ambayo si yake,anatembea katika kusudi ambalo si lake,anatembea katika njia ya mtu mwingine,Je ulikuwa ni mpango wa Mungu Lutu aende na Abram,Lutu hakujikubali yeye kama yeye,alitakiwa amuulize Mungu na yeye aende na Abram au aendelee kubaki na Tera, Mungu alikuwa na Great mission na Abram siyo Lutu,Lutu angetafuta na yeye kwa Mungu mission yake ni ipi?.... (MUNGU ROHO MTAKATIFU AWASAIDIE MUELEWE HILI.).........Kwahiyo kuanzia hapa Lutu anakosea so hope hata destinity(mwisho) wake hauwi mzuri,ANGALIA SANA USITOKE KATIKA KUSUDI LA MUNGU ALILOKUKUSUDIA WEWE HAPA DUNIANI, UTAHARIBU SYSTEM NZIMA YA MAISHA YAKO( Bwana uturehemu tusahihushe makosa yetu).
Mwanzo 13 tunaona jinsi walivyobarikiwa na Bwana,Ukitembea na mpakwa mafuta wa Bwana hutabaki wa kawaida,kwahiyo wote wawili wanakuwa na mali nyingi isiyotosha ardhi kiasi kwamba ugomvi unatokea kati ya wafanyakazi wa Lutu na Abram,Abram anamwambia Ndugu yake Lutu usiwepo ugomvi kati yao,achague upande ambao ataona unafaa,akienda kulia Abram ataenda kushoto,akienda kushoto yeye ataenda kulia n.k(Hapa ulikuwa mtego mkubwa kwa Lutu)
"Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla BWANA hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya BWANA, kama nchi ya Misri hapo unapokwenda Soari. Basi Lutu akajichagulia Bonde lote la Yordani; Lutu akasafiri kwenda upande wa mashariki; wakatengana wao kwa wao."
MWANZO. 13:10-11
KOSA LA PILI LUTU ANAFANYA,AKACHAGUA SEHEMU AMBAYO KWA MACHO YAKE ALIIONA NI NZURI YA KUPENDEZA NA KUFURAHISHA MOYO(Rejea Edeni Eva aliona tunda ni zuri lapendeza macho sana na lafaa kwa kuliwa watamanika kwa maarifa Mwanzo 3:6) tunajifunza nini basi? Hata waswahili husema "si kila king'aacho ni dhahabu" fikiri sana kabla ya kutenda kwa yale unayoyaona,tamaa huanza katika macho,kisha wazo(akili na moyo) kisha dhambi huzaliwa. Tunajifunza kwamba kabla ya kila jambo tumshirikishe Mungu hata katika yale ambayo mioyo yetu ingependa macho yetu yangetamani,ipo njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu lakini mwisho wake ni mauti na kuangamia( Mithali 14:12,) Tunapaswa kulinda moyo maana moyo ni mdanganyifu( Mithali 4:23, Yeremia 17:9) , Ukimkabidhi Bwana atanyoosha mapito na njia yako(Mithali 3:5-7).
Laiti Lutu angeyajua haya asingefanya kosa la Pili kwenda kukaa katika nchi ya uovu ambayo inakuwa ni hasara moja kwa moja kwake na familia yake anaharibu mfumo mzima wa maisha yake,katoka nje ya kusudi lake,Mke anampoteza,Watoto wake wanamnywesha kilevi wanalala na baba yao laana moja kwa moja inaendelea kuyaandama maisha yake na kizazi chake.
Halafu sasa mikosi haikuanzia hapo soma Mwanzo 14:8-16,Kunatokea vita kati ya mfalme wa Sodoma,Gomora ,Adma,Seboimu na mfalme wa Bela mwisho Wafalme wa Sodoma na Gomora wanashindwa hatimaye miji ile inatekwa na Lutu naye anatekwa na mali yake yote kisha mtu anampasha Abramu habari kuwa ndugu yake katekwa,Abram anatoka usiku wa manane anaenda kumpigania ndugu yake na akamkomboa yeye na mali yake yote,basi hapa PANGEMFIKIRISHA TENA LUTU JE YUPO MAHALI SAHIHI?? (MUNGU SIYO DIKTETA AMETUPA AKILI YATUPASA TUZIFIKIRISHE NA TUKIMUOMBA ANAJIBU ANATUONESHA (Yeremia 33:3).
Inaendelea.........
Inaendelea...
Katika Mwanzo 13:14-18 Tunaona Bwana anamwambia Abram ainue macho yake atazame kutoka alipo, upande wa kaskazini,wa kusini na Mashariki na Magharibi,halafu anamwambia aondoke akatembee katika nchi hiyo kwa mapana yake,kwa marefu yake..kisha anapewa ahadi ya kwamba nchi hiyo atapewa yeye na uzao wake na utakuwa mwingi kama mavumbi ya nchi,mtu akiweza kuhesabu mavumbi ya nchi basi uzao wake Abram utahesabika, Daaahhh!!! Acha kabisa ukitembea katika kusudi ambalo Mungu anakutaka huwezi kuwa wa kawaida.... hapa Abramu anapewa nafasi ya kufanya evaluation,afanye research yake mwenyewe ajionee mwenyewe,hapa anapewa nafasi ya kusema lipi ni lipi angetamani liwepo kwenye nchi yake,halafu Mungu anamwambia aanze kutazama pale alipo eeehhhh hili ni somo jingine pia kumbe kuna mambo ambayo unaweza kuyaona siyo mazuri lakini utakapokubali kumtii Mungu ukachukua hatua hayo mambo hayatabaki jinsi yalivyo. Kumbuka Abramu aliambiwa atoke katika nchi yake na jamaa yake na nyumba ya baba yake lakini hakuambiwa aende wapi,ilikuwa ni utii wa hali ya juu sana na maamuzi magumu ambayo sijui hata kama mimi ningeweza leo from nowwhere Mungu aniambie nitoke Dar yangu niliyoizoea niende huko nisikokujua unakuta najiendea huko Katavi sina ndugu, jamaa,rafiki wala chochote khaa!! Acha tu abarikiwe Abramu....
Kutembea ndani ya kusudi ni njema sana, halafu kuna watu/mambo ambayo ili kusudi litimie vizuri inabidi uachane nayo tu,ilikuwa by any means kutengana na Lutu lazima kutokee tu maana Aliitwa yeye kama yeye. Mhh!! Hapa tujiangalie na sisi tumebeba kina Lutu gani maishani mwetu(Mungu ana kusudi na kila mtu na kila mtu aliye tayari kuwa naye ana mpango naye ndo maana kila mtu ana DNA yake kila mmoja ni wa kipekee hakuna anayefanana na mwenzake,everyone is unique).Pengine ilibidi Abram amsaidie Lutu kujua kusudi lake nini mwee damu nzito kuliko maji alishindwa kujua hilo.
Mwanzo 17 tunaona sasa Mungu anambadilisha Abramu jina kutoka Abram kuwa Ibrahimu kwamba baba wa mataifa mengi,na mkewe kutoka Sarai mpaka Sara mama wa mataifa. Dohhj kumbe majina nayo yanamatter eehhh??... sasa Mungu anaweka agano kabisa na Ibrahimu na inakuwa ni agano la milele ambalo liliendelea kupiga kelele katika uzao wote wa Ibrahimu hata pale Mungu alipotaka kuangamiza kizazi cha Ibrahimu hili agano liliendelea kumsumbua na hatimaye ataamua kusamehe tu na kurehemu( Anaitwa Mungu wa maagano)Soma hapo utaona ni agano gani.
Mwanzo 18 tunaona Malaika wa Bwana wanamtembelea Ibrahimu na pale Ibrahimu anawahudumia kisha wanaacha ujumbe mwakani majira kama yale Sara atakuwa na mtoto.
Mstari wa 16 tunaona Ibrahimu anawasindikiza wakiwa wanaondoka wanaelekeza nyuso zao Sodoma,Agano linapiga kelele masikioni pa Bwana anajiuliza " Je nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo?" Kweli kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi na dhambi zao zimeongezeka sana,Mstari wa 21 anasema"basi nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia na kama sivyo nitajua".....duhhh patamu hapa!.....kumbe Mungu bado alikuwa hajaamua kuingamiza Sodoma na Gomora alikuwa kwenye mpango ila bado pia rehema zake zilikuwa kubwa kwa Miji ile......
Mstari wa 22 Watu wale ambao ni malaika wakaachana na Ibarahimu lakini bado Ibrahimu aliendelea kukaa uweponi mwa Bwana wakaendelea na mazungumzo yao....
Mstari wa 23 Ibrahimu anasema na Bwana je ataharibu mwenye haki na mwovu? Na je wakiwepo wenye haki Hamsini je Bwana ataangamiza?,Mungu akajibu la hasha wakiwepo hao nitapaacha mahali pote kwaajili yao,wakaendelea kushushana mpka kumi (Mstari wa 26-32) ....kumbe hapa Ibrahimu naye ilibidi afikiche akili yake yaani katika nchi yote hamna wenye haki 50,45,40,30,20,10.... basi angefikiri chap chap aombe nini tena siyo kushushana namba na Mungu,ukisoma katika jicho la tatu hiyo nchi haikuwa na mwenye haki hata mmoja na pengine hata Lutu hakuwa mwenye haki ila kwasababu ya Agano la Mungu na Ibrahimu aliloliweka katika Sura ya 17,na ukisoma pia Mungu anajaribu kuangalia itakuwaje akiangamiza Sodoma na Gomora bila kumjulisha Ibrahimu ili hali pale kuna damu ya Ibrahimu ambaye ni ndugu yake Lutu(Mwanzo 18:19) Agano linamsumbua Mungu anaamua kumjulisha tu Ibrahimu,na KWA NAFASI AMBAYO IBRAHIMU ALIKUWA NAYO MBELE ZA MUNGU HATA ANGESEMA WOTE MUNGU WASAMEHEWE MUNGU ANGESAMEHE NA ASINGEANGAMIZA MIJI ILE ANGELETA NAMNA NYINGINE YA WOKOVU KWA MIJI ILE.
Ibrahimu anashindwa kuitumia vizuri fursa ile mashaka mashaka yake na uoga wake anashindwa kujiamini,kifupi hapa Ibrahimu hakutambua nafasi aliyonayo mbele za Mungu aitumie vizuri,bado alikuwa wa mashaka mashaka maana alikuwa anamsihi Mungu asione hasira naye hakulielewa lile agano vyema na nafasi yake mpya,Yeye bado anaishi kiAbramu Abram, wakati yeye Mungu anamjua kama Ibrahimu kwa lugha ya kileo tunaweza kusema ameshakuwa bonge la mshikaji. Kumbe tukipewa fursa tuzitumie vizuri,tujitambue nafasi tulizonazo mbele za Mungu hasa yule aliyeamua kutembea na Mungu kwa ukamilifu.
Inaendelea.....
Aslam alyekum. Sifa njema ni zake Allah(s.w),Rehma na Amani zimfikie kiongozi wa umma Nabii Mohammad(s.a.w) na ahali zake na maswahaba zake.
Mshana Jr Quran ni kitabu cha haki kimeelezea kisa cha Nabii Lutt(a.s) na umma wake.Quran11:6-9
Kumbuka wageni wawili walipokuja kwa Nabii Ibrahim (a.s) wakati wa jioni walikaribishwa na Ibrahim akawaomba wajitambulishe wageni wakasema "Sisi ni wajumbe kutoka kwa M/Mungu tumetumwa kwa kaumu ya Lutt.Ibrahim akawaambia lakini kuna Lutt,Wajumbe wakasema tutamwokoa Lutt na ahali zake zake isipokuwa mke wake.Wajumbe wakasema" TUMETUMWA KWA KAUMU YA WAKOSEFU YA NABII LUTT KUWA HILIKI TUTAMWOKOA LUTT NA AHALI ZAKE ISIPOKUWA MKE WAKE TUNAKADILIA NI MWENYE KUBAKI NYUMA.Wajumbe walishasema kuwa mke wa Lutt hakuwa miongoni mwa waje wema Hivyo ange adhibiwa tu.
Kwani hata Wajumbe wale walipofika na Kaumu ya Lutt,Lutt alikuwa mnyonge sana kwa kuwa alijuwa tabia za Umma wake.Baada ya kufika wageni wale ndipo watu wake walikuja kwa Lutt mbiombio kuwafuta wageni wale.Lakini wageni wakamwambia Lutt usiwe na wasi wasi sisi tumetumwa na M/Mungu kuja kuwaangamiza Hivyo ondoka usiku na watu wako(walio mfwata Lutt) isipokuwa mke wako atakuwa miongoni mwa watakaoangamia.Kwa hiyo utaona kuwa hukumu ya mke wa Lutt ilikuwa imshatolewa zamani na M/Mungu ilikuwa bado utekelezaji tu.
My take;Hakukuwa na fumbo lolote Katika hukumu ya mke wa Lutt.Mshana kr
Inaendelea......
Katika mwanzo 19 tunaona Malaika wale wawili wanaingia katika mji wa Sodoma na Lutu alikuwa amekaa mlangoni mwa Sodoma akawaona na akaenda kuwalaki na kuinama hata kifudifudi akawakaribisha nyumbani mwake,tunakuja kuona yaliyoendelea pale watu wa mji ule wanawataka wale malaika,Lutu anawasihi sana na anakuwa tayari hata kuwatoa binti zake wawili ambao walikuwa bikra wafanywe na wale watu wa mji ule vyovyote vile watakavyo na si wale malaika, bado watu wa mji ule wakakataa mpaka malaika wakaingilia kati kwa kuwapofusha macho watu wale wakubwa kwa wadogo wakatafuta mlango wa Lutu hata wasiweze kuuona(Mwanzo 19:1-11) yaani kutembea nje ya kusudi ni mbaya sana nakaa nafasi ya Lutu inaumiza kiasi gani mzazi anakubali kutoa binti zake wafanywe vyovyote vile,ni uchungu mzito na maamuzi magumu sana,jamani tufanye maamuzi mazuri na tutembee njia nzuri tusijewapa gharama watoto wetu na vizazi vijavyo mambo ambayo hawakustahili kupata,kuyaona wala kuyasikia, inaumiza sanaa!!! ( Mungu turehemu tu).
Mungu wetu ni wa rehema bado katikati ya hukumu anatangaza rehema,anaamua kuiokoa nyumba yote ya Lutu na jamaa zake wote(Mwanzo 19:12). Lutu anajulishwa kinachoendelea na kitakachoendelea(Mstari wa 13). Katika mstari wa 12 tunaona Lutu alikuwa na nafasi kubwa sana ya kuwaokoa wengi maana anaambiwa..." na wowote ulionao katika mji uwatoe mahali hapa"....ilikuwa ni fursa kubwa sana ya kutoka na wengi katika mji huo lakini anashindwa kuiona fursa na anashindwa kuitumia vyema fursa hiyo,kwa rehema aliyopewa alikuwa na uwezo wa kuambukiza rehema hiyo kwa wengine,akaja akawafundisha mema watu wale ambao angetoka nao na kuanza upya na Bwana.
Mstari wa 14,Lutu anawakumbuka wakweze ambao walikuwa wamewaposa mabinti wale,lakini akawa kama achezaye machoni pa wakweze,Mhh!! Mara nyingu Mungu kabla hajaleta adhabu huwa anatujulisha na kutuonya lakini mara nyingi tumekuwa watu wa kupuuza tu na kudharau(rejea wakati wa Nuhu pia).
Katika Mstari wa 15 Lutu anaambiwa aondoke amtwae mke wake na binti zake wawili ili asipotee katika maovu ya mji huo, Mstari wa 16..Lutu akawia-kawia maana yake akawa anajivuta-vuta,anajichelewesha,kama vile bado haamini- amini,kama vile bado anaipenda penda bado sodoma ikabidi Malaika wale wawashike mkono Lutu,mkewe na binti zake wakamtoa kwa nguvu wakamweka nje ya mji ule kwa jinsi Bwana alivyokuwa anamuhurumia. KOSA LINGINE LUTU ANAFANYA BADO MOYO WA LUTU ULIKUWA SODOMA PAMOJA NA KUAMBIWA KILA KITU KINACHOENDELEA KATIKA MSTARI WA 13 BADO LUTU ALIJIVUTA- VUTA,HAKUWA TAYARI KUIACHIA KIRAHISI SODOMA,TENA ALIAMBIWA AONDOKE MWENYEWE LAKINI BADO HAKUTAKA MPAKA MALAIKA WANAAMUA KUMTOA KWA NGUVU, Mara nyingi nasi Mungu anatutaka tutoke kwenye maovu ila hatusikii tunamwambia bado bado Mungu subiri mimi ikifika uzee nitakuwa mtakatifu,au ndo nitakutumikia,au subiri Mungu kidogoo nifanye hili nitaacha uovu kabisa,NDUGU YANGU TUBADILIKE TUSIKIAPO SAUTI YA MUNGU TUSIFANYE MIOYO YETU MIGUMU.
Mstari wa 17 Lutu anapewa agizo ajiponye nafsi yake asitazame nyuma wala asisimame katika hilo bonde popote,ajiponye mlimani asije akapotea... Kumbuka ni Lutu aliyepewa agizo hili,ni Lutu aliyekuwa anajua nini kinaendelea toka mwanzo,ni Lutu aliyeambiwa katika mstari 13 kwamba mahali pale panaenda kuangamizwa,Ni Lutu ambaye ni kichwa cha Familia,Ni Lutu mwenyewe aliyejichagulia nchi ile,ni Lutu mwenyewe aliyeamua kutoka Uru pamoja na Ibrahimu,its all about Lutu,sijui Lutu alimtoa wapi huyu mke wake,nimejaribu kutafuta sijaona tufanye uchunguzi sote tujue mke wa Lutu alikuwa wa taifa gani? .....Je tujiulize mimi na wewe Lutu alisimama vyema katika nafasi yake?,hii inaumiza sana!! Turejee Edeni kwa Adamu (Mwanzo 2:16-17),Adamu naye ndiye aliyepewa agizo na Mungu ndiye aliyeumbwa kwanza,sijui alihakikisha jambo hili linatimilika vipi kwa mkewe Eva?,Lutu anafanya makosa ambayo Adamu aliyafanya.
WANAUME SIMAMENI KATIKA ZAMU ZENU,WANAUME NINYI NDIYO KICHWA CHA NYUMBA,NINYI NDIYO MLIOPEWA MAAGIZO NA MUNGU,MWANAUME AKIWA GIZA NI UWEZEKANO MKUBWA GIZA HILO LITAENDELEA KATIKA FAMILIA NZIMA,MWANAUME AKIKOSEA DUNIA YOTE IMEKOSEA,MWANAUME JITAMBUE UMEBEBA MAJUKUMU MAZITO,WANAUME MBONA MMEMPOTEZA LENGO NA KUSUDI MLILOKUWA MMEUMBIWA NALO(naandika nabubujikwa na machozi),LAITI MNGELIJUA NYIE NI KINA NANI? LAITI MNGELIJUA WAJIBU WENU?,LAITI MNGETAMBUA ILE NAFASI MLIYONAYO KWA MUNGU?,Ni rahisi sana leo kutoa shutuma za kila aina kwa mke wa Lutu kama ilivyo rahisi kutoa shutuma kwa Eva,sikatai wanawake tunamakosa yetu(hili nalo ni somo jingine),JE LUTU ALIHAKIKISHA VIPI HILI AGIZO LINAUKAMATA MOYO WA MKE WAKE,LINAPENYA VIPI KIASI HALIGEUZI MOYO WA MKE WAKE NA KUMRUDISHA NYUMA?....TUKUMBUKE MAKOSA YOTE YALIANZIA TOKA MWANZO NA LUTU MWENYEWE KISHA HATA KATIKA HATARI BADO LUTU ANALETA UZEMBE WA KUJICHELEWESHA-CHELEWESHA,ALISHAAMBIWA AONDOKE MWENYEWE LAKINI ANAJIVUTA VUTA TU MPAKA ANATOLEWA KWA NGUVU,HII NI HATARI KUBWA SANA!!.....KWA UZEMBE HUU ULITEGEMEA MKE WAKE NAYE AWE NI WA TOFAUTI? AISEEE VILE ULIVYO NDIYO NA MKE WAKO ALIVYO!! MWANAUME UNA WAJIBU/NAFASI KUBWA SANA WA KUMJENGA MKE WAKO AU KUMUANGAMIZA,MKE NI MSAIDIZI TU ANATAKIWA KUPOKEA MAELEKEZO KUTOKA KWAKO, KAZI KWAKO KUHAKIKISHA MAAGIZO YAKO YANATEKELEZWA......ASHUKURIWE MUNGU AMERUDISHA ILE MANHOOD YA MWANAUME KUPITIA YESU KRISTO,TENA ASHUKURIWE MUNGU AMEUMBA JAMBO JIPYA DUNIANI KWAMBA MWANAMKE ATAMLINDA MWANAUME(Yeremia 31:22).
Inaendelea....
Inaendelea...
"Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea. Lutu akawaambia, Sivyo, bwana wangu! Tazama, mtumwa wako ameona kibali machoni pako, nawe umezidisha rehema zako ulizonifanyia kwa kuponya nafsi yangu, nami siwezi kukimbilia mlimani nisipatwe na yale mabaya, nikafa. Basi mji huu u karibu, niukimbilie, nao ni mdogo, nijiponye sasa huko, sio mdogo huu? Na nafsi yangu itaishi. Akamwambia, Tazama, nimekukubali hata kwa neno hili, kwamba sitauangamiza mji huo uliounena. Hima, ujiponye huko, maana siwezi kufanya neno lo lote, hata uingiapo humo. Kwa hiyo jina la mji ule likaitwa Soari."
MWANZO. 19:17-22.
Tukiangalia mistari hiyo hapo juu Lutu bado anaendelea kufanya makosa, amepewa maagizo kwanza asitazame nyuma ili ajiponye nafsi yake,pili asisimame katika bonde hilo popote pale ajiponye nafsi yake aende milimani asije akapotea....ameshaambiwa wapi aende nini afanye lakini Lutu akakataa ushauri ule na kusema kwamba hataweza kukimbilia mlimani asipatwe na mabaya yale asije akafa,akachagua mji mdogo ulio jirani yake ambao ulikuwa kwenye plan ya kuangamizwa,akafanya makosa ya uchaguzi kama aliyofanya mwanzo lakini hapa anapata rehema anaambiwa amesikilizwa mji huo hautaangamizwa. Mungu wetu ni wa rehema huchukuliana nasi hata katika madhaifu tuliyonayo.
Mstari wa 23-26 tunaona Lutu akiwasiri Soari na ndipo miji ya sodoma na Gomora ilipoangamizwa,sijui Lutu alikuwa anasisitiza kiasi gani kwa familia yake walitii agizo hilo,sijui alikuwa akiwakumbusha familia yake namna gani yale waliyoambiwa kwamba Mungu anaenda kuangamiza miji ile?
Mstari wa 26 tunaona mkewe akigeuka nyuma na anageuka kuwa nguzo ya chumvi,nyuma tunaweza kutafsiri vyovyote vile tupendavyo au tunaonavyo na kama nilivyosema awali kila mtu anaweza kufunuliwa kama Bwana apendavyo na kwa ufahamu wake aweze kuelewa,kama ambavyo ilikuwa agizo kwa Adamu asile tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya(kumbuka kulikuwa na miti mingi pale ila katikati kulikuwa na mti wa uzima na mwingine wa ujuzi wa mema na mabaya,mti huu kila mtu anatafsiri vile apendavyo,na ndiyo hapo shetani alipomuweza mwanamke) "Agizo ni moja tu usigeuke nyuma ujiponye nafsi yako,Usile tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya maana utakapokula Hakika utakufa".....Je ni kwa namna gani tunatii maagizo ya Mungu anayotuagiza ni hilo tu ndo Mungu anataka,anasema utii ni bora kuliko sadaka( 1Samweli 15:22)...undani wa kile kitu wakati mwingine hauhitajiki kuujua mambo yote utayajua baada ta kutii,ndo hapa ambapo palimfurahisha Mungu hata kumuita Ibrahimu ni rafiki yake,kwanza alimtii kuondoka katika jamaa yake kwenda kusikojulikana,alitii kumtoa Isaka Sadaka hata hakutaka kujua maisha yangekuwaje bila ya Isaka,vipi ahadi za Mungu zingetimia baada ya Isaka kutolewa sadaka je ungekuwa mwisho wa uzao wake? ALITII TU KAMA BWANA ALIVYOMUAGIZA.
Tuendelee kujifunza kwa Lutu katika Mwanzo hiyo 19.....
Mstari wa 29 unatuthibitishia moja kwa moja Lutu na nyumba yake aliokolewa kwa neema tu ni kwasababu ya Ibrahim,agano la Ibrahimu na Mungu lilipiga kelele na ikawa neema hata kwa ndugu yake,kumbe sisi tukisimama imara tukatembea vizuri na Mungu tunakuwa sababu ya wengine kuponywa kupitia sisi.
Lutu anaendelea kufanya makosa tu, Mstari wa 30 anatoka Soari akakaa katika pango yeye na binti zake,tukumbuke katika mstari wa 20 yeye mwenyewe ndo aliomba akae katika mji huo na akapata kibali cha Mungu,halafu yeye mwenyewe tena anaogopa kukaa hapo anaenda tena mahali ambapo hapakuwa na kibali cha Mungu,hivi alitegemea angekuwa na mwisho mzuri? Mungu amemrehemu amemleta tena kwenye kusudi akakataa option ya Mungu kwenda mlimani ikawa siyo tatizo kwa Mungu,akajichagulia alipopataka akapewa baraka zote bado tena anapakimbia!!,naamini Lutu angeendelea kukaa Soari wokovu wa Bwana ungemtokea huko maana mahali pale palikuwa na kibali tayari cha Mungu.
Anakimbilia pangoni yeye na wanawe tu,hivi tujiulize tu kwa akili zetu ndogo nini kingeendelea tena pale? Kama si Lutu kuwabaka wanae basi ndo kama hivyo wanae wakambaka baba yao,tunajifunza kwamba mazingira nayo yanachangia sana haijalishi ni nini wala nini miili yetu ni dhaifu,tunashinda ni kwa neema ya Bwana,usiintatein(chochea) mazingira ya kutenda dhambi,usijitengenezeee nafasi ya kutenda dhambi,mara nyingi tunamsingizia shetani eti alinipitia,kweli umepita anga zake utegemee utoke salama kweli??? Tuache visingizio visivyo na maana!!!
Lutu hakuwa na mwisho mzuri yeye na uzao wake,uzao wake ukaja kuwa adui wakubwa wa Israel(Waamoni na Wamoabi)dhambi ya uzinzi na usaliti wa sheria za Mungu hakuwaacha,Katika yote haya yamemfikisha Lutu hapo alipokuwa ni sababu ya kutotembea katika kusudi lake,hata alipoletwa kwenye kusudi lake bado akashindwa,Inaumiza sana kupoteza mke uliyempenda,inaumiza sana kulala na watoto wako wa kuwazaa,inaumiza sana kuwa na kizazi chenye maovu. Inaumiza sana kuishi maisha ya kutanga tanga.
Mungu tusaidie tusahihishe makosa yetu,Mungu tusaidie tukuelewe pale unaposema nasi,Mungu tusaidie tulielewe kusudi la kuumbwa kwetu hapa duniani.Sisi peke yetu hatuwezi ila tunayaweza mambo yote katika wewe ututiaye nguvu,Katika Jina la Yesu tunarudi kwenye kusudi letu,Amina.
mshana jr asante sana kutumiwa na Mungu kuleta mada hii nimejifunza mengi,Umenifanya nami nijitafakari kwa upya safari yangu,Mungu amesema nasi sisi sote,ubarikiwe sana na Bwana azidi kukutumia na akufunulie siri nyingine nyingi ambazo macho hayakupata kuona,wala sikio halikupata kusikia wala hayakuwepo katika moyo wa mwanadamu yoyote yule.