Asante sana
mshana jr kutufikirisha haya.
Neno la Mungu ni jipya kila siku na ukitulia na Mungu vizuri kupitia Roho Mtakatifu utafunuliwa mambo ya ajabu ambayo hata ulimwengu haukuyajua wala sikio halikusikia wala macho hayakupata kuyaona. Na kazi ya Roho Mtakatifu ni kufumbua mafumbo ya Mungu( 1Wakoritho 2:9-11,Yohana 16:7-15,Yohana 14:17,26 N.B mambo ya Rohoni hutafsiriwa na Watu wa rohoni kama siyo wa rohoni huwezi yaelewa haya itakuwa upuuzi tu kwako).
Katika hili la mke wa Lutu yapo mambo mengi sana ya kujifunza ambayo kila mtu anaweza kufunuliwa kwa namna ya pekeyake kadri Mungu anavyotaka mtu huyo aelewe kwa lugha yake na kulingana na ufahamu wake. Yote yaliyosemwa humu yanaweza kuwa sahihi kadri kila mtu alivyofunuliwa kama Bwana na Roho yule yule apendavyo.
Mimi kwangu nataka tujifikirishe kidogo kosa lilianzia wapi mpaka haya yote yakatokea,Lutu alikosea wapi,au alianzia wapi? Napenda tujifunze zaidi chanzo ambacho tukikijua wote hatutafanya makosa kama aliyofanya Lutu.
Tukisoma Mwanzo 12 tunakutana na Habari ya Lutu na Abram,ila tukianzia Mlango wa 11 utajifunza kuanzia kizazi cha Abram kilitoka wapi hadi ule mstari wa 24 tunaona baba yake Abram anazaliwa ambaye ni Tera,halafu mstari wa 27 tunaona Abram na Lutu wanatokea. Sasa basi katika Hiyo Mwanzo 12 tunaona Abram anaambiwa na Mungu atoke yeye katika jamaa yake na nyumba ya baba yake na Mungu anampa ahadi ya kuwa taifa na uzao mkubwa. Mstari wa 4 tunaona Abram anatii lakini Lutu akaondoka pamoja naye(hapa pana somo la kujifunza sijui Lutu alilia/alijiamuria tu kuondoka na Abram au sijui Abram aliamua kumbeba???) Makosa pia yalianzia hapa.... usidandie baraka za mtu funuliwa na wewe vyako uvikamatie,usiige vya mtu,Abram aliitwa yeye kama yeye na Mungu alimtaka yeye peke yake atoke so Lutu anaanzia hapa Kufanya makosa,anatembea katika njia ambayo si yake,anatembea katika kusudi ambalo si lake,anatembea katika njia ya mtu mwingine,Je ulikuwa ni mpango wa Mungu Lutu aende na Abram,Lutu hakujikubali yeye kama yeye,alitakiwa amuulize Mungu na yeye aende na Abram au aendelee kubaki na Tera, Mungu alikuwa na Great mission na Abram siyo Lutu,Lutu angetafuta na yeye kwa Mungu mission yake ni ipi?.... (MUNGU ROHO MTAKATIFU AWASAIDIE MUELEWE HILI.).........Kwahiyo kuanzia hapa Lutu anakosea so hope hata destinity(mwisho) wake hauwi mzuri,ANGALIA SANA USITOKE KATIKA KUSUDI LA MUNGU ALILOKUKUSUDIA WEWE HAPA DUNIANI, UTAHARIBU SYSTEM NZIMA YA MAISHA YAKO( Bwana uturehemu tusahihushe makosa yetu).
Mwanzo 13 tunaona jinsi walivyobarikiwa na Bwana,Ukitembea na mpakwa mafuta wa Bwana hutabaki wa kawaida,kwahiyo wote wawili wanakuwa na mali nyingi isiyotosha ardhi kiasi kwamba ugomvi unatokea kati ya wafanyakazi wa Lutu na Abram,Abram anamwambia Ndugu yake Lutu usiwepo ugomvi kati yao,achague upande ambao ataona unafaa,akienda kulia Abram ataenda kushoto,akienda kushoto yeye ataenda kulia n.k(Hapa ulikuwa mtego mkubwa kwa Lutu)
"Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla BWANA hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya BWANA, kama nchi ya Misri hapo unapokwenda Soari. Basi Lutu akajichagulia Bonde lote la Yordani; Lutu akasafiri kwenda upande wa mashariki; wakatengana wao kwa wao."
MWANZO. 13:10-11
KOSA LA PILI LUTU ANAFANYA,AKACHAGUA SEHEMU AMBAYO KWA MACHO YAKE ALIIONA NI NZURI YA KUPENDEZA NA KUFURAHISHA MOYO(Rejea Edeni Eva aliona tunda ni zuri lapendeza macho sana na lafaa kwa kuliwa watamanika kwa maarifa Mwanzo 3:6) tunajifunza nini basi? Hata waswahili husema "si kila king'aacho ni dhahabu" fikiri sana kabla ya kutenda kwa yale unayoyaona,tamaa huanza katika macho,kisha wazo(akili na moyo) kisha dhambi huzaliwa. Tunajifunza kwamba kabla ya kila jambo tumshirikishe Mungu hata katika yale ambayo mioyo yetu ingependa macho yetu yangetamani,ipo njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu lakini mwisho wake ni mauti na kuangamia( Mithali 14:12,) Tunapaswa kulinda moyo maana moyo ni mdanganyifu( Mithali 4:23, Yeremia 17:9) , Ukimkabidhi Bwana atanyoosha mapito na njia yako(Mithali 3:5-7).
Laiti Lutu angeyajua haya asingefanya kosa la Pili kwenda kukaa katika nchi ya uovu ambayo inakuwa ni hasara moja kwa moja kwake na familia yake anaharibu mfumo mzima wa maisha yake,katoka nje ya kusudi lake,Mke anampoteza,Watoto wake wanamnywesha kilevi wanalala na baba yao laana moja kwa moja inaendelea kuyaandama maisha yake na kizazi chake.
Halafu sasa mikosi haikuanzia hapo soma Mwanzo 14:8-16,Kunatokea vita kati ya mfalme wa Sodoma,Gomora ,Adma,Seboimu na mfalme wa Bela mwisho Wafalme wa Sodoma na Gomora wanashindwa hatimaye miji ile inatekwa na Lutu naye anatekwa na mali yake yote kisha mtu anampasha Abramu habari kuwa ndugu yake katekwa,Abram anatoka usiku wa manane anaenda kumpigania ndugu yake na akamkomboa yeye na mali yake yote,basi hapa PANGEMFIKIRISHA TENA LUTU JE YUPO MAHALI SAHIHI?? (MUNGU SIYO DIKTETA AMETUPA AKILI YATUPASA TUZIFIKIRISHE NA TUKIMUOMBA ANAJIBU ANATUONESHA (Yeremia 33:3).
Inaendelea.........