Waziri Gwajima: Kuna haja ya kuweka mfumo maalumu wa kuwatambua "Beach Boys" maeneo ya Fukwe

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,120
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk Doroth Gwajima amesema kuna haja ya kuweka mfumo maalumu katika fukwe ili huduma zinazotolewa kutambulika na watu wanaotoa huduma pia kutambulika lengo ni kuepuka watu matapeli ambao wanafanya ukatili.

Dk Gwajima ameeleza hayo wakati alipofanya ziara katika fukwe za Coco na Kawe ili kujadiliana na watoa huduma za kuogelea (Beach boy) ikiwa ni hatua za kukomesha vitendo vya ubakaji kwa wasichana, vinavyofanywa na watu wachache wasiowaaminifu.

"Nilichoona hapa ni kuwa hawa vijana wanahitaji kuweka mifumo maalum ya watu kujua huduma wanazotoa na nimewaagiza watoe matangazo na vipeperushi vya huduma ili wanaokuja hapa wasikutane na matapeli kwani hii inachafua taswira yenu,” amesema Gwajima

Hongera GENTAMYCINE kwa ushauri wako umepokelewa

Soma:
- Waziri Dkt. Gwajima, fanya yafuatayo ili kuwakomesha wahuni (beach boys) wote katika fukwe zetu za Dar es Salaam

Source: EastAfricaTV
 
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk Doroth Gwajima amesema kuna haja ya kuweka mfumo maalumu katika fukwe ili huduma zinazotolewa kutambulika na watu wanaotoa huduma pia kutambulika lengo ni kuepuka watu matapeli ambao wanafanya ukatili...
Asante kwa Taarifa Mkuu. Tuko pamoja.
 
Nchi zingine kuna beach patrols,

Sisi tuna police marine, tuna jeshi la wanamaji (Nevy patrol) tukae na police Blue Nevy zimamoto na jiji tuone namna gani tuweze kusimamia fukwe zetu.

Tuufufue ule mpango wa kuikodisha coco beach kama jiji lilivyotaka kumkodishia yusuf Manji

Pia tutangaze tenda ya beach patrol na marine rescue team.

Huku kwetu beach za wamama na wababa ziko tofauti pia wabibi na wajawazito walikuwa na fukwe zao, sasa nyie dar usijekuta kibinti kinasaula mbele ya wazazi wake kisa wako beach
 
"Nilichoona hapa ni kuwa hawa vijana wanahitaji kuweka mifumo maalum ya watu kujua huduma wanazotoa na nimewaagiza watoe matangazo na vipeperushi vya huduma ili wanaokuja hapa wasikutane na matapeli kwani hii inachafua taswira yenu,” amesema Gwajima

Kwa hiyo kwa kutamka tu hivyo ndio mheshimiwa kakomesha tatizo sio !!!

🤔🤔🤔
 
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk Doroth Gwajima amesema kuna haja ya kuweka mfumo maalumu katika fukwe ili huduma zinazotolewa kutambulika na watu wanaotoa huduma pia kutambulika lengo ni kuepuka watu matapeli ambao wanafanya ukatili.

Dk Gwajima ameeleza hayo wakati alipofanya ziara katika fukwe za Coco na Kawe ili kujadiliana na watoa huduma za kuogelea (Beach boy) ikiwa ni hatua za kukomesha vitendo vya ubakaji kwa wasichana, vinavyofanywa na watu wachache wasiowaaminifu.

"Nilichoona hapa ni kuwa hawa vijana wanahitaji kuweka mifumo maalum ya watu kujua huduma wanazotoa na nimewaagiza watoe matangazo na vipeperushi vya huduma ili wanaokuja hapa wasikutane na matapeli kwani hii inachafua taswira yenu,” amesema Gwajima

Hongera GENTAMYCINE kwa ushauri wako umepokelewa

Soma:
- Waziri Dkt. Gwajima, fanya yafuatayo ili kuwakomesha wahuni (beach boys) wote katika fukwe zetu za Dar es Salaam

Source: EastAfricaTV
Ila huyu mheshimiwa anaweza kutoa agizo na asifatile

Tunamjua khaswa

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Nchi zingine kuna beach patrols,

Sisi tuna police marine, tuna jeshi la wanamaji (Nevy patrol) tukae na police Blue Nevy zimamoto na jiji tuone namna gani tuweze kusimamia fukwe zetu.

Tuufufue ule mpango wa kuikodisha coco beach kama jiji lilivyotaka kumkodishia yusuf Manji

Pia tutangaze tenda ya beach patrol na marine rescue team.

Huku kwetu beach za wamama na wababa ziko tofauti pia wabibi na wajawazito walikuwa na fukwe zao, sasa nyie dar usijekuta kibinti kinasaula mbele ya wazazi wake kisa wako beach
Uko wapi mkuu?
 
Kama nchi tuna tatizo kubwa zaidi, Tanzania haina mfumo wa kuwatambua raia wake, nchi ilitakiwa tuwe na ID za kidigitali,mzazi anamtambua mtoto wake kwa kumpa jina,je serikali yetu inawatambua raia wake kivipi?,faida ya ID hizi ni pamoja na kuweka kumbukumbu za raia, mbakaji, mkatili wa GBV akishakuwa blacklisted kwenye systems, kote anakokwenda anatambulika,sio sasa nafanya ukatili pale CoCo beach, kesho nahamia kigamboni beach kuendeleza ukatili ule, tuanze upya kama nchi, tutambuane
 
Beach boys wapigwe marufuku sehem zote za Bahari,,
Wawepo rescue guards tu pamoja na kuwa security (police) ambao wataangalia usalama wa raia na Mali zao.

Mambo ya kujifunza kuogelea yawepo swimming pools..

Sijawahi kuona popote dunia Kuna beach boys wanafundisha watu kuogelea..
 
Simple and clear
 
Back
Top Bottom