FT: Singida Fountain Gate 1 - 2 Simba SC | NBC Premier League | CCM Liti Singida | Oktoba 8, 2023

uran

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
7,580
10,814
Match Day
📅 October 8, 2023.
⚽ NBC Premier League
Singida Fountain Gate vs Simba Sc
🏟️ CCM Liti, Singida.
⏰ 4:00Pm.

Haya, kumekucha vyema.
Baada ya michezo ya jana ya ligi kuu Tanzania Bara kupigwa,

Tukishuhudia Yanga kutoa kipigo kwa Geita Gold cha 3-0
Huku Ihefu akizamishwa na KMC kwa 1 - 0
Leo ni zamu ya Wanasingida (Singida Fountain Gate dhidi ya Simba Sports Club ya Dar es salaam.
Mchezo utapigwa mida ya saa kumi jioni.
Viva Simba, Viva Mnyama.
Tutarudi kileleni kwa kishindo.

20231008_150352.jpg
Kikosi cha Simba kinachoanza.
20231008_155930.jpg

Kikosi cha Simba kinachoanza.
Mchezo umeanza
'5 Timu zinaendelea kusomana taratibu
10' Simba wanfanya mashambulizi makali langoni mwa Singida
15' Kipa wa Singida, Beno Kakolanya anaonesha ubora wa kushomoa mashuti kadhaa
26' Gooooooooooooooooooooo
Simba wanaongoza goli 1-0, Siido kafunga kwa shuti kali akimalizia pasi ya Kibu Denis
40' Timu zinapeana zamu kumiliki mpira
41' Beki wa Simba, Shomari Kapombe anaokoa hatari langoni kwake
45' Zinaongezwa Dakika 3 za nyongeza
MAPUMZIKO
F76-4PyXkAAUcLS.jpeg
Kipindi cha pili kimeanza
45' Mabadiliko kwa Simba anatoka John Bocco anaingia Moses Phiri
47' Singida wanapata faulo, inapigwa inatoka nje
50' Singida wanafanya mashambulizi makali langoni kwa Simba
Gooooooooooooooooo!
51' Kaseka anasawazisha
53' Simba wameanza kwa kasi ya chini
80’ Simba wanapata faulo karibu na lango la Singida, anapiga Luis inaokolewa
82’ Gooooooooooooooooooooooooo
Moses Phiri anafunga goli la pili kwa Simba
85' Luis anapata nafasi akiwa na kipa ashindwa kufunga
90' Zinaongezwa dakika 4 za nyongeza
FULL TIME
 
Singida hana ubavu wa kumzuia Simba wa Teranga asiungurume huko kwao.
Vijana wana njaa ya kucheza kikosi cha kwanza cha CAF Poti ya pili.
 
Back
Top Bottom