FT: Tanzania 0-1 Uganda | AFCON Qualifier | Benjamin Mkapa Stadium | 28.03.2023

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,714
45,103
Majira ya Saa 2:00 Usiku kwa Masaa ya Afrika ya Mashariki, Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itashuka dimbani Benjamin Mkapa kuwaalika Uganda (The Cranes) katika mchezo wa nne wa kundi F kuelekea kufuzu Afcon mwaka 2023..

Taifa Stars yenye point 4 iliyopo nafasi ya pili nyuma ya vinara Algeria ambao washafuzu itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu yakuibuka na ushindi wa 1-0 siku chache zilizopita.

Taifa Stars ikishinda itafikisha alama 7 na kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa mashindano hayo makubwa na adhimu kwa bara la Afrika kwa mara ya 3 katika historia ya mashindano hayo.

Tujitokeze kwa wingi tushangilie timu yetu ya Taifa, hatuna timu nyingine jamani.

Mechi itakuwa mubashara AzamtV, Dstv kupitia chaneli 225 ya kifurushi cha POA.

Kila la heri Taifa Stars!
Kila la heri Tanzania!!!
 
Nahodha wa Uganda, Emanuel Okwi mwenye miaka 30 anasema wana uhakika wataibuka na alama 3 na kufufua matumaini ya The Cranes kufuzu.
B478AD50-455B-49B7-80E7-F324BBF4A133.jpeg
 
Majira ya Saa 2:00 Usiku kwa Masaa ya Afrika ya Mashariki, Timu ya Taifa ya Tanzania ( Taifa Stars ) itashuka dimbani Benjamin Mkapa kuwaalika Uganda ( The Cranes ) katika mchezo wa nne wa kundi F kuelekea kufuzu Afcon mwaka 2023..

Taifa Stars yenye point 4 iliyopo nafasi ya pili nyuma ya vinara Algeria ambao washafuzu itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu yakuibuka na ushindi wa 1-0 siku chache zilizopita.

Taifa Stars ikishinda itafikisha alama 7 na kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa mashindano hayo makubwa na adhimu kwa bara la Afrika kwa mara ya 3 katika historia ya mashindano hayo.

Tujitokeze kwa wingi tushangilie timu yetu ya Taifa, hatuna timu nyingine jamani.

Mechi itakuwa mubashara AzamtV, Dstv kupitia chaneli 225 ya kifurushi cha POA.

Kila la heri Taifa Stars!
Kila la heri Tanzania!!!
Asante Kwa uzi mkuu
 
Back
Top Bottom