Freeman Mbowe, tueleze CHADEMA mlipompeleka Ben Saanane

Freeman Mbowe, tueleze CHADEMA mlipompeleka Ben Saanane

Mbowe anaendesha kikao Mwanza, Lowasa yuko sijui Geita, Tundu lisu ndo hata habari hana yuko kwenye redio za Wazungu kumsema Raisi wetu, wakti huo huo B.Saanane amepotea kwa miezi 2 sasa, hili linawezekana vipi? Yaani Mbowe afanye kikao Mwanza kuongelea kuhusu Lowasa na siyo B.Saanane?
Serikali ndio yenye jukumu la kulinda raia na mali zao. Mpaka leo hii kama unavyosema hakuna kauli ya serikali inayoeleza imefikia wapi katika kumtafuta Ben. Mpaka leo hii hakuna taarifa ya kutafutwa kwake. Mpaka leo hii sijasikia Jeshi la polisi limefika wapi katika uchunguzi wa kadhia ya kupotea (kutekwa, kufichwa, kuuawa) au kushikiliwa na vyombo vya dola unaohusiana na Ben.

Ni jukumu la serikali kutoa taarifa kuhusu Ben.
 
RkiK4XLcj.jpg
Ben Saa8. Wenzako wanapiga misele tu,wamekuwa watabiri (ghafla)wa hali ya hewa.
 
Mkuu,mtu alishatumiwa msg za vitisho kwamba atakuja kujikuta peke yake na chatu,we bado unaamini yupo hai? Ukute alishaliwa na chatu tayari
 
Hata ndugu na wazee wake sasa wapo kimya.

Wameshamfanyia arubaini?
 
Familia ifanye HITIMA ili tujue kuwa kweli hawana mawasiliano,tumuombee dua huko aliko.
 
Hata ndugu na wazee wake sasa wapo kimya.

Wameshamfanyia arubaini?
Mbowe ni hatari sana...hata Lissu ameshindwa kuhoji kauli yake ya kusema hatoweza kuongea kwani anaweza kuwaakera watekaji...sasa sijui Mbowe alijuaje kama Ben ametekwa?
 
CDM LIKIKUPATA LOLOTE BAYA HATA KAMA ULIKUWA MPIGANAJI WAO WANAKUSAHAU FASTA. HUYO NDIYO MBOWE NA CDM YAKE
 
Ndio basi tena Ben story yake imepoteza mvuto agenda kubwa ya Chadema kwa sasa ni baa la njama nchini
 
Stori ya Ben imepitwa na Wakati agenda kubwa ya Chadema kwa sasa ni baa la njaa
 
Mbowe anaendesha kikao Mwanza, Lowasa yuko sijui Geita, Tundu lisu ndo hata habari hana yuko kwenye redio za Wazungu kumsema Raisi wetu, wakti huo huo B.Saanane amepotea kwa miezi 2 sasa, hili linawezekana vipi? Yaani Mbowe afanye kikao Mwanza kuongelea kuhusu Lowasa na siyo B.Saanane?
Hivi huwa una akili timamu kweli wewe boya?
Ulitaka Lowassa, Mbowe, Tundu Lissu na CHADEMA yote wafanyeje kuhusu kupotea Kwa Ben?
Hujui kuwa kuna serikali yenye jukumu la kulinda uhai wa raia wote pamoja na kujua Ben alipo?
Wewe ni mhaini unachochea uasi dhidi ya serikali takatifu halali, unataka Mbowe aanzishe serikali yake ndani ya Jamhuri ya muungano Wa Tanzania ambayo ndo itabeba jukumu la kumtafuta Ben?
Wewe jamaa huwa unakera kuliko kinyesi kibichi.
 
Mbowe anaendesha kikao Mwanza, Lowasa yuko sijui Geita, Tundu lisu ndo hata habari hana yuko kwenye redio za Wazungu kumsema Raisi wetu, wakti huo huo B.Saanane amepotea kwa miezi 2 sasa, hili linawezekana vipi? Yaani Mbowe afanye kikao Mwanza kuongelea kuhusu Lowasa na siyo B.Saanane?
Ndugu zangu, hapa kuna link siielewi sana. Kwanini kupatikana kwa Ben tunakuelekeza kuwa ni Wajibu wa hiyo Chadema siyo Polisi?
 
Isije kuwa huyu Ben kabambwa na bwimbwi na chadema wanaona haya kuleta hizo habari, maana kuwa msaidizi wa Mbowe kuna mambo mengi sana na kuwa punda wala sishangai.

Kazi za kuuza wanawake na kuendesha vilabu vya usiku ni za kishetani sana imagine boss wake yupoje?
 
Ndugu zangu, hapa kuna link siielewi sana. Kwanini kupatikana kwa Ben tunakuelekeza kuwa ni Wajibu wa hiyo Chadema siyo Polisi?


Sijaongelea upatikanaji wa Saanane na wala nani anapaswa kumtafuta, weka mambo ya kiserikali na kisheria pembeni na turudi kwenye ubinadamu ndicho nilichokiongelea, kwamba haingii akilini mtu ambaye amefanya kazi kwenye Chama kwa muda na mtu mwenye cheo kikubwa chamani apotee kwa mazingira ya kutatanisha zaidi ya miezi 2 halafu hakuna chochote, hatusikii chochote watu wanaendelea na shughuli zao kana kwamba hakuna kilichotokea, hapo ndipo ninaposhindwa kuelewa, kwani hata kama ni jukumu la Serikali kumtafuta miezi 2 hakuna jibu ktk kwa Serikali kwa hali ya kawaida nilitegemea shinikizo kubwa ktk chadema kwa Serikali, mbona mambo mengine kama njaa hotuba za Raisi kukamatwa kwa lowasa chadema wanaongela kila siku? Mbona Tundu Lisu mpaka ankwenda kwenye redio za Wazungu kuongelea njaa an hotuba za Raisi kwa nini pia hakuongelea kupotea kwa mwenzao?
 
CHADEMA wako smart. Wanamfahamu mwenye nguvu aishie gizani anayefanya uhalifu wa aina hii, wa kuteka, kuua, kuwatia kwenye viroba binadamu na kuwatupa. Kwa hali ilivyo kungekuwa na hata chembe ya shuku juu ya uhusiano wa CHADEMA au ingekuwa watawala wangekuwa kweli hawajui Ben aliko CHADEMA kusingelalika, pengine hata chama kingefutwa!
Polisi wanamgwaya "mgomvi" wa Ben, aliyekuwa akikosolewa na aliyebanwa na huyo kijana mzalendo aliyekutana wenye nguvu wa gizani, wachawi wakubwa wanaojifanya wacha Mungu!
Serikali ingependa Ben au yoyote aliyempoteza angepatikana ndani ya wiki moja, jiulize nani anawazuia Polisi, TCRA kusema ni nani aliyewasiliana naye mara ya mwisho na ilikuwa wapi? Na Emmanuel Joseph aliyemtumia jumbe za vitisho alikamatwa? Yuko wapi na anafanya kazi gani ya kulipwa na nani? Kwa mfano huyu Emmanuel angehusika kutuma ujumbe wa kitisho dhidi ya mamlaka angekuwa huru hadi leo?
Uhalifu ni kuua au kuhujumu maisha ya wana CCM au vibaraka wao, utatafutwa popote na hapo utaona jinsi Polisi "wanavyojua" kazi, Ila uhalifu unapofanywa dhidi ya raia wa daraja la Pili; (ndiyo wapinzani) kesi itavutwa miezi, miaka hadi kupotea!
Si mnaona "ujambazi" wa Lipumba akishirikiana na dola kukwapua mamilioni ya CUF kwa kesi iliyo wazi na inayoweza sikilizwa hata na hakimu wa ngazi ya cheti na kumalizwa kwa siku moja tu na ambayo sasa inavutwa vutwa taratibu ili vibaka wanaomfadhili wanufaike na hivi kuwakomoa raia wa daraja la Pili?
Mliokuwa mkiwadhihaki Uganda kuwa na Iddi Amin rudini kutubu maana uzoefu umedhihirisha Iddi Amin ni mtakatifu mbele ya nduli tuliozalisha kumbe Tanzania inaweza zalisha Nduli zaidi yake kwa mamia kupitia. CCM!
 
Acha uboya wewe kwani kwa hiyo kama Ben hajapoteza na Chadema ndio walizike tu wakae kimya, wanatoa wapi nguvu za kuendelea na mikutano yao ili hali mtu wao wa karibu kabisa hajulikani alipo
Sasa wafanyeje?we ni kilaza.baada utilize dola yenye vyombo vya kiuchunguz na kiintelijensia.
 
Kwani wapi ilitangazwa kwamba Ben amepotezwa na Chadema??

Kama huna hoja sio lazima kuanzisha thread hapa.
Hata kama angekuwa hajapotezwa na chadema, bado ni mtu wenu, viongozi wenu hawafanyi sawa kuendelea na maisha as if hawajapotelewa na mtu muhimu kama Saanane. Kuna kitu mnaficha ndio maana akitokea mtu kukumbushia suala hilo mnatokwa mapovu mengi na mishipa ya shingo inawasimama
 
Thanks best kwa kumuona huyu
View attachment 461012
Amesahau dhulma walizokwisha wafanyia na kuwafanya wapinzani wao kimtizamo waziishi kwa miaka nenda rudi (ni kumbumbu mbaya kwa kweli)ambazo kwao wao wanaona wapinzani yawastahil kuziishi.
Ajifanya punguani hajui hata wa kuwauliza "kimya hiki cha Mpendwa Ben",huku moyoni akifurahia na kutamani damu zaidi kumwagika kisa neno 'mpinzani'.
~~~NA KAMA KWELI WAMEMTANGULIZA KAMA WALIVYOWATANGULIZA MAWAZO NA WENGINEO "AMIN,AMIN,AMIN DAMU HIZO ZA KILIO CHA HAKI HAZITAENDA BURE KATU ASLAN".
View attachment 461029
Weka akiba ya maneno
 
Back
Top Bottom