Freeman Mbowe, kwanini maridhiano sasa?

Freeman Mbowe, kwanini maridhiano sasa?

In politics muda bado Sana Kabla ya October 2020 kubadilisha mind za watanzania kuamini Nini mbowe anakisudia. Km approach yake itashindwa atarudi na muda Ni mwingi sn. Siasa za Tanzania Ni cheap Kwasababu ya kuwa na mtaji mkubwa wa wananchi ambao hawana elimu ya uraia, kuwashawishi haihitaji nguvu Sana.
 
Maridhiano juu ya nini? Sema Chadema imenyoosha mikono. Imeushindwa muziki wa Jiwe sasa wanaomba poo kiaina, eti maridhiano. Na vijana wa Chadema mliojana humu mmeshupalia maridhiano, maridhiano! Yapi? Ninyi si mna msemo "mpaka kieleweke"? Vipi sasa kubembeleza maeidhiano!!!?
Hujitambui Hadi Sasa? Ninyi mapanyabuku ya lumumba hakika hampendi amani na mnaomba kila dk, ipitayo kisanuke mpore kilichobakia! Bado mpo na akili za kale Sana huku mkiea hamjui dhima halisi ya kucompromise badala ya confrontation mnayoililia itokee!
Magu, shtuka! Hao ccm wenzako hawana Nia njema na amani ya nchi!
 
Mkuu kama umeusoma uzi wangu nimeligusia hilo na nimeepeza pia wasiwasi wangu kwamba Kama mkandamizaji ana chuki binafsi alitaka kukukomoa sawa anaweza kuingia kwa maridhiano lau si hivyo hawezi acha kwakua lake halijatimia.

Uko sahihi kabisa. Lakini nchi siyo mali ya mtu mmoja wala kikundi kidogo cha watu. Ushindani wa kisiasa unayo misingi yake iliyokubalika duniani kote. Tangu nchi hii iingie kwenye mfumo wa vyama vingi imekuwa ikijaribu kuheshimu misingi hiyo na ndiyo maana idadi ya wawakilishi kutoka upinzani imekuwa ikiongezeka kila uchaguzi unapofanyika. Mtu anayekerwa na hali hiyo hafai kuwa kiongozi. Kama kwa bahati mbaya amepata uongozi lazima utafika wakati ataambiwa kuwa huo mchezo wake mbaya ni mauti kwa taifa na haukubaliki. Nadhani uchaguzi wa serikali za mitaa umetufikisha hapo.
 
Ni bahati mbaya sana watu hawajadili hoja iliyotolewa na Chadema (kupitia mdomo wa Mbowe) na wanamjadili Mbowe kama vile hoja ile ni yake katika nayo nyumbani au anatabia kama za Magufuli kutoa kauli za kisera tokea kichwani mwake bila ridhaa ya chama.
Nchi kwa wale walioitembelea na kuifahamu vyema ni kuwa imekwisha bomoka bado kidogo tuu migogoro chungu nzima itaibuka kila upande hasa baada ya uchaguzi wa SM.
Watu waliochomekewa viongozi huko vijijini wana uelewa na kimeanza kuwaka maeneo mbalimbali kuwakataa.View attachment 1287773
Nchi ilibomoka wakati Mbowe juzi ameziba nyufa zote zilisababishwa na Magufuli... Magufuli anawaangalia tu kwenye tv mlivyojichanganya.
 
Mkuu umeongea vema.
Mbowe na wanao mpondea hili wazo lake la maridhiano nawafananisha Luther King Jr na Malcolm X.
Mbowe ni kama Luther King Jr na wakosoaji wake ni kundi la Malcolm X.

Wakati fulani lazima utumie njia za kidiplomasia zaidi kulingana na mazingira ya vita na aina ya adui wako na nyenzo zake.
Nasimama na Mbowe, maridhiano sio kushindwa vita.
Wakutafuta maridhiano alikuwa ni Magufuli alievuruga mfumo wa uchaguzi.
 
Sexless, Miguna miguna yuko Canada alijaribu kurudi Kenya akaishia uwanja wa Ndege kwa kubebwa mzobemzobe.

wakati Odinga akigongeana glass na Kenyata.

Lissu Juzi amejaribu kurudi, baada ya kufika Kenya akaona upepo unasoma vibaya akageuzia huko huko.

Huku Mbowe akifanya maridhiano na Serikali ya CCM.
 
Watanzania tufanye kazi kwa manufaa ya familia zetu, we are too young to deal with this dirty games ( politics)..

Hakuna wanasiasa hapa tuna watu njaa wapo kwa maslahi yao na familia zao..

RIP Mawazo, RIP Wangwe nk,Pole sana LISSU hamkujua masikini mmevamia michezo msioijua undani wake dah inasikitisha sana maana mngalijua mngekuwa mnafanya kazi zenu na familia zenu zingeenjoy maisha..

Narudia tena, Watanzania fanyeni kazi achaneni na hawa watu aka wachezaji wa hizi dirty games maana wapo kwa ajili circles zao na si vinginevyo..
 
Wakutafuta maridhiano alikuwa ni Magufuli alievuruga mfumo wa uchaguzi.
Naheshimu mawazo yako.
Nafikiri kuna wakati busara ni kuangalia mpinzani wako ni mtu wa aina gani.
Kama wewe unaumizwa na hali ya mpasuko na unawapenda watu wako basi una 'sacrifice your ego' na kujaribu kumbadili msimamo mshindani wako kwa kujishusha..
Wakati flani humility huweza kumfanya mshindani wako alainike kiasi cha kukupa zaidi ya kile ulicho kuwa unadai.

Uongozi ni kitu kigumu sana, na mzigo mzito. Ukiweka mashindano kila wakati sababu ya pride au self esteem ni hatari.
 
Hujitambui Hadi Sasa? Ninyi mapanyabuku ya lumumba hakika hampendi amani na mnaomba kila dk, ipitayo kisanuke mpore kilichobakia! Bado mpo na akili za kale Sana huku mkiea hamjui dhima halisi ya kucompromise badala ya confrontation mnayoililia itokee!
Magu, shtuka! Hao ccm wenzako hawana Nia njema na amani ya nchi!
Nimeuliza swali; maridhiano kuhusu nini? Unataka kitu ambacho huwezi kukielezea?
 
Usipotoshe nia nzuri ya Mbowe

Maridhiano ndiyo njia pekee ya kistaarabu kufikia maelewano

Ngoja nikuulize swali dogo tu, hivi kina Mandela walifkia maridhiano Afrika Kusini, kuna mtu alilaumu uamuzi huo??

Hivi Uhuru Kenyatta wa Kenya kufanya maridhiano na Odinga, kuna watu wanalaumu??

Unapoweka nchi mbele zaidi ya ubinafsi, unaweza ukafikia maridhiano, lakini unaooweka ubinafsi mbele ni lazima hutapendekeza yafikiwe maridhiano

Kwa hiyo wapinzani wa nchi hii wanalazimika kumpongeza Mbowe, kwa kuamwambia Rais Magufuli kuwa wao upinzani wako tayari kwa maridhiano..........

Kwa hiyo kazi kwake yeye Rais Magufuli, kama ataweka mbele.maslahi ya Taifa, ataridhia ombi hilo la Mbowe na kama ataweka mbele maslahi binafsi yake yeye mwenyewe binafsi, atayakataa
Kaka kuonewa nionewe Mimi na MARIDHIANO niombe Mimi, unajua maana yake mkuu UMENISHINDA unaweka nukta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua kabla Miguna Miguna hajawa kambi ya Raila ule uchaguzi ambao Raila alikuwa anashiriki kama waziri mkuu mstaafu Miguna alikuwa anamchukilia vipi? Emb fuatilia kisha ujue tofauti zilizopo.."Come baby come..I have all things right here..." Unajua huo msemo ulitoka wapi? Uwe unafuatilia kwanza kabla ya kulipuka!
"hivi hamjaelewa tu kwamba mambo yamebadilika"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu fanyeni hata tafiti kidogo ndipo mtagundua appearance ya KUB kwenye sherehe za uhuru ni maazimio yaliyopitishwa na kamati kuu ya Chadema na sio maamuzi binafsi ya Kamanda Mbowe na taarifa ya kamati kuu ipo ilisambazwa.
Zijazungumzia Aikael kama mtoto wa Mbowe nimezungumzia Aikael Mwenyekiti wa Chama kikuu cha UPINZANI Ndegelec.

CCM wakivurunda Magufuli kama Mwenyekiti wa Chama hawezi kimbia lawama, hivyo sasa rudi kwenye hoja ya msingi FREEMAN MBOWE KWANINI SASA?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom