Freeman Mbowe, kwanini maridhiano sasa?

Cherenganya

JF-Expert Member
Jan 21, 2018
2,309
1,775
Wananzengo habari zenu.

Takribani saa 24 zilizopita nimekuwa nikijaribu kusoma na kutafakuri kwa kina yaliyotokana na mambo mawili, kwanza CHADEMA kushiriki katika sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru la kwanza na lapili hotuba ambayo Mh. Mbowe aliyoiunda na kuhakikisha arafa yake inapatikana katika dakika tatu tu! (Sina hakika kama protokali ndizo zilimtaka afanye hivyo au Ni utashi wake)

Zitto kasema, kaponda, kalaumu kakosoa na kaonyesha ni namna gani moyo wake umesambaratika. Maria Sarungi kachana kanung'unika, kaonyesha ni namna gani wanasiasa hawana muamana. Shangazi Fatma kashindwa kuwa muwazi kajikuta anasema tu I WAS WRONG japo Nina mashaka kama anajua kweli kwamba SHE WAS WRONG.

Hayo Ni ya kwao nami ninayo yangu. Ila kabla ya yangu ni pende kusema kwamba Mh. Mbowe ni aina ya watu wanaojua kurisk na ni aina ya kiongozi ambaye hudumbukiza mkono kwenye shimo lenye kiza na asijue ataambulia nini.

Mh. Mbowe kwanini Sasa Kama ambavyo kichwa cha habari hii kinavyouliza, kwa takribani miaka mitatu na ushee CHADEMA wamekua wakisusia kabisa shughuli zote za serikali kitaifa, na lililonistua zaidi yapata miezi 2 iliyopita aliita waandishi wa vyombo vya habari na kutangaza kujitoa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa sababu wagombea wake hawakutendewa haki. Ghafla msimamo ule umeyeyuka na Sasa kilio katika MARIDHIANO, unataka kuridhia nini? Je Ni uhalali wa Rais Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania, au kuridhia yeye kuendelea kuchepusha baadhi ya Sheria ili kuleta maendeleo ya haraka nchini?.

Je, Maridhiano haya ni yapi ya kuomba Uhuru wa kufanya mikutano ya siasa ya nje na ndani pahala popote na wakati wowote? Au Ni Maridhiano ya kumkosoa na yeye kuwachekea?, Unahitaji kuridhia nini naye kwakua CCM na yeye mwenyewe wanayatenda haya kimkakati kwakua muda wa miaka mitano ni mdogo na mambo wanayotaka kufanya ni mengi.

Katika ridhaa mwenye mamlaka ni mtoa ridhaa na sio mpewa ridhaa, Kwanini Magufuli aridhie maoni yako ili hali yakwakwe bado hajaridhika nayo.

TUAMBIE MH. MBOWE KWANINI SASA?
Wamesimama nawe, wamehuzunika nawe wamepambana nawe, umeamua kuachana nao? Au unamkimbiza mwizi kimya kimya?

Mh. Mbowe, mimi naamini ninyi wanasiasa mna dini yenu, mnaye Mungu wa kwenu, na mnayo maisha yasiyoamiliana na yakwetu.

Ulichokitenda kwa walio na hasira watakiita usaliti (bahati zuri unahistoria pana kwenye hili) Ila kwa wenye busara watakuuliza kwanini Sasa? hudhani kwamba maridhiano, wakati umeshindwa vita ni woga? Wataenda mbali zaidi na kuhoji Mh. Mbona inaonekana kama ZILONGWA MBALI NA ZITENDWA MBALI.

Kesho ukituambia tuandamane tunaweza kuthubutu kunjanyua tendegu zetu na kuzipeleka barabarani? Ili baada ya kuvunjwa miguu na mikono ukae uombe kuridhiana?

KAMA NI KWELI NINACHOWAZA NDICHO
1. Umeamua ku-feki kunyoosha mikono ili maumivu yapungue uweze kujipanga kwa ajili ya nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais kwa mwaka 2020. Kimsingi mbinu hizi husaidia kwa mtu aliyekua akilifanya Jambo hilo kukukomoa lakini si kwa mtu aliyekua au anayeyafanya kwa ajili ya kutimiza mambo yake, atakukanyaga tu utapo thubutu kusimaa kwenye nyia yake hatokua na msalie Mtume.

2. Umeamua kuziaminisha jumuia za kimataifa kwamba CHADEMA wanayo nia ya kuendesha siasa za kistaarabu, ukapewa jukwaa ukaandika speech fupi iliyolenga kusudio lako, sawa na Safi ambacho hujatizama kwa undani ni kwamba Mh. Magufuli hazihofii hizo jumuia na wala hatokosa usingizi, Ipo mifano inayodhihirisha kwamba hilo halimuumizi kichwa.

3. Kama lengo Ni kuomba huruma japo mwakani chama kipate WABUNGE ili kiendelee kuishi kwa ruzuku, utakua umejitekenya na kujikuta unacheka mwenyewe.

Mlituaminisha kwamba ananunua wapinzani. Iwapo waliweza kuingia mfukoni kuwanunua wapinzania leo mnajitongozesha wenyewe kweli hata hela ya sabuni kuwapa baada ya tendo si itakua ni hiari yake?

NAWASHAURI NINI
Nimegundua kwamba dunia inakawaida ya kuheshimu watu walio katika makundi haya matatu

1. Msimamo juu ya kile unachokiamini, MARTIN LUTHER KING JR, MALCOM X (Malick al Shabaaz), ERNEATO CHE, FIDEL CASTO na wengine wengi.

2. Wasema kweli hata kama unawadhalilisha, heshima aliyoipata BILL CLINTON ALIPOKUBALI KUCHEPUKA MAMA AKATOKA HADHARANI AKAMTEYEA AKAUAMBIA UMMA YEYE NDIYE MWENYE MAKOSA, Mzee Nelson Mandela alipoutangazia UMMA kwamba mwanae kafa kwa UKIMWI, na mengine mengi.

3. Kukubali kushindwa, Ni dhahiri, nafsi haitajisikia vizuri lakini jamii iliyokuzunguka inaridhika kwamba tumejaribu na tumeshindwa na sasa tujopange upya au tuendelee na mambo mengine.

Wasalaam.
 
Mbowe ameonyesha udhaifu sana na pia hi inaonyesha Mbowe anaiogopa serikali kuliko wananchi

Wewe Fanya siasa kama serikali inakuonea sisi wapiga kura tunaona siku ya kupiga kura ikifika tutawaadhibu

Kwa kweli Mbowe umenisikitisha sana na pia hujiami na pia inawezekana na wewe ccm wamesha kununua
 
Mbowe ameonyesha udhaifu sana na pia hi inaonyesha Mbowe anaiogopa serikali kuliko wananchi

Wewe Fanya siasa kama serikali inakuonea sisi wapiga kura tunaona siku ya kupiga kura ikifika tutawaadhibu

Kwa kweli Mbowe umenisikitisha sana na pia hujiami na pia inawezekana na wewe ccm wamesha kununua
Siku ya kupiga kura utawaadhibu kivipi mkuu wakati wanapita bila kupingwa?
 
Siku zote nasema dhaifu haombi maridhiano bali anajisalimisha kwa mwenye nguvu, Mbowe amejisalimisha kwa Magufuli, CHADEMA imeshindwa vita na CCM , wanachofanya sasa ni kuomba huruma ili mwakani kwenye uchaguzi wasijekupotea kabisa kwenye ramani ya siasa
Acheni unafiki kwani hakuna msilolijua. Chadema haijawahi kupambana na ccm bali vyombo vya kimamlaka vilivyoko chini ya ccm. Mf rahisi kabisa ni majuzi tu kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Chadema walikumbana na vikwazo toka kwa Watendaji Kata/Vijiji na siyo ccm.
 
Ulichokitenda kwa walio na hasira watakiita usaliti (bahati zuri unahistoria pana kwenye hili) Ila kwa wenye busara watakuuliza kwanini Sasa? hudhani kwamba maridhiano, wakati umeshindwa vita ni woga? Wataenda mbali zaidi na kuhoji Mh. Mbona inaonekana kama ZILONGWA MBALI NA ZITENDWA MBALI.
Wote tumemsikia Mbowe lakini kila mtu anatafsiri yake - hii ni kawaida. Magufuli na CCM ni watu wanao amini uCHAMADOLA. Wameshika mpini na bahati mbaya hilo panga wanalitumia ndivyo sivyo hasa zidi ya wapinzani. Waliosimama karibu wote wamekaia mshikamano na amani. Mbowe ameona ili kuwe na mshikamano na amani iendelee kuwepo kuna haja ya maridhiano. Na hapo ndio akatumia muda wake wa kutoa salamu kuomba kuwe na maridhiano.

Na hii siyo mara ya kwanza kwa CHADEMA kusema hivyo-mkumbukeni Mnyika kwenye uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kimara-ujumbe wake haupitani na wa Mbowe ambae wakati huo alikua Lupango. Binafsi sioni kama maneno ya Mbowe ni maneno ya mtu aliyeshindwa na mwenye woga.

Ni maneno ya jasiri-angekuwa muoga pale ANGEPONGEZA na KUUNGA mkono juhudi mwanzo hadi mwisho kama walivyofanya wote wengine ukiacha Bwana Yule (Le Professori Lipumba). Watu mnapenda kusahau-kumbuka wakati wa UKUTA viongozi wa dini waliahidi kuongea na mshika mpini ili alete hali ya maridhiano bahati mbaya ikashindikana jamaa kala jiwe tu.
 
Acheni unafiki kwani hakuna msilolijua. Chadema haijawahi kupambana na ccm bali vyombo vya kimamlaka vilivyoko chini ya ccm. Mf rahisi kabisa ni majuzi tu kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Chadema walikumbana na vikwazo toka kwa Watendaji Kata/Vijiji na siyo ccm.

Mbowe na labda CHADEMA wajanja sana. Lengo ni kumwezesha Lissu arudi nchini na asifunguliwe mashtaka ya jinai anayostahili. Sisi Watanzania tunapenda maridhiano kwa sababu yatawezesha maendeleo kutokea nchini. Lakini kuruhusu mtu ambaye ameisema nchi kila aina ya tusi kwa jambo alilojitengenezea yeye haikubaliki eti msingi wa maridhiano ndio aachiwe bila mambo yote kufahamika mahakamani na ushahidi wote uwe wazi. Hata kesi ya kina Mbowe iliyosababisha mwanachuo kupigwa risasi na polisi ni lazima iamuliwe mahakamani sio eti maridhiano yasananishe kesi za uhaini zifutwe.
 
Mkuu kubali yaishe, utetezi huu haubadili uhalisia wa mambo ulivyo, game over.
Nimejibu baadhi ya maswali aliyo uliza na wala sitetei kitu. Sasa kama mambo yatabadilika au la hilo lita tegemea na aliyeombwa kusimamia upatikanaji wa maridhiano.
 
Kinachonifurahisha na upande mwingine kunishitua mimi ni Mh. Mwenyekiti wa Chama kikuu cha upinzani Tanzania - CHADEMA kupata dakika zisizozidi tatu tu kusema jambo ambalo sasa ni mjadala wa kitaifa....

Hii inafunika hata maana ya siku yenyewe pamoja na ujumbe wa hotuba ya Rais Magufuli juu ya kumbukumbu ya siku ya Uhuru wa Tanganyika!!

Hizo ni dakika 3 tu. Sijui ingekuwaje tu CHADEMA wangekuwa na platforms za kufanya mikutano ya hadhara na kurushwa kwenye digital medias kama TV, Radio nk kama anavyopata publicity Rais Magufuli hata kwenye tukio la kuzindua choo cha shule tu...!!.

AMA KWELI CHEMA CHAJIUZA NA KIBAYA KILA SAA NA SIKU KWENYE TV KUTANGAZWA....huyu ndiye Magufuli!!

Ni wazi kuwa Bw. Magufuli na propaganda za maendeleo za serikali anayoingoza zingekuwa doomed kitambo sana pasingekuwapo msaada wa media...

By the way; kwa ishu ya maridhiano,Rais Magufuli/CCM ni hiari yao kuona mantiki ya kuwafanya watu waishi kama jamii moja yenye utengamano au waendelee na mbinu yao chafu kuongoza jamii inayokwenda kutumbukia kwenye vurugu na machafuko....

Binadamu siku zote utaweza kumnyanyasa na kumuonea kwa muda fulani tu, lakini itafika point utakuwa umemsukumizia hadi kwenye ukuta na kamwe hatakubali kujigonga ukutani....ni lazima atajibu mapigo tu!!

Inashangaza sana kuona CCM na serikali wanayoingoza eti wanaogopa hata hiki kinachoitwa "maridhiano"....yaani kukaa meza ya mazungumzo na wanaowaongoza kujadili changamoto mbalimbali zinazolikabili taifa....

Duuh, inatisha sana. Kwa kweli hili ni " Giza" na giza siku zote linaiogopa Nuru.... Mwanga!
 
December 9, 2019
Mwanza, Tanzania

Magufuli alivyowaona vigogo wa CHADEMA alijongea na kuwasalimia

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, amesalimiana na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani katika sherehe za miaka 58 ya uhuru.

Vigogo wa chama cha CHADEMA waliopata nafasi ya kusalimiana na Rais Magufuli ni Mwenyekiti Kanda ya Kati CHADEMA Lazaro Nyarandu, mbunge John Heche, Meya Boniface Jacob, mbunge Joseph Mbilinyi Sugu, mbunge John Mnyika na mbunge Godbless Lema katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Pia Mwenyekiti wa Taifa CHADEMA na Kiongozi wa Upinzani Bungeni (KUB) Mh. Freeman Mbowe (MB) aliitwa kusalimia halaiki wa watu uwanjani CCM Kirumba na watanzania kwa jumla waliokuwa wakifuatilia sherehe hizo za uhuru wa Tanganyika majumbani mwao ktk televisheni zao.

Katika sherehe hizo za miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika kulikuwepo pia mabalozi wa nchi za Afrika, Ulaya, Marekani ya Kaskazini, Asia na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa kama Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya n.k


Source: Global online TV
 
Hii inafunika hata maana ya siku yenyewe pamoja na ujumbe wa hotuba ya Rais Magufuli juu ya kumbukumbu ya siku ya Uhuru wa Tanganyika!!
Mkuu wala haijafunika maana ya siku yenyewe bali imeakisi maana ya siku hiyo. Kama ndiyo siku tulipata "uhuru" basi ni vizuri watanzania wajisikie wako huru kwenye nchi yao kufanya maamuzi ya msingi.
Raisi amepewa ujumbe na ni juu yake kuutafakari na kuamua au kuupuza hata bila kutafakari. Wengi tunamzungumzia Freeman Mbowe lakini bila kujali muonekano wa Prof. Lipumba hapa jukwaani-nae kwa njia yake amelizungumzia hilo kitu ambacho si wengi wangemtegemea atoe ushauri huo hadharani. Kwangu mimi wamefanya kitu kizuri hasa ikiwa ni siku ya uhuru-wamedai uhuru wa kidemokrasia na utawala bora ambao kwa kweli ni shida kutokana na katiba yetu.
 
Siku zote nasema dhaifu haombi maridhiano bali anajisalimisha kwa mwenye nguvu, Mbowe amejisalimisha kwa Magufuli, CHADEMA imeshindwa vita na CCM , wanachofanya sasa ni kuomba huruma ili mwakani kwenye uchaguzi wasijekupotea kabisa kwenye ramani ya siasa
Hii sintofahamu alitoitengeneza kwa mara ya pili sasa Kuna siku itamuhukumu.

Alimleta yule tuliyeimba nyimbo na mapambio kuwa fisadi akampa kugombea Urais akawatosa watu aliovuja nao jasho. Sasa katuletee balaa hili tena.
 
Mbowe ameonyesha udhaifu sana na pia hi inaonyesha Mbowe anaiogopa serikali kuliko wananchi

Wewe Fanya siasa kama serikali inakuonea sisi wapiga kura tunaona siku ya kupiga kura ikifika tutawaadhibu

Kwa kweli Mbowe umenisikitisha sana na pia hujiami na pia inawezekana na wewe ccm wamesha kununua
Huyu Mwamba katunyorosha kweli kweli. Ifahamike tu kwamba sipingi yeye kwenda kwenye Sherehe wapa kutoa speech ya kuomba poo, lakini tujiulize?

Mawazo, Mdude, Roma, Ben na wanaharakati wenzie hayo ndio malipo wanayostahili?
 
Masiya, Mkuu huyu jamaa kafeli katika kila kitu, Hawezi itisha maandamano, hawezi kukiongoza chama, hawezi kuliongoza Jimbo lake, sasa hivi hawezi hata mtuma mtoto dukani akaenda kimsingi CHADEMA unahitaji MTU NA NUSU wa kuiongoza huyu ashakua MTU KASOROROBO.
 
Ni bahati mbaya sana watu hawajadili hoja iliyotolewa na Chadema (kupitia mdomo wa Mbowe) na wanamjadili Mbowe kama vile hoja ile ni yake katika nayo nyumbani au anatabia kama za Magufuli kutoa kauli za kisera tokea kichwani mwake bila ridhaa ya chama.
Nchi kwa wale walioitembelea na kuifahamu vyema ni kuwa imekwisha bomoka bado kidogo tuu migogoro chungu nzima itaibuka kila upande hasa baada ya uchaguzi wa SM.
Watu waliochomekewa viongozi huko vijijini wana uelewa na kimeanza kuwaka maeneo mbalimbali kuwakataa.
 
Back
Top Bottom