Freeman Mbowe, kwanini maridhiano sasa?

Freeman Mbowe, kwanini maridhiano sasa?

Lakini damage waliyoifanya ccm kwa upinzani ni kubwa sana na itachukuwa other five years or ten years to amend.

Hali ya nchi haiko upande wa Magufuli hivyo ni lazima atafute Chaka la kujifichia.
Kalazimishwa na wastaafu alete mshikamano wa kitaifa lasivyo wenye chama wampoke tiketi ya kugombea 2020.

So tegemeeni ushirikiano wa kutosha kati yake na wapinzani kuelekea uchaguzi 2020 na baada ya uchaguzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KLM bhana, Mfalme wenu keshekaa vibaya, mtafanyaje sasa? Mtamcheka au kumfunika? Chaguo ni lenu!
 
Naona sasa huko cdm mtumbwi umetoboka rasmi kila mtu anaongea lake! Hata wewe mfia chama lialia unaanza kumdoubt the permanent chairman ila angalia huyo ni mtu mzito na sio wa mchezomchezo usaliti utakuhusu
 
Mimi mpaka leo sijajua maana halisi ya kuwa Mpinzani wa kisiasa hasa kwa nchi za kiafrika,
Nilitegemea Vyama vya upinzani kuikosoa Serikali na Kuishauri njia mbadala haya yote iwe kwa maslahi ya taifa letu, badala yake wao ni kupinga na kukatisha tamaa hata yale ambayo ni msaada wa wazi kwa wananchi wao,

Nilitegemea Serikali iliyoko madarakani kuchukua ushauri wa msingi kutoka kwa wapinzani wao kisiasa badala yake ni Kuwaminya wasisikike, kuwakosakosa na wengine kupotezwa kabisa.

Halafu wote wanajinasibu kujenga taifa moja na kuleta mshikamano.
 
Kwanza sitaki kuamini kuwa Mbowe alishiriki katika lile tukio hivi hivi tu bali kushawishiwa na watu wa sytem na wasaidi wengine wa Bwana mkubwa na pia sitaki kuamini kuwa alikwenda kushirikia bila kushirikisha viongozi wenzake ndani ya chama(teyari Lissu katetea kauli ya Mbowe kwa mujibu wa gazeti moja la leo) hivyo kuna uwekano mkubwa Mbowe alitoa kauli ile akijua kinachoendelea ingawa pia inawezekana kaingia katika mtego kwa faida ya Bwana yule asietaka kuonekana kuwa anaweza kushindwa katika misimamo yake(nitaeleza huko mbele).

Kosa alilolifanya Mbowe na chama chake kwa ujumla, ni kushiriki tukio lile bila kushauriana na viongozi wengine wa upinzani ambao naamini wangeshirikishwa,basi aliyoyasema Zitto yasingetokea hata kama wasingefikia muafaka wa pamoja kuwa Mbowe ashiriki.

Nikirudi kwenye mada,nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa Bwana yule alikuwa hajui Mbowe ataongea alichoongea bali alitaka tu Mbowe ndio aonekana mtafuta suluhu kwanini yeye siku zote hataki kuonekane ameshindwa(hataki kupangiwa).

Na ndio maana baada tu ya Mbowe kuongea,vijana wa Lumumba wakaanza propaganda za kusema Mbowe kaomba suluhu na maneno mengine mengi ili mwisho wa siku wapinzani ndio waonekane wameshindwa katika mapambano ya kudai haki na sasa wanategemea huruma ya Bwana yule kumbe Bwana yule nae anabanwa na pressure ya ndani na nje ya nchi kutokana na aina ya uongozi wake hasa uminyaji wa demokrasia na unyanyasaji kwa wapinzani.

Naamini katika kujisafisha na ili asiendelee kuvurugana na Bwana wakubwa wa hii dunia,Bwana yule ameona kuna umuhimu wa kujirudi japo kidogo, hivyo anaweza kuja kufanyia kazi wazo la Mbowe ingawa anaweza kufanya hivyo kwa kuwazuga tu mabeberu kwahiyo wawe makini nae.

Ni imani yangu pia, Mbowe kwa upande wake, aliamua kujishusha ili atumie fursa iliojitokeza(akijua kinachoendelea) hivyo akaongea alichoongea ikiwa ni utekelezaji wa kinachoendelea chini ya kapaeti.

Inawezekana kabisa watu wa system hawakumshirikisha Zitto na chama chake hasa kutokana na Zitto kwa sasa kuonekana ni mtu anaemkosoa na kumpinga vibaya sana Bwana yule na pia wakiamini chama cha Zitto hakina wafuasi wengi kama CHADEMA hivyo impact yake haitokuwa kubwa ingawa kwa hili wanaweza kuwa hawakuwaza sawaswa.

Huu ni mtazamo wangu ila muda ndio msema kweli.
Kama ndivyo basi Chadema hamuaminiki kuchukua dola. Geugeu/ndumilakuwili
 
Hali ya kisiasa ipi kilaza? Mbona unaogopa kuelezea? Eleza mtu akuelewe!
Ingekuwa raia wa Tanzania ningekuelezea Hali ilivyo kwani ingekuhusu! Mbona unahangaika Sana na hii Hali iliyopo? Inakunufaisha siyo? Maridhiano yapo na yatakuwepo ili Kama utakosa kazi Basi, Rudi kwenu Rwanda! Yaani unaitamani zitokee vurugu ili uibe Mali zetu siyo?
 
Tuendelee kueleweshana. Hata katika vita hutokea mazingira ya kukubaliana kusimamisha mapigano. Tumeshasikia mara kadhaa siku hutengwa kusiwe na mapigano kupisha kwa mfano sherehe ipite au raia wakimbia mapigano waende mahali salama.
Alichofanya Mbowe kina faida maradufu kulilo hasara zinazohesabiwa na wachangiaji humu.
Isitoshe sote hatujui mkuu atakubali au la. Na hata asipojibu hamuoni kama CDM itakuwa imepata mahali pa kuendelezea?
Akijibu kwa kukataa hoja si bado CDM itakuwa na plan B.
Hivi watu waseme Mbowe pale ilitakiwa aseme nini hasa ambacho hakusema?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kalazimishwa na wastaafu alete mshikamano wa kitaifa lasivyo wenye chama wampoke tiketi ya kugombea 2020.

So tegemeeni ushirikiano wa kutosha kati yake na wapinzani kuelekea uchaguzi 2020 na baada ya uchaguzi.
JPM si mtu wa kutoa nafasi ya maridhiano hasa na mijitu mijinga mijinga, wangekua watu ambao wapo kimkakati labda lakini hawa wanaoshangilia nchi ikipata hasara, walioamua kumzushia kifo silioni hilo likitokea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingekuwa raia wa Tanzania ningekuelezea Hali ilivyo kwani ingekuhusu! Mbona unahangaika Sana na hii Hali iliyopo? Inakunufaisha siyo? Maridhiano yapo na yatakuwepo ili Kama utakosa kazi Basi, Rudi kwenu Rwanda! Yaani unaitamani zitokee vurugu ili uibe Mali zetu siyo?
Wakati wa maridhiano wanaenda kuongea kuhusu nini? Mbona hulisemi?
 
Wananzengo habari zenu.

Takribani saa 24 zilizopita nimekuwa nikijaribu kusoma na kutafakuri kwa kina yaliyotokana na mambo mawili, kwanza CHADEMA kushiriki katika sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru la kwanza na lapili hotuba ambayo Mh. Mbowe aliyoiunda na kuhakikisha arafa yake inapatikana katika dakika tatu tu! (Sina hakika kama protokali ndizo zilimtaka afanye hivyo au Ni utashi wake)

Zitto kasema, kaponda, kalaumu kakosoa na kaonyesha ni namna gani moyo wake umesambaratika. Maria Sarungi kachana kanung'unika, kaonyesha ni namna gani wanasiasa hawana muamana. Shangazi Fatma kashindwa kuwa muwazi kajikuta anasema tu I WAS WRONG japo Nina mashaka kama anajua kweli kwamba SHE WAS WRONG.

Hayo Ni ya kwao nami ninayo yangu. Ila kabla ya yangu ni pende kusema kwamba Mh. Mbowe ni aina ya watu wanaojua kurisk na ni aina ya kiongozi ambaye hudumbukiza mkono kwenye shimo lenye kiza na asijue ataambulia nini.

Mh. Mbowe kwanini Sasa Kama ambavyo kichwa cha habari hii kinavyouliza, kwa takribani miaka mitatu na ushee CHADEMA wamekua wakisusia kabisa shughuli zote za serikali kitaifa, na lililonistua zaidi yapata miezi 2 iliyopita aliita waandishi wa vyombo vya habari na kutangaza kujitoa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa sababu wagombea wake hawakutendewa haki. Ghafla msimamo ule umeyeyuka na Sasa kilio katika MARIDHIANO, unataka kuridhia nini? Je Ni uhalali wa Rais Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania, au kuridhia yeye kuendelea kuchepusha baadhi ya Sheria ili kuleta maendeleo ya haraka nchini?.

Je, Maridhiano haya ni yapi ya kuomba Uhuru wa kufanya mikutano ya siasa ya nje na ndani pahala popote na wakati wowote? Au Ni Maridhiano ya kumkosoa na yeye kuwachekea?, Unahitaji kuridhia nini naye kwakua CCM na yeye mwenyewe wanayatenda haya kimkakati kwakua muda wa miaka mitano ni mdogo na mambo wanayotaka kufanya ni mengi.

Katika ridhaa mwenye mamlaka ni mtoa ridhaa na sio mpewa ridhaa, Kwanini Magufuli aridhie maoni yako ili hali yakwakwe bado hajaridhika nayo.

TUAMBIE MH. MBOWE KWANINI SASA?
Wamesimama nawe, wamehuzunika nawe wamepambana nawe, umeamua kuachana nao? Au unamkimbiza mwizi kimya kimya?

Mh. Mbowe, mimi naamini ninyi wanasiasa mna dini yenu, mnaye Mungu wa kwenu, na mnayo maisha yasiyoamiliana na yakwetu.

Ulichokitenda kwa walio na hasira watakiita usaliti (bahati zuri unahistoria pana kwenye hili) Ila kwa wenye busara watakuuliza kwanini Sasa? hudhani kwamba maridhiano, wakati umeshindwa vita ni woga? Wataenda mbali zaidi na kuhoji Mh. Mbona inaonekana kama ZILONGWA MBALI NA ZITENDWA MBALI.

Kesho ukituambia tuandamane tunaweza kuthubutu kunjanyua tendegu zetu na kuzipeleka barabarani? Ili baada ya kuvunjwa miguu na mikono ukae uombe kuridhiana?

KAMA NI KWELI NINACHOWAZA NDICHO
1. Umeamua ku-feki kunyoosha mikono ili maumivu yapungue uweze kujipanga kwa ajili ya nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais kwa mwaka 2020. Kimsingi mbinu hizi husaidia kwa mtu aliyekua akilifanya Jambo hilo kukukomoa lakini si kwa mtu aliyekua au anayeyafanya kwa ajili ya kutimiza mambo yake, atakukanyaga tu utapo thubutu kusimaa kwenye nyia yake hatokua na msalie Mtume.

2. Umeamua kuziaminisha jumuia za kimataifa kwamba CHADEMA wanayo nia ya kuendesha siasa za kistaarabu, ukapewa jukwaa ukaandika speech fupi iliyolenga kusudio lako, sawa na Safi ambacho hujatizama kwa undani ni kwamba Mh. Magufuli hazihofii hizo jumuia na wala hatokosa usingizi, Ipo mifano inayodhihirisha kwamba hilo halimuumizi kichwa.

3. Kama lengo Ni kuomba huruma japo mwakani chama kipate WABUNGE ili kiendelee kuishi kwa ruzuku, utakua umejitekenya na kujikuta unacheka mwenyewe.

Mlituaminisha kwamba ananunua wapinzani. Iwapo waliweza kuingia mfukoni kuwanunua wapinzania leo mnajitongozesha wenyewe kweli hata hela ya sabuni kuwapa baada ya tendo si itakua ni hiari yake?

NAWASHAURI NINI
Nimegundua kwamba dunia inakawaida ya kuheshimu watu walio katika makundi haya matatu

1. Msimamo juu ya kile unachokiamini, MARTIN LUTHER KING JR, MALCOM X (Malick al Shabaaz), ERNEATO CHE, FIDEL CASTO na wengine wengi.

2. Wasema kweli hata kama unawadhalilisha, heshima aliyoipata BILL CLINTON ALIPOKUBALI KUCHEPUKA MAMA AKATOKA HADHARANI AKAMTEYEA AKAUAMBIA UMMA YEYE NDIYE MWENYE MAKOSA, Mzee Nelson Mandela alipoutangazia UMMA kwamba mwanae kafa kwa UKIMWI, na mengine mengi.

3. Kukubali kushindwa, Ni dhahiri, nafsi haitajisikia vizuri lakini jamii iliyokuzunguka inaridhika kwamba tumejaribu na tumeshindwa na sasa tujopange upya au tuendelee na mambo mengine.

Wasalaam.
Mbowe amenusa harufu ya chama chao kukosa jimbo hata moja mwakani ndio maana akaona bora aombe poo mapema
 
Back
Top Bottom