Freeman Mbowe aungwe mkono uchaguzi ndani CHADEMA

Uchaguzi ni mwaka huu December.Taratibu nyingine tutazitoa baada ya vikao vya Kamati Kuu
Okey.ni vizuri mkaujulisha umma pia.maana licha ya kuwajibika kwa wanachadema, pia mnawajibika kwa umma pia..
 
Kuna mambo yanajirudia kila wakati mpaka yanachosha. Unapokaribia uchaguzi ndani ya Chadema kuna maneno kuhusu Mbowe lazima uyasikie

– Mbowe anajilipa ruzuku yote. Kateka mali zote za chama. Mbowe anaendesha chama kama ofisi binafsi.n.k

Maneno haya yanajirudia kila msimu wa uchaguzi wa chama hicho.

Tuliyasikia wakati wa Chacha Wangwe. Wakati wa Zitto Kabwe. Sasa Kigogo wa ‘twita’ anayarudia kwa namna ileile. Kwa mwenye akili timamu hii inachosha.

Kama hizi ndiyo propaganda basi hizi ni za kipumbavu. Kichekesho zaidi ni wanaozitumia kushindwa kuelewa kuwa hazina mashiko. Uchaguzi wao ukiisha na haya maneno yanaisha.

Tuwekane sawa kwenye hili. Chama kinachopigania ukombozi au kutaka kushika dola, kikipata kiongozi imara hakimbadilishi ovyoovyo. Hii ni ‘prinsipo’. Yasser Arafat kafa akiwa kiongozi wa PLO kwa miaka mingi kule Palestina.

Dunia nzima, kiongozi wa namna hii huondolewa kwa kushindwa kustawisha chama na si vinginevyo. Huyu ndiye Mbowe.

Ukiwa na kiongozi asiye na msimamo mtaishia kuwa na vyama visivyosikika. Akili za Mbowe, msimamo wake, uchumi wake. Ndiyo yaliyopelekea akute chama kina wabunge watano na sasa wako sabini.

Unamuondoaje? Labda kama huna nia ya kushika dola. Propaganda za kula ruzuku lazima zife kibudu.

Kuna watu wakisikia shamba la Mbowe limeharibiwa na DC wanawaza matembele, nyanya chungu, sukuma wiki, kabeji na matuta ya viazi – wanalifananisha na mashamba ya bibi na babu zao huko Mpwapwa au Malinyi kama siyo Matombo.

Tunatakiwa kumshangaa Mbowe kuacha utajiri chekwa wa familia yake na kuja kuhangaika na siasa huku mitaani na kina Sugu.

Mwanzoni watu walikuwa ‘bize’ na Kigogo huko ‘twitani’. Kuna wakati akataka aniteke kiakili na mimi. Lakini kuanzia kwenye suala la ‘flash’ za ajali ya yule kigogo wa ukweli. Nikaanza kupata shaka. Ni sampuli ya watu wanaoamua kujipa nafuu ya nafsi zao kwa kuandika wanachojisikia.

Lowassa, aliitwa fisadi kila siku. Watu wakachoka kuona mtu mmoja anabebeshwa zigo lote la ufisadi. Kwanini hashtakiwi? Kwanini sasa hafungwi? Maswali yasiyo na jibu yalipelekea ageuke shujaa 2015.

Ndiyo Mbowe, shutuma anazopewa mbona Msajili wa vyama na CAG hawajawahi kusema lolote? Hata wapinzani wa Mbowe wamechoshwa nazo.

Tufanye siasa safi, zenye tija na manufaa kwa nchi. Hizi za ovyo ni upuuzi.

#Mbowe Tano Tena#
2020 Chadema itafanana na TLP na Mbowe atakuwa kama Mrema.

Chadema haitakuwa na mbunge hata mmoja!
 
Wewe mwanaCCM si ndiyo itakuwa furaha yako? Sasa kinakuuma nini tunapomchagua tena Mbowe?
 
Hakika kaka wote wanao kesha wakipiga kelele za Mbowe ni vibaraka na maadui wa cdm huo ndiyo ukweli tusimame na mwenyekiti wetu ili chama kisonge mbeleView attachment 1218268

Ni wendawazimu kuendelea kumpigia debe kiongozi aliyekaa madarakani zaidi ya miaka 15 huku chama kikifanyiwa hujuma na mwenyekiti mwenyewe akiwa muhanga wa hizo hujuma. Kama yeye mwenyewe anafanyiwa hujuma za wazi na hana uwezo wa kujitetea ndio ataweza kukitetea chama? Huyo mwenyekiti yuko na katibu mkuu domo zege na wala hana uwezo wa kumbadili. Ni hakika chama kinahujumiwa wazi wazi na rais, lakini ukweli hata mwenyekiti ni sehemu ya kulea hizo hujuma.

Tuwe wakweli tu, mwenyekiti wetu kafikia mwisho wa mbinu, na ni aibu kwa chama chenye watu waerevu kama cdm kuendelea kuongozwa na mtu mmoja zaidi ya miaka 15, huku kukiwa na watu mashupavu kama John Heche, Ole Sosopi, John Mnyika, Marcus Albanie nk. Mbowe bado ni mwanachama hata akiachia uwenyekiti heshima yake itakuwepo na ataendelea kutoa ushauri, lakini kuendelea kuwa mwenyekiti hapana, maana hiyo sio demokrasia bali ni uhuni.
 
Haahaa Mkuu wenzako wanasema huko chadema hakuna mwenyekiti uwezo Wa kuwa mwenyekiti kumzidi mbowe.Angalia utaitwa msaliti soon.
 
Mbowe Tano Tena
 
Mwanachama wa CCM hawezi kuwa msaliti ndani ya CDM.Kasaliti nini?
 
Unakaribishwa sana siku ya kupiga kura ili utimize haki yako
 
Haahaa Mkuu wenzako wanasema huko chadema hakuna mwenyekiti uwezo Wa kuwa mwenyekiti kumzidi mbowe.Angalia utaitwa msaliti soon.
Hatuna muda wa kupoteza kubishana na watu kama nyinyi mnao tumiwa
 
Mbowe Tano Tena

Ni kweli, ila sio kwa cdm ile iliyokuwa inashine. Kaa kumtetea Mbowe kwa maslahi yako binafsi, lakini ujue Mbowe ataiongoza cdm inayoshuka, moja ni kwa hujuma za vyombo vya dola, na pili kwa yeye kuchuja na kuifubaza cdm kwa kuishiwa na mbinu. Wakati ukuta hata atanyeje kwa sasa ni muda wake wa kushuka, hivyo ni bora ashuke mwenyewe kuliko akishushe na chama.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom