Free talk: Mwanamke shtuka!

Free talk: Mwanamke shtuka!

Unasema nyumba tu...mwingine anasema unanipangia watoto wangu wasome shule gani?...
Wanasahau kila kitu ni vya kwenu wote....
Acha tujijenge tuwe na vyetu na sisi tupate nafasi ya kushiriki maamuzi ya kifamilia...sio kuwa mtekelezaji tu
Badala mkae mjadiliane wewe unapewa comand tu mweeh!!
 
Unamtumia sms, "wahi kurudi nyumbani leo uhakikishe watoto wameoga mapema,wamefanya home work na wale na kulala mapema, mie nipo sehemu na friends tunapata moja moto moja baridi"
Wanaume wa namna hiyo Mungu awatie nguvu, nafikiri siwezi
 
Unamtumia sms, "wahi kurudi nyumbani leo uhakikishe watoto wameoga mapema,wamefanya home work na wale na kulala mapema, mie nipo sehemu na friends tunapata moja moto moja baridi"
Kabisa....maana na wewe mke lazima ukutane na marafiki kutengeneza madili ya kuingiza pesa
 
Umenena vyema Espy, kwa kweli ni wanawake wachache sana kwasasa wanaofikiria maendeleo kwa jitihada zao wenyewe pasipo kuwepo mkono wa mwanaume.

Unakuta dada kaajiriwa (binafsi/serikali) na ana muda hata wa zaidi ya miaka mitatu kazini lakini hana lolote alilowekeza zaidi ya kuhangaika na fashion kila siku... Wengi hatukumbuki kuwa nafasi na muda tulionao sasa baadaye tunaweza tusiupate, nyakati zinabadilika uchumi nao unakuwa sio rafiki.. Siku utakayoingiwa na akili ya kufanya kitu angalau kikaonekana cha manufaa kwako na kwa yeyote ajaye (mume/watoto) ndo utakapo ng'amua kuwa huna tena uwezo wa kufanya hivyo na ndipo itabaki tu simulizi kuwa yule dada enzi zake alikuwa yuko vizuri kiuchumi...Muda huo akili unayo lakini huna vitendea kazi.

Mambo mengine tuwe tunayaacha yanatupita, si lazima kuyumbishwa na dunia, kushoto upo, huku upo , kule upo yaani kila kinachokuja umo....

Tujaribu pia kuangalia na aina ya marafiki wa kuambatana nao, wao kila siku wazungumzia fashion mpya tu na kutambiana madanga, wafikiri lini utapata wazo la kusema uinvest kwenye kitu cha maana???

Nimewahi kuwa na rafiki, alinizidi kwa umri (miaka 6) lakini sioni alichokuwa akinifaidisha zaidi ya kunipa stori tu za kupelekana maduka ya mikoba + nguo + viatu + stori za madanga aliyonayo...

Nikimshauri mawazo mazuri utasikia maisha yenyewe hayaeleweki, tutumie....Nikaona hili BOX halinifai...

*Kama una uwezo na nafasi ya kufanya kitu fanya, huyo mume endapo utajaaliwa aje akute angalau una pa kuegemea...Mkiunganisha nguvu pamoja angalau mnakuwa mmejisogeza sogeza....
Umesema vyema.
 
Hahahaaaaa!! Kwahiyo wewe hautaki 50/50 my kaka?
Kimsingi mimi ni miongoni mwa wanaume wanaojali sana hasa kwa jambo lililo ndani ya uwezo wangu..care&love lkn ninaamini zaidi ktk kuwa mimi ndiye kichwa kwa kila kila kitu kama mwanaume.
Namudu majukumu yangu yote tena kwa bidii.
Lkn siamini ktk 50/50 isipokuwa ktk mgawanyo wa majukumu ktk familia.
Nitakuruhusu ujumuike na wenzio, biashara but kuwe na mipaka.
Urudi nyumbani kabla kiza/giza.
Home ndiko ofisi yako kuu, watoto wakae vizuri, uwaandalie chakula mapema na ninapofika unihudumie wew na sio house gel
 
Back
Top Bottom