Franco vs Madilu who is the best

Franco vs Madilu who is the best

Tabora Jazz nadhani na Nyanyembe zote zilikuwa zikimilikiwa na jamaa mmoja mtu wa hapohapo Tabora. Nilikuwa silifahamu hili hadi jamaa mmoja akaniambia ilikuwa Band ya mjomba wake. Sikufuatilia sana kwani nilijua atakuwa anajua tu ilikuwa band ya mjomba ila zaidi ya hapo kwa umri wake atakuwa hawafahamu wanamuziki na historia yao.

naam mkuu mimi ni mtu wa tabora. Na ni mpenzi sana wa muziki wa Dansi. Band hizi zikipata msukumo zinaweza kufufuka. Nilisikia pia Vijana Jazz imefufuka. Kwanza nijue tabora jazz ilikua inamilikiwa na nani?
 
Kulingansha wanamuziki au watu walio katika fani moja ni kitu cha kawaida, lakini lazima kuwe na uwiano wa aina fulani kati ya hao wanao linganishwa. Katika hili kumlinganisha Franco na Madilu kwa kiasi si sawa. Madilu alipotoka Afrisa International baada ya kuachwa safari ya nje na Tabu Ley 1980 alihamia TP OK Jazz ambako aliimba hadi 1983 Franco baada ya Chock Chock Chock session alitoka na kibao Non. Inasemekana Franco alitaka kubadilisha upepo wa waimbaji wake hivyo akamjaribu Madilu na kumkubali na hiyo siyo kama wengi wanavyofikiri ndiyo rekodi iliyomtoa Madilu System na kumsogeza katika kundi la Ntessa Dalienst na Josky Kiambukuta (waimbaji na watunzi mahiri wa TP OK Jazz). Na Franco akawa anatunga nyimbo zinazo endana na uimbaji wake na Madilu. Franco na Lutumba ndio waliomuweka Madilu kwenye kundi la waimbaji mahiri. Madilu baada ya kufariki kwa Franco alisema "anapoingia studio huwa "anamuona Franco" ambaye "humuongoza" kwenye muziki wake. Hivyo hakuna swali la kuwlinganisha kama mhusika mwenyewe anakiri.
Kama ni kumlinganisha Franco nita mlinganisha na Grand Kalle, Tabu Ley, Vicky Longomba, Dr Nico na Le Grand Poete Lutumba Simarro ingawa ukimuuliza Simaro atakuambia Franco ni habari nyingine na amekua bossi wake toka 1961 hadi 1989.
 
Kwangu wote ni wazuri, Franco alikuwa kiongozi mzuri miaka kwa miaka, na madilu ni mwimbaji mzuri sana na mwenye nyimbo nzuri sana, kwa sisi vijana huwa tunaangalia zile ambazo zinabamba sana nyimbo za madilu alipoimba peke yake kipindi Franco amefariki ni Kali sana na hata alizoshiriki kuimba pamoja na Franco pia ni zuri sana pia, ila kiongozi mzuri ni Franco, mwenye akili amenielewa hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau wa mikito hiyo tunasema unamkosea sana Franko le Luambo Makiadi na Madilu System.
Hata madilu afufuke leo atakwambia usinifananishe na huyo Mukubwa Franko,mi nguchiro ye Tembo.
 
Back
Top Bottom