Franco vs Madilu who is the best

Franco vs Madilu who is the best

Kwa wale wapenzi wamziki napendeni tushirikishane nani ni bora na katika nyimbo zipi kati ya wanamziki hawa wawili


Sent using Jamii Forums mobile app
The heading should have been written Who WAS The Best as both of them are dead.. Asking who is the best is as if they are still with us...u can as Between Diamond and Kiba who is the best as wapo bado na wanaendelea na Music but with Franco & Madilu I think you used a wrong tence
 
Sina hakika sana kama wanapaswa kufananishwa, sbb franco ndie mwalimu wa madilu. Sbb huwa wanafananishwa watu wa kizazi kimoja. Sema moja ya sifa ya madilu ni sauti iliyotulia hadi kufananishwa na music system. Waliokuwepo enzi zao wanamajibu zaidi.
 
Swali lako halipishani na swali kama hili hapa:-

Hivi Samsung S8 original na S8 Copy ni ipi zaidi?
 
The heading should have been written Who WAS The Best as both of them are dead.. Asking who is the best is as if they are still with us...u can as Between Diamond and Kiba who is the best as wapo bado na wanaendelea na Music but with Franco & Madilu I think you used a wrong tence
Ushamba huu jf hadi lini kutumia lugha ya taifa kama mwanzisha mada unaona shida gani?
 
Ushamba huu jf hadi lini kutumia lugha ya taifa kama mwanzisha mada unaona shida gani?


Usiwatukane JamiiForums maana ndimo humo umepata nafasi ya kuweka uzi wako, hebu tazama mfumo wote wa JF umejengwa kwa lugha hiyo unayoikandia
 
Ushamba huu jf hadi lini kutumia lugha ya taifa kama mwanzisha mada unaona shida gani?
Hicho kichwa cha habari cha mada hii kiko kwenye lugha gani?... Kilichoandikwa kwa hiyo lugha yakukera sana kinatokana na maana inayopatikana kwa lugha hiyo aliyotumia kuweka kichwa cha habari..
 
Sasa kama hujui mbona unaandika kuwa ndiyo alikuwa Mwalimu wake?
Madilu aliletwa kwenye Band ya TP OK Jazz na Josky Kiambukuta. Ila kabla ya hapo, tayari alishakuwa Mwanamuziki hadi kuwa na kibendi chake. Ila umaarufu mkubwa aliupata akiwa Ok Jazz hasa baada ya kuimba Mario.

Ni ngumu kuwalinganisha hawa kwani kwenye Band walikuwa na kazi tofauti ila muhimu sana kwa Band. Franco alikuwa kiongozi na Meneja wa Band. Alitumia uzoefu na wenyeji wake kuipaisha Band. Alipiga gitaa na kuimba ingawa kwa kuimba jamaa alikuwa msanii. Alipendwa na Wanawake kwa kuimba nyimbo za matusi yaliyofichwa. Kama wimbo wa Mamou ambao jamaa kampeleka Mpenzi kusoma na alikipiga simu anasikia sauti ya mchepuko ikiunguruma. Ila mwisho wa siku alikuwa ni Meneja mzuri mno kwa Band.

madilu yeye aliimba na alipofika tu akawekwa mbele kama Sura ya band. Franco yeye siku zote alikaa nyuma ya Waimbaji. Hakupenda sana kuonekana mbele ingawa alikuwa kiongozi. Hiyo iliwapa nafasi wanamuziki wa OK Jazz kufanya show hata bila ya Franco kuwepo.

Ila wote hao walihitaji MTUNZI wa Nyimbo mzuri mno. Hapo ndipo anaingia Mwana Mashairi ambaye bado yupo hai aitwaye Simalo Lutumba Masiya. Huyu jamaa anetunga zaidi ya nusu ya nyimbo za OK Jazz na alizoimba Madilu. Nyimbo zake nyingi kama unauzoefu utazijua kwani magitaa hupigwa sawa kama mawili au matatu ukiacha Bass gitaa.



Sina hakika sana kama wanapaswa kufananishwa, sbb franco ndie mwalimu wa madilu. Sbb huwa wanafananishwa watu wa kizazi kimoja. Sema moja ya sifa ya madilu ni sauti iliyotulia hadi kufananishwa na music system. Waliokuwepo enzi zao wanamajibu zaidi.
 
Taborian .... kama sikosei ni wa Tabora. Vipi Band yetu ya Tabora Jazz au Nyanyembe kuna mpango wa kuzifufua siku moja kwa nyie vijana?

Au ndiyo tumebaki na ZILIPENDWA?
 
Taborian .... kama sikosei ni wa Tabora. Vipi Band yetu ya Tabora Jazz au Nyanyembe kuna mpango wa kuzifufua siku moja kwa nyie vijana?

Au ndiyo tumebaki na ZILIPENDWA?

naam mkuu mimi ni mtu wa tabora. Na ni mpenzi sana wa muziki wa Dansi. Band hizi zikipata msukumo zinaweza kufufuka. Nilisikia pia Vijana Jazz imefufuka. Kwanza nijue tabora jazz ilikua inamilikiwa na nani?
 
Kwa wale wapenzi wamziki napendeni tushirikishane nani ni bora na katika nyimbo zipi kati ya wanamziki hawa wawiliSent using Jamii Forums mobile app

Kuna watu wanasoma zaidi ya ulichoandika. Kama unauliza who is the best kati ya Madilu na Franco, una maana comparison sio kati yao, bali ni wao kulinganisha na wanamziki wengine wote? You cant have the best when you compare two items. The best inakuja unapo compare kuanzia three items.
 
jibu la harakaharaka nani alikuwa zaidi ni pale alipofariki FRANCO , na bendi nayo ikamfuatia nyuma , waliobaki walikusanyika na kuendeleza band kwa jina la BANA OK, na kumfanya SIMARO kuwa Kiongozi lkn walishindwana, Madiluu akaunda band yake lkn ubunifu ukamshinda ,akawa anapiuga music wa OK JAZZ, familia ya Franco wakamtaka waingie mkataba kwani si zake , hakudumu saana . hakuna mwanamusic alikuwa nyota ktk safu ya uimbaji kama Sam mangwana , lkn aliondoka TP OK JAZZ IKABAKI, na ikahit pia, KOFI OLOMIDE anaweza ingawa si saana kufananishwa na FRANCO kwa maana ya kipaji, wataondoka wanamuziki wooote anabaki peke yake lkn akiibuka na wanamusic wapya ngoma atakayotoa ni kali.
 
Ilo swali ni zuri sana, na nilishwahi kujiuliza mara kadhaa japo wengi tunajua na kuamini Franco his best *yawezakuwa kweli* kwa point hizi,
1. Uwezo wa kuongoza bendi na utemi haswa.

2. Hakufukuzi ovyo ovyo ila ukiondoka kibabe ukirudi anakupokea bila tatizo(Sam Mangwana, Veck kamangwana)

3. Uwezo wa kupiga rhythm guitar [emoji450] haswa kwenye African Jazz

4. Kuwa na band kubwa (moja inabaki Kinshasa nyingine international) so kila weekend Ok Bar lazima ilipuke.

Madilu ni Jembe ila alifichwa na Franco, kuna watu kwanza wanashindwa kutofautisha sauti ua madilu na franco, pia kwa Franco HATA UIMBE VIPI WIMBO NI WA FRANCO AND TP OK JAZZ na sio madilu ma Tp ok jazz zaidi. Kuna mengi ila hayo machache.
 
Back
Top Bottom