Fountain Gate Academy Tabata rekebisheni Barabara za kuingia Shuleni, mnatesa Watoto

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Jana nimepita mitaa ya Shule ya Moja ya Shule za Fountain Gate iliyopo Tabata Sigara jijini Dar es Salaam, nimekutana na tatizo kubwa sana la Barabara inayoingia katika Shule hiyo, na mbaya zaidi ni Barabara inayotumika na Watoto kufika shuleni hapo cha kushangaza barabara hiyo imekuwa mbovu kwa zaidi ya miaka 5 hainafanyiwi marekebisho yoyote,

Sasa najiuliza hizo fedha zinazolipwa kwenye ada za watoto zinasadia nini kama Shule inashinda kurekebisha njia inayotumiwa na Magari, Wafanyakazi na Watoto wa shule hiyo. Pale kwa haraka tu ni kifusi gari 5 tu pameisha lakini hawajiongezi kufanya hilo.

Hebu wawajibike maana wananyanyasa sana Watoto wadogo wanaotumia njia hiyo.
 
Back
Top Bottom