Form 4 na wengine, angalieni hapa!

Samahan mkubwa kuna dogo langu yeye limefaulu phys D na bios D je linaweza kupata vyuo vya nursing maana kuna kademu ka 1 kalimaliza mwaka jana o lever yy kalipata BIOS D na KISW D akapata chuo cha nursing je na huyu dogo langu anaweza kupata? Nifahamishe mkubwa.
 
Jamani msaada p'se, mdogo wangu kapata div4 pt 32. Ana D 3, ya Civ, Biol na Geog. Masomo mengine kapata F. Hivi huyu anafaa kusoma nini maana nilitaka arudie shule.
 
Hahaaaaa, safi sana!! Kapasua sana huyu dogo...kama kajaza HGE as first choice, mbaie ale bata tu atapelekwa shule nzuri sana by government, kwa ufupi huyo kafaulu sana Hist na Geography, so ondoa wasi asianze complication zozote, atasoma tu economics ingawa inahitaji hesabu kiaina, kwani wewe wasiwasi wako upo wapi hasa?

Lakini ana F ya hesabu, si kwamba kusoma HGE, kama ilivo kwa combinations za science, anahitajika kufaulu hesabu katika mtihani wa form four?
 
Wakuu naomba msada wa mawazo kwa dogo langu anapend unesi lakini ana 4 ya 33 yani kafaulu civic=D na Bios=D je anaweza fanikisha ndoto zake?
 
Wakuu naomba msada wa mawazo kwa dogo langu anapenda unesi lakini ana 4 ya 33 yani kafaulu civic=D na Bios=D je anaweza fanikisha ndoto zake?
 
civ.c hist d geo.c.kisw d eng.c phy.c chem.b bios b b/math .a add.math .d shule ya kwanza kuchagua ni tosamaganga pcm ya pili minaki pcb ya tatu njombe cbg. nk.sasa uamuz wake ni kusoma pcb ili awe dr.je kwa matokeo haya ya mwaka huu unaweza kumkadiriwa kuenda shule gani?na je shule hizo tatu zinaweza kuwa na ubora sawa au ipi bora zaidi? samahani wakuu maswali nahisi ni mepes lakn ynahtaj majib magumu hebu nifumbuwen au aende privet kama ndvyo shule gani kwa pcb? nawaskisha

Ujue kuna kitu watu wanamislead!! Hivi kwanini wanafunzi wengi hawajiamini?? Sasa mtu kama huyu kwanini first selection yake isiwe Special School??(Kibaha, Tabora Boys,Mzumbe au Ilboru)? Kwanini?? Hii ni kutojiamini...bt kwa matokeo ya mwaka huu huyu mtu anaweza kwenda PCM special school...Kwa mfano hhili tatizo hata mimi nilikuwa nalo...at my time(baada ya kudanganyana shuleni) shule ya kwanza kujaza ilikuwa tosamaganga, lakini ikatokea nikapata A masomo ya PCM...ikawa nina pt 3, sasa piga ua siwezi kwenda Tosa,walichokifanya wakanipeleka Tabora Boys(may be it was my lucky).

Back to point Phy C Chem B na Math A hapa ana point 6 kwa perfomance mbaya ya mwaka huu huyu angeenda special bila wasi endapo angejaza(may b atapelekwa Tabora Boys) otherwise ategee kwenda Tosa alikoomba PCB as 1st choice!! Kwa hali ya sasa Tosa ni shule nzuri sana compared to hizo nyingine ulizotaja(Nakumbuka mwaka 2006 ama 7) Tanzania One Best student alitoka Tosa for the first time advance, so atachaguliwa hapo ila akoma e tu!!

Nawakilisha.

 
Wakuu naomba msada wa mawazo kwa dogo langu anapenda unesi lakini ana 4 ya 33 yani kafaulu civic=D na Bios=D je anaweza fanikisha ndoto zake?

Duh aiseee!! hapa bana nisikudanganye!! unesi kwa D 2 ni ngumu, 33 ni 4 ya mwisho, arudie atafute D ya 3 halafu ajaribu kuomba ingawa kiasi flani ni ngumu due to compitition
 
Lakini ana F ya hesabu, si kwamba kusoma HGE, kama ilivo kwa combinations za science, anahitajika kufaulu hesabu katika mtihani wa form four?

Perfomance ya hesabu itamsaidia huko mbeleni kwenye kuomba nafasi za vyuo..ila kwa kwenda f5 hesabu sio inshu
 
Jamani msaada p'se, mdogo wangu kapata div4 pt 32. Ana D 3, ya Civ, Biol na Geog. Masomo mengine kapata F. Hivi huyu anafaa kusoma nini maana nilitaka arudie shule.

Kurudia shule ni wastage of time...ilhali ana D 3 basi yupo subjected kuanza na certificate ya baadhi ya kozi...jaribu kuitia sredi hii full utapata vyuo na kozi zake!
 
Samahan mkubwa kuna dogo langu yeye limefaulu phys D na bios D je linaweza kupata vyuo vya nursing maana kuna kademu ka 1 kalimaliza mwaka jana o lever yy kalipata BIOS D na KISW D akapata chuo cha nursing je na huyu dogo langu anaweza kupata? Nifahamishe mkubwa.

Anaweza akapata kwa ngazi ya certificate, its better to try than never bro...let her try
 


Ujue kuna kitu watu wanamislead!! Hivi kwanini wanafunzi wengi hawajiamini?? Sasa mtu kama huyu kwanini first selection yake isiwe Special School??(Kibaha, Tabora Boys,Mzumbe au Ilboru)? Kwanini?? Hii ni kutojiamini...bt kwa matokeo ya mwaka huu huyu mtu anaweza kwenda PCM special school...Kwa mfano hhili tatizo hata mimi nilikuwa nalo...at my time(baada ya kudanganyana shuleni) shule ya kwanza kujaza ilikuwa tosamaganga, lakini ik mr sizinga senks very "february' kusema kweli nakubaliana nawe kwa mambo kadhaa hapa ya msingi moja kubwa ni kutojiami na kudanganyana kijana wangu baada ya kufanya exm.nilmshau
 
Mkuu Sizinga narudi tena kwasababu kuna dogo wajirani kaniomba ushauri baada ya kusikia nikisema haya mlo andika humu.

Matokeo yake yako hivi:-
Civ D
Hist D
Geo D
Kisw F
Engl F
Phy F
Chem D
Bio D
Agri D
B/Math F
yaani Division IV ya 29.

Sasa Mkuu huyu anaweza kwenda Diploma wakati amefeli Hesabu na English? Na kama anaweza ni kwa course ipi katika chuo kipi?
Au kama hawezi kusomea diploma afanyeje mkuu?
 
Haya matokeo ndiyo hayo yametoka!! Kila kitu hadharani, sasa ukiwa hapa JF ndo mpango nzima!! Manake watu washaanza kuhoji, mi nina hiki au kile nitafanyaje, haya ngoja nitajaribu kuweka mwongozo na alternatively nyingine due to spme perfomances kwa wote, manake naona huku kitaa watu wanadanganyana sana!!

Hii ni kwa kadri ninavyofahamu mimi, kama kuna marekebisho basi yafuatie:

=> Credit Qualification kwa hali ya kawaaida ni 'C'-Na ili uende Form 5 unahitaji uwe na C 3, hapa ni either umebalance Combination(Comb) au hujabalance. Sasa kama una C 3 na comb hujabalance, hautachaguliwa serikalini bali shule binafsi utaenda kusoma mchepuo utakaofanana na masomo yako.
[ Mfano: Civ-C, Kisw-C, Geo-C...unaweza fanya HGK ama HGL ama kozi nyingine hata kama english na History una D].

=>Ukiwa na C 2 na D kadhaa(lets say 4 ya 26), hapa utaweza kwenda Form 5 shule za Private lakini utatakiwa utafute C ya 3 kw kureset wakati upo form 5. Same na C 1 You need to re-sit.

=> Hapa sasa ndipo kwenye utata. Ukiwa na D 3, kiukweli sahau Form 5 kama hauhitaji kurisit, sasa qualification hizi zina option zifuatazo:
1. Unahitaji kupiga long pass kwa kwenda Chuo kwa ngazi ya Certificates. Duraation ya hii kozi ni 1 year Certificate. Sasa hapa kuna vyuo kadhaa vinavyotoa certificates. Hapa ni D za masomo yoyote yale Basic(sina uhakika kama B/Knwoledge na Islam zinazingatiwa na ndio maana nasema D za Basic Subjects)
Mfano: Unaweza kufanya Certicates vyuo vya CBE-Mambo ya Biashara, IFM, TIA, Utumishi wa Umma(Public Service) Vyuo vya Kilimo na Ualimunk.
Nakozi nyingi tu wanatoa kwa certificates..mfano Procurement, Accounts, Public Admistration, Recording, Clearing and Forwarding, Social Development, Secretarial Duties, Education nk.

=> Ukiwa na D 4 upo qualified kufanya ngazi ya certificate kama nilivyoanisha hapo juu.

=> Ukiwa na D 5 sasa hapa wewe umeula!! Hapa unaruhusiwa kabisa kufanya Basic Diploma katika vyuo vyote wanavyotoa Duploma. Kwa mfano vyuo hivyo nilivyovitaja hapa JUU, chukua form yako kwa maringo achana na biashara ya kurisit omba kozi ya diploma, Teana kama una D ya hesabu na English ndo inakuwa rahisi zaidi kuchukuliwa.

=> Kwa wale waliosoma mahesabu kuna vyuo vingine kama DIT(Daar Institute), AIT(Arusha Inst) na Mbeya Tech Msishau kufanya maombi, na kwale waliopiga fresh Biology with minimum of D angalieni option za Nursing ni nzuri sana na katika vyuo vya MATC na COTC.

Kama kuna marekebisho yanakaribishwa na kama hoja ama daubt basi uwanja ndio huu. Most welcome!!

2i9m911.jpg

jidhjp.gif

samahan mkubwa kuna dogo langu yy limepata D mbil tu ya PHYS na BIOS JE linaweza kupata vyuo vya nursing?
 
Mkuu Sizinga narudi tena kwasababu kuna dogo wajirani kaniomba ushauri baada ya kusikia nikisema haya mlo andika humu.

Matokeo yake yako hivi:-
Civ D
Hist D
Geo D
Kisw F
Engl F
Phy F
Chem D
Bio D
Agri D
B/Math F
yaani Division IV ya 29.

Sasa Mkuu huyu anaweza kwenda Diploma wakati amefeli Hesabu na English? Na kama anaweza ni kwa course ipi katika chuo kipi?
Au kama hawezi kusomea diploma afanyeje mkuu?

Huyo aende vyuo vya nursing wanamchukua bila tatizo lolote.
 
Back
Top Bottom