Asante mkuuPole sana Mkuu!
USHAURI WANGU
1. Muulize anapenda nini.
Katika maelezo yake kama unashindwa kumuelewa anapenda nini basi fanya yafuatayo.
2. Mpeleke shule aanzie na masomo ya Form III kwa mwaka huu na mwakani apige NECTA. Dhumuni la kuanza Kidato cha 3 ni kujipanga zaidi, na Kidato cha ndani ndo msingi mzuri wa kufanya vema kidato cha 4. Wakati anarudia hakikisha unamtafutia sehemu inayotoa elimu bora. Pia na wewe uwe mfatiliaji sana kwake, uwe na namba hata za walimu na unawapa ela ya vocha ili wakufatilie zaidi. Wakisema wanahitaji tuition basi fanya hivyo. Mtoto aliyepata O mpaka aje kupata IV yenye D walau 5 sio kazi rahisi Mkuu. Pia nitapendekeza asome Sayansi, Sayansi inalipa sana Mkuu huko mbeleni, tofauti na Arts.
3. Akimaliza Form IV peleka Chuo, achana na mambo ya Advances, kupitia Form IV akienda chuo na kupata Diploma kama ya sayansi hivi anaweza akaajiriwa. Hapa atakupunguzia mzigo Mkuu, Diploma za Sayansi zinauzika maana mtu anakuwa na maarifa mengi tuu, akiendelea Degree akitokea Diploma haitamsumbua sana kama mtu aliyetokea Six.
***** KILA LA HERI MKUU *****
Asante mkuu, hakika nimepata kitu kutoka kwako13 mega pixel,
Kwanza pole sana, hususani kwa huyo mtoto!! Nimeona ushauri wa watu mbalimbali huku wengi tu wakishauri umpeleke ufundi. Binafsi sikushauri umpeleke ufundi mtoto mwenye sifa za Darasa la Saba!
- Kwanza kabisa usimfokee, na kama umeshafanya hivyo basi jirudi kwake! Kwavile Waafrika tuna viburi kiasi cha kwamba hatuoni kwamba tunalazimika kuwaomba msamaha watu wanaokula ugali wetu, basi unaweza kumuomba msamaha in other way round kama vile kuanza kumchangamkia as if nothing happened. The idea behind is to make her not to feel like amefanya serious crime ambayo haiwezi kuwa repelled. Akishaona upo nae, hata kurudia mtihani atakuwa tayari.
- Two, kwanini unasema hukutegemea na wala mwenye hakutegemea kwamba angepata zero? Je, ulikuwa unafuatilia matokeo yake vizuri? Kama ulikuwa unafuatilia kwa karibu, je alikuwa anasoma shule ya aina gani? Ukitaka kufahamu aina ya shule, kama mwenyewe huifahamu vizuri basi angalia ufaulu wa wanafunzi wengine. Mamia ya shule zetu huwa wanapata Division IV darasa zima lakini kabla ya hapo usidhani kwamba hapakuwapo wakali wa darasa ambao wao piga ua wapo kwenye 5 bora na walikuwa wanapiga paper ile mbaya! Kumbe kimsingi walikuwa wanaongoza darasa la wajinga na walimu walikuwa wanatoa paper zinazokidhi viwango vya darasa la wajinga! Kwahiyo ikiwa binti yako alikuwa anasoma darasa la wajinga; hapo hakuna suala la "hakutarajia kupata Zero.... hiyo ilikuwa given."
- Ukijiridhisha hayo, jaribu kutafiti level yake ya written English. Hili suala la kizungu ni jipu kwa watoto wa O-Level na tatizo zaidi ni kwamba kinawaondolea confidence. Kimsingi ninaposema level yake ya kizungu ni ile confidence aliyonayo kutumia lugha... I don't care how grammatically correct she is. Ukiona hapo kuna shida, mpeleke pale British Council. Si kwamba akitoka pale ndo atapiga ile ya Queen Lizzy, not at all but suala la yeye kwenda kusoma Kiingereza kwenye madarasa ya wenye lugha kutamjengea confidence! Atakuwa anatiririka huyo na ma-broken kibao lakini huku mwenyewe akidhani yupo right! This's all what's needed. Mtu mwenye broken English lakini ana confidence ni much better kuliko mwenye good English but hana confidence ya ku-communicate. Na huyo akishajiona amesoma English course, hamu ya kurudia mtihani atakuwa nayo.
- Baada ya yote hayo; hapo hakuna cha VETA wala nini... mrudishe mtoto darasani. Mtoto unaweza kumpeleka sehemu kama VETA angalau akishahitimu na kuwa na cheti cha Form IV na sio Darasa la Saba. Kama mfuko wako upo vizuri na unaongea na watu; jaribu kumtafutia shule ambayo atakuwa anaingia darasani kama wenzake lakini kwa yeye atakuwa anajiandaa as a private candidate. Back then Jitegemee walikuwa wanafanya hivi... mimi mwenyewe wakati tupo O-Level kidato cha IV, tulisoma na msichana ambae nae alikuwa anajiandaa as a private candidate ingawaje pale shuleni hili halikuwa jambo la kawaida sana but penye connection, nothing is impossible. Ukipata shule ya hivyo, hapo hakuna cha hakutegemea Zero wala nini; aanze tu Form III. Kufeli kwa kutogemea hakuzidi masomo mawili... unakuta mtu alikuwa fit sana kwenye Biology lakini paper inarudi F ingawaje masomo mengine amefaulu! Lakini mtu umekula F mwanzo mpaka mwisho na masomo yenyewe ali-sit kwa siku tofauti tofauti... dah, ngoja niishie hapa manake naona naongea lugha kali sana!!!
...mijitu inayo support Chama Cha Majipu utaijua tu,full kupayuka.!!Nisiwe MNAFIKI Mtafutie Bodaboda Apige Kazi Kwani Kichwa Chake Hakina Urafiki Na Shule.
Nina uncle wangu kapata matokeo mabaya sana, ambayo sikuyategemea na wala yeye hakuyategemea ila all is well.
Nimekuja kwenu wakuu kuomba ushauri, najua wapo na wengine wengi watakaofaidika na ushauri huu.
Lengo langu nataka asome. Ni options zipi ambazo zinaweza kumsaidia akaendelea kupata elimu kwa hii div 0 yake, binafsi sijakata tamaa na hata yeye nitamshawish asikate tamaa. Ni binti wa miaka 17 alikuwa huko moshi sasa nikamchukua tupo nae hapa Dar
duh hii ni kiboko!Mdada wa miaka 17 kupata 0 form 4,ni vema mpate muda wa yy kujikubal na kuachnowladge hayo matokeo. Na awe vigilant ku realise and recognise core factors zilizomfanya aface those poor results. Hii itamsaidia atakapo rud class aweze kuonyesha man's ability and man's resilience to rise from the ashes of destruction.
Mkuu, ufundi upi kwa Div O? Labda hivi vya mitaaniMpeleke ufundi
hapo hamna namna arudie tu mtihani ili apate cheti cha form 4 ambacho kitamsaidia kuendelea mbele. Kama kwenda ufundi kama wengi wanavyoshauri ni baada ya kurudia na kupata cheti otherwise atakuwa sawa na mtu aliyemaliza darasa la saba hivyo muda wote wa miaka minne itakuwa amepoteza bure.Nitafanya hivyo mkuu, ningoje atulie kwanza
Wewe ulikuwa unafuatilia maendeleo yake shuleni kwa ukaribu?
Angalia usije ukawa unatupa pesa yako mkuu. Nakushauri km hukuwa nae karibu jaribu kudurusu taarifa zake za maendeleo ya shule. Hapo utapata mwanga wapi aelekee. Vinginevyo najua dini yako inaruhusu kufuga na kula nguruwe, kama ndivyo basi mtengenezee mabanda ya kutosha na umnunulie piglets haraka sana aanze ufugaji. Utakuwa umemkomboa sana kuliko kupoteza muda wa miaka3 ya kusoma akikomaa na huu mradi hakika utamtamani na hatakusahau maishani.
Mi niko tayari kuozeshwaNina uncle wangu kapata matokeo mabaya sana, ambayo sikuyategemea na wala yeye hakuyategemea ila all is well.
Nimekuja kwenu wakuu kuomba ushauri, najua wapo na wengine wengi watakaofaidika na ushauri huu.
Lengo langu nataka asome. Ni options zipi ambazo zinaweza kumsaidia akaendelea kupata elimu kwa hii div 0 yake, binafsi sijakata tamaa na hata yeye nitamshawish asikate tamaa. Ni binti wa miaka 17 alikuwa huko moshi sasa nikamchukua tupo nae hapa Dar