Forever Living!

Forever Living!

Hodi wana JF! Hivi karibuni kulikuwa na thread kuhusu Forever Living. Wachangiaji wengi waliponda sana hii kitu. Lkn nimeambiwa kuwa jana jioni baada tamasha pale Jamhuri Stadium Dodoma, JK alienda kula chakula cha jioni na hawa jamaa pale St Gasper. Na leo mchana anahudhuria mkutano wa hawa jamaa pale Dodoma Hotel. Ataomba yana na mawaziri 6. Nasikia Forever living ni wa pili au wa tatu kulipa kodi kubwa serkalini.
Hii imekaaje? Mimi nilikuwa nadhani (na watu wengine wengi) hawa jamaa ni matapeli fulani hivi. Inaelekea shughuli zao ni halali!
Nawasilisha!

Ndio!
Shughuli zao ni halali na zinatambulika kisheria!
Yes ni wa pili kwa ulipaji kodi mi mwenyewe shahidi!
Bt lazima ujitoe kufanya kazi ukiwa mvivu huwezi, mi mwenyewe kiukweli ilinishinda!
 
Dawa ya meno 14, 000? we acha masihara nina familia ya mtu saba hapo kwenye hiyo hesabu napata colget tube saba.

Kama hizo nyingine hazikupi shida mkuu ni safi...

Bt kama mimi nilikuwa na matatizo ya meno na imenisaidia so diangalii bei hapo!
Siwapigii debe mkuu
 
Mi nawajua vzr sn in n out!
Bt kiukweli nilishindwa ila ukiamua kupiga kazi inalipa na cash uwe nayo unless utajuta
 
Hawa watu ukiwasikiliza wanakubadili akili. Kuna mmoja ni rafiki yaani imebidi hadi nibadili namba maana kila saaa lini twafanya biashara.
 
Kama hizo nyingine hazikupi shida mkuu ni safi...

Bt kama mimi nilikuwa na matatizo ya meno na imenisaidia so diangalii bei hapo!
Siwapigii debe mkuu

Matatizo ya meno si unaenda hosp mkuu au imeshauriwa kutumia product yao?
umewahi kutumia censodyne?
 
Hivi hiyo 750k napata bidhaa zipi na zipi? niorodhosheheni hapa.
Na kwanini bei za bidhaa zao ni siri. Mtu anatangaza then ukimuuliza bei anakuambia njoo inbox au impigie simu. Kwani bei zinatofautiana ktk bidhaa moja lets say lotion?!
 
Ile promosheni ya wanachama wakongwe kutafuta wanachama wapya 3.. Anapewa milioni 1 iliniachia maswali.
By the way: Wengi wao wapo njema pesa
^^
 
Nimewahi kuhudhuria semina zao na wakajaribu kunivuta lakini nilipochanganya zangu na za kuambiwa nikaona hapana hii siyo njia ya kwenda.
Kwanza, sharti lao la kwanza ni kwamba HURUHUSIWI KUFUNGUA DUKA NA KUZIWEKA BIDHAA ZAO DUKANI, YAANI KUUZA KWA MTINDO WA DUKA HAURUHUSIWI!!!!

Pili hakuna namna serikali inaweza kukata kodi ya mnufaika mmoja mmoja kulingana na commision anayopata!!. JAPO FOREVER LIVING KAMA KAMPUNI INALIPA KODI, WANALIPA KODI LAKINI KIMSINGI WAMETENGENEZA STRUCTURE YA KUKWEPA KODI ZAIDI, YAANI ILE KODI YA KIPATO CHA KILA MEMBER WAKE ANAPOPATA COMMISSION SERIKALI NI VIGUMU KUTRACE HII.

Kibaya zaidi kwa sababu ya ndoto za kupata mshiko mkubwa mkubwa kuliko kuumia kupitia njia za kawaida, BIASHARA HII IMEWAONDOA VIJANA WENGI KATIKA PROFESSIONS WALIZOSOMEA TENA KWA KODI YA WATANZANIA MASIKINI, NA KUJIKUTA WANAANZA KUWA MADALALI WA BIDHAA HIZI. Unakuta kijana/mtu alisomea udaktari, uinjinia, ualimu, uanasheria n.k LAKINI KWA KUWA HUKU ANAPOKEA KAMILIONI KAMOJA KWA MWEZI, NA HANA MUDA WA KUTOSHA KUFANYA ISHU ZA UTAFUTAJI WA WATEJA WAPYA ANAONA BORA AACHE KAZI, ILI APATE MUDA AKAKAUZE NETWORK YAKE!. at the end of the day, kweli atapata mapesa mengi ya commission lakini jamii inapata hasara kwa kukosa daktari, mwalimu, injinia etc.

hii ni pyramid scheme, ni miongoni mwa schemes za Kuinslave the masses huku wakubwa huko ng'ambo wakizidi kuneemeka, na mawakala wao katika mataifa masikini wakiambulia makombo (amabayo wengine tunaona eti ni pesa nyingi).

Kuna watu wanazinasibisha Kampuni hizi na Freemasonry na Illuminatti. JAPO MEMBER WAKE WATAKANUSHA HILI, LAKINI NI KWA SABABU HAWA WANATUMIKA TU (PAWNS) NA WAKO LEVEL YA CHINI SANA KIASI KWAMBA HAWAJUI KINACHOENDELEA KATIKA LEVELS ZA JUU ZA HII PYRAMID, HATA HIVYO WAKIPANDA NGAZI ZA JUU HUENDA WAKAELEWA THE WHOLE GAME!
 
Niko na rafiki angu kanivuta sana kuingia huko ila roho ilisita zaman sana sijui ni kwanini
 
huu uzi uwekwe sticks hpo juu halafu tutafutane baada ya miaka mitano na uhakika mnaoponda asilimia 90 mtakuwa mnajuta au mshajijiunga na hizi business
 
Lazima utumie mfumo wa kutembeza bidhaa hata kama una cash?

Kuna vitu ambavyo lazima uelekezwe jinsi ya kupata kitu kinaitwa cc! Unatakiwa upate 4 cc kwa miezi miwili inayofuatana ili uwe unapanda na ndo jinsi una earn cash.....cc ina stand insted of money ....cjui umenipata!!?
Hili somo pana...

So njia 1mojawapo ni kuuza hizo bidhaa(ndo kuna wengine wanatembea kutafutabwateja/ wanayembeza)
Pili kwa kutumia mwenyewe hizo bidhaa! Coz wanazo za matumizi ya home. ..
Tatu ni kwa kufanya watu/mtu ajiunge/join kwenye hyo bness. ...bt its not a joke! !

Nasisitiza mi nilishindwa kwakweli! !
 
Matatizo ya meno si unaenda hosp mkuu au imeshauriwa kutumia product yao?
umewahi kutumia censodyne?

Nishatumia senso naijua vzr sn..
Huko hospital ndo nilikoshauriwa na Namshukuru Mungu imenisaidia mpaka leo nipo fresh....

So product zao nazotumia ni pamoja na za nywele kwakweli suala la mmba imebaki story!

Bt bness ilinishinda!
So natumia ambavyo vinanisaidia
 
Wazee wa ushuhuda hawa, utasikia ooh sijui nilikuwa nimeajiriwa nikaacha kazi, wengine ooh mimi ni fresh graduate hamna kampuni inaweza kunilipa kipato nnachopata kupitia forever killing. Mwisho wa siku katika watu 10 wanafaidika wa 2 nane chalii.
 
Back
Top Bottom