Forever Living!

Forever Living!

Kuna DECI inapigiwa chapuo Clouds 360 muda huu, yaani watu wanadanganyana juu ya kupata pesa bila kufanya kazi!!!?
 
Kuna mambo kadhaa inapaswa uyafahamu kuhusu biashara ya Forever Living Product hasa hapa Tanzania.

1/Ni kweli kabisa bidhaa hizo zina ubora wa kimataifa lakini ni GHALI MNO. Kiufupi ubora wake hauendani kabisa na thamani ya bei zake kwa mtanzania wa kawaida (Kwa mfano Dawa ya meno ya shilingi 15,000/= ya Forever Living ni sawa na kununua Colgate za kawaida 7)

2/Sio kweli kuwa bidhaa zao ni bora sana na za kipekee kama wauzaji wake wengi wanavyoaminisha watu. Nyingi ya bidhaa zao hazina tofauti kubwa na bidhaa za kawaida zilizopo hapa Tanzania.

3/Sio kweli kabisa kuwa bidhaa zao ni dawa kamili au kinga mahsusi dhidi ya magonjwa mbali mbali. Ukweli ni kwamba bidhaa zao zina virutubisho vya kawaida sana ambavyo unaweza kuvipata kwenye vyakula vya kawaida au bidhaa zingine za virutubisho.

4/Hii ni biashara iliyokaa kimtindo wa Pyramid Scheme. Yaani faida yake kubwa iko kwa kutengeneza mnyororo na matawi ya wafuasi nyuma yako. Hivyo ukijiunga tu ujue umemtajirisha aliyekutangulia katika huo mnyororo na itakuwa hivyo milele. Na wewe ukitaka kutajirika inabidi uvutie wengine wajiunge kwenye mnyororo wako nyuma yako.

5/Bidhaa hizo haziuziki vizuri hapa nchini, wengi waliojiunga kwenye hiyo biashara waliishia kuzitumia wao wenyewe hizo bidhaa au kuzigawa kwa watu wengine, na kama waliweza kuziuza basi waliuza kwa uchache sana.

6/Biashara hii ni halali na halisi. Sio biashara ya kubabaisha au utapeli. Wanafanya biashara katika mazingira rasmi ya kisheria. Japokuwa wahamasishaji wake wengi sio realistic kabisa, watakupa maelezo ya upande mmoja tu(Faida kubwa na urahisi wa kuifanya) na watakuvutia kupitia mafanikio ya wachache waliofanikiwa vyema lakini hatakwambia kama mafanikio ya watu hao ni kupitia migongo ya maelfu walioingia kwenye hiyo biashara bila kuvuna chochote.
 
hizi porojo za kutajirika Kwa kuuza dawa asili ni hatari...wanajua sana jinsi ya kushawishi ukiudhuria seminar zao,makofi mengi mengi...mnaambiwa kujiunga uanachama Kwa zaidi ya laki nne,alafu utaanza kulipwa ukileta mtu ajiunge kwako,kama mnyororo wanaita...hapa ndipo huwa sijaelewa hawa jamaa,wanakwambia ukishalipia hiyo pesa ya kujiunga,unapewa kifurushi cha dawa zote zilizopo,in reality unakuwa umeuziwa dawa Kwa Na wewe kuwa mwanachama mojakwamoja.uhondo unakuja wanakwambia wakijiunga watu watano chini yako,unalipwa ten percent ya pesa walizotoa kujiunga.inakujaje wakati nao watakuwa wameuziwa dawa ili wawe wanachama!!!hapo ndipo utapeli unaanzia...
 
Back
Top Bottom