Una Degree, Masters au PhD lakini unaamini hawa manabii wa Leo?

Una Degree, Masters au PhD lakini unaamini hawa manabii wa Leo?

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
12,371
Reaction score
27,302
Msomi uliyefikia kiwango hicho kama nilivyo taja juu na bado akili yako haijajua kupambanua nyeusi na nyeupe ni ipi wewe ni galasa Type1

Ni ajabu kwa kweli wafuasi wakubwa wa hawa manabii matapeli ni wasomi.

Mfano unaambiwa waumini/washiriki wa makanisa ya wahuni masanja mkandamizaji na
Kapola ni wanachuo!

Yaani at least wa elimu ya chini kabisa kamaliza form4 hao ndo wanao jazana kutapeliwa na hao wahuni.

Basi ukisogea pale Tanganyika packers utakuna na kila aina ya wasomi hapo wakichunwa kama kamongo.

Kila kitengo wapo pale kutapeliwa pale kwa Mnyakyusa Elimu zote utazikuta hapo zikitapeliwa na ambae hajabahatika kabisa hata kukanyaga hata mlango wa darasa lolote pale wanakutana wote kutapeliwa!

Hapo wataambiwa watoe sadaka ya kujimaliza watatoa kweli.

Wengi tu wakiwemo na ndg zangu Mfalme zumaridi kawatapeli!

Imagine mtu ni Lecture wa chuo kikuu fulani hapa nchini anatapeliwa na zumaridi asiyejua hata kusoma a e i o u ana mtapeli professor tena kwa hiari yake kabisa bila kutumia nguvu yoyote Ile.

Huyu naye ni msomi na ana macheti ya level na level za elimu.

Lakini ukikaa ukamtafakari msomi wa namna hii utagundua kwamba ukiondoa hayo makaratasi yanayoitwa cheti anabaki na kukalilishwa tu huko shuleni na chuoni na ukiondoa haya aliyo kalilishwa anabaki empty kabisa (Pumpuni)

Hao manabii wengi wametajirika kwa muda mfupi sana na amini usiamini walio watajirisha ni hawa hawa tunaowaita wasomi wetu.

Siku moja nilikuwa kwa ndg yangu mahali fulani mkuu wa kitengo (bandarini) mida ya saa2 usiku alikuja jamaa kavaa kihuni halafu shingoni ana skafu ya Bendera ya Israel.

Alichokuwa anakuja kufanya hapo nyumbani ni kumuombea msure yule apande cheo !

Baada ya maombi kama dk7-10 hivi akachukua sadaka ya kitita cha laki5 kwa macho yangu naona.


Mwezi haukupita likatokea la kutokea hapo bandarini akafukuzwa kazi.

Kwa Wenzetu huko ulaya mambo ni tofauti kidogo wengi wa wasomi wa level za juu hata kuamini tu kuwa kuna Mungu hawaamini.

Hawa hapa ni baadhi ya wanasayansi (wasomi) ambao kamwe hawaamini uwepo wa Mungu.

1. Richard Dawkins – Mwanabiolojia wa mageuzi; mwandishi wa The God Delusion


2. Stephen Hawking – Mwanafizikia (cosmology); alisema ulimwengu unaweza kujieleza bila Mungu


3. Carl Sagan – Mwanaastronomia; alisisitiza ushahidi wa kisayansi zaidi ya imani


4. Neil deGrasse Tyson – Mwanaastronomia; mara nyingi hutofautisha sayansi na imani ya kidini


5. Albert Einstein – Hakuwa muumini wa Mungu wa dini; aliamini zaidi “Mungu wa Spinoza” (sheria za asili, si mungu binafsi)


6. Francis Crick – Mmoja wa wagunduzi wa muundo wa DNA


7. James Watson – Mshirika wa Crick katika ugunduzi wa DNA


Wengine wapo wanao amini uwepo wa Mungu kama
Isaac Newton, Gregor Mendel, Francis Collins, n.k.

Lakini Bara jeusi wasomi ndo wako mbele ya muda kutapeliwa na kuliwa kekundu daily.

Unapokuwa msomi lazima kila kitu utataka kujua/kujirizisha kilianzaje
Nasi kuambiana mambo ya imani msomi makini hayupo hivyo.



Huwezi amini huyu jamaa kwenye picha tulipiga kelele za kufa mtu humu tukiwaonya kuwa hili ni tapeli la wazi wazi humu humu kondoo zake zilitukalia kooni kumtetea.

Baada ya kufukuzwa hapa nchini bado kondoo zilikuwa zinalilia humu arudishwe.

Kesho pia kuna wasomi wetu kibao wamejiandaa vilivyo kwa kupiga pasi nguo,kusuka,malashi, suti na viatu vipya bila kusahau sadaka na zawadi kedekede ili wakatapeliwa na kuhani Musa,mwamposa, kapola na masanaja mkandamizaji.

Wengine huwaambii kitu kuhusu mchungaji hananja! Safari ni ndefu kama ulijua kunakaribia kucha unajidanganya.

FB_IMG_1765640299437.jpg
 
Ukitafakari tu yale ya Mo29 unajiuliza kazi ya Mungu sasa ni ipi?

Kama ni tunatafuta wenyewe
Chakula tunahangaika wenyewe
Tukiumwa tunachangishana wenywewe tunaenda mahospitalini na ukikosa huduma bora ndio nitolee.

Sasa kazi Yake Yeye ni ipi? Kiukwel8 kazi za Mungu zimebaki ni za kufikirika tu
 
Uchawi upo ndugu yangu
Mbona sisi hatulogwi mkuu? Mambo mengine nikuyapigia chepeo tu.

Mimi nimewahi kumpeleka dada yangu kwa malisa nikijua kabisa tunaenda kutapeliwa na hakuna kitu kitafanyika hapa. Na nikweli yote hayo hadi naenda ni kuwafurahisha tu hao waliokuwa wanalipigia chepeo.

Ukizingatia hela zimechangwa mimi nikikataa kuwapeleka tu itakuwa nina langu jambo.

Nilimapigia simu Malisa nikamwambia aache utapeli.
 
Ukitafakari tu yale ya Mo29 unajiuliza kazi ya Mungu sasa ni ipi?

Kama ni tunatafuta wenyewe
Chakula tunahangaika wenyewe
Tukiumwa tunachangishana wenywewe tunaenda mahospitalini na ukikosa huduma bora ndio nitolee.

Sasa kazi Yake Yeye ni ipi? Kiukwel8 kazi za Mungu zimebaki ni za kufikirika tu
Mkuu hivi alieita neno jua ni nani?
Nani aliliweka pale lilipo?
Je hatuwezi kwenda kulichukua?
 
Tofauti ya elimu na dini ni ipi?
Elimu inalenga:

Kupata maarifa kwa ushahidi (majaribio, utafiti, mantiki)Kuhoji na kuthibitisha mambo.

Dini: Ni jumla ya imani kadhaa za binadamu pamoja na mafundisho wanayotoa ....dini naweza kusema imejengeka kwenye imani(kiroho)
 
Ukitafakari tu yale ya Mo29 unajiuliza kazi ya Mungu sasa ni ipi?

Kama ni tunatafuta wenyewe
Chakula tunahangaika wenyewe
Tukiumwa tunachangishana wenywewe tunaenda mahospitalini na ukikosa huduma bora ndio nitolee.

Sasa kazi Yake Yeye ni ipi? Kiukwel8 kazi za Mungu zimebaki ni za kufikirika tu
Naamini uwepo wa Mungu lajini kamwe siamini hawa matapeli wa wazi wazi
 
Kuna mambo yanashangaza sana
hasa haya mambo ya dini na imani.
 
Wasomi gani mkuu?wa hivi vyuo vya Tz walivyo hitimu wakina mwijaku??hizi ni glorified secondary schools with professors hazijawahi kutoa "Msomi" by the way masuala ya imani na elimu ya darasani ni vitu viwili tofauti...
 
Back
Top Bottom