Forever Living and GNLD Products Business

Kaniki1974

JF-Expert Member
Dec 2, 2008
352
22
Hivi ni vitu gani wanajamvi? Vina tofauti na DECI? Vinatofauti na zile stori za 'alikuwa kipofu sasa anaona; alikuwa kiwete sasa anatembea'?

kindly update.
 
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Click here: MLM [/FONT][FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Rankings
[/FONT]
[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif](MLM stands for [/FONT]Multi-level marketing)
Katika hizo hapo juu, zifuatazo zina-operate Tanzania.

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]Kuna nyingine unayoifahamu?
[/FONT]
 
This is a list of Wikipedia pages about companies which utilize multi-level marketing, also known as "network marketing", for most of their sales.

Sio sahihi kulinganisha na DECI, kwani ni food supplements ambazo mtu hununua kwa cash.Hata mimi natumia!!!.
 
tatizo langu ni kwamba
pamoja na umahiri wa TFDA kuhalt metakelfin na kuteketeza madawa yasiyo na tija kwa binadamu lakini haya madude wameyakalia kimya kabisaa. Sijui kama TBS wanalo la kutueleza kama endapo waliishu cheti au vyeti vya ithibati vya haya madaijested foods. Pia Fair competition commission inasubiri nini kutembelea magodauni ya hawa walamula kuharibu maprodakti haya?

Ila utakuta madaktari ndo wa kwanza kupromoti hizi bidhaa za forevalivingi, na hata ukienda famasi utakuta wameweka spesho fremu kudisplay hizi products. Na makanisani (borne again) kuna mitandao mipana zaidi ya products hizi.

Naona mmezitaja nyingi ila kuna moja inaitwa swissgrade sijui kama ipo. Na Tianshi kutoka china sijui kama mnaifahamu. Ngoma ni mule mule wizi....
 
Nilidhani swissgarde ni moja ya products za GNLD.

Mimi nina neno la kuwaambia watu wanaotaka kujiunga kwenye hizi MLM, kwamba wajifunze kuhusu MLM na schemes kama ponzi, pyramid wazielewe. Pia kuna material mengi tu kwenye Internet watafute na kujifunza.

Asilimia kubwa ya watu wanaojiunga hujuta baadae. Kuna udanganyifu mwingi.
 
Naona mmezitaja nyingi ila kuna moja inaitwa swissgrade sijui kama ipo. Na Tianshi kutoka china sijui kama mnaifahamu. Ngoma ni mule mule wizi....

Msanii hiyo Tianshi imeenea sana bongo? Nimewahi kuisikia tu ila naona gnld na fl ndo zenyewe yani watu wengi wamejiunga..
 
Msanii hiyo Tianshi imeenea sana bongo? Nimewahi kuisikia tu ila naona gnld na fl ndo zenyewe yani watu wengi wamejiunga..
Ukitaka kujua kama tianshi ipo au la.

tembelea makanisa ya wazaliwa upya. akina mama wamejiunga humo na inakwenda fasta kweli. hii gnld imeshuka maana si sana kama awali. Nina bahati sana ya kuona uanzishwaji wa hizi schemes na huwa nina bahati ya kutoamini haya madudu.

Ukiwasikiliza ni stories ya mafanikio wala hamna swot. pia watu hawajui kwamba haya makampuni yanasaka vendors wanaojilipia wenyewe. Hivyo utakuta watu jasho linawatoka kupromoti bidhaa za haya madudu ili wapate cha juu (hewa) maana wataambiwa unakua ndani ya scheme na utapewa cheque yako very soon ukifikia somewhere silver sijui gold ah takataka tupu.

Jamani muungeni mkono Pinda na sera yake ya kupromoti kilimo ili tujikomboe kiuchumi na tuwe na akiba ya kutosha mwe! labda haya makampuni yatakuja kununua malighafi kutoka mbarali au kyela n.k
 
Hakuna kitu rahisi/cha bure duniani.

Ni kweli kabisa kuwa Network/Multi-level marketing zinalipa lakini ni kwa wale walio tayari kujituma na wenye malengo kujenga mtandao/timu imara. Kwa mfano kuna watu ninaowafahamu wameingia kwenye forever living na hivi ninavyongea wanalipwa hadi dola 10,000 kwa mwezi, lakini walichapa kazi kweli kweli kufikia hapo sio lelemama.

Watu wengi wanakosea kufikiria ukiingia kwenye biashara hii hela inapatikana bwerere lakini inabidi kweli ukaze buti ujitume kujenga mtandao wako.
 
Mtu kama huyo ni dhahiri atakuwa tayari kuwaonyesha wengine namna alivyoweza kufikia hatua hiyo. Hasa ukizingatia kwamba kwa kufanya hivyo atafanikiwa kukushawishi na ku-recruit members wapya. Ukitaka kujua kuna longolongo, jaribu kuulizia hiyo kitu.

The emphasise iko kwenye kununua bidhaa. Ili uweze kuingia kwenye hatua inayofuata (which translate to more pay), inakubidi ununue bidhaa kila mwezi tena kwa kufululiza. Forever living unatakiwa kununua (minimum) $264 per month.

Ili uweze kulipwa hiyo 10,000, timu yako lazima iweze kununua na kuuza bidhaa za thamani kubwa ile mbaya. Je huyo anayekwambia analipwa 10,000 ataweza kukuonyesha mahesabu yanavyokwenda?
 
Eee bwana wakuu heshima mbele!aisee haya madudu huku bongo yamekamata watu wengi kichizi!wengine wanaacha hata kula msosi fresh ili wapate kubuy hizo FLP Products!sie tulio na vibarua tunapata vishawishi kwa wengi ambao wapo na FLP tujiunge!kuna washikaji wameuza viwanja wakachanga nauli wakaenda Zambia ili kusaka wateja ili wapate zaidi.Swali langu ni je hizo products za FLP ni nchi gani zipo?

Ambao labda mpo huko nje ya nchi hebu tujuze!hizo products zinasemekana ni za USA?JE zina exist huko?

Huku bongo shubiri(Aloe vera) zipo kibao!kama unataka unachuma mmea wako shambani unachemsha una mix na asali unakunywa!ni dawa tosha kwa afya yako!na si mixer ya chemicals unaambiwa ni Aloe vera WIZI MTUPU!!!!!!!!wana JF TUPIGE VITA HII KITU ITATUTIA UMASIKINI.
 
Mtu kama huyo ni dhahiri atakuwa tayari kuwaonyesha wengine namna alivyoweza kufikia hatua hiyo. Hasa ukizingatia kwamba kwa kufanya hivyo atafanikiwa kukushawishi na ku-recruit members wapya. Ukitaka kujua kuna longolongo, jaribu kuulizia hiyo kitu.

The emphasise iko kwenye kununua bidhaa. Ili uweze kuingia kwenye hatua inayofuata (which translate to more pay), inakubidi ununue bidhaa kila mwezi tena kwa kufululiza. Forever living unatakiwa kununua (minimum) $264 per month.

Ili uweze kulipwa hiyo 10,000, timu yako lazima iweze kununua na kuuza bidhaa za thamani kubwa ile mbaya. Je huyo anayekwambia analipwa 10,000 ataweza kukuonyesha mahesabu yanavyokwenda?

The emphasis iko kwenye kujenga timu yenge nguvu chini yako, mafanikio yatatokana na effort ya timu nzima uliyojenga chini yako na sio mtu binafsi. Unanunua na kutumia bidhaa pamoja na kuwashirikisha wengine, then unaanza kujenga timu chini yako ukiwafundisha to do the same...in other words you duplicate yourself.
 
Sawa, hivyo ndivyo inavyotakiwa ili kufanikiwa, ila ni wachache wameweza kutengeneza hizo duplicates. Halafu wangapi wanaopewa salesmanship skills baada ya kujiunga, na kabla ya kuanza kusaka wateja? The number is very small.
Ukiwa na upline mmbovu (aliyeingizwa kwenye biashara bila kuwa well informed and without networking marketing skills), failure is invevitable.

Nakubali pia kuwa wapo wachache wanaofanikiwa sana tu, lakini ni wachache mno. Mande ametaja waliofikia kwenda hata nje ya nchi. Nami nimesikia mtu na mume wameacha kazi, wakauza shamba, nao wanasafiri kwenda nje ya nchi.
Sasa hii ya kwenda kutafuta wateja nje ya nchi unaionaje?

Narudia kusema kuwa, watu wajifunze vizuri kujua what MLM is all about and what it takes to succeed.
 
A quote from Wikipedia

It is sometimes difficult to distinguish legal and reputable MLMs from illegal [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Pyramid_scheme"]pyramid[/ame] or [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Ponzi_scheme"]Ponzi schemes[/ame]. MLM businesses operate in the United States in all 50 states and in more than 100 other countries, and new businesses may use terms like "affiliate marketing" or "home-based business franchising". However, many pyramid schemes try to present themselves as legitimate MLM businesses.

In the most legitimate MLM companies, commissions are earned only on sales of the company's products or services. No money may be earned from recruiting alone ("sign-up fees"), though money earned from the sales of members recruited is one attraction of MLM arrangements. If participants are paid primarily from money received from new recruits, or if they are required to buy more product than they are likely to sell, then the company may be a [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Pyramid_scheme"]pyramid[/ame] or [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Ponzi_scheme"]Ponzi scheme[/ame], which is illegal in most countries.

New salespeople may be asked to pay for their own training and marketing materials, or to buy a significant amount of inventory. A commonly adopted test of legality is that MLMs follow the so-called 70% rule which prevents members "inventory loading" in order to qualify for additional bonuses. The 70% rule requires participants to sell 70% of previously purchased inventory before placing new orders with the company. There are however variations in interpretations of this rule. Some attorneys insist that 70% of purchased inventory should be sold to people who are not participants in the business, while many MLM companies allow for self-consumption to be a significant part of the sales of a participant [2].
 
.....
Huku bongo shubiri(Aloe vera) zipo kibao!kama unataka unachuma mmea wako shambani unachemsha una mix na asali unakunywa!ni dawa tosha kwa afya yako!na si mixer ya chemicals unaambiwa ni Aloe vera WIZI MTUPU!!!!!!!!wana JF TUPIGE VITA HII KITU ITATUTIA UMASIKINI.
kuna siku nilekwenda shamba na nikakuta all land imejaa shubiri zilizojiotea zenyewe. Nikapata hasira sana kwa kuwa wabongo wangefikiria kidogo tu haya makampuni yangekuwa exchange wazuri sana kwa malighafi kutoka kwetu ndipo nasi tununue madudu yao.
Eti mchele unageuzwa kuwa dawa. eh we acha tu
 
Hakuna kitu rahisi/cha bure duniani.
Ni kweli kabisa kuwa Network/Multi-level marketing zinalipa lakini ni kwa wale walio tayari kujituma na wenye malengo kujenga mtandao/timu imara. Kwa mfano kuna watu ninaowafahamu wameingia kwenye forever living na hivi ninavyongea wanalipwa hadi dola 10,000 kwa mwezi, lakini walichapa kazi kweli kweli kufikia hapo sio lelemama.
Watu wengi wanakosea kufikiria ukiingia kwenye biashara hii hela inapatikana bwerere lakini inabidi kweli ukaze buti ujitume kujenga mtandao wako.

....In This Very Tanzania?? Hebu cheki nao tena mkuu. halafu tuambiane!!
 
BabaDesi,

What happens ni kwamba mwenye timu kwa kupitia timu members wake anaweza kugenerate cheki moja au mbili za $10,000 lakini vitu ambavyo huwa wanaficha ni:

1. Expenses (unakuta mtu anaingiza $10,000 kwa gharama ya $8,000)
2. Is it recurring income? (unakuta mtu analamba $10,000 mwezi huu, lakini mwezi ujao chali ... labda kafanikiwa kuuza $3,000 tu lakini hasemi hilo)

Kuna njemba ya FLP ilikuwa inanisalandia nijiunge na scheme yao nikamdrill akanipa Bank Statement yake (maana alikuwa anatamba kuwa anamake $6,000 kwa mwezi ... na kuwaambia wadau wake kwamba mshahara wake ni zaidi ya waziri)

Kucheki kumbe operations costs ziko juu pia, na inamwachia margin ya 25% to 30% hivi.

Kwa yeyote anayejiuliza MLM ni nini ... ufupi ni kwamba kwenye MLM ni utaratibu wa kuuza bidhaa mkono-kwa-mkono. Badala ya kuingia gharama kujenga liofisi likubwa, kuajiri sales team na kulipia matangazo una-recruit watu wanakufanyia marketing na sales.

MLM ni njia mojawapo kupanua biashara yako duniani kote hata kama huna mtaji mkubwa. By the way ili kumfaidisha mwanzilishi mfano wa FLP aliyeko Arizona kuna mark-up kubwa kwenye bei za bidhaa zao hapa nchini.

Mfano Aloe Vera made-in-Tanzania toka kiwanda cha Kilimanjaro bei yake ni chini ya nusu ya bei ya Aleo Vera toka Marekani ya FLP.

Wadau wa FLP watakushawishi kwamba Aloe-Vera yao ni bora zaidi ... but you know what? Mungu alitengeneza aloe vera zote sawa. Zingine ni porojo tu.

Gharama za ziada ndio malipo ya hao wadau wa FLP. Hakuna zaidi. Same goes for all other MLM products.

NENO LA ZIADA KUHUSU QUESTNET

Jihadharini na QuestNet. Wanapromoti kiglasi kinaitwa "bio disc". Glass hii ni kiini macho tu haina value yoyote inayoshabihiana na bei ya $500 hadi $600 wanayouza.

Nimeichunguza glasi yenyewe, nikakaa nayo kwa muda wa wiki moja kwenye friji kama wanavyopendekeza na hakuna chochote ilichobadilisha.

Ni glasi ilinayotengenezwa nchini Ujerumani kwa kutumia material yale yale wanayotengenezea glass za madirisha. Sema QuestNet wameongeza porojo nyingi sana kuhusu huto tuglass eti kwamba ina nguvu za ziada (+ve energy) za kuimarisha chakula na mwili wako.

Gharama ya kutengeneza unit moja ni $10 mpaka $15. Lakini wao ili waweze kukuibieni vizuri wanauza $500 mpaka $600. Cha juu hapo kati ndio chakula cha wazee wa upline.

Nimekutana na watu sita mpaka sasa ambao wametapeliwa na QuestNet na hawana cha kufanya maana walikubali kununua wenyewe kwa hiyari yao.

Inasikitisha sana. Ndio maana wahenga walisema ikiwa unaona elimu ni ghali basi jaribu ujinga.
 
Back
Top Bottom