BabaDesi,
What happens ni kwamba mwenye timu kwa kupitia timu members wake anaweza kugenerate cheki moja au mbili za $10,000 lakini vitu ambavyo huwa wanaficha ni:
1. Expenses (unakuta mtu anaingiza $10,000 kwa gharama ya $8,000)
2. Is it recurring income? (unakuta mtu analamba $10,000 mwezi huu, lakini mwezi ujao chali ... labda kafanikiwa kuuza $3,000 tu lakini hasemi hilo)
Kuna njemba ya FLP ilikuwa inanisalandia nijiunge na scheme yao nikamdrill akanipa Bank Statement yake (maana alikuwa anatamba kuwa anamake $6,000 kwa mwezi ... na kuwaambia wadau wake kwamba mshahara wake ni zaidi ya waziri)
Kucheki kumbe operations costs ziko juu pia, na inamwachia margin ya 25% to 30% hivi.
Kwa yeyote anayejiuliza MLM ni nini ... ufupi ni kwamba kwenye MLM ni utaratibu wa kuuza bidhaa mkono-kwa-mkono. Badala ya kuingia gharama kujenga liofisi likubwa, kuajiri sales team na kulipia matangazo una-recruit watu wanakufanyia marketing na sales.
MLM ni njia mojawapo kupanua biashara yako duniani kote hata kama huna mtaji mkubwa. By the way ili kumfaidisha mwanzilishi mfano wa FLP aliyeko Arizona kuna mark-up kubwa kwenye bei za bidhaa zao hapa nchini.
Mfano Aloe Vera made-in-Tanzania toka kiwanda cha Kilimanjaro bei yake ni chini ya nusu ya bei ya Aleo Vera toka Marekani ya FLP.
Wadau wa FLP watakushawishi kwamba Aloe-Vera yao ni bora zaidi ... but you know what? Mungu alitengeneza aloe vera zote sawa. Zingine ni porojo tu.
Gharama za ziada ndio malipo ya hao wadau wa FLP. Hakuna zaidi. Same goes for all other MLM products.
NENO LA ZIADA KUHUSU QUESTNET
Jihadharini na QuestNet. Wanapromoti kiglasi kinaitwa "bio disc". Glass hii ni kiini macho tu haina value yoyote inayoshabihiana na bei ya $500 hadi $600 wanayouza.
Nimeichunguza glasi yenyewe, nikakaa nayo kwa muda wa wiki moja kwenye friji kama wanavyopendekeza na hakuna chochote ilichobadilisha.
Ni glasi ilinayotengenezwa nchini Ujerumani kwa kutumia material yale yale wanayotengenezea glass za madirisha. Sema QuestNet wameongeza porojo nyingi sana kuhusu huto tuglass eti kwamba ina nguvu za ziada (+ve energy) za kuimarisha chakula na mwili wako.
Gharama ya kutengeneza unit moja ni $10 mpaka $15. Lakini wao ili waweze kukuibieni vizuri wanauza $500 mpaka $600. Cha juu hapo kati ndio chakula cha wazee wa upline.
Nimekutana na watu sita mpaka sasa ambao wametapeliwa na QuestNet na hawana cha kufanya maana walikubali kununua wenyewe kwa hiyari yao.
Inasikitisha sana. Ndio maana wahenga walisema ikiwa unaona elimu ni ghali basi jaribu ujinga.