Inalipa kama utaweza kuuza hizo bidhaa zao kwa wingi na uwaingize watu wengine wawe wanachama. The more the wanachamas the greater the reward (wenyewe wanaita points). Ukiwa na points nyingi ndo unalipwa vizuri. Nakwambia ni kazi ngumu. Kwanza bidhaa zao zina bei kubwa kiasi kwamba si rahisi kwa mtz wa kawaida kumudu kununua mara kwa mara, kwa hiyo utakuwa na kazi nzito ya kupiga debe na kuuza. Labda kama una marafiki wenye pesa na uelewa mzuri wa bidhaa hizo (of course, depending on how you convince them). Pili kupata wanachama wapya si kazi ndogo. Kama ambavyo wewe unasita kuingia kichwa kichwa ndivyo ambavyo nawe utakumbana nao hao potential members. Kwa ujumla: It's not as easy as it sounds.
Sijui kama nimeeleweka. Wenye ufafanuzi zaidi watakumwagia hapa.