Flash Back Memories: Matukio ya Boarding School

Duuuh!!! Magamba noma ndio maana kuna jamaa shule ikiwa inafungua siku anaenda shule alikuwa analia kabisa.
 
Ilikuaje mkuu sikuipata hiyo kwenye taarifa ya habari au kuisoma kwenye magazeti? maana hilio sio tukio dogo ujue?
Dah....walilificha tu mkuu...kwasababu za ''kiusalama''🙂
 
Umemsahau Mpande na mchaka mchaka wa saa 11 asubuh...mzee ugegede na kina dada Asha. Long live MTS
 
Duh huu uzi nimecheka hadi inabidi nikabadili nguo za ndani yani hahahaaaa
 
Hahaaaaa huu uzi umenikumbusha mbali sana nakumbuka kulikua na ticha mmoja alikua bingwa wa kukariri yani hata akiona kisogo tu anajua we ni nani sa siku moja tulikua tunajipikilisha wali kwenye mashimo yaliyotokana na adhabu tulizokua tunapewa za kufyatua matofali, sasa tukasikia sauti ya viatu inakuja upande wetu kucheck hv ni huyo ticha tulichokifanya ni kukimbia huku sketi tumezinyanyua juu kuficha kisogo mwalimu asitujue huku tukiacha sehemu za makalio wazi afu ticha mwenyewe ni wakiume daaah
 
Nyumbu, maana form one walikuwa wanaongozana kwa ugeni wao.
Hahahaha kama namuona ticha alivyokuwa kaganda akitizama wowowo
 

1. Gambian ni noma mkuu, mapeas yanafungwa kwenye shuka linakuwa kama rungu, halafu usiku ukifika, taa zinazimwa, form one wanaanza kutandikwa na hayo marungu ya mapeas.

2. Ikifika siku ya kula nyama sharti ujiandae vyema, maana muda wa kugawana chakula, vijana wanasukuma mlango kwa nguvu halafu kila mmoja anachukua atakachoweza kubeba kulingana na ubavu wake. Watu wanakimbia na sufuria zima la ubwabwa vichakani, ukizembea utalala njaa.

3. Kuna kijiji cha jirani kilikuwa kinaitwa minor(Maina), kule kulikuwa na ubwabwa unauzwa sh 100, ilikuwa amazing.

4. Shughuli ilikuwa ni siku za kichezo pale mabinti kutokea kifungilo na Mazinde juu wanapokuja, watu walikuwa wanakula tizi la kuongea kiingereza.
 
Siku ya wali (English day )
 
Dah..Cha ajabu walipotukamata sasa....tulikuwa na njaa sana basi walitugawia chakula na tulipo shiba wakatuachia huru bila masharti 🙂
Dah wanajeshi wetu ni wema sana wacha tuungane nao kufanya usafi kesho.
 
Hahahhaha,umekumbusha tulivyokuwa tunafoji stemp,jamani tunafuta mhuri halafu tunatumia hiyo stemp kutuma barua,pia shida ya maji ndo ilisababisha watu tupige passport size,yaani nilishaapa kamwe wanangu hawawezi kusoma boarding schools
Nakumbuka Nilikuwa nikirudi Likizo Demu Akiniambia tuwe tunawasiliana Bhas hata Kwa Barua Namwambia anza Wew!! Akituma Nachukua Colget Naweka Mambo Kitu Kipya Narudisha majibu hahaahahahhaa
 
Mimi hamna kitu nilikuwa nachukia kama kupiga deki kipindi cha mvua,maana lazima ulime sakafu
 
Nakumbuka shule zikifunguliwa ukichelewa ku ripoti shule,unapokelewa na wanafunzi wenzako kama mfalme wakijua umekuja na mazagazaga kutoka home
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…