Josephine my dear!
I have no many words but I feel responsible to preach the gospel, kukanya pale inapotakiwa kupongeza ninaposhuhudiwa yote haya bila unafiki lakini kwa staha bila kuaibisha ama kuvunja moyo. Niko na ninyi katika yote mema lakini katika dhambi sintashiriki maana inanipasa kuwa mwaminifu mpaka kufa. You got married to a man which I believe wewe ndiye ubavu wake (maana uliapa hivyo kwenye madhabahu ya Mungu) ukawa na watoto naye which means you have even a blood convenant, kama utanisikiliza mumeo yuko hai hajafa na alichokiunganisha Mungu mwanadamu katu hatakitenganisha you being one amongst hao binadamu. Sheria za kibinadamu na sympathy zote haziwezi kuondoa ukweli wa Mungu. Kama kulikuwa na tatizo neno la Mungu liko wazi ukae ulivyo wala usimjue mume mwingine tena na yeye asimjue mke mwingine mpaka Mungu awatenganishe (kifo cha mmoja wenu) kwani mkifanya hivyo mnazini. Najua nitashambuliwa na JF wote lakini ninakubali kuwajibika kwaajili ya kristo ninakuomba ukae tena chunguza moyo wako neema ya Mungu itakufungua nawe utaijua kweli. Ni bora upoteze heshima ya dunia hii lakini uiokoe roho yako na ya mtu umpendaye ambayo itabaki milele. God bless you!
Mungu akubariki unapoendelea kuihubiri injili ya Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai, lakini ninakushauri uwe makini kwenye uelewa wa injili. Yesu alikuja kusamehe dhambi siyo kuhukumu, wale wote wanaokubali makosa yao husamehewa mara moja na makosa hufutwa kwenye vitabu vya kumbukumbu. Umesoma maandiko ya Josephine, yametoka ndani ya moyo wake, ni kilio chake kwenda kwa yeye aliyemwaga damu kwa ajili ya wenye dhambi, sasa wewe ni nani tena unaehukumu? Mungu anaangalia na kuhukumu mioyo, wanadamu tunaangalia na kuhukumu miili. Mungu anajua siri za moyoni. Kwa kawaida binadamu tunaficha uovu wetu na ndio maana Mungu anawasamehe wale tu wanaokiri hadharani na kutubu dhambi zao na kuomba msamaha. Josephine amefanya hivyo, sasa jiulize wewe mwenyewe mangapi ya sirini umefanya na hutaki yajulikane?
Kumbuka dada msamaria kwenye kisima cha maji, Yesu alimwambia aende kumwita mmewe, yeye akasema hana mme, Yesu akamwambia umesema vyema kwani umeishaolewa mara tano, na huyu unaeishi nae sasa hivi hamjaoana. Maandiko yanasema yule dada wa watu alishangaa Yesu kujua historia yake yote na akaenda mbio mbio kuwaambia watu juu ya Yesu nao wakaja kwa maelfu. Yule dada na mapungufu yake hayo, alikuwa mwinjilisti wa kwanza katika maeneo yake. Mbona Yesu hakumwambia arudi kwanza kwa mme wake wa mwanzo halafu ndo amtume kueneza habari za injili? Hata baada ya tukio hatuelezwi kuwa Yesu alimwambia arudi tena kwa mme wa mwanzo.
Fikiria, fundisha injili sahihi.