Finally: Hongereni Wana-CCM Online!!

Status
Not open for further replies.

hongera mkuu,
ni wanaccm wachache sana wenye mtazamo chanya kama wako.

Hatari:
Weka Mbali na Tembo.
 
Mkuu Mchambuzi unatisha wewe ni moja kati ya wana CCM wachache ambao huwa natumia Muda wangu kusoma Mabandiko yao kuanzia yanapoanza mpaka yanapoishia. Usitegemee kabisa akina Ritz ambao tumeambiwa hapa na Mutuz Le Baharia kwamba ndio wajibu hoja wa CCM Mtanadaoni waje kujibishana kwa Hoja na wewe. Infact sijawahi kumuona mtu kama Ritz akishiriki Mijadala kama hii. Yeye hoja zake ni Dr. Slaa na Mbowe. Yaani Hoja Nyepesi Nyepesi. Hongera sana keep it up Mkuu
 
Last edited by a moderator:

- Nimeshindwa kusoma yote maana it is toolong daamn! however naomba kusema hivi kama unaaamini CCM itameguka basi wahi Chadema, kama unaamini CCM imemeguka tayari basi wahi Chadema, CCM ni treni inaondoka haiwezi kusimama, ninasema CCM itshinda mwaka 2015, hakuna atakayemeguka wala kutoka, Chadema best net ilikuwa Sitta labda angetoka, lakini Slaa amemkorofisha na kusema sana now hakuna hope tena!!

- Mbowe hawezi kugombea na akigombea atashindwa vibaya sana, kwa sababu ana matatizo mengi sana ambayo yakijitokeza kwenye kampeni itakuwa ndio mwisho wa Chadema yote!! na besides alishwahi kushindwa sasa kitakuwa chama gani hicho cha wagombea walioshindwa kila uchaguzi? Slaa ndio kabisaa, kwanza umri wake ni mkubwa mno maana by 2015 atakuwa 75, hawezi kugombea na huo umri na pia ameshashindwa mara nyingi sana hana jipya tena!!

- Zitto ndio huyo wenye hiyo NGO hawamutaki, so see Chadema ipo kwenye big trouble kuliko unavyofikiri, CCM sasa ipo sawa sana, yaaani Kinana na huu moto wa sasa mwendo ni kwa mbele tu!!

Le Mutuz!!
 

Naona mzimu wa Ritz, unazidi kukutafuna na bado kwa siku lazima umtaje Ritz, zaidi ya mara 10...sasa hapa kuna mjadala gani wa maana.
 
Last edited by a moderator:
Mijadala migumu eeh? Mnataka.msifiwe. Kwani hamkupoteza viti kwenye huo.uchaguzi? Kama una maembe kumi, ukapokonywa na aliekuwa na mawili moja, huwezi kujisifia kuwa i still have 8! Mibhange tu hii.

kwani ukizaa mtoto hawezi kukua.sasa akikua ukadai kamzidi mamake watu watakushangaa.
MTOTO ATAKUA LAKINI KAMWE HAWEZI KUMZIDI UMRI MZAZI WAKE.
So muache kujipa matumaini fake.2015 mnaeza pata heart failure kama si higypatention.
 

Eti hili nalo ni Jembe la CCM Online ha ha haa

1. Mama Kilango amegombea Mara Mbili UWT na ameshindwa

2. Mzee Malecela ameshwahi kushindwa na akagombea tena

3. Mkuu Umesoma Mahojiano ya Zitto jana hapa JF au unaleta Hoja Peremende hapa
 
Majembe ya CCM Online hayo ha ha ha huyu Jamaa mtu wa ajabu sana CCM na Ritz wapi na Wapi?

Ritz ni UAMSHO na CCM haiwataki Uamsho ha ha haaa

Ha haa haaa!! Ritz, ni noma anatisha...
 
Last edited by a moderator:
Naona mzimu wa Ritz, unazidi kukutafuna na bado kwa siku lazima umtaje Ritz, zaidi ya mara 10...sasa hapa kuna mjadala gani wa maana.

Mkuu Le Mutuz amekutaja kama Jembe la CCM online tena unasema hajaleta Mjadala wa Maana?
 

Nashukuru kwa kunirekebisha juu ya generalization ya viongozi; ni kweli, sio viongozi wote wana matatizo, lakini matumizi yangu yalilenga zaidi katika kujenga hoja juu ya uwoga wa kufanya maamuzi magumu ya kukiokoa chama, nje ya kuhimiza kila mtu arudi kundini; Pia sikubaliani na mwenyekiti aliposema kwamba nje ya makundi ya Urais, CCM ni chama imara na hakina matatizo yoyote makubwa; Ukweli ni kwamba CCM has lost its political hegemony, hence legitimacy kwa miaka zaidi ya 20 sasa na hata Kolimba alizungumzia hili tena wakati ambao hapakuwa na makundi yoyote;

Kuhusu kuisambaratisha CCM mapema kuliko kusubiria isambaratishwe na upinzani - maana yangu ya msingi ni kwamba leo hii CCM bado ni moja sio kwa sababu ya wanachama na viongozi kushiba imani, bali ni kutokana na woga unaowatawala - aidha wengi sio safi na wanaogopa kuumbuliwa watakapoamua kufanya maamuzi magumu, wengi wapo kimaslahi zaidi, na pia wengi hawaoni agenda ya kufanya maamuzi magumu itakuwa ni ipi nje ya ufisadi wakati ukweli ni kwamba agenda zipo nyingi sana na nilizijadili katika uzi wangu mwingine 'Mangula, Kinana na hatima ya Taifa Letu';

Wapo wachache wenye uelewa kwamba CCM haiwezi kujisahihisha bila ya kuvunjika lakini tunarudi pale pale - uwoga ambao unatawaliwa na siasa za ANZA WEWE;

Naomba nikusumbue kwa kusoma kidogo maneno ya Mwalimu kisha tusaidiane kujadili iwapo CCM inaweza kujisahihisha bila ya kumeguka:

Miaka karibia 50 iliyopita, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alitoa kitabu chake cha “TUJISAHIHISHE” (May 1962).

Katika kitabu chake cha ‘TUJISAHIHISHE’. Mwalimu anasema:

[“Ukiondoa matatizo wayapatayo binadamu kwa sababu kama mafuriko, nzige, kiangazi, n.k, matatizo yao mengi hutokana na unafsi. Unafsi ni wa aina nyingi. Swali ambalo twalisikia mara kwa mara, “Hali yetu ya baadae itakuwaje?”, ni swali ambalo sina shaka kuna wanaouliza kwa nia safi kabisa. Lakini mara nyingi linatokana na unafsi. Mtu anayeuliza anafikiri TANU iliundwa kwa faida yake binafsi. Ni kama kwamba TANU ilipoundwa ilimwahidi kwamba ikiwa atakubali kuwa mwanachama, au kiongozi, basi TANU itamfanyia yeye jambo fulani kama tunzo!

Anasahau kabisa kuwa TANU inajishughulisha na haja za Jumuiya kwa ujumla. Lakini kwa mtu wa aina hiyo, hata kama TANU inatimiza madhumuni yake kwa jumuiya, ataona kuwa ni umoja ambao hauna maana kwa sababu haumtimizii haja zote za nafsi yake.
Huu ni unafsi. Kama wanachama wa TANU, na hasa viongozi, hawatakihukumu chama chetu kwa mahitaji na nafsi zao wenyewe, chana hakitadumu. Wanachama wa aina hiyo ni ugonjwa katika chama.

Dalili nyingine ya unafsi, na ambayo ni ugonjwa mbaya sana ni fitina. Kanuni moja ya TANU inasema hivi: “Nitasema Ukweli Daima. Fitina Kwangu ni Mwiko.” Lakini bado tunao wanachama ambao ni wafitini wakubwa bila kujitambua. Ni wa aina mbali mbali. Wengine humwona mwenzao anafanya kosa. Badala ya kumwambia pale pale kijamaa kwamba atendalo ni kosa, watanyamaza kimya. Lakini hawanyamazi kabisa. Watakwenda kumteta katika vikundi vya siri. Mateto haya si ya kumsaidia mwenzao, ni ya kumdhuru. Hii ni aina moja ya fitina. Wengine hugawa watu katika mafungu. “Fulani” japo kafanya kosa kubwa sana hasemwi. Lakini “Fulani” wa pili akifanya kosa japo dogo, kosa lile hukuzwa likawa kama mlima Kilimanjaro. Hawa hutafuta sababu ya kumtetea “Fulani” wa kwanza, au za kumaulumu “Fulani” wa pili, ambazo hazifanani kabisa na ukweli.

Kwa watu wa aina hii, ukweli ni jambo ambalo hutegemea mtu, si kitu kinachojitegemea chenyewe bila kujali mtu.
“Fulani” wa kwanza akisema katika majadiliano kuwa mbili na mbili ni tano, wao watakubali. Lakini “Fulani” wa pili akisema sivyo, mbili na mbili ni nne, watamwona ni mtu mbaya kabisa ambaye hastahili hata kusikilizwa. Hawa hawajali ukweli, hujali nafsi tu. Kwao, ukweli ni maoni yao na matakwa yao. Hatuna budi, hasa katika majadiliano na mazungumzo yanayohusu jumuiya, tujifunze kusikiliza hoja zenyewe zinazotolewa na wenzetu, na kuzijibu zile hoja kwa kuzikubali au kuzikataa, bila kujali kama anaezitoa ni rafiki au si rafiki. Pia wanaopingwa hawana budi wakubali kuwa kinachopingwa ni zile hoja zao, sio wao wenyewe. Bila mazoea haya, mazungumzo hayana maana; yanakuwa ni kupoteza wakati, maana huwa tumekwisha kuzihukumu hoja za mtu hata kabla hajazitamka; kadhalika, hoja zetu zikijibiwa kwa kupingwa halafu tunawakasirikia waliozipinga tunafanya mazungumzo yasiwe na maana, kwa sababu tunapenda hoja zetu zikubaliwe tu hata kama si hoja safi.

Ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo; haujali adui wala rafiki. Kwake, watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa. Ukiniona nataka kulipiga teke jiwe kwa kuwa unafikiri kuwa ni dongo au mpira, natumaini utanionya. Lakini nikilipuuza onyo lako kwa sababu eti wewe ni mdogo au kwa sababu sikupendi, nikalipiga teke, basi litanivunja dole japo ningekuwa nani. Ukweli haupendi kupuuzwa.

Wakati mwingine, mtu tunayempinga huwa ana makosa kweli lakini hoja tunazozitoa ni za kinafsi na hazihusiani kabisa na hoja zake. Nikisema mbili na tatu ni sita, nakosa. Lakini ni bora kunionyesha kwamba pengine nafikiri tunazidisha kumbe tunajumlisha. Ni kweli mbili mara tatu ni sita; lakini mbili na tatu ni tano, siyo sit.a Lakini ukijaribu kuwashawishi wenzetu wakatae mawazo yangu na kukubali yako kwa kusema kuwa meno yangu ni machafu, au natoa kamasi daima, utakuwa unatumia hoja ambazo hazina maana. Huu ni mfano wa upuuzi; lakini mara nyingi hoja tunazotumia kuwashawishi watu wakatae mawazo ya wale tusiowapenda, au kukubali mawazo yetu, huwa hazihusiani kabisa na mambo tunayoyajadili.

Makosa yetu mengine hutokana na woga; woga unaotuzuia kumlaumu mkubwa japo tunajua kuwa kakosa, au unaotuzuia kumtetea mdogo anayelaumiwa na wakubwa japo tunajua hana makosa. Na msingi wa woga ni unafsi. Pengine huwa tunaogopa sisi wenyewe kulaumiwa au kupata hasara fulani. Pengine twaweza kuwa hatuna cheo chochote ambacho tunaogopa kupoteza; pengine huwa hatuna tamaa yoyote ya kupata cheo fulani. Lakini woga unaweza kutokana na tamaa ya kila binadamu kupendwa na binadamu wenzake. Sisi sote tunayo tama hii, au sivyo tusingekuwa binadamu. Woga huu huweza kumfanya mtu kuvumilia maovu, hasa kama maovu yale yanatendwa na walio wengi kwa walio wachache, au yanatendwa na wakubwa kwa wadogo. Kwa kuogopa kuwaudhi wengi tunawaacha watende makosa bila kuwasahihisha, wasije wakatuchukia. Huu ni unafsi mbaya sana Ni kweli kwamba demokrasi haiwezi kudumu ikiwa wachache watakubali matakwa ya wengi. Lakini matakwa ya wengi hujulikana katika majadiliano au mazungumzo wa wazi.

Kadhalika, matakwa ya wachache hujulikana katika majadiliano na mazungumzo. Bila wachache kusema wazi wazi matakwa yao, majadiliano hayana maana. Wakati mwingine, hata baada ya majadiliano, wachache – japo wamekubali kutii uamuzi wa wengi wanaweza kuendelea kuamini kwamba mawazo yao ni sawa, na ya walio wengi yamepotoka. Demokrasi inawapa haki, na ukweli unawapa wajibu wa kuendeleza mawazo yao mpaka wengi waone kuwa ni ya kweli. Bila hivyo Maendeleo katika mawazo hayawezekani, kwani mara nyingi wazo zuri hutokana na mtu mmoja tu. Mwanzo laweza likapingwa, pengine kwa nguvu kabisa, na walio wengi, lakini hatimaye wengi hulikubali. Huu ndio msingi wa Maendeleo katika mawazo ya binadamu.

Makosa ni makosa na dhuluma ni dhuluma, japo watendao makosa hayo au dhuluma ile ni wakubwa au ni wengi. Chama kinachopenda ukweli na haki hakina budi kiwape wanachama wake uhuru na nafasi ya kusahihisha makosa na kuondoa dhuluma. Wanachama hawana budi waone kuwa ni wajibu wao kuutumia uhuru huo, na nafasi hiyo. Wanachama wasiotumia uhuru huo na nafasi hiyo, kwa sababu ya kuogopa kuchukiwa au kupoteza nafasi zao, wanafanya kosa kubwa la unafsi, ambalo ni adui wa haki na ukweli.

Kosa jingine linalotokana na unafsi tunalifanya wakati wa kuchagua viongozi. Wakati mwingine hufanywa na wanachama; wakati mwingine hufanywa na viongozi wenyewe, au wale wanaotaka uongozi. Nimesema mahali pengine kwamba viongozi wetu hawana budi watokane na WATU. Viongozi wa TANU hawana budi watokane na wanachama wa TANU wenyewe, bila hila, vitisho, rushwa, au ujanja wa aina yoyote. Lakini mara nyingi wanachama huchagua viongozi bila kufikiri kwa makini kama viongozi hao wanaiweza, au hawaiwezi, kazi wanayochaguliwa kufanya.

Wanachama wetu watafanya makosa makuwa sana ikiwa watachagua viongozi wa ovyo tu. Hii ni jambo la hatari kwa demokrasi na chama chetu, na maadui wa TANU wanaweza kusema kwamba demokrasi haina maana kwa sababu haizai viongozi wanaoweza kazi zao. Hii ni kweli, maana wote twajua kwamba demokrasi inaweza kuchagua viongozi wazuri. Lakini ni wajibu wetu katika kuhifadhi demokrasi kuona inachagua viongozi ambao wanaziweza kazi zao. Kazi za kuchagua viongozi ni kazi ya wanachama wetu; lakini viongozi wetu wanaweza kusaidia kwa kuelezea wanachama wetu kwamba jambo la kuchagua viongozi ni kubwa sana. Haifai kuchagua kiongozi kwa sababu ni mjomba, au binamu au ana sauti au sura nzuri. Wala haifai kuacha kumchagua mtu kuwa kiongozi kwa sababu kama hizo. Jambo kubwa ni kuchagua kiongozi mwenye tabia nzuri na anayeiweza kazi. Hatuna budi tutii kanuni hii katika kuajiri wafanya kazi katika TANU au Serikalini. Hawa pia hawana budi wachaguliwe kwa sababu wanaiweza kazi wanayoajiriwa kufanya, na ni watu wenye tabia nzuri.

Kosa jingine ni kutojielimisha. Kanuni yetu moja inasema: “Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu wote na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote”. Wengi wetu hufikiri kuwa kujielimisha ni kwenda Kivukoni, au kupata nafasi kwenda kusoma katika nchi za nje. Wengine hufikiri kuwa kujielimisha ni kujua kusoma na kuandika. Hilo ni kosa, lakini sio kubwa kama la pili. Wengi wetu, hasa baadhi ya viongozi, hufikiri kuwa tunajua kila kitu na hatuna haja ya kujifunza jambo lolote zaidi. Mtaalamu mmoja wa zamani alisema kuwa “mwanzo wa elimu ni kutambua kuwa haujui kitu.”]

Mwalimu Nyerere, Tujisahihishe, kurasa 1- 4, May 1962.
 
Eti hili nalo ni Jembe la CCM Online ha ha haa

1. Mama Kilango amegombea Mara Mbili UWT na ameshindwa

2. Mzee Malecela ameshwahi kushindwa na akagombea tena

3. Mkuu Umesoma Mahojiano ya Zitto jana hapa JF au unaleta Hoja Peremende hapa

- Powa now look, Slaaa amegombea Urais ameshindwa akaishia kupata kura yake mwenyewe, Mbowe pia akaishia kupata kura yake mwenyewe, Mtei aligombea na yeye akaishia kuapta kura yake mwenyewe tu, meaning kwamba wananchi hawawataki, Mama Kilango ni Mbunge wa Same East, Malecela ni Makamu wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, sasa utawalinganisha vipi na Viongozi losers?

- I mean sometimes sitaki kusema mnanilazimisha tu, huna hoja wala idea ya kinachosemwa hapa sasa wewe tulia pembeni, sasa unataka nisome mahojiano na Zitto ambaye wenyewe huko Chadema mmsema mko tayari kufa lakini hawezi kuwa mgombea wenu, wewe na wenzako Chadema hamtaki kumsikiliza lakini unataka mimi ndio nimsikilize? REally?

Le Mutuz!!
 

Mkuu kuna option nyingine. Kama mtu ni mkereketwa wa chama na akaona na kuamini kama chama kinaenda vibaya na bado anakipenda, nadhani kuna option ya kujikosoa na kukosoana kwa nia njema.

Mtambuzi ameongea juu ya kujikosoa na amenukuu mwongozo. Tusione kama watu wanaolenga kukosoa ili kujiimarisha ni maadui wa chama, wala tusiwashinikize waondoke.

Kwani tukibaki na wapumbavu wanaotupigia makofi kwa kila kitu tutafaidika nini na makofi ya wapumbavu?
 
le mutuz
Pamoja sana! hapa makamanda wanaweweseka wapo wengi sana ila kwasababu wao kazi yao ni kupiga kelele mchana kutwa hoja hawana! CCM mwendo mdundo!!

Chama
Gongo la mboto DSM

CC: Ritz; zomba
 
Last edited by a moderator:
Mkuu @W.J. Malecela Heshima mbele

Sijawai kuelewa wewe umekuwa na siasa za namna gani

Maana ya picha au muonekano wa picha unaweza kuleta maana nyingi

Hebu tofautisha hizi picha na jiulize unaishi maisha ya namna

HIVI UNA NYEGE NA WADADA?

















 

- Mchambuzi ana nia moja tu nayo ni kujaribu kuuvuruga huu mjadala, maana mada inaongelea ishu tofauti na anazozisema, mimi nimewapongeza watetezi wa CCM online, yeye anasema nini sielewi kabisa, CCM ipo sawa sana mabishano ya makundi ndio Demokrasia yenyewe, tumekutana Dodoma na mambo yamekwenda powa sana!!

- Sasa tunajikosoa wapi? majuzi tu CCM tumeshinda Udiwani, tumewashinda Chadema mpaka Mwanza wameanza kurushiana viti, sasa hapa nani wanatakiwa kujikosoa walioshinda au walioshindwa udiwani?

I mean Kidumu CCM!!

Le Mutuz!!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…