Fimbo aitumiayo Spika ina maana gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fimbo aitumiayo Spika ina maana gani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng'wanza Madaso, Apr 14, 2010.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Wakuu kuna ule mkongojo unaobebwa kwa ulinzi mkali na Spika akiwa nyuma yake una maana gani? Na je bila siwa kikao cha Bunge hakiwezi kuendelea?
  [​IMG]
   
 2. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Wajinga ndio waliwao. Tabia ya kuiga mambo ya kijinga, kwenye bunge la UK spika wao hutumia mkongojo huo kugonga mlango kuashiria kwamba malkia anaingia bungeni hivyo wabunge (subjects) wakae kimya maana malkia anaingia au pengine one day Charles akiukwaa mfalme anaingia wakati wa kufungua vikao vya bunge na wote lazima wasimame sio wakae chini kama sikosei tena huwa wanaitwa kwenye chamber nyingine. yaani ni ujinga mtupu, sasa waswahili na u-loafer wao wakaona nalo hilo ni tija.
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  teh teh teh teh teh teh heheheheheheheheheheheheh
   
 4. R

  Rubabi Senior Member

  #4
  Apr 14, 2010
  Joined: Nov 30, 2006
  Messages: 174
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Good point.
  Kama wabunge wetu mpaka vitu basic kabisa kama hicho kifimbo lazima wageze waingereza unategemea nini?Ndiyo inferiority complex yetu i.Huu ujinga unakwenda mpaka chini kabisa.Ndio hayo, tunashangaa nini?Mpaka ujuzi wa kulima nyanya wasomi utasikia raisi anataka wataalamu kutoka nje.

  Bongo utaona wasomi wanasheria wanavaa wigss zile nyeupe uliza hizo wigs zilianzia wapi na ni za nini

  Ujinga wa mwafrika.
   
 5. nyaunyau

  nyaunyau Senior Member

  #5
  Apr 14, 2010
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  matumizi ya ile siwa bungeni si ujinga,ni tendo la heshima ya pekee bungeni.
   
 6. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  si kila kitu ni ujinga jamani, dah, ikiwa ni hivo basi hata elimu tulizo nazo

  ni ujinga maana ni hao hao wazungu zilianzia kwao, si hivo tu bali hali

  hata matumizi ya hizi computer tunazong'ang'ana nazo kubofya key bord ni ujinga maana pia ni

  elimu toka kwao, na kama jambo ni jema na halina athari kwa jamii? kwa nini

  usiige? acheni hizo hayo pia ni mawazo ya ujuha na kujikinai

  kiujumla sisi hatuna cha kujivunia, labda majungu na umbea
   
 7. MARIJANI

  MARIJANI Member

  #7
  Apr 14, 2010
  Joined: Mar 31, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kaka unaonekana mfurutwa kama huna mahaba ya dhati na ujuha unaolifunika si tu bunge bali hata hao wanaoliongoza ila ni vema na haki yako ya kikatiba kama mnavyodai kwa lugha zenu kaka. Ila ukweli ni kwamba fimbo yenu hiyo haina maana yoyote. Kama ipo weka hadharani sio porojo tuu. Ingekua heshma kama kingetengenezwa hata kinyago chenye asili ya TZ lakini siwa inafanana na kitu gani TZ? Basi tengenezeni hata iwe na taswira ya mlima K'njaro inakshiwe na tanzanite angalau unaweza sema ni heshma kwa rasilimali zetu hii heshma unayosema ni ipi kaka? Tuweke wazi sio heshma kama wimbo tuu mkuu.
   
 8. MARIJANI

  MARIJANI Member

  #8
  Apr 15, 2010
  Joined: Mar 31, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Heshma kivipi mkuu? sema ni utaratibu wa pekee labda nao bado sio maana ni kitu cha kuiga tweke wazi acha porojo maana hazijengi kitu tueleze uhusiano wa siwa na hoja bungeni au siwa na spika. Au siwa na miongozo kama hamna tukubali tu kuwa siwa ni alama ya kuiga na haina msaada wowote wala mahusiano yoyote kati ya siwa na bunge. Mkuu weka wazi ikibidi mpaka mwisho wa uelewa wako usihofu challenge ni mambo ya kawaida. SIWA hamna kitu pale.
   
 9. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #9
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Ndugu punguza jazba kidogo... Thread inazungumzia kuiga taratibu za Muingereza na si matumizi ya technology... Watanzania tulikuwa na mabunge yetu tangia enzi kabla mkoloni hajaja, ni kiasi cha kufufua zile taratibi za Kitanzania (Kiafrika) na kuzikarabati kidogo ili ziendane na wakati.

  Sasa nambie uigaji wa kuvaa wig kwa wanasheria unasaidia kitu gani, kama si ulimbukeni!?
   
 10. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mkuu naomba unieleweshe uwepo wake pale una wakilisha nini?
   
 11. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #11
  Apr 15, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280

  Mkuu unaiga mambo ya maana sio kila kitu, unapolinganisha computer ndio unapopotea njia ni sawa na lugha ya kiingereza waswahili wanaitukuza kama vile sijui ni kitu gani. Nchi nyingi duniani hazitumii kiingereza kama nchi zetu zilivyoikumbatia angalia nchi kama japan, au scandinavian countries wanatumia lugha zao sisi kushadidia kiingereza tu na kukandia lugha yetu ya kuzaliwa ni ujuha tu hakuna lolote.
   
 12. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #12
  Apr 15, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Kwanza wewe umeuliza ule mkongojo mbona hujauliza hata lile joho analovaa. Mimi nakwambia majuha wengi sana hapa Tanzania, utakuta jua kali na joto tele jamaa kafunga tai na jacket juu sasa hapo utasema nini? Sisi tunaiga hata mambo yasiyokuwa na ulazima angalia Viongozi wa chama cha majambazi kila uchwao kiguu na njia kwenda London kufanya shopping za nguvu yaani hawaridhiki na walichonacho. wataagiza matunda kutoka ulaya fenicha toka ulaya kila kitu hata madawati yatengenezwe ulaya. Yaani wasomi wengi bado ni mambumbumbu akili zao bado zipo kwenye utumwa.

  Hivi lile joho ameanza kuvaa lini? Sikumbuki wakati wa enzi za spika Sapi Mkwawa kuliona.
   
 13. T

  Tom JF-Expert Member

  #13
  Apr 15, 2010
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Halafu ulizia hilo joho na siwa vyatoka wapi na bei gani. WanaCCM watasema hata tuwe na shule bila madawati na walimu lakini hivyo lazima vinunuliwe. CCM ndivyo walivyo.
   
 14. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #14
  Apr 15, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hujakosea mkuu, lakini kumbuka kuwa toto baya zuri kwa mama yake

  nadhani mimi na wewe twaweza tusijue vizuri maana yake zaidi ya

  walio iga, svyo, nikipendacho si rahisi kikapendwa na wote, na

  wakipendacho wote naweza nisikipende mimi, hapo ni self service
  zaidi
   
 15. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #15
  Apr 15, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hapo jazba ni mtizamo wako mbovu tu, labda nikuulize wewe una kipi cha kijivunia

  kama taifa? pengine hata avatar ([​IMG]) yako yenyewe haina hata fundisho, na ni ya kuiga pia.
   
 16. m

  mtemi Member

  #16
  Apr 16, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimekubali changamoto hiyo, mambomengi watz tunaiga kama hatuna akiri hasa ukianza na viongozi wetu wameshashindwa kufanya ubunifu kwa kutumia asili yetu hasa makabila yetu yapatayo 120 tumeshindwa kubuni vazi la spika ,wanasheria,nk ina maana hapo kale hakukuwa na mabaraza ???????

  hatuna jipya kweli tumefuliaaaa kimawazo
   
 17. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #17
  Apr 16, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Kaazi kweli kweli!
   
 18. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #18
  Apr 16, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Jamani eh hebu acheni malumbano khs hicho ki Fimbo.km mna ki maindi si mchonge vya kenu.
   
 19. F

  FM JF-Expert Member

  #19
  Apr 16, 2010
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pamoja Mkuu, nijuavyo mimi siwa ni ishara ya mamlaka ya bunge full stop.
   
 20. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #20
  Jun 28, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kuiga kubaya tufuate tamaduni zetu.
   
Loading...