Je, msimamo kuhusu vijana kwenda kusoma nje ya nchi bado ni uleule?

Braza Kede

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
1,731
3,369
Wakuu

Wasaalam

Kumradhi, naomba niwarejeshe siku za nyuma kidogo kulikuwa na mjadala humu juu ya vijana kwenda kusoma nje ya nchi na mwelekeo ulikuwa ni vijana hawa wasiende huko nje badala yake wasome hapahapa maana wakienda huko nje wanakuwa kama dodoki wanafyonza kila kitu wanachokutana nacho huko pasipo hata kuchuja matokeo yake wengine wanarudi ni mashoga, wala unga, wengine malesbian nk., almradi tafrani.

Na wengi walishauri kama ni lazima kijana husika aende basi awe na umri wakuweza kuchambua pumba na mchele.

Sasa muda mrefu umepita toka mjadala huu kujadiliwa hapa na huku duniani mambo yanakwenda yakibadilika. Je bado ule mtazamo wa kuwa vijana wasalie kuhitimu muungano primary skul una mashiko?
 
Back
Top Bottom