Filamu za kitanzania: Mazuri na mabaya

mkuu muda wa kuingia youtube hawana wako utamu wanajibu comments......
 

Niliiona movie hiyo nikaona kweli upumbavu mtupu; sijaona movie nyingine nyingi ila nilipata kopi ya hiyo OPRAH kutokana na matangazo yake nikadhani huenda itakuwa nzuri. Hakuna professionalism yoyote hata chembe moja. Wangemwoma jamaa wa Bongoland awe anawasaidia kutengeza movie zao.
 
My take to Bongos movies:

Actors/actresses are school dropouts who seek refuge in the industry to swindle easy monies. The so called movie directors are mere conmen!!

There is no professionalism at all. My suggestion if at all they plan to understand me is that they should start with DRAMA. oh, wait a minute... do we have drama theaters? No! So, no movies, no industry! Wizi mtupu!!!!
 
Movie Bongo!!! Msinitapishe Nyie hizo ni Video Game Ndugu zangu Movie mchezo! ....Filamu iliotengenezwa nchini Kenya Mwaka 1977 MLEVI Mpaka leo ipo katika mahadhi ya Kifilamu Kuliko hizi Tamthilia zenu za Leo.
Hiyo movie ya Mlevi kwa kweli ilitengenezwa kwa ubora wa hali ya juu, hakuna ubishi katika hilo.
 
Ni kweli kabisa filamu zetu zina ubora mdogo na maudhui ambayo hayakupangika hata kidogo. kila siku utaona watu katika magari na nyumba kama wanigeria vile. Nafikiri kwa mazingira yetu tuna kazi ya kufanya. Ni hawa hawa wanatayarisha video za wanamuziki wetu ambazo hazina ubora kabisa. utakuta video iliyopigwa na Komedi Original ni nzuri kuliko ile halisi ya mwanamuziki wanayemuigiza. lazima tufanye kazi ya ziada na kuwekeza katika ulimwengu wa filamu.
 

If the wheel is invented, you dont have to re-invent. Kwanini wewe upitie uchuro huo huo wakati unajua kuna jinsi ya kuruka? usilete sababu za namna hii, kwani ndio maana waafrika hatuendelei.
 
Haha kuna Movie moja nilikua naangalia kuna scene jamaa yuko chumbani na demu, sasa mle chumbani kuna kabati lenye kioo, basi camera man na yule sound tech wakawa wanaonekana full length!!! na sio for a few seconds ilikua ni karibu scene nzima!!
Sidhani kama inawezekana kuwa hawakugungua hilo, kweli hawapo serious na kazi!!!
 
I am a big movie fan. I am a big Nollywood (Nigeria) and Bongowood (Tanzania) films. Ama kwa hakika mwanzo mgumu kwa wote.

Nadhani kitu kimoja lazima tuangalie between Nollywood and Bongowood ni kwamba they are both African stories and they are bound to be the same! Bollywood has copied tremendously from Hollywood, Hollywood has copied tremendously from Hong Kong movies. These are from different continents but us here in Afrika our stories are the same, these movies, though I agree they are sometimes not of the best quality, are truly African.

To those who are exposed to WWE, many say its fake but they are missing the point! Its about entertainment - watch it for the entertainment value and don't watch it searching for the falseness. Watch Bongowood with the facts that the movies are made on limited budgets, technology, and maybe even newness. Zina makosa madogomadogo lakini how many western movies you also see mistakes or even microphones etc? Remember the bogus movie "Belly" starring Nas - there was a couple of scenes in there that showed the mic. In "Commando" after Arnold rolled a yellow Porsche denting it he was seen driving it off as if new! and many more.

Bongowood is suffering from kutokuwa makini but actually there are some gems - have you watched "Masaa 24"? Some of the movies written and starring Lucy Komba are pretty good. The acting groups such as those like Kaole or that which has Mzee Small and Bi Chau and Kingwendu are also good entertainment. "Simu ya Kifo" and if you fail you can't miss Bongoland II - afterall it is a Bongowood film isn't it?
 

Mkuu Vindunda thanks a million times kwa mchango wako ndugu na ubarikiwe.
You said it all mkuu.

Ni kweli kuna factors nyingi sana zinazofanya movies za kibongo zinaonekane na katika kiwango kisichoridhisha ikiwa mojawapo ni budget finyu, uzoefu mdogo kny sanaa hii, soko la sanaa hiyo etc. Hata na hivyo sijui mtoa mada hii ameshaangalia movie ngapi za kibongo, mi naamini sio zote ni mbaya zipo ambazo ni nzuri sana kama zile zilizo washilikisha kina Kanumba, Kigosi etc so kuzijumlisha zote kuwa ni bomu tunakuwa hatuwatendei haki wasanii wetu wanaojitahidi kujikwamua kutokana na umasikini kwa njia hii.
 
Tatizo letu tunapenda mno kukurupuka, mtu ukiwa na camcorder moja na computer yenye adobe premiere au final cut tayari unataka kuwa movie producer halafu unkimbilia kutengeneza film iishe in one week sababu unabana matumizi. Pia hatutaki kujifunza kuhusu utengenezaji filamu, internet hii hii ina materials za kumwaga kuhusu film making (tafuta hata kwenye google) lakini do we do that? nooooo....tunaishia kwenye ze utamu!

Tuache kuangalia nigeria kama ndio waalimu wetu pekee katika filamu za africa. Tuwe na vitu original kutoka hapa hapa kwetu na sio kung'ang'ania themes za nollywood (uganga, uchawi, mashetani na majini)...uigizaji wetu tunawaiga wanigeria wanavyoongea kwa msisitizo huku wametoa mimacho, uvaaji tunawaiga wao pia ili mradi vurugu tupu!

Kuna nchi nyingi za africa zinatengeneza film nzuri sana kuanzia misri, algeria, senegal, mali, afrika kusini nk...kuna watengenezaji filamu magwiji wa kiafrika kama Sembene Ousmane... tujifunze kutoka kwao pia. Hivi karibuni tu kulikuwa na Pan African Film festival huko Burkina Faso, natumaini tumeweza kujifunza chochote toka huko.
 
movie za kibongo ni za kisenge sana...
i dont watch them...ni usenge mtupu...
i'd rather go for american movies...
thats all

Duh post ya kwanza na matusi makubwa hivi... Mkuu nadhani ndani ya JF kuna watu wana matusi zaidi yako ila sio mahala pake... people are here kujifunza na kupata consrtuctive criticism - JARIBU KU-EDIT POST YAKO MKUU

Back to the point, ni kweli movie za bongo bado, lakini nadhani tujitahidi kukosoa na kuwapa feedback waandishi, waongozaji na mabaraza husika ili kuweza kuwashauri... Nimeangalia africa movie kwenye dstv kuna baadhi ya hizo movie sio mbaya sana

na pia tugundue bado tuko kwenye home video status, safari bado ndefu na kuwasaidies hao wasanii kusonga mbele
 
Well said,

Nimeunganisha hizi topics na naamini hii itakuwa mada ambayo ni fundisho kwa watengenezaji wa filamu zetu na waigizaji wake.

Kila la heri wakuu katika kuzipitia filamu zetu na kuwaonesha wapi wanakosea na wapi wanatakiwa kuongeza juhudi zaidi.
 
Nimeshindwaaaaa, nimevumilia; Oooops, ulimi hauna mfupa-kumbe inawezekana ndo tatizo linalowakabili watengeneza sub-titles za filamu za kibongo!Nilichokususdia kusema ni kwamba, nimevumiliaaa; nimeshindwa na sasa nimeamua kuweka wazi!hivi, ni nani anatengeneza sub-titles za filamu zetu? Ni kwamba kidhungu kimewapiga chenga kiasi hicho au ni haraka ya kuiwaisha filamu sokoni? Au ndo tuseme mambo ya kufupisha maneno kama tulivyozoea kwenye sms ( kwa simu za mkononi)?Binafsi, hamna sababu yoyote kati hizo ambayo ni ya msingi zaidi ya kuonesha kwamba watengenezaji wa subtitles na filamu zetu kwa ujumla, hawapo serious katika kazi zao. Hivi sasa, kwenye filamu nyingi wanajitahidi ku-include na subtitles, bila shaka ili kuzifanya zivuke mipaka ya nchi yetu! GOOD IDEA!! Sasa kama lengo ni kuzifanya zivuke mipaka ya nchi yetu; sasa mbona hawapo serious kwenye subtitles zenyewe? Wacha nitoe mfano wa filamu moja ambayo jana nimeiona kupitia kituo cha televisheni ya CITIZEN. Jina la filamu hii silifahamu, isipokuwa muhusika mkuu ni Blandina Chagula/Johari (lakini katumia jina la Martha). Martha alianza kama msichana mdogo mwenye kufurahia maisha kabla baba yake hajafungwa jela kwa miaka 7 na mama yake kufariki kutokana na mshituko kufuatia kifungo cha mumewe! Baada ya tukio hilo, shangazi wa Martha akahodhi mali zote za kaka yake(baba yake Martha) na Martha kupelekwa kijijini ambako baada ya kumaliza elimu ya msingi tu akawa analazimishwa kuolewa na chapombe mmoja hivi( nazani huyu bwana anajiitaga Kenyatta(sina hakika sana)! Baada ya kufuatilia subtitles hizo, niligundua kwamba katika kila subtitles 3 zinazotokea kwenye screen, basi 2 zina mapungufu makubwa ambayo mengine ni ya kubadilisha maana mzima(na kuweka opposite meaning). Sikufuatilia sana, lakini pamoja na hayo, niliziona zifuatazo:
· Nina she was going……hivi tangu lini noun na pronoun zikakaa pamoja?
· You are a big layer, wakimaanisha huyo mtu ni muongo mkubwa na badala yake kawa mtaga mayai mkubwa!
· I promise I never let me down…eti wakimaanisha siwezi kukuangusha!
· You show as good discipline… wakimaanisha Martha anaonesha nidhamu mzuri
· Hello my fiancé …ni Martha huyo anakuwa fiancé, yaani mchumba!
· I waiting to you….wala sijajua walitaka kusema nini!
· Why you fos me…jamani, hivi si utani huu ikiwa lengo ni ku-capture international market?
· You parents…eti walikuwa na maana ya “wazazi wako”!!
· Stand up out….jamani, inawezekana ni punctuation problem, lakini kwanini wasiwe serious kwenye mambo muhimu kama haya?
· Thans so much…si mzaha huu?mnakimbilia wapi jamani?
· As long as your here…..sehemu nyingi sana kuna tatizo kati ya “you are” na “your”!
· Next week your going…..hata mimi kidhungu sikifahamu, but this is too much!
· What ca I do…..? acha wajanja wawaibie filamu zenu kwavile mnafanya mchezo kwenye kazi, manake hii “ca” imetumika sehemu nyingi sana!
· Your doing good……au ndo mimi nisiyejua ninachoongea?!
· I can’t leave in this life……eti nasikia kuna baadhi ya shule wanataka kufundisha kijeremani huku bado tukifahamu leave ni kuishi!

Sawa, Kiingereza sio lugha yetu, lakini utafanyaje masihara kwenye serious issues namna hii? Kwanini hiyo kazi wasipewe watu wanaofahamu lugha kidogo? Wahusika wa filamu hii ni miongoni mwa waigizaji wakubwa hapa TZ (Kuna Blandina, Dr. Cheni, kuna akina mama wawili ambao nao ni waigizaji wakubwa tu, kuna Aunt Ezekiel, Issa (nimesahau jina lake la kisanii, ila nazani ni m zanzabri huyu bwana kutokana na lafudhi na rangi yake, na ni muigizaji mkubwa tu); vilevile kuna binti mmoja mdogo ambae ambae ali-act kama Martha alipkuwa mdogo; zamani alikuwa mtangazaji wa kipindi cha watoto ITV, nae ni muigizaji mkubwa tu haya kama ni binti mdogo!Nimetaja wahusika hao kuonesha kwamba naamini waandaji wa filamu hi wababaishaji vinginevyo wasingeweza kuwa-recruit wasanii wakubwa hivyo! Sasa kama hivyo ndivyo, kwanini wameshindwa kuwa serious kwenye issue muhimu ya subtitles? NAJENGA HOJA!
 

Nadhani tukiiwekea font nzuri kama hiyo itakuwa friendlier!..( iam playing with forties dear!)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…