Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
- Thread starter
- #81
Naomba nitumie nafasi hii kuchambua aliyosema Mwalimu na kuonesha ni kwanini karibu wachangiaji wote wamekwepa alichosema na badala yake wameenda kwenye mambo ya luninga, kula yanga, n.k Najaribu kuongoza mjadala on an intellectual level ya kuangalia alichosema Nyerere na idea zake kuzichambua kwa kuziangalia idea hizo na si kingine. Philosophically, kujaribu kuona the validity of their assumptions and the plausability of their contents.
Natumaini tunavyoendelea mbeleni watu watazungumzia idea zenyewe na si kitu nje ya hizo kwani kufanya hivyo tutakuwa tunashikiri katika mjadala muhimu sana kuhusu mawazo na fikra za Mwalimu.
Afrika lazima ibadilike; kutoka bara ambalo linasubiri matukio nje yake yenye kusababisha mabadiliko kuelekea bara ambalo watu wake wanasimamia mabadiliko yao wao wenyewe. Ni nini kuarticulate ukweli kuwa lazima tuwe "a continent which challenges the environment and adapts it to mans need." Hakuna aliyeonesha ubaya wa fikra hii.
Mwalimu anasema pasipo utata kuwa Africa must change her Institutions. Kwa maana ya kwamba vile vyombo ambavyo tulikuwa tumevizoea au ambavyo vilikuwa dhaifu havina budi kubadilishwa na kuboreshwa. Na ukiangalia utaona kuwa wazee wenzangu hapa ndicho wanachosema kwamba kuna vitu (institutions) ambazo hata leo hii vinahitaji kubadilika. Ni ubaya gani wa fikra hizi za Mwalimu kuwa "Africa must change her institutions to make feasible her new aspirations" What is wrong with this self-evident truth? Hakuna aliyeonesha hadi hivi sasa.
Mwalimu alisema vizuri tena kama prophetically ( I use the term rather liberally) kuwa Bara letu lazima libadili mitazamo na vitendo vyake. Ukiangalia hili ndilo ambalo wengi tunalijadili tunapoangalia mapungufu ya Mwalimu n.k tunasema tunataka tubadilike, tunasema tubadili attitudes zetu na matendo yetu. Ili tufikie malengo (objectives) ya kujenga taifa la kisasa na la watu wenye kufurahia Taifa lao. Tunasema tunataka tubadilike. Tunapozungumzia kuzingatia misingi ya utawala wa sheria, kuwa na maadili n.k tunachosema ni kuwa vitu hivyo havipo sasa na tunataka tubadilike. Hivyo tunakubaliana na Mwalimu kuwa we need to change our "attitudes and practices to accord with the objectives." Kuna ubaya gani katika ukweli huu mwingine kuwa kama kweli tunataka kufikia malengo yetu hatuna budi kubadilika? Hakuna aliyeonesha hadi hivi sasa.
Mwalimu anasema mabadiliko hayo hayana budi yawe mazuri. Kwa maana kubadilika kuelekea ubaya si mabadiliko tunayoyataka. Alichosema na ambacho kinashuhudiwa na wachangiaji wengi hapa ni kuwa tubadilike kuelekea upande chanya. Tunapoangalia historia yetu na kuona mapungufu ya viongozi waliotutangulia tunaona ipo haja ya kubadilika. Kubadilika huko siyo kurudia kanuni, na mifumo ambayo imeonekana imefeli au ilikuwa na kasoro kubwa lakini ni kubadilika kufuatia kitu kilichobora zaidi.
Na katika kufanya hivyo twaweza kujikuta tukirudia baadhi ya kanuni za msingi au fikra za msingi zilizotujenga sisi kama Taifa (kama tutakavyoona huko mbeleni). Kurudia ubovu au vitu hasi Mwalimu alikataa; kasema wazi mabadiliko tunayoyahitaji ni yale mazuri. Sasa kuna ubaya gani katika hoja hii ya Mwalimu kuwa "Changes must be positive"? Hadi hivi sasa hakuna aliyeonesha ubaya wa hoja hiyo ya Mwanafalsafa Mwalimu.
Mwalimu hapa anaonesha wazi kuwa Afrika inaweza kuchagua watu wengine waamue mabadiliko ndani yake au yenyewe ibadilike yenyewe. Kwamba waafrika wenyewe waamue hatima ya maisha yao na kiasi cha mabadiliko wayatakayo. Leo hii tunapozungumzia mabadiliko wengi tutachukia na kukasirishwa wakija wazungu na kutuambia tufanye hivi au vile kwa vile wanaamini hivyo ni vitu vizuri kwetu.
Wengi tutaona tumetukanwa na kudharauliwa kama Wamarekani wakija na kusema "badilisheni Katiba yenu", fanyeni hivi au vile. Yawezekana wakawa wanasema kweli lakini yawezekana wengi tungependa kuona kuwa ni sisi wenyewe tunaamua nini tunachotaka. Sasa kwa Mwalimu kusema "Africa must initiate and shape" these changes kuna makosa gani hapo? Je tunataka wengine watubadilishe na sisi tuwe wajibuo yale yafanywayo na wengine? Hakuna aliyeonesha ubaya wazo hilo. Hakuna.
Mwalimu hakuwa anazungumzia "Mapinduzi ya kijamaa" alikuwa anazungumzia "revolution" in terms of rapid change, yaani mabadiliko yaliyolazimishwa. Na mapinduzi hayo ya nchi za Afrika kujipatia uhuru na kuwa mataifa (kumbuka haya maandishi yalikuwa ni ya 1966) yalikuwa ni mapinduzi ambayo yasingeweza kuzuiwa.
Na anasema wazi kuwa mapinduzi hayo (mabadiliko hayo) yana lengo moja nalo ni "the extension of all African citizens of the requirements of human dignity". Je, haikuwa lengo la uhuru na utaifa wetu kuwa na sisi tuwe na utu na heshima kama ya wanadamu wengine? Je halikuwa lengo na limebakia lengo kuwa tuweze kujichagulia viongozi wetu na kuamua hatima ya maisha yetu? Sasa kuna ubaya gani kwa Mwalimu kusema kuwa mabadiliko haya lazima yatupeleke kwenye lengo moja nalo ni "extension of all Africans citizens of the requirements of human dignity"? Hakuna aliyeonesha wapi Mwalimu amekosea kwenye hilo. Hakuna.
Mwalimu hakuahidi luninga kwa kila mtu, hakuahidi maisha Rais, hakuahidi "maisha bora kwa kila Mtanzania" na wala hakuahidi kuwa njia ya kufikia maendeleo na mafanikio itakuwa ni nyepesi na isiyohitaji watu kuhangaika. Mwalimu hakuwa mtu wa kufikirika kuwa maneno matamu basi ndiyo huliwa. Alitambua kuwa kujenga Taifa siyo lele mama; Angeweza kutoa ahadi ya "maziwa na asali" kwenye hiyo nchi ya ahadi. Hakufanya hivyo. Alituambia mapema kabisa kuwa "the task is a big and complicated one".
Kujenga Taifa from scratch siyo lele mama. Na kama nilivyosema mahali pengine, ninafuraha na fahari kuzaliwa ndani ya Taifa lililojengwa na Mwalimu kuliko kuzaliwa katika Taifa la viongozi wasio kuwa na principles zenye kujenga Taifa. Leo hii wapo viongozi ambao wanafikiri tumeshajenga Taifa sasa tuanze kulila tu; wameacha kulijenga Taifa wamebakia kujenga mahekalu yao. Wanafikiri kazi ya kulijenga Taifa ilikuwa rahisi na imeshamalizika. Kumbe bado ni kibarua.
Sasa kuna ubaya gani kwa mwalimu kutuambia mapema kabisa kuwa "the task before is big and complicated one"?. Hakuna mtu aliyeonesha kuwa "the task should have small one and uncomplicated one". Hakuna.
Ni kiongozi ambaye huweza kuona matokeo ya maamuzi yake na kwa mbali anaweza kuyaona katika fikra. Mwalimu aliona ugumu wa maamuzi mengine na alituambia mapema kabisa kuwa yawezekana katika kujenga hili Taifa tutakutana na maamuzi ambayo yana "involve the clashes of principle". Huu ni ukweli. Leo hii tunashindwa kuchagua nini cha kufanya kwa sababu tumepoteza principles zenyewe na hatuna cha kushilikia au pa kuanzia. Kuna makosa gani katika kutambua kuwa katika kufanya maamuzi huko mbeleni tunaweza "kugonganisha kanuni" mbalimbali na maslahi mbalimbali? Hakuna aliyeonesha ubaya wa kauli hiyo ya Mwalimu; hakuna.
Ametoa mfano ambao kwa wengine naona umewapita kwa haraka. Katika kujenga Taifa na unakutana na migongano ya principle hauna budi kuchagua. Nitatoa mfano. Baada ya matukio ya Septemba 11 Marekani ilijikuta inagonganisha principles mbili ambazo zimelijenga Taifa hilo; Usalama wa nchi na Uhuru wa kila mtu (security and individual liberties). Sasa walipokuwa wanajaribu kuja na sheria ambayo ingeweza kuwasaidia baadaye (positive change) wakajikuta na jukumu "big and complicated one".
Matokeo yake ni kupitishwa kwa sheria ya "Patriotic Act" ambayo ilikuwa inajaribu kutafuta uwiano wa mambo haya mawili katika kujaribu kuja na sheria nzuri. Hadi leo hii karibu miaka nane baadaye bado wanahangaika kutafuta "balance" ya clashing principles.
Sasa, kuna makosa gani katika kauli ya Mwalimu kuwa tunaweza kujikuta tunagonganisha principles? Hakuna mtu aliyeonesha mapungufu ya kauli hiyo ya Mwalimu zaidi ya watu kuleta hadithi na stori za maisha yao. (If you have noticed I have not interjected my own experiences.. nimezaliwa, nimesoma, na kukulia katika Tanzania hiyo hiyo ya Mwalimu.. lakini sijengi hoja kupitia mwanga wa hisia, kumbukumbu na vionjo vyangu; najenga hoja kwa kutumia intellectual argument).
If this is not "Bam!!" I don't know. Mwalimu anaeleza wazi kuwa hakuna jibu jepesi katika kuleta mabadiliko. Kuna watu wanazungumza humu kana kwamba Mwalimu angebonyeza hiki au kile na vitu vingekuwa hivi au vile; watu wanazungumza kana kwamba Mwalimu angeweza kuandika sheria hii basi mambo yote yangekuwa mswano.
Hapana; Mwalimu alijua na akaelezea wazi na mapema kuwa hakuna jibu jepesi katika kuleta mabadiliko ya kweli katika maisha ya Taifa hili. Alisema kuwa mabadiliko na maamuzi yoyote ya kuelekea mabadiliko hayo hayana budi kufanywa "in the light of historifcal circumstances and the conflicting needs of (the)present and future". Kuna ubaya gani katika kauli hiyo ya Mwalimu? Je mabadiliko hayaangalia "needs" za wakati uliopo au wa mbeleni au tunabadilika in a vacuum or empty space. Hakuna aliyeonesha mapungufu katika kauli hiyo ya Mwalimu zaidi ya kuzungumzia mambo elfu nje ya text tunayoiangalia. Hakuna.
Nobody could have said it better! Nani anapinga ukweli huo, ni nani haoni the majestic and glorious truth in such an eloquent utterance!? Hakuna ambaye amepinga zaidi ya kulaumu "KAMATA"!! Tulikulia kipindi hicho hicho, tunakumbuka mabasi ya RELWE (na mistari yake ya kahawia), nakumbuka kupita vilima vya Lukumburu siku chache baada ya askari wetu kuanguka tena nikiwa kwenye mabasi ya Kauru! Hivyo tukileta experience of "how life was so hard" nani alisema ilitakiwa iwe rahisi!? Yaani Marekani ya 1776 ilikuwa ni ile ile ya miaka hamsini baadaye na watu wangemlaumu George Washington na mababa wa US kwamba hawakuwa na Luninga na walikuwa na matatizo 1001 wakati wa kuanza kuijenga Marekani? Ndio maana watu leo wanafurahia ahadi za maneno matamu na ahadi za peponi lakini hawataki kuzifanyia kazi.
Watu wamesalimu amri mbele ya woga na kudai kuwa "haiwezekani"; wanachoshindwa kukiri ni kuwa "haiwezekani" kwa sababu hatuko tayari kujaribu na kufanya kazi kufanya iwezekane. Tunataka Mwalimu angetutengenezea njia nyeupe sisi tupite tu kama Watakatifu wanapoingia mji wa Yerusalemu! Hatutaki kushughulisha.
Nimeona hapa mara nyingi, mtu anakuja na kuuliza "jamani tuwekeeni Katiba" badala ya kuuliza "hiyo katiba iko wapi na mimi niisome"? Yaani watu wanataka mtu mwingine angewafanyia kazi zote, kusafisha shamba, kulima, kupanda, kupalilia, kuvuna na kuwawekea ghalani; wao wawe wanaenda kuchukua na kula tu! Na wangepata mtu wa kuwalisha wangeshukuru!
People are afraid to seive the opportunity. Ndio maana tunawaona wenzetu wa Zimbabwe wakitumia nafasi yao to seize this opportunity.
What a truth! Ni kweli tunaweza kukaa na kusubiri mabadiliko yatokee, au tunaweza kushiriki katika mabadiliko hayo. Mugabe ameshindwa kubadilika na sasa anabadilishwa na nguvu zilizo nje ya uwezo wake.
Mwalimu aliona mbali na aliona kuwa kuna mabadiliko yanakuja na yeye akaamua kuyawahi. Mzee Kitila amesema vizuri kabisa kuwa Kama Nyerere angeendelea kukaa madarakani yangeweza kumkuta ya Mugabe, siwezi kupinga; lakini kufikiri hivyo ni kwa mtu asiyemjua Nyerere. Nyerere asingeweza kuendelea kukaa madarakani kwa sababu intellectually he could see the upcoming change and he could not stop it. Ndio maana akaamua kukaa pembeni na kujaribu kuyaelekeza yaende vizuri. Leo hii tunazungumzia hali ya kisiasa nchini bila kukiri kuwa uamuzi wa Mwalimu kung'atuka ulikuwa ni uamuzi wa kijasiri sana na ulisaidia sana kulipeleka Taifa letu kwenye mabadiliko badala ya kusubiri nguvu za nje kutubadilisha kama yaliyomkuta Kibaki.
Well said; tusingeweza kuendelea na "jinsi ilivyo" lazima tubadilike na ilibidi tubadilike. Lakini ni sisi wenye kusimamia mabadiliko hayo. Wakati mwingine mabadiliko yataudhi watu wachache au kusababisha usumbufu lakini kutofanya mabadiliko kwa kuogopa usumbufu ni woga.
Leo, US na nchi nyingi bado zinafanya mabadiliko na watu wanasumbuka kidogo lakini wanajifunza kuishi nayo. Kuna mabadiliko kadhaa ya sheria mbalimbali n.k na watu wanatakiwa kuadjust. Sisi tunaogopa kubadilika kwa sababu tuko kwenye comfort zones zetu.
Ndio maana hawa wakuu Butiama wamepatwa na woga na pale magogoni wanasitasita kufanya maamuzi kwa sababu wakibadilisha vitu basi tunaweza kusumbua watu kama kina Mkapa, Yona, na wengineo, na hivyo hawafanyi mabadiliko. Kwa wengine wetu hilo linaonekana ni jambo zuri.
Lakini utaona kuwa watu hapa wanataka mabadiliko katika Tanzania lakini hawatuambii ni usufumbufu na shida gani zinaweza kutokea kwa wananchi tukileta mabadiliko? Tukitunga sheria ambazo zitasababisha usumbufu kwa watu je tuzipitishe?
Kwa mfano, tukipitisha sheria inayosema kuanzia sasa hadi ndani ya miaka kumi ijayo, nyumba zote za Tanzania ni lazima ziwe aidha za matofali ya kuchoma au ya sementi na ziwe zimeezekwa mabadi au vigae. Lengo likiwa ni hatimaye kuondokana na nyumba za udongo na makuti na mitete! Je sheria kama hiyo ni nzuri au kwa vile itasababisha usumbufu basi tusifanye hivyo?
Vipi tukisema kuwa Jiji la Dar linahitaji mifereji mipya ya kupitisha maji yatuwamayo na kuyapeleka baharini. Katika kufanya hivyo kuna majengo na nyumba ambazo itabidi zivunjwa ili kulitengeneza jiji la kisasa; je tufanye hivyo licha ya usumbufu kwa wakati na wananchi wa Dar. Wanaoogopa usumbufu watasema "hapana" tusiwasumbue watu. Lakini leo hii hata Marekani wanafanya mambo hayo tena kwa sababu za kiuwekezaji kupitia sheria kama za "eminent domain" ambazo hata Tanzania tunazo na zimewekwa kwenye mikataba ukiwemo wa Barrick Gold kule Bulyanhulu na Buzwagi.
Sasa mwalimu kuelezea ukweli huo kuwa yaweza kusababisha usumbufu imekuwa ni ubaya? Je angesema mabadiliko yatakuwa kama kwaya ya mbinguni si watu wangepiga makofi? Leo watawala wetu wanashinda kufanya maamuzi magumu kama ya kusimamisha uchimbaji Mererani hadi utaratibu na miundo mbinu mizuri umewekwa italeta usumbufu.
Sasa kuna ubaya gani katika hoja ya Mwalimu kuwa
Je hiki si ndicho mzee ES unakijenga hoja? Kuwa ni sisi wenyewe tuamua tunataka Taifa la namna gani na ni sisi wenyewe tushiriki katika kujenga Taifa hilo? Kwamba sisi ndio tuwe masters of "our own destiny and captains of souls"? Kuna ubaya gani katika maneno hayo ya Mwalimu kuwa "we have the resolution and the ability to overcome difficulties", kwani hatuna? Najua wengine hawawezi kwa sababu wanaogopa kubadilika au mabadiliko yatawasumbua; lakini ni watu wale wenye mawazo ya kuamini kuwa wanaweza kujenga Taifa walitakalo na wana resolve kufanya hivyo.
Kuna ubaya gani to state such a magnificent proposition kuwa tunaweza kushinda vikwazo vyote?

. Throughout these speeches and writings, and through all the activities of the Governments which I have been privileged to lead and support, there is however one recurring practical theme. It is the theme of change. For Africa must change; change from an area where people (take?) out an existence and adapt themselves to their environment, to a continent which challenges the environment and adapts it to mans need.
Afrika lazima ibadilike; kutoka bara ambalo linasubiri matukio nje yake yenye kusababisha mabadiliko kuelekea bara ambalo watu wake wanasimamia mabadiliko yao wao wenyewe. Ni nini kuarticulate ukweli kuwa lazima tuwe "a continent which challenges the environment and adapts it to mans need." Hakuna aliyeonesha ubaya wa fikra hii.
Africa must change her institutions to make feasible her new aspirations;
Mwalimu anasema pasipo utata kuwa Africa must change her Institutions. Kwa maana ya kwamba vile vyombo ambavyo tulikuwa tumevizoea au ambavyo vilikuwa dhaifu havina budi kubadilishwa na kuboreshwa. Na ukiangalia utaona kuwa wazee wenzangu hapa ndicho wanachosema kwamba kuna vitu (institutions) ambazo hata leo hii vinahitaji kubadilika. Ni ubaya gani wa fikra hizi za Mwalimu kuwa "Africa must change her institutions to make feasible her new aspirations" What is wrong with this self-evident truth? Hakuna aliyeonesha hadi hivi sasa.
her people must change their attitudes and practices to accord with the objectives.
Mwalimu alisema vizuri tena kama prophetically ( I use the term rather liberally) kuwa Bara letu lazima libadili mitazamo na vitendo vyake. Ukiangalia hili ndilo ambalo wengi tunalijadili tunapoangalia mapungufu ya Mwalimu n.k tunasema tunataka tubadilike, tunasema tubadili attitudes zetu na matendo yetu. Ili tufikie malengo (objectives) ya kujenga taifa la kisasa na la watu wenye kufurahia Taifa lao. Tunasema tunataka tubadilike. Tunapozungumzia kuzingatia misingi ya utawala wa sheria, kuwa na maadili n.k tunachosema ni kuwa vitu hivyo havipo sasa na tunataka tubadilike. Hivyo tunakubaliana na Mwalimu kuwa we need to change our "attitudes and practices to accord with the objectives." Kuna ubaya gani katika ukweli huu mwingine kuwa kama kweli tunataka kufikia malengo yetu hatuna budi kubadilika? Hakuna aliyeonesha hadi hivi sasa.
And these changes must be positive,
Mwalimu anasema mabadiliko hayo hayana budi yawe mazuri. Kwa maana kubadilika kuelekea ubaya si mabadiliko tunayoyataka. Alichosema na ambacho kinashuhudiwa na wachangiaji wengi hapa ni kuwa tubadilike kuelekea upande chanya. Tunapoangalia historia yetu na kuona mapungufu ya viongozi waliotutangulia tunaona ipo haja ya kubadilika. Kubadilika huko siyo kurudia kanuni, na mifumo ambayo imeonekana imefeli au ilikuwa na kasoro kubwa lakini ni kubadilika kufuatia kitu kilichobora zaidi.
Na katika kufanya hivyo twaweza kujikuta tukirudia baadhi ya kanuni za msingi au fikra za msingi zilizotujenga sisi kama Taifa (kama tutakavyoona huko mbeleni). Kurudia ubovu au vitu hasi Mwalimu alikataa; kasema wazi mabadiliko tunayoyahitaji ni yale mazuri. Sasa kuna ubaya gani katika hoja hii ya Mwalimu kuwa "Changes must be positive"? Hadi hivi sasa hakuna aliyeonesha ubaya wa hoja hiyo ya Mwanafalsafa Mwalimu.
they must be initiated and shaped by Africa and not simply be a reaction to events which affect Africa.
Mwalimu hapa anaonesha wazi kuwa Afrika inaweza kuchagua watu wengine waamue mabadiliko ndani yake au yenyewe ibadilike yenyewe. Kwamba waafrika wenyewe waamue hatima ya maisha yao na kiasi cha mabadiliko wayatakayo. Leo hii tunapozungumzia mabadiliko wengi tutachukia na kukasirishwa wakija wazungu na kutuambia tufanye hivi au vile kwa vile wanaamini hivyo ni vitu vizuri kwetu.
Wengi tutaona tumetukanwa na kudharauliwa kama Wamarekani wakija na kusema "badilisheni Katiba yenu", fanyeni hivi au vile. Yawezekana wakawa wanasema kweli lakini yawezekana wengi tungependa kuona kuwa ni sisi wenyewe tunaamua nini tunachotaka. Sasa kwa Mwalimu kusema "Africa must initiate and shape" these changes kuna makosa gani hapo? Je tunataka wengine watubadilishe na sisi tuwe wajibuo yale yafanywayo na wengine? Hakuna aliyeonesha ubaya wazo hilo. Hakuna.
For a revolution has begun in Africa. It is a revolution which we hope to control and channel so that our lives are transformed. It is a revolution with a purpose, and that purpose is the extension to all African citizens of the requirements of human dignity.
Mwalimu hakuwa anazungumzia "Mapinduzi ya kijamaa" alikuwa anazungumzia "revolution" in terms of rapid change, yaani mabadiliko yaliyolazimishwa. Na mapinduzi hayo ya nchi za Afrika kujipatia uhuru na kuwa mataifa (kumbuka haya maandishi yalikuwa ni ya 1966) yalikuwa ni mapinduzi ambayo yasingeweza kuzuiwa.
Na anasema wazi kuwa mapinduzi hayo (mabadiliko hayo) yana lengo moja nalo ni "the extension of all African citizens of the requirements of human dignity". Je, haikuwa lengo la uhuru na utaifa wetu kuwa na sisi tuwe na utu na heshima kama ya wanadamu wengine? Je halikuwa lengo na limebakia lengo kuwa tuweze kujichagulia viongozi wetu na kuamua hatima ya maisha yetu? Sasa kuna ubaya gani kwa Mwalimu kusema kuwa mabadiliko haya lazima yatupeleke kwenye lengo moja nalo ni "extension of all Africans citizens of the requirements of human dignity"? Hakuna aliyeonesha wapi Mwalimu amekosea kwenye hilo. Hakuna.
The task before us is a big and complicate one.
Mwalimu hakuahidi luninga kwa kila mtu, hakuahidi maisha Rais, hakuahidi "maisha bora kwa kila Mtanzania" na wala hakuahidi kuwa njia ya kufikia maendeleo na mafanikio itakuwa ni nyepesi na isiyohitaji watu kuhangaika. Mwalimu hakuwa mtu wa kufikirika kuwa maneno matamu basi ndiyo huliwa. Alitambua kuwa kujenga Taifa siyo lele mama; Angeweza kutoa ahadi ya "maziwa na asali" kwenye hiyo nchi ya ahadi. Hakufanya hivyo. Alituambia mapema kabisa kuwa "the task is a big and complicated one".
Kujenga Taifa from scratch siyo lele mama. Na kama nilivyosema mahali pengine, ninafuraha na fahari kuzaliwa ndani ya Taifa lililojengwa na Mwalimu kuliko kuzaliwa katika Taifa la viongozi wasio kuwa na principles zenye kujenga Taifa. Leo hii wapo viongozi ambao wanafikiri tumeshajenga Taifa sasa tuanze kulila tu; wameacha kulijenga Taifa wamebakia kujenga mahekalu yao. Wanafikiri kazi ya kulijenga Taifa ilikuwa rahisi na imeshamalizika. Kumbe bado ni kibarua.
Sasa kuna ubaya gani kwa mwalimu kutuambia mapema kabisa kuwa "the task before is big and complicated one"?. Hakuna mtu aliyeonesha kuwa "the task should have small one and uncomplicated one". Hakuna.
In the process we shall have many decisions to make which involves clashes of principle
Ni kiongozi ambaye huweza kuona matokeo ya maamuzi yake na kwa mbali anaweza kuyaona katika fikra. Mwalimu aliona ugumu wa maamuzi mengine na alituambia mapema kabisa kuwa yawezekana katika kujenga hili Taifa tutakutana na maamuzi ambayo yana "involve the clashes of principle". Huu ni ukweli. Leo hii tunashindwa kuchagua nini cha kufanya kwa sababu tumepoteza principles zenyewe na hatuna cha kushilikia au pa kuanzia. Kuna makosa gani katika kutambua kuwa katika kufanya maamuzi huko mbeleni tunaweza "kugonganisha kanuni" mbalimbali na maslahi mbalimbali? Hakuna aliyeonesha ubaya wa kauli hiyo ya Mwalimu; hakuna.
where we have to choose, let us say, between rapid development and individual freedom, or between efficiency and equality.
Ametoa mfano ambao kwa wengine naona umewapita kwa haraka. Katika kujenga Taifa na unakutana na migongano ya principle hauna budi kuchagua. Nitatoa mfano. Baada ya matukio ya Septemba 11 Marekani ilijikuta inagonganisha principles mbili ambazo zimelijenga Taifa hilo; Usalama wa nchi na Uhuru wa kila mtu (security and individual liberties). Sasa walipokuwa wanajaribu kuja na sheria ambayo ingeweza kuwasaidia baadaye (positive change) wakajikuta na jukumu "big and complicated one".
Matokeo yake ni kupitishwa kwa sheria ya "Patriotic Act" ambayo ilikuwa inajaribu kutafuta uwiano wa mambo haya mawili katika kujaribu kuja na sheria nzuri. Hadi leo hii karibu miaka nane baadaye bado wanahangaika kutafuta "balance" ya clashing principles.
Sasa, kuna makosa gani katika kauli ya Mwalimu kuwa tunaweza kujikuta tunagonganisha principles? Hakuna mtu aliyeonesha mapungufu ya kauli hiyo ya Mwalimu zaidi ya watu kuleta hadithi na stori za maisha yao. (If you have noticed I have not interjected my own experiences.. nimezaliwa, nimesoma, na kukulia katika Tanzania hiyo hiyo ya Mwalimu.. lakini sijengi hoja kupitia mwanga wa hisia, kumbukumbu na vionjo vyangu; najenga hoja kwa kutumia intellectual argument).
There is and will be no simple universal answer to such problems; the choice will have to be made in the light of historical circumstances and the conflicting needs of present and future.
If this is not "Bam!!" I don't know. Mwalimu anaeleza wazi kuwa hakuna jibu jepesi katika kuleta mabadiliko. Kuna watu wanazungumza humu kana kwamba Mwalimu angebonyeza hiki au kile na vitu vingekuwa hivi au vile; watu wanazungumza kana kwamba Mwalimu angeweza kuandika sheria hii basi mambo yote yangekuwa mswano.
Hapana; Mwalimu alijua na akaelezea wazi na mapema kuwa hakuna jibu jepesi katika kuleta mabadiliko ya kweli katika maisha ya Taifa hili. Alisema kuwa mabadiliko na maamuzi yoyote ya kuelekea mabadiliko hayo hayana budi kufanywa "in the light of historifcal circumstances and the conflicting needs of (the)present and future". Kuna ubaya gani katika kauli hiyo ya Mwalimu? Je mabadiliko hayaangalia "needs" za wakati uliopo au wa mbeleni au tunabadilika in a vacuum or empty space. Hakuna aliyeonesha mapungufu katika kauli hiyo ya Mwalimu zaidi ya kuzungumzia mambo elfu nje ya text tunayoiangalia. Hakuna.
The only certain thing is that if we forget any of our principles, even when we are ignoring or breaking them, then we shall have betrayed the purpose of our revolution and Africa will fail to make its proper contribution to the development of mankind.
Nobody could have said it better! Nani anapinga ukweli huo, ni nani haoni the majestic and glorious truth in such an eloquent utterance!? Hakuna ambaye amepinga zaidi ya kulaumu "KAMATA"!! Tulikulia kipindi hicho hicho, tunakumbuka mabasi ya RELWE (na mistari yake ya kahawia), nakumbuka kupita vilima vya Lukumburu siku chache baada ya askari wetu kuanguka tena nikiwa kwenye mabasi ya Kauru! Hivyo tukileta experience of "how life was so hard" nani alisema ilitakiwa iwe rahisi!? Yaani Marekani ya 1776 ilikuwa ni ile ile ya miaka hamsini baadaye na watu wangemlaumu George Washington na mababa wa US kwamba hawakuwa na Luninga na walikuwa na matatizo 1001 wakati wa kuanza kuijenga Marekani? Ndio maana watu leo wanafurahia ahadi za maneno matamu na ahadi za peponi lakini hawataki kuzifanyia kazi.
Watu wamesalimu amri mbele ya woga na kudai kuwa "haiwezekani"; wanachoshindwa kukiri ni kuwa "haiwezekani" kwa sababu hatuko tayari kujaribu na kufanya kazi kufanya iwezekane. Tunataka Mwalimu angetutengenezea njia nyeupe sisi tupite tu kama Watakatifu wanapoingia mji wa Yerusalemu! Hatutaki kushughulisha.
Nimeona hapa mara nyingi, mtu anakuja na kuuliza "jamani tuwekeeni Katiba" badala ya kuuliza "hiyo katiba iko wapi na mimi niisome"? Yaani watu wanataka mtu mwingine angewafanyia kazi zote, kusafisha shamba, kulima, kupanda, kupalilia, kuvuna na kuwawekea ghalani; wao wawe wanaenda kuchukua na kula tu! Na wangepata mtu wa kuwalisha wangeshukuru!
But the opportunity is before us provided we have to courage to seize it.
People are afraid to seive the opportunity. Ndio maana tunawaona wenzetu wa Zimbabwe wakitumia nafasi yao to seize this opportunity.
For the choice is not between change or no change; the choice for Africa is between changing or being changed changing our lives under own direction, or being changed by impact of forces outside our control.
What a truth! Ni kweli tunaweza kukaa na kusubiri mabadiliko yatokee, au tunaweza kushiriki katika mabadiliko hayo. Mugabe ameshindwa kubadilika na sasa anabadilishwa na nguvu zilizo nje ya uwezo wake.
Mwalimu aliona mbali na aliona kuwa kuna mabadiliko yanakuja na yeye akaamua kuyawahi. Mzee Kitila amesema vizuri kabisa kuwa Kama Nyerere angeendelea kukaa madarakani yangeweza kumkuta ya Mugabe, siwezi kupinga; lakini kufikiri hivyo ni kwa mtu asiyemjua Nyerere. Nyerere asingeweza kuendelea kukaa madarakani kwa sababu intellectually he could see the upcoming change and he could not stop it. Ndio maana akaamua kukaa pembeni na kujaribu kuyaelekeza yaende vizuri. Leo hii tunazungumzia hali ya kisiasa nchini bila kukiri kuwa uamuzi wa Mwalimu kung'atuka ulikuwa ni uamuzi wa kijasiri sana na ulisaidia sana kulipeleka Taifa letu kwenye mabadiliko badala ya kusubiri nguvu za nje kutubadilisha kama yaliyomkuta Kibaki.
In Africa there is no stability in stagnation in this twentieth century; stability can only be achieved through maintaining balance during rapid change.
Tanzania has chosen to ride and try to harness the whirlwind which is sweeping through this continent. We know that some human dislocation is inevitable in this process, but we believe that much more would ultimately be involved in doing nothing. For we recognize that to try to maintain the status quo is to try to ignore the world.
Well said; tusingeweza kuendelea na "jinsi ilivyo" lazima tubadilike na ilibidi tubadilike. Lakini ni sisi wenye kusimamia mabadiliko hayo. Wakati mwingine mabadiliko yataudhi watu wachache au kusababisha usumbufu lakini kutofanya mabadiliko kwa kuogopa usumbufu ni woga.
Leo, US na nchi nyingi bado zinafanya mabadiliko na watu wanasumbuka kidogo lakini wanajifunza kuishi nayo. Kuna mabadiliko kadhaa ya sheria mbalimbali n.k na watu wanatakiwa kuadjust. Sisi tunaogopa kubadilika kwa sababu tuko kwenye comfort zones zetu.
Ndio maana hawa wakuu Butiama wamepatwa na woga na pale magogoni wanasitasita kufanya maamuzi kwa sababu wakibadilisha vitu basi tunaweza kusumbua watu kama kina Mkapa, Yona, na wengineo, na hivyo hawafanyi mabadiliko. Kwa wengine wetu hilo linaonekana ni jambo zuri.
Lakini utaona kuwa watu hapa wanataka mabadiliko katika Tanzania lakini hawatuambii ni usufumbufu na shida gani zinaweza kutokea kwa wananchi tukileta mabadiliko? Tukitunga sheria ambazo zitasababisha usumbufu kwa watu je tuzipitishe?
Kwa mfano, tukipitisha sheria inayosema kuanzia sasa hadi ndani ya miaka kumi ijayo, nyumba zote za Tanzania ni lazima ziwe aidha za matofali ya kuchoma au ya sementi na ziwe zimeezekwa mabadi au vigae. Lengo likiwa ni hatimaye kuondokana na nyumba za udongo na makuti na mitete! Je sheria kama hiyo ni nzuri au kwa vile itasababisha usumbufu basi tusifanye hivyo?
Vipi tukisema kuwa Jiji la Dar linahitaji mifereji mipya ya kupitisha maji yatuwamayo na kuyapeleka baharini. Katika kufanya hivyo kuna majengo na nyumba ambazo itabidi zivunjwa ili kulitengeneza jiji la kisasa; je tufanye hivyo licha ya usumbufu kwa wakati na wananchi wa Dar. Wanaoogopa usumbufu watasema "hapana" tusiwasumbue watu. Lakini leo hii hata Marekani wanafanya mambo hayo tena kwa sababu za kiuwekezaji kupitia sheria kama za "eminent domain" ambazo hata Tanzania tunazo na zimewekwa kwenye mikataba ukiwemo wa Barrick Gold kule Bulyanhulu na Buzwagi.
Sasa mwalimu kuelezea ukweli huo kuwa yaweza kusababisha usumbufu imekuwa ni ubaya? Je angesema mabadiliko yatakuwa kama kwaya ya mbinguni si watu wangepiga makofi? Leo watawala wetu wanashinda kufanya maamuzi magumu kama ya kusimamisha uchimbaji Mererani hadi utaratibu na miundo mbinu mizuri umewekwa italeta usumbufu.
Sasa kuna ubaya gani katika hoja ya Mwalimu kuwa
Hakuna aliyeonesha ubaya wa hoja hiyo ya Mwalimu. Hakuna.We know that some human dislocation is inevitable in this process, but we believe that much more would ultimately be involved in doing nothing. For we recognize that to try to maintain the status quo is to try to ignore the world.
We prefer to participate in the shaping of our own destiny, and we believe that we have the resolution and the ability to overcome difficulties and build the kind of society we want.
Je hiki si ndicho mzee ES unakijenga hoja? Kuwa ni sisi wenyewe tuamua tunataka Taifa la namna gani na ni sisi wenyewe tushiriki katika kujenga Taifa hilo? Kwamba sisi ndio tuwe masters of "our own destiny and captains of souls"? Kuna ubaya gani katika maneno hayo ya Mwalimu kuwa "we have the resolution and the ability to overcome difficulties", kwani hatuna? Najua wengine hawawezi kwa sababu wanaogopa kubadilika au mabadiliko yatawasumbua; lakini ni watu wale wenye mawazo ya kuamini kuwa wanaweza kujenga Taifa walitakalo na wana resolve kufanya hivyo.
Kuna ubaya gani to state such a magnificent proposition kuwa tunaweza kushinda vikwazo vyote?
For those with courage to aspire, to believe, and to work, Tanzania is a challenging and exciting land. It is my privilege and my happiness to dedicate myself to its future.[/B]
What a dare! Kwa wale ambao hawana courage to aspire, or believe or work Tanzania kwao is not challenging and not exciting at all. Kwa sisi wengine ambao tunaamini change is necessary basi tunaona fahari kuhusishwa na mabadiliko hayo na tuko tayari kuhakikisha kuwa mabadiliko hayo yanatokea.
Kwa kifupi:
Hadi hivi sasa hakuna aliyeonesha hata kwa karibu ubaya wa hoja ya Mwalimu kuhusu mabadiliko na kama alichosema hakikuwa sahihi. Ukiondoa malalamishi ya kukosa luninga, kula yanga n.k hakuna aliyeangalia kwa kina substance ya alichosema Mwalimu na kusema it was substantially untrue, illogical, beyond belief and inherently redundant. None whatsoever.
Kwa maneno mengine, fikra za Mwalimu kuhusu haja ya mabadiliko katika Afrika na katika Tanzania still stand today as it stood 42 years ago! My friends, we need to change for a change is necessary. The changes we need are the changes that we will be masters of. We can not wait for other people to come and change us or let other external forces to impact us so that we change. We have to take charge of of whatever idea we aspire to and work hard to bring it about.
This is the main idea in this piece. Do you agree?