Fikra kuhusu watu wakimya

Fikra kuhusu watu wakimya

Mm ni mkimya hasa kwa watu wagen kwangu ila mkimya kias kidogo nyumbani. Ila megundua ukimya umenifanya baadhi ya watu siwez kuongea nao kabisa wala kuwa nao karibu. Sifa mojawapo ya watu wakimya hupenda kusikiliza kwa makin na kuzisoma tabia na hisia za wengine hivyo hujikuta wale ambao umewaona huendan nao ni vigumu sana kuwa nao karibu na huwa wakimya wengi wanajua mengi juu ya mawazo ya wengine
Kwel mkuu
 
Hizi ndio sifa za watu wakimya:
1. Sio wacheshi
2. Wana kiburi
3. Sio rahisi kukubali kosa alilo fanya
4. Ni watu waku jitenga
5. Hawapendi uguse vitu vyao
6. Ni wazuri kwa u spy / upepelezi
7. Ni watu waku jiweka local sana hata kama fedha ipo
8. Hawana muda sana wanawake.
9.
Mulemule yaani
 
Ukimya ni tabia.lakini kwa vile wakimya huongea zaidi kwa vitendo ndo utaona mjumuisho wa tabia nyingine zinajitokeza kama dharau., kiburi tena kile cha uzima hasa.! Kedi ., pozi.,na jeuri iliyokomaa .lakini pia wenye tabia hii huwa wana kisirani cha kuua......na huwa wagumu kubadilisha maamuzi.! Ila ukiwajulia mbona utastarehe...! Kiufupi akili zao huwa bize kutafakari zaidi na hawapendi mpinzani.wala kero.!
umewahi kushuhudia wakiua??
 
Mm nimepata majaribu sana ktk maisha yangu kwa tabia yangu ya ukimya, unaishi na watu kila m1 anakunyooshea kidole kuwa una dharau, kumbe hata kidogo???

Ilifikia hatua nikajifunza kunywa pombe nilewe ili walau nipate maneno ya kuropoka niwafurahishe walio karibu yangu!

Sio kila mtu mkimya anakuwa na dharau, big #NOO !
vipi bado mkimya hadi leo?
 
Tufafanulie kidogo utofauti ni upi?
Ukiwa ni hali tu ya kutokuwa muongeaj, wala maneno mengi. Unaweza kaaa na mtu hata usipige soga nyiingi, lakini endapo mtu au jambo likakuudhi reaction yake ni hatari. Kuna wengine unakuta hata kusamehe jambo au kuliacha au kusahau ni ishu lazima afanye kitu

Lakin kuna mtu ni mpole, lakina ni mtu wa watu, story. Sasa upole unaonekana jinsi anavyo yakabili mambo, mwitikio yake katk kukasilishwa n. K
 
Ukimya unaweza kuwa tabia ya asiri tu,lakini wakimya wengi ni watu ambao hawana cha kuongea au hawajiamini kama wanacho kitu sahihi cha kuongea kwahyo kuepusha kuonekana wa hovyo huchagua kukaa kimya,atleast wana busara ya kujua udhaifu wao na kuchagua kuuficha kwa kukaa kimya kuliko walopokaji ambao hawajui kwamba hawajui
 
Hizi ndio sifa za watu wakimya:
1. Sio wacheshi
2. Wana kiburi
3. Sio rahisi kukubali kosa alilo fanya
4. Ni watu waku jitenga
5. Hawapendi uguse vitu vyao
6. Ni wazuri kwa u spy / upepelezi
7. Ni watu waku jiweka local sana hata kama fedha ipo
8. Hawana muda sana wanawake.
9.
Hiyo namba 7 uongo kaka hapo inategemea na mtu mwenyewe
 
Mtu mkimya wakati wewe unaongea kwa mdomo yeye anaongea kwa ubongo.

Ndio maana ukiona unaongea na mtu lakini yeye amekaa kimya achana nae.

Wakati wewe unaongea moja mdomoni yeye anawaza na kujibu mara nyingi zaidi kimoyo moyo.

Hivyo usishangea unavyoongea nae ukajua anakusikiliza kumbe yeye anatafuta namana ya kukujibu iwe kwa maneno au vitendo.

Na mbaya zaidi kila unachokiongea hasahau.!
Hii ndo inaitwa Reasoning Capacity,wana uwezo mkubwa wa kuchanganua maneno kabla ya kuyaongea kitu ambacho wengi hatuna na kuwa waropokaji..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom